"Kumbe sasa naanza kupata picha kamili ya sakata hili, nakumbushwa kuwa kwenye historia ya Derby ya Kariakoo, huwa wote wawili hawafanyi mazoezi pale uwanjani siku moja kabla ya mchezo, uwe Mgeni au uwe Mwenyeji huruhusiwi kuugusa uwanja, imekuwa hivyo kwenye historia ya mechi zao na uwanja unalindwa, kila mmoja anapaswa kufanya mazoezi anapofanyiaga, japo hii haipo kikanuni hii kitu ndio nimejua leo, imenishangaza sana.

Maswali yanakuja, kama mchakato huu haupo Kikanuni na walikuwa wanafuata wote wawili, je walikuwa wanasimamiwa na nani wote wawili kutekeleza kanuni hii mficho? Maana hata mechi ya raundi ya kwanza Mgeni Yanga hakusogea kabisa kwa Mkapa, nimetumiwa picha kuwa walifanya mazoezi Kigamboni, hili sakata

Ligi ina kanuni au utaratibu au makubaliano ambayo hatuyajui ama? Rasmi nimefunga mikono yangu, siandiki tena hii kitu kumbe ina mambo mengi sana, tunaweza kukomaa na Kanuni kumbe wala watu hawapo huko kwenye karatasi zetu" - Farhan JR, Mchambuzi.

"Kumbe sasa naanza kupata picha kamili ya sakata hili, nakumbushwa kuwa kwenye historia ya Derby ya Kariakoo, huwa wote wawili hawafanyi mazoezi pale uwanjani siku moja kabla ya mchezo, uwe Mgeni au uwe Mwenyeji huruhusiwi kuugusa uwanja, imekuwa hivyo kwenye historia ya mechi zao na uwanja unalindwa, kila mmoja anapaswa kufanya mazoezi anapofanyiaga, japo hii haipo kikanuni hii kitu ndio nimejua leo, imenishangaza sana. Maswali yanakuja, kama mchakato huu haupo Kikanuni na walikuwa wanafuata wote wawili, je walikuwa wanasimamiwa na nani wote wawili kutekeleza kanuni hii mficho? Maana hata mechi ya raundi ya kwanza Mgeni Yanga hakusogea kabisa kwa Mkapa, nimetumiwa picha kuwa walifanya mazoezi Kigamboni, hili sakata🙌😀 Ligi ina kanuni au utaratibu au makubaliano ambayo hatuyajui ama? Rasmi nimefunga mikono yangu, siandiki tena hii kitu kumbe ina mambo mengi sana, tunaweza kukomaa na Kanuni kumbe wala watu hawapo huko kwenye karatasi zetu" - Farhan JR, Mchambuzi.
0 Comments ·0 Shares ·93 Views