Rais wa Nchi ya Burundi , Evariste Ndayishimiye anasema kuwa Nchi ya Rwanda ina mpango wa kuivamia Burundi kupitia Congo ambapo anasema Nchi hiyo itakuwa imekosea sana.

“Tunajua kwamba Rwanda inajaribu kutushambulia kupitia eneo la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kupitia vuguvugu la Red-Tabara. Lakini tunawaambia kwamba ikiwa wanataka kushambulia Bujumbura kupitia Congo na sisi Kigali hatuko mbali kupitia Kirundo,” alisema Rais Evariste Ndayishimiye

Baada ya kauli hiyo, Msemaji wa Serikali ya Rwanda Yolande Makolo amesema kuwa, ameshangazwa na kauli ya Rais Evariste Ndayishimiye huku akihoji Rais Ndayishimiye anaeleza kuwa ana taarifa za kuaminika kuwa Rwanda ina mpango wa kushambulia Burundi ?. Msemaji huyo alisema pia endapo hali hiyo ikitokea basi migogoro inaweza kuwa na maafa kwani inaweza kusambaa katika ukanda mzima wa Afrika Mashariki na kati.

Rais Ndayishimiye amemalizia kwa kusema kuwa tayari ameshatuma Wajumbe kadhaa kwa Rais wa Rwanda Paul Kagame wa kumtaka atekeleze makubaliano ambayo yatazileta pamoja Nchi hizo mbili pamoja lakini hadi leo hii hakuna majibu yoyote yaliyotolewa na bado anayasubiri pia.

Rais wa Nchi ya Burundi 🇧🇮, Evariste Ndayishimiye anasema kuwa Nchi ya Rwanda 🇷🇼 ina mpango wa kuivamia Burundi kupitia Congo ambapo anasema Nchi hiyo itakuwa imekosea sana. “Tunajua kwamba Rwanda inajaribu kutushambulia kupitia eneo la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kupitia vuguvugu la Red-Tabara. Lakini tunawaambia kwamba ikiwa wanataka kushambulia Bujumbura kupitia Congo na sisi Kigali hatuko mbali kupitia Kirundo,” alisema Rais Evariste Ndayishimiye Baada ya kauli hiyo, Msemaji wa Serikali ya Rwanda Yolande Makolo amesema kuwa, ameshangazwa na kauli ya Rais Evariste Ndayishimiye huku akihoji Rais Ndayishimiye anaeleza kuwa ana taarifa za kuaminika kuwa Rwanda ina mpango wa kushambulia Burundi ?. Msemaji huyo alisema pia endapo hali hiyo ikitokea basi migogoro inaweza kuwa na maafa kwani inaweza kusambaa katika ukanda mzima wa Afrika Mashariki na kati. Rais Ndayishimiye amemalizia kwa kusema kuwa tayari ameshatuma Wajumbe kadhaa kwa Rais wa Rwanda Paul Kagame wa kumtaka atekeleze makubaliano ambayo yatazileta pamoja Nchi hizo mbili pamoja lakini hadi leo hii hakuna majibu yoyote yaliyotolewa na bado anayasubiri pia.
Like
1
· 0 Commentaires ·0 Parts ·115 Vue