Upgrade to Pro

  • DOUBLE AGENTS NGULI WANNE KUWAHI KUTOKEA KATIKA ULIMWENGU WA UJASUSI

    Mustakabali wa taifa lolote lile hutegemea pamoja na mambo mengine mifumo ya ulinzi, kwani hii ndio nguzo mhimu katika kuhakikisha ustawi wa maslahi ya taifa husika

    Ni kwa msingi huo basi mataifa yote duniani yameunda vyombo tofauti tofauti vya ulinzi mojawapo ikiwemo idara za ujajusi, mifano ipo mingi, CIA, M16, BND, MOSSAD, TISS n.k!

    Lakini kuwa na taasisi au vyombo hivyo vinahiyaji nguvu kazi, nguvu kazi hii sharti iwe yenye weledi na uzalendo wa kutukuka, kwani kazi wanayoifanya ni kazi nyeti mno na inayozungukwa na mambo mengi sana, hivyo kuteleza kwa namna yoyote ile basi kunaacha madhara makubwa mno! Na kiukweli wapo walioteleza na kuleta madhara yasiyoelezeka, sasa Leo nimeona tuangalie kwa ufupi baadhi ya wanausalama walioteleza na kujikuta walitumia pande mbili au zaidi maarufu kwa jina la *DOUBLE AGENT*

    *Lakini kwanza kabisa double agent ni nani?*

    Tunaweza tukasema ni afisa usalama wa tasisis au serikali ambaye amepewa majukumuu ya kuichunguza taasisi au nchi nyingine lakini wakati huo huo anakuwa tena anafanya kazi hiyo hiyo kwa ajiri ya taasisi au nchi anayopaswa kuichunguza dhidi ya taasisi au nchi iliyomtuma! Wengi wanasem double agent anaweza kuwa matokeo ya tamaa ya pesa, kulazimishwa( baada ya kutishiwa kufanyiwa kitu kibaya), mapenzi tu, yaani mtu anapenda tu kuwa double agent, kupandikizwa kwa makusudi( marekani wamefaidika sana na aina hii hasa Mashariki ya kati) au inaweza kuwa ni sababu ya mitazamo…

    Hawa wafuatao ni baadhi ya double agents nguli kuwahi kutokea na balaa

    *Human Khalid Al-Balawi*

    Huyu jamaa alikuwa daktari kitaaluma na alikuwa raia wa Jordan, alikamatwa na mamlaka za Jordan kipindi akiwa mwanafunzi kwenye chuo kikuu cha Isntanbul nchini Uturuki baada ya kuonekana akiwa na muelekeo wa misimamamo mikali, inasemekana baadae CIA waliingilia na kumshawishi awe double agent kwa ahadi ya kusamehewa. Jamaa alikubali na CIA wakamuandaa kikamilifu kwa kazi hiyo ambapo baada ya kuiva wakampeleka Pakistan na Afghanistan na kumpa jukumuu la kufuatilia nyendo na shughuli za alqaida nchini humo.

    Human aliifanya kazi hiyo kwa uaminifu mkubwa mno na akafanikiwa kuwashawishi CIA ambao walionekana kumwamini 100%. Kumbe hawakujua kuwa aliqaida walikuwa tayari wamembadilisha na alikuwa akifanya nao kazi.

    Siku moja akawaeleza kuwa alikuwa na taarifa muhimu kuhusu kiongozi wa juu wa alqaida bwana Ayman- Al-Zawahili na akawapa masharti kuwa angependa taarifa hizo azifikishe kwa viongozi wakuu wa CIA katika eneo hilo, kwakuwa walikuwa wanamtafuta sana Zawahili hawakusita kumkubalia na kumuagiza afike kwenye Ofisi za CIA eneo la Khost Afghanistan, Khalid alifika kwa kuchelewa na kutokana na kimuhe muhe cha taarifa waliyokuwa wanakwenda kuipokea basi wakasahau hadi kumkagua, kumbe jamaa alikuwa amevaa mabomu, baada ya kufika ndani kwa wakubwa jamaa alijilipua na kuua maafisa kadhaa wa ngazi za juu wa CIA katika eneo hilo.

    *Arthur Owens*

    Arthur alikuwa mwingereza kutoka kisiwa cha Wales na kabla ya vita ya dunia ya pili alikuwa akifanya kazi kama mkandarasi na alikuwa akifanya serikali zote mbili, Ujerumani na England, baada ya vita kuanza aliajiriwa kama mhandisi kwenye meli vita za England akifanya kazi kama fundi betri, baadae Wajerumani walianza kumuomba awape taarifa hasa kuhusu meli vita za England na yeye bila hiana akifanya kazi hiyo, baadae alijiunga nao rasmi na akawa anafanya kazi nao huku pesa na wanawake wazuri yakiwa ndo malipo kwa kazi yake hiyo tukufu.

    Baadae alirudi England na kujipeleka moja kwa moja kwa M15 na kuwaeleza ukweli wake na wajerumani, M16 walimpokea na kumtumia ambapo aliwasaidia kufichua zaidi maofisa 120 wa kijeruman nchini England na wakamtumia kuwalisha Wajerumani hao habari za uongo na zile zisixokuwa na athari kubwa kwao.

    Mwaka 1941 Arthur na mwenzake mmoja walikamatwa na wajerumani lakini cha ajabu mwenzake alinyongwa huku yeye akiachwa hali iliyowatia wasiwasi England na alivyorudi walimkamata na kumtia kolokoloni hadi baada ya vita, baadae aliwalazimisha England wamlipe fedha kwa maadai ya kumfunga bila makosa na kama watagoma basi ataweka hadharani kila kitu, England walinywea na hadi anakufa hakuwahi kusema chochote.

    *Kim Philby*

    Kim Philby alikuwa ni afisa wa idara ya usalama ya England, yeye na wenzake wanne walitengeza a spy ring iliyopewa jina la the Combridge five, na wakifanya kazi kwa niaba ya KGB, ni kipindi ambacho wote watano walikuwa wakisoma chuoni hapo, wenzake walikuwa ni pamoja na Donald MacLean, Guy borguess na Anthony Brunt ambapo mtu wa tano kwenye kundi hilo hadi Leo hajawahi kujulikana! Kimsingi Borguess ndiye aliyemsajili Kim na wakati huyo tayari yeye alikuwa ni double agent.

    Kilichomsukuma Kim ilikuwa ni imani yake katika falsafa za kijamaa, pamoja na kuwa double agent lakini Kim anasemwa kama mtu aliyefanya kazi kwa weledi mkubwa sana na alipata kutunukiwa nishani kadhaa kwa utumishi uliotukuka kabla ya kuja kumgundua kuwa alikuwa akifanya kazi na KGB, wakati wenzake wanakamatwa yeye alikuwa ameshaacha kazi na alikuwa Lebanon na hakurudi tena England Bali aliekea Jamhuri ya Usovieti ambako alipewa kazi kwenye idara kadhaa za ulinzi, alifariki mwaka 1988 akiwa huko huko Usovieti, Kim aliandika kitabu alichokipa jina la *My secret war* akieleza namna alivyopambana na ubepari.

    *Juan Pujol Garsia*

    Garsia alikuwa mhisipania ambaye maisha yake yalionekana kutokua na muelekeo kwani kwenye umri wa miaka 32 alikuwa ameshindwa karibia kila kitu, shule, biashara na hata familia, vyote alikuwa amejaribu na vikamshinda.

    Baadae wakati wa vita kuu ya pili ya dunia aliamua kwenda kuomba kazi kwenye idara za usalama za England na Marekani lakini aligonga mwamba kwa madai mtu ambaye hakuwa na uwezo hata wa kufuga kuku angeweje kufanya kazi nyeti kama hii tena katika wakati tete. Baada ya kukataliwa akaona isiwe taabu akaenda zake kwa Wajerumani na kujifanya mmoja wa wanazi kindakindaki wa Hitler, manazi baadae walimuamini na kumpa kazi ambapo walimpangia kwenda England! Alielekea huko akipitia Porto Ureno na alianza kazi kwa kukusanya habari kwenye magazeti na redio, baadae alianza kupiga hatua kwa kusajili watu mhimu kutoka wazara ya habari na mawasiliano pamoja na masekretari kwenye wizara mbalimbali, baadae pia alifanikiwa kuingia hadi jeshini na jusajili watu huko.

    Garsia alikuja kuumbuliwa na double agent wa kijerumani ambaye aliwatonya England juu ya uwepo wake nchini humo.

    Baada ya kubumbuluka Garsia akijipeleka mwenyewe kwa M15 ambapo walikubali kuendelea kutumia mara hii wakimtumia kuwalisha habari za uongo.

    Garsia anakumbukwa sana kutokana na kazi tukufu aliyoifanya wakati majeshi ya muungano wa England, Canada, Marekani na baadhi ya wanajeshi wa Ufaransa yalipoanza oparesheni ya kukomboa maeneo yaliyokuwa yamekamatwa na Ujerumani na hasa katika uvamizi wa eneo la Normandy, baada ya wanajeshi wa muungano kuelekea katika eneo hilo wajerumani walipata intelejensia na wakawa wametuma vikosi kwenda kupambana na majeshi ya muungano huku vikosi vingine vikiwekwa tayari nchini ubelgiji, lakini Garsia kwa ujasiri wa hali ya juu akamtumia telegraphy na kumwambia hakukuwa na mashambulizi yoyote katika eneo hilo na kwamba habari alizokuwa amepewa Hitler ulikuwa ni uongo, kwakuwa Hitler alikuwa anamuamini sana basi akaiamini taarifa hii na akaviamrisha vikosi vyake vilivyokuwa njiani kurejea na vile vilivyokuwa ubelgiji kuendelea kubaki.

    Wengi wanachukulia hatua hii kama mwanzo wa majeshi ya muungano kuanza kujizatiti kwani hadi hapo Ujerumani ilikuwa tayari imekamata karibu ulaya nzima na ndio maana Garsia anachukuliwa kama double agent aliyefanya kazi ya kutukuka, lakini pia anatajwa kama double agent aliyetunukiwa tunzo nyingi mno kutoka pande zote yaani Ujerumani na England, baada ya vita Garsia alikwenda zake Amerika kusini ambapo alifungua maktaba na kumalizia maisha yake huko.

    OUR MOTTO
    ========
    KIJANA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USITUMIKE VIBAYA KUICHAFUA NCHI YAKO.
    DOUBLE AGENTS NGULI WANNE KUWAHI KUTOKEA KATIKA ULIMWENGU WA UJASUSI Mustakabali wa taifa lolote lile hutegemea pamoja na mambo mengine mifumo ya ulinzi, kwani hii ndio nguzo mhimu katika kuhakikisha ustawi wa maslahi ya taifa husika Ni kwa msingi huo basi mataifa yote duniani yameunda vyombo tofauti tofauti vya ulinzi mojawapo ikiwemo idara za ujajusi, mifano ipo mingi, CIA, M16, BND, MOSSAD, TISS n.k! Lakini kuwa na taasisi au vyombo hivyo vinahiyaji nguvu kazi, nguvu kazi hii sharti iwe yenye weledi na uzalendo wa kutukuka, kwani kazi wanayoifanya ni kazi nyeti mno na inayozungukwa na mambo mengi sana, hivyo kuteleza kwa namna yoyote ile basi kunaacha madhara makubwa mno! Na kiukweli wapo walioteleza na kuleta madhara yasiyoelezeka, sasa Leo nimeona tuangalie kwa ufupi baadhi ya wanausalama walioteleza na kujikuta walitumia pande mbili au zaidi maarufu kwa jina la *DOUBLE AGENT* *Lakini kwanza kabisa double agent ni nani?* Tunaweza tukasema ni afisa usalama wa tasisis au serikali ambaye amepewa majukumuu ya kuichunguza taasisi au nchi nyingine lakini wakati huo huo anakuwa tena anafanya kazi hiyo hiyo kwa ajiri ya taasisi au nchi anayopaswa kuichunguza dhidi ya taasisi au nchi iliyomtuma! Wengi wanasem double agent anaweza kuwa matokeo ya tamaa ya pesa, kulazimishwa( baada ya kutishiwa kufanyiwa kitu kibaya), mapenzi tu, yaani mtu anapenda tu kuwa double agent, kupandikizwa kwa makusudi( marekani wamefaidika sana na aina hii hasa Mashariki ya kati) au inaweza kuwa ni sababu ya mitazamo… Hawa wafuatao ni baadhi ya double agents nguli kuwahi kutokea na balaa *Human Khalid Al-Balawi* Huyu jamaa alikuwa daktari kitaaluma na alikuwa raia wa Jordan, alikamatwa na mamlaka za Jordan kipindi akiwa mwanafunzi kwenye chuo kikuu cha Isntanbul nchini Uturuki baada ya kuonekana akiwa na muelekeo wa misimamamo mikali, inasemekana baadae CIA waliingilia na kumshawishi awe double agent kwa ahadi ya kusamehewa. Jamaa alikubali na CIA wakamuandaa kikamilifu kwa kazi hiyo ambapo baada ya kuiva wakampeleka Pakistan na Afghanistan na kumpa jukumuu la kufuatilia nyendo na shughuli za alqaida nchini humo. Human aliifanya kazi hiyo kwa uaminifu mkubwa mno na akafanikiwa kuwashawishi CIA ambao walionekana kumwamini 100%. Kumbe hawakujua kuwa aliqaida walikuwa tayari wamembadilisha na alikuwa akifanya nao kazi. Siku moja akawaeleza kuwa alikuwa na taarifa muhimu kuhusu kiongozi wa juu wa alqaida bwana Ayman- Al-Zawahili na akawapa masharti kuwa angependa taarifa hizo azifikishe kwa viongozi wakuu wa CIA katika eneo hilo, kwakuwa walikuwa wanamtafuta sana Zawahili hawakusita kumkubalia na kumuagiza afike kwenye Ofisi za CIA eneo la Khost Afghanistan, Khalid alifika kwa kuchelewa na kutokana na kimuhe muhe cha taarifa waliyokuwa wanakwenda kuipokea basi wakasahau hadi kumkagua, kumbe jamaa alikuwa amevaa mabomu, baada ya kufika ndani kwa wakubwa jamaa alijilipua na kuua maafisa kadhaa wa ngazi za juu wa CIA katika eneo hilo. *Arthur Owens* Arthur alikuwa mwingereza kutoka kisiwa cha Wales na kabla ya vita ya dunia ya pili alikuwa akifanya kazi kama mkandarasi na alikuwa akifanya serikali zote mbili, Ujerumani na England, baada ya vita kuanza aliajiriwa kama mhandisi kwenye meli vita za England akifanya kazi kama fundi betri, baadae Wajerumani walianza kumuomba awape taarifa hasa kuhusu meli vita za England na yeye bila hiana akifanya kazi hiyo, baadae alijiunga nao rasmi na akawa anafanya kazi nao huku pesa na wanawake wazuri yakiwa ndo malipo kwa kazi yake hiyo tukufu. Baadae alirudi England na kujipeleka moja kwa moja kwa M15 na kuwaeleza ukweli wake na wajerumani, M16 walimpokea na kumtumia ambapo aliwasaidia kufichua zaidi maofisa 120 wa kijeruman nchini England na wakamtumia kuwalisha Wajerumani hao habari za uongo na zile zisixokuwa na athari kubwa kwao. Mwaka 1941 Arthur na mwenzake mmoja walikamatwa na wajerumani lakini cha ajabu mwenzake alinyongwa huku yeye akiachwa hali iliyowatia wasiwasi England na alivyorudi walimkamata na kumtia kolokoloni hadi baada ya vita, baadae aliwalazimisha England wamlipe fedha kwa maadai ya kumfunga bila makosa na kama watagoma basi ataweka hadharani kila kitu, England walinywea na hadi anakufa hakuwahi kusema chochote. *Kim Philby* Kim Philby alikuwa ni afisa wa idara ya usalama ya England, yeye na wenzake wanne walitengeza a spy ring iliyopewa jina la the Combridge five, na wakifanya kazi kwa niaba ya KGB, ni kipindi ambacho wote watano walikuwa wakisoma chuoni hapo, wenzake walikuwa ni pamoja na Donald MacLean, Guy borguess na Anthony Brunt ambapo mtu wa tano kwenye kundi hilo hadi Leo hajawahi kujulikana! Kimsingi Borguess ndiye aliyemsajili Kim na wakati huyo tayari yeye alikuwa ni double agent. Kilichomsukuma Kim ilikuwa ni imani yake katika falsafa za kijamaa, pamoja na kuwa double agent lakini Kim anasemwa kama mtu aliyefanya kazi kwa weledi mkubwa sana na alipata kutunukiwa nishani kadhaa kwa utumishi uliotukuka kabla ya kuja kumgundua kuwa alikuwa akifanya kazi na KGB, wakati wenzake wanakamatwa yeye alikuwa ameshaacha kazi na alikuwa Lebanon na hakurudi tena England Bali aliekea Jamhuri ya Usovieti ambako alipewa kazi kwenye idara kadhaa za ulinzi, alifariki mwaka 1988 akiwa huko huko Usovieti, Kim aliandika kitabu alichokipa jina la *My secret war* akieleza namna alivyopambana na ubepari. *Juan Pujol Garsia* Garsia alikuwa mhisipania ambaye maisha yake yalionekana kutokua na muelekeo kwani kwenye umri wa miaka 32 alikuwa ameshindwa karibia kila kitu, shule, biashara na hata familia, vyote alikuwa amejaribu na vikamshinda. Baadae wakati wa vita kuu ya pili ya dunia aliamua kwenda kuomba kazi kwenye idara za usalama za England na Marekani lakini aligonga mwamba kwa madai mtu ambaye hakuwa na uwezo hata wa kufuga kuku angeweje kufanya kazi nyeti kama hii tena katika wakati tete. Baada ya kukataliwa akaona isiwe taabu akaenda zake kwa Wajerumani na kujifanya mmoja wa wanazi kindakindaki wa Hitler, manazi baadae walimuamini na kumpa kazi ambapo walimpangia kwenda England! Alielekea huko akipitia Porto Ureno na alianza kazi kwa kukusanya habari kwenye magazeti na redio, baadae alianza kupiga hatua kwa kusajili watu mhimu kutoka wazara ya habari na mawasiliano pamoja na masekretari kwenye wizara mbalimbali, baadae pia alifanikiwa kuingia hadi jeshini na jusajili watu huko. Garsia alikuja kuumbuliwa na double agent wa kijerumani ambaye aliwatonya England juu ya uwepo wake nchini humo. Baada ya kubumbuluka Garsia akijipeleka mwenyewe kwa M15 ambapo walikubali kuendelea kutumia mara hii wakimtumia kuwalisha habari za uongo. Garsia anakumbukwa sana kutokana na kazi tukufu aliyoifanya wakati majeshi ya muungano wa England, Canada, Marekani na baadhi ya wanajeshi wa Ufaransa yalipoanza oparesheni ya kukomboa maeneo yaliyokuwa yamekamatwa na Ujerumani na hasa katika uvamizi wa eneo la Normandy, baada ya wanajeshi wa muungano kuelekea katika eneo hilo wajerumani walipata intelejensia na wakawa wametuma vikosi kwenda kupambana na majeshi ya muungano huku vikosi vingine vikiwekwa tayari nchini ubelgiji, lakini Garsia kwa ujasiri wa hali ya juu akamtumia telegraphy na kumwambia hakukuwa na mashambulizi yoyote katika eneo hilo na kwamba habari alizokuwa amepewa Hitler ulikuwa ni uongo, kwakuwa Hitler alikuwa anamuamini sana basi akaiamini taarifa hii na akaviamrisha vikosi vyake vilivyokuwa njiani kurejea na vile vilivyokuwa ubelgiji kuendelea kubaki. Wengi wanachukulia hatua hii kama mwanzo wa majeshi ya muungano kuanza kujizatiti kwani hadi hapo Ujerumani ilikuwa tayari imekamata karibu ulaya nzima na ndio maana Garsia anachukuliwa kama double agent aliyefanya kazi ya kutukuka, lakini pia anatajwa kama double agent aliyetunukiwa tunzo nyingi mno kutoka pande zote yaani Ujerumani na England, baada ya vita Garsia alikwenda zake Amerika kusini ambapo alifungua maktaba na kumalizia maisha yake huko. OUR MOTTO ======== KIJANA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USITUMIKE VIBAYA KUICHAFUA NCHI YAKO.
    ·55 Views
  • KHALID AUCHO WABONGO WAMEKUITA DAKTARI!!!

    Aucho amecheza soka katika vilabu mbalimbali, kama vile Halmashauri ya Manispaa ya Jinja F.C. kutoka 2009 hadi 2010, Water F.C kutoka Uganda kutoka 2010 hadi 2012, Simba FC kutoka Uganda, Tusker kutoka Kenya, Gor Mahia kutoka Kenya, na Baroka kutoka Ligi Kuu ya Soka ya Afrika Kusini.

    Kipindi kile anasajiliwa jangwani, mwaka mmoja nyuma alikuwa anawindwa na klabu moja kubwa hapa nchini lakini dili lake halikukaa sawa na panapo muda kuwadia, akatua mizigo yake Jangwani!

    Mpaka hivi sasa ndiye kiungo wa kati wa Kigeni aliyedumu nchini kwa Ubora usiomithilika licha ya sasa kasi yake kuonekana inapungua na hii ni changamoto ya kucheza michezo msimu mzima bila kupata msaidizi halisi!..

    Kabla Hujaniuliza kwanini nimemsifia huyu AUCHO kutoka kwa Wananchi njoo apa uniambie kwani Aucho kijana wa watu Aliwahi kukukosea wapi ili Tujue kabla hatujakutafsiri kama mtu mwenye nongwa binafsi!

    Yess,, Utani upo lakini sio kila wakati!

    Unyamani namuona akija FABRICE NGOMA licha naye bado hajajisimika vizuri kwenye mwendelezo bora wa kila msimu...!!!

    SEMA "WABONGO" KILA MTU KWAO #DAKTARI
    Khalid Aucho8
    #UkweliUnaumaSana🫴
    #neliudcosiah

    KHALID AUCHO WABONGO WAMEKUITA DAKTARI!!! 🤏 Aucho amecheza soka katika vilabu mbalimbali, kama vile Halmashauri ya Manispaa ya Jinja F.C. kutoka 2009 hadi 2010, Water F.C kutoka Uganda kutoka 2010 hadi 2012, Simba FC kutoka Uganda, Tusker kutoka Kenya, Gor Mahia kutoka Kenya, na Baroka kutoka Ligi Kuu ya Soka ya Afrika Kusini. Kipindi kile anasajiliwa jangwani, mwaka mmoja nyuma alikuwa anawindwa na klabu moja kubwa hapa nchini lakini dili lake halikukaa sawa na panapo muda kuwadia, akatua mizigo yake Jangwani! Mpaka hivi sasa ndiye kiungo wa kati wa Kigeni aliyedumu nchini kwa Ubora usiomithilika licha ya sasa kasi yake kuonekana inapungua na hii ni changamoto ya kucheza michezo msimu mzima bila kupata msaidizi halisi!.. Kabla Hujaniuliza kwanini nimemsifia huyu AUCHO kutoka kwa Wananchi njoo apa uniambie kwani Aucho kijana wa watu Aliwahi kukukosea wapi ili Tujue kabla hatujakutafsiri kama mtu mwenye nongwa binafsi! Yess,, Utani upo lakini sio kila wakati! Unyamani namuona akija FABRICE NGOMA licha naye bado hajajisimika vizuri kwenye mwendelezo bora wa kila msimu...!!! SEMA "WABONGO" KILA MTU KWAO #DAKTARI 🤣✍️ Khalid Aucho8🇺🇬 #UkweliUnaumaSana🫴🤔 #neliudcosiah
    Like
    2
    ·184 Views
  • Je ni kweli Nelson Mandela alifia gerezani mwaka 1985?

    🗣Habari zenu wadau, katika pitapita zangu nimekutana na machapisho mengi ya watu wa afrika ya kusini yanayodai kuwa mtu anayefahamika kwa jina la Nelson Mandela, si huyu tuliye mfahamu sisi, Nelson original alifia jela mwaka 1985. Kwa mujibu wa maelezo nikwamba huyu tuliye mzika sisi hivi karibuni ama tuliye mfahamu hakuwa Nelson mwenyewe. Makaburu waliamua kutafuta mtu anayeendana naye kidogo na alilazimishwa kutoa talaka kwa Winnie Mandela maana wangekaa pamoja mwanamama huyu angejua kuwa huyu jamaa hakuwa Mumewe Original.

    Inasemekana mwanamuziki Johnny Clegg alishawahi pia kuimba kitu hiki katika wimbo wake wa "Asimbonanga" yaani hatujamwona yeye. Kwenye wimbo huo kuna maneno Asimbonang' uMandela thina akimaanisha hatujamwona Mandela Laph'ekhona - mahali alipo Laph'ehleli - mahali alipo zikwa. Wimbo huu ulitoka mwaka 1987. Ikumbukwe South Africa ilitoka amri kuwa ni marufuku kukutwa unasikiliza ama una miliki album zenye nyimbo za Jonh Clegg, tangu kipindi cha makaburu mpaka kipindi cha mandera huyu aliyetoka gerezani. Maana ngoma za jamaa huyo zilikuwa zinahamasisha harakati za kupinga ubaguzi.

    Nani aliyetolewa gerezani 1990?

    Inasemekana ni mtu ajulikanaye kwa jina la Gibson Makanda, ambaye alipelekwa katika gereza la Pollsmor mwezi May mwaka 1985. Akiwa huko alifanyiwa plastic surgery iliyofanywa na timu ya madaktari wachache toka London Uingereza. Mara baada ya zoezi hilo kufanikiwa alipatiwa mazoezi ya kuongea na kutembea kama Nelson Mandela mpaka alipo fuzu ndipo mpango wa kumtoa ukatekelezwa. ndomaana hata baada yakutoka alilegeza sana masharti kwa watu weupe. na aliamua kuunda tume ya msamaha. Ambayo iliwapa nafasi makaburu kutubu waliyowafanyia wazulu kwenye hadhara.

    Kwa hivyo kundi hili la watu wanaoamini katika njama hii wanaona uwezekano mkubwa sana kwamba Nelson Mandela lazima aliuawa wakati wa maandamano, na kwamba serikali ya Makaburu Afrika Kusini ilijibu kwa kuwapa mfano ili kuzuia maandamano mengine kwa kuwa walijua aliyekufa alikuwa kiongozi mpendwa na mtu mwenye ushawishi mkubwa.

    Inasemekana jamaa baada ya kumpa taraka mama Mandera alitokea kumpenda mke wa raisi wa msumbiji, Samora Machel. Ndio maana baada ya raisi huyo kufariki mchizi akaamua kumuoa mama Machel. Mama akashika rekodi ya kuwa mke wa raisi katika nchi mbili tofauti. Pia usisahau kuwa msumbiji kwa Samora Machel ndipo kulikuwa na kambi ya kikundi cha wapiganaji wa South Afrika waliokuwa wanapinga serikali ya Makaburu, Maarufu kama Umkhonto we Sizwe(Mkuki wa taifa).

    Nilipitia pia vyanzo mbalimbali mtandaoni nikakutana na zaidi ya waandishi 50 tofauti wakizungumzia juu ya Gibson Makanda kuigiza kama Nelson Mandela. mwaka wa 2018 wakati programu maarufu ya Android inayoitwa Face App ilitolewa. Programu hii inaweza kuonyesha nyuso za watumiaji jinsi watakavyokuwa katika siku za usoni (athari za uzee). Mtumiaji wa Twitter @Jether_Calypso alitumia picha ya ujana inayopatikana ya Nelson Mandela na ​​kuifanyia kazi, akitumia athari ya uzee na matokeo yalionekana kuwa tofauti na sura ya Nelson Mandela katika miaka yake ya hivi majuzi kabla ya kifo.
    #dorka🗣
    Je, nikweli Nelson Mandela alifariki mwaka 1985?
    Je ni kweli Nelson Mandela alifia gerezani mwaka 1985?🤔 🗣Habari zenu wadau, katika pitapita zangu nimekutana na machapisho mengi ya watu wa afrika ya kusini yanayodai kuwa mtu anayefahamika kwa jina la Nelson Mandela, si huyu tuliye mfahamu sisi, Nelson original alifia jela mwaka 1985. Kwa mujibu wa maelezo nikwamba huyu tuliye mzika sisi hivi karibuni ama tuliye mfahamu hakuwa Nelson mwenyewe. Makaburu waliamua kutafuta mtu anayeendana naye kidogo na alilazimishwa kutoa talaka kwa Winnie Mandela maana wangekaa pamoja mwanamama huyu angejua kuwa huyu jamaa hakuwa Mumewe Original. Inasemekana mwanamuziki Johnny Clegg alishawahi pia kuimba kitu hiki katika wimbo wake wa "Asimbonanga" yaani hatujamwona yeye. Kwenye wimbo huo kuna maneno Asimbonang' uMandela thina akimaanisha hatujamwona Mandela Laph'ekhona - mahali alipo Laph'ehleli - mahali alipo zikwa. Wimbo huu ulitoka mwaka 1987. Ikumbukwe South Africa ilitoka amri kuwa ni marufuku kukutwa unasikiliza ama una miliki album zenye nyimbo za Jonh Clegg, tangu kipindi cha makaburu mpaka kipindi cha mandera huyu aliyetoka gerezani. Maana ngoma za jamaa huyo zilikuwa zinahamasisha harakati za kupinga ubaguzi. Nani aliyetolewa gerezani 1990? Inasemekana ni mtu ajulikanaye kwa jina la Gibson Makanda, ambaye alipelekwa katika gereza la Pollsmor mwezi May mwaka 1985. Akiwa huko alifanyiwa plastic surgery iliyofanywa na timu ya madaktari wachache toka London Uingereza. Mara baada ya zoezi hilo kufanikiwa alipatiwa mazoezi ya kuongea na kutembea kama Nelson Mandela mpaka alipo fuzu ndipo mpango wa kumtoa ukatekelezwa. ndomaana hata baada yakutoka alilegeza sana masharti kwa watu weupe. na aliamua kuunda tume ya msamaha. Ambayo iliwapa nafasi makaburu kutubu waliyowafanyia wazulu kwenye hadhara. Kwa hivyo kundi hili la watu wanaoamini katika njama hii wanaona uwezekano mkubwa sana kwamba Nelson Mandela lazima aliuawa wakati wa maandamano, na kwamba serikali ya Makaburu Afrika Kusini ilijibu kwa kuwapa mfano ili kuzuia maandamano mengine kwa kuwa walijua aliyekufa alikuwa kiongozi mpendwa na mtu mwenye ushawishi mkubwa. Inasemekana jamaa baada ya kumpa taraka mama Mandera alitokea kumpenda mke wa raisi wa msumbiji, Samora Machel. Ndio maana baada ya raisi huyo kufariki mchizi akaamua kumuoa mama Machel. Mama akashika rekodi ya kuwa mke wa raisi katika nchi mbili tofauti. Pia usisahau kuwa msumbiji kwa Samora Machel ndipo kulikuwa na kambi ya kikundi cha wapiganaji wa South Afrika waliokuwa wanapinga serikali ya Makaburu, Maarufu kama Umkhonto we Sizwe(Mkuki wa taifa). Nilipitia pia vyanzo mbalimbali mtandaoni nikakutana na zaidi ya waandishi 50 tofauti wakizungumzia juu ya Gibson Makanda kuigiza kama Nelson Mandela. mwaka wa 2018 wakati programu maarufu ya Android inayoitwa Face App ilitolewa. Programu hii inaweza kuonyesha nyuso za watumiaji jinsi watakavyokuwa katika siku za usoni (athari za uzee). Mtumiaji wa Twitter @Jether_Calypso alitumia picha ya ujana inayopatikana ya Nelson Mandela na ​​kuifanyia kazi, akitumia athari ya uzee na matokeo yalionekana kuwa tofauti na sura ya Nelson Mandela katika miaka yake ya hivi majuzi kabla ya kifo. #dorka🗣 Je, nikweli Nelson Mandela alifariki mwaka 1985?🤔
    Like
    1
    ·211 Views
  • NOUMA 50/50 KUWAVAA KAGERA
    “Tunahitaji kufuatilia ripoti ya daktari kujua atakuwa tayari ama laa…! Alipata majeraha kidogo kwenye mchezo uliopita lakini ndiye mchezaji pekee tuliyesafiri naye ambaye naweza kusema hatuna uhakika naye sana kutumika”

    - Fadlu Davids, Kocha wa Simba SC kuelekea mechi ya Kagera Sugar

    #paulswai
    🚨 NOUMA 50/50 KUWAVAA KAGERA “Tunahitaji kufuatilia ripoti ya daktari kujua atakuwa tayari ama laa…! Alipata majeraha kidogo kwenye mchezo uliopita lakini ndiye mchezaji pekee tuliyesafiri naye ambaye naweza kusema hatuna uhakika naye sana kutumika” - Fadlu Davids, Kocha wa Simba SC kuelekea mechi ya Kagera Sugar #paulswai
    Like
    1
    ·175 Views
  • Mama John alienda kumuona daktari ambaye ni ***** yake na mazungumzo yao yalikuwa hivi:-

    Mama John: Best mume wangu haniridhishi kabisa kwenye tendo la ndoa kama una dawa yoyote nipatie kabla uzalendo haujanishinda.

    Daktari: Mh sawa kuna dawa hapa wacha nikupatie ukaijaribu (akafungua droo akatoa kikopo kidogo cha dawa) umuwekee shemeji kidonge kimoja kila siku kwenye kinywaji chochote kabla ya tendo.

    Basi Mama John akaondoka na kile kikopo, kweli mume wake aliporudi aliandaa juis akaweka na kidonge kimoja akampa mumewe akanywa. Siku ile walifanya tendo mpaka roho yake ikasuuzika.

    Siku ya pili akaona amuwekee vidonge viwili aone itakuaje, walifanya tendo mara mbili ya jana. Akazidi kufurahi.

    Siku ya tatu akafikiria hivi akimuwekea vidonge vyote vilivyobaki show yake itakuwaje? Mbona daktari ni ***** yake atampatia vingine hata kwa gharama yoyote atavinunua. Mumewe aliporudi akaandaa juisi kama kawaida akavimimina vyote.

    Siku ya nne yule daktari aliamua kumpigia simu baada ya kuona kimya ili apate mrejesho wa ile dawa

    Cha kustaajabisha simu yake ilipokelewa na mtoto wa kiume huku akitweta, ambaye bila shaka ndiye John. Alipouluzwa mama yake yupo wapi ndio akaanza kufunguka...

    "Mama yupo ICU muhimbili, shangazi naye kalazwa hukohuko, dada wa kazi katoroka, mimi mwenyewe hapa mk *** unaniuma vibaya mpaka damu zinatoka"

    Kengele ya hatari ikagonga kichwani kwa daktari akamuuliza baba je yupo wapi? Akajibu

    "Baba yupo huko nje kachanganyikwa yupo uchi uchi anakimbiza kila anayepita huku anaimba ...nataka k*. nataka... k*. mpaka kuku na mbwa wote wanamkimbia kunusuru maisha yao

    @highlight@highlightaPeter Joram
    Mama John alienda kumuona daktari ambaye ni shoga yake na mazungumzo yao yalikuwa hivi:- Mama John: Best mume wangu haniridhishi kabisa kwenye tendo la ndoa kama una dawa yoyote nipatie kabla uzalendo haujanishinda. Daktari: Mh sawa kuna dawa hapa wacha nikupatie ukaijaribu (akafungua droo akatoa kikopo kidogo cha dawa) umuwekee shemeji kidonge kimoja kila siku kwenye kinywaji chochote kabla ya tendo. Basi Mama John akaondoka na kile kikopo, kweli mume wake aliporudi aliandaa juis akaweka na kidonge kimoja akampa mumewe akanywa. Siku ile walifanya tendo mpaka roho yake ikasuuzika. Siku ya pili akaona amuwekee vidonge viwili aone itakuaje, walifanya tendo mara mbili ya jana. Akazidi kufurahi. Siku ya tatu akafikiria hivi akimuwekea vidonge vyote vilivyobaki show yake itakuwaje? Mbona daktari ni shoga yake atampatia vingine hata kwa gharama yoyote atavinunua. Mumewe aliporudi akaandaa juisi kama kawaida akavimimina vyote. Siku ya nne yule daktari aliamua kumpigia simu baada ya kuona kimya ili apate mrejesho wa ile dawa Cha kustaajabisha simu yake ilipokelewa na mtoto wa kiume huku akitweta, ambaye bila shaka ndiye John. Alipouluzwa mama yake yupo wapi ndio akaanza kufunguka... "Mama yupo ICU muhimbili, shangazi naye kalazwa hukohuko, dada wa kazi katoroka, mimi mwenyewe hapa mk *** unaniuma vibaya mpaka damu zinatoka" Kengele ya hatari ikagonga kichwani kwa daktari akamuuliza baba je yupo wapi? Akajibu "Baba yupo huko nje kachanganyikwa yupo uchi uchi anakimbiza kila anayepita huku anaimba ...nataka k*.😯 nataka... k*.😯 mpaka kuku na mbwa wote wanamkimbia kunusuru maisha yao😂😂😂😂😂😂😂😂 @highlight@highlightaPeter Joram
    Like
    Love
    Haha
    3
    ·332 Views
  • WACJEZAJI 4 HATIHATI KUKOSEKANA LEO
    .
    Daktari wa Yanga, Moses Etutu amethibitisha kuwa Boka, Aucho, Mzize na Aziz Andabwile ni majeruhi. Etutu amesema; “Aucho aliumia akiwa na timu ya taifa na Mzize aliumia Taifa Stars baada ya kurejea kambini tumewafanyia vipimo taarifa ya nini shida zao tutazitoa hivi karibuni.”
    .
    “Kuhusiana na Boka na Andabwile kama taarifa ilivyotolewa awali kuwa wataendelea kuwa nje hadi hapo hali zao zitakapotengamaa.”
    WACJEZAJI 4 HATIHATI KUKOSEKANA LEO . Daktari wa Yanga, Moses Etutu amethibitisha kuwa Boka, Aucho, Mzize na Aziz Andabwile ni majeruhi. Etutu amesema; “Aucho aliumia akiwa na timu ya taifa na Mzize aliumia Taifa Stars baada ya kurejea kambini tumewafanyia vipimo taarifa ya nini shida zao tutazitoa hivi karibuni.” . “Kuhusiana na Boka na Andabwile kama taarifa ilivyotolewa awali kuwa wataendelea kuwa nje hadi hapo hali zao zitakapotengamaa.”
    Like
    Love
    4
    ·253 Views
  • Mama John alienda kumuona daktari ambaye ni ***** yake na mazungumzo yao yalikuwa hivi:-

    Mama John: Best mume wangu haniridhishi kabisa kwenye tendo la ndoa kama una dawa yoyote nipatie kabla uzalendo haujanishinda.

    Daktari: Mh sawa kuna dawa hapa wacha nikupatie ukaijaribu (akafungua droo akatoa kikopo kidogo cha dawa) umuwekee shemeji kidonge kimoja kila siku kwenye kinywaji chochote kabla ya tendo.

    Basi Mama John akaondoka na kile kikopo, kweli mume wake aliporudi aliandaa juis akaweka na kidonge kimoja akampa mumewe akanywa. Siku ile walifanya tendo mpaka roho yake ikasuuzika.

    Siku ya pili akaona amuwekee vidonge viwili aone itakuaje, walifanya tendo mara mbili ya jana. Akazidi kufurahi.

    Siku ya tatu akafikiria hivi akimuwekea vidonge vyote vilivyobaki show yake itakuwaje? Mbona daktari ni ***** yake atampatia vingine hata kwa gharama yoyote atavinunua. Mumewe aliporudi akaandaa juisi kama kawaida akavimimina vyote.

    Siku ya nne yule daktari aliamua kumpigia simu baada ya kuona kimya ili apate mrejesho wa ile dawa

    Cha kustaajabisha simu yake ilipokelewa na mtoto wa kiume huku akitweta, ambaye bila shaka ndiye John. Alipouluzwa mama yake yupo wapi ndio akaanza kufunguka...

    "Mama yupo ICU muhimbili, shangazi naye kalazwa hukohuko, dada wa kazi katoroka, mimi mwenyewe hapa mk*nd* unaniuma vibaya mpaka damu zinatoka"

    Kengele ya hatari ikagonga kichwani kwa daktari akamuuliza baba je yupo wapi? Akajibu

    "Baba yupo huko nje kachanganyikwa yupo uchi uchi anakimbiza kila anayepita huku anaimba ...nataka k*ma... nataka... k*ma... mpaka kuku na mbwa wote wanamkimbia kunusuru maisha yao

    Mama John alienda kumuona daktari ambaye ni shoga yake na mazungumzo yao yalikuwa hivi:- Mama John: Best mume wangu haniridhishi kabisa kwenye tendo la ndoa kama una dawa yoyote nipatie kabla uzalendo haujanishinda. Daktari: Mh sawa kuna dawa hapa wacha nikupatie ukaijaribu (akafungua droo akatoa kikopo kidogo cha dawa) umuwekee shemeji kidonge kimoja kila siku kwenye kinywaji chochote kabla ya tendo. Basi Mama John akaondoka na kile kikopo, kweli mume wake aliporudi aliandaa juis akaweka na kidonge kimoja akampa mumewe akanywa. Siku ile walifanya tendo mpaka roho yake ikasuuzika. Siku ya pili akaona amuwekee vidonge viwili aone itakuaje, walifanya tendo mara mbili ya jana. Akazidi kufurahi. Siku ya tatu akafikiria hivi akimuwekea vidonge vyote vilivyobaki show yake itakuwaje? Mbona daktari ni shoga yake atampatia vingine hata kwa gharama yoyote atavinunua. Mumewe aliporudi akaandaa juisi kama kawaida akavimimina vyote. Siku ya nne yule daktari aliamua kumpigia simu baada ya kuona kimya ili apate mrejesho wa ile dawa Cha kustaajabisha simu yake ilipokelewa na mtoto wa kiume huku akitweta, ambaye bila shaka ndiye John. Alipouluzwa mama yake yupo wapi ndio akaanza kufunguka... "Mama yupo ICU muhimbili, shangazi naye kalazwa hukohuko, dada wa kazi katoroka, mimi mwenyewe hapa mk*nd* unaniuma vibaya mpaka damu zinatoka" Kengele ya hatari ikagonga kichwani kwa daktari akamuuliza baba je yupo wapi? Akajibu "Baba yupo huko nje kachanganyikwa yupo uchi uchi anakimbiza kila anayepita huku anaimba ...nataka k*ma... nataka... k*ma... mpaka kuku na mbwa wote wanamkimbia kunusuru maisha yao😂😂😂😂😂😂😂😂
    Like
    Yay
    2
    1 Σχόλια ·378 Views
  • HALI HALISI YA MAISHA HUKO MTAANI .

    Baada ya kumaliza shule
    Wale wote uliosoma nao wanaenda maeneo mbalimbali duniani.

    Wengine wamemaliza chuo na sasa ni Madaktari, Wahandisi, Waalimu, Wanasheria, Wahasibu nk.

    Wengine wameoa/kuolewa. Wengine wana watoto. Wengine ndo bado wanatafuta ajira. Wengine wamekufa, usisahau hilo pia. Wengine ni wagonjwa vitandani, wengine wameendelea na elimu ya juu zaidi nk. Wengine wanamiliki kampuni, wengine ni mabosi na wanamiliki hisa katika makampuni makubwa duniani.

    Ila vipi wewe UNAJISIKIAJE unapokutana na wale uliosoma nao, ambao inaonekana wamefanikiwa katika NDOTO zao, wakati wewe bado unasuasua hata hujafanya chochote na hata kimshahara ulicho nacho hakikusogezi popote isipokuwa kula na kubadili nguo pamoja na kodi ya nyumba tu?

    Ni mawazo mengi huja akilini, Je huwa unawaonea wivu? Na huo wivu wako ni wa aina gani? Je ni wa kuwachukia au ule wivu wa wewe kupambana ufikie mafanikio kama wao?
    Kwanza watu wa namna hii huwa wanafikiria Mungu hawapendi kabisa.

    Usisahau pia kuna wale waliofariki... Bado unafikiria vilevile na unawaonea wivu?

    MY TAKE

    Usiruhusu nafasi ya KUKATA TAMAA. Sisi ni tofauti na njia zetu za kufanikiwa ni tofauti.

    Wengine wanafanikiwa haraka kabla yako na wengine baada yako na wewe unakuja kufanikiwa baada yao ndivyo ilivyo katika maisha. Ila katika hali yoyote unayojikuta upo sasa, tafadhali endelea kuvunja vizuizi na songa mbele huenda njia uliyo nayo ndiyo itakayo kutoa kamwe usijaribu kuishi maisha wanayoishi wengine kumbuka maisha ni vile unavyoamua kuishi wewe na si mwingine anavoishi.

    Unapoona wengine wanafanikiwa basi jitume na wewe uweze kufanikiwa, kubwa ni kuongeza juhudi katika kazi zako.

    Rafiki yako akinunua gari leo, furahi, kumbuka wakati utakaponunua la kwako litakuwa jipya zaidi kuliko la kwake na utatamba kwa wakati huo kiasi cha wao kukuonea wivu pia.
    Hakuna washindi wa kudumu katika maisha, ila kuna washindi kwa muda.

    Maisha siyo mashindano, usishindane na yoyote, kumbuka, kuwa maisha ni kama kitabu kwamba tunasoma kitabu kimoja lakini kurasa tofauti katika muda tofauti na kila mtu anafanikiwa kwa nafasi na wakati wake, inategemea unaanda mazingira yapi ya kufanikiwa...

    Usiruhusu woga ndani yako kuuwa ndoto ndani yako, baki ukichochea matamanio yako pia jaribu kuthubutu kufanya usiwe mtu wa kuogopa hasara katika jambo la mafanikio kwani bila changamoto huwezi kutoboa.

    Ni nini unatamani Leo...!?
    Andika kwa sababu siku moja dunia itatamani kukusoma, na itakuwa ni sehemu ya historia yako ya mafanikio.

    Hakuna mahali usipoweza kufika isipokuwa juani tu, jiamini, fanyia kazi malengo yako, tambua changamoto na zisikukatize tamaa. Usiumie kwa kuona wenzako wanafanikiwa, kumbuka anga ni pana sana na kila ndege anaweza kupaa bila kumgusa mwenzake.

    Thamini kila jambo dogo ambalo linakujia katika maisha. Chini ya dunia kila kitu kinawezekana ukiamua epuka kupoteza muda mwingi kuumizwa na vitu visivyo na msingi katika maisha yako na pindi litokeapo jambo ambalo unaona litakurudisha nyuma basi weka pembeni jambo hilo kisha elekeza akili katika njia ya kutafuta mafanikio ipo siku utafanikiwa na mambo yote yataenda sawa.

    Nahitimisha kwa kusema "Katika harakati za mafanikio kuna vitu vingi sana ambavyo huwa tunatamani viende kwa pamoja lakini kwa bahati mbaya kuna vingine huangukia njiani hivyo basi vyote ambavyo vinaonekana kukukwamisha fanya kuviweka kando kwa muda kisha chukua hata moja katika vingi hivyo lipeleke hadi mwisho kisha anza kuyarudia haya mengine baada ya mafanikio.
    HALI HALISI YA MAISHA HUKO MTAANI . Baada ya kumaliza shule Wale wote uliosoma nao wanaenda maeneo mbalimbali duniani. Wengine wamemaliza chuo na sasa ni Madaktari, Wahandisi, Waalimu, Wanasheria, Wahasibu nk. Wengine wameoa/kuolewa. Wengine wana watoto. Wengine ndo bado wanatafuta ajira. Wengine wamekufa, usisahau hilo pia. Wengine ni wagonjwa vitandani, wengine wameendelea na elimu ya juu zaidi nk. Wengine wanamiliki kampuni, wengine ni mabosi na wanamiliki hisa katika makampuni makubwa duniani. Ila vipi wewe UNAJISIKIAJE unapokutana na wale uliosoma nao, ambao inaonekana wamefanikiwa katika NDOTO zao, wakati wewe bado unasuasua hata hujafanya chochote na hata kimshahara ulicho nacho hakikusogezi popote isipokuwa kula na kubadili nguo pamoja na kodi ya nyumba tu? Ni mawazo mengi huja akilini, Je huwa unawaonea wivu? Na huo wivu wako ni wa aina gani? Je ni wa kuwachukia au ule wivu wa wewe kupambana ufikie mafanikio kama wao? Kwanza watu wa namna hii huwa wanafikiria Mungu hawapendi kabisa. Usisahau pia kuna wale waliofariki... Bado unafikiria vilevile na unawaonea wivu? MY TAKE Usiruhusu nafasi ya KUKATA TAMAA. Sisi ni tofauti na njia zetu za kufanikiwa ni tofauti. Wengine wanafanikiwa haraka kabla yako na wengine baada yako na wewe unakuja kufanikiwa baada yao ndivyo ilivyo katika maisha. Ila katika hali yoyote unayojikuta upo sasa, tafadhali endelea kuvunja vizuizi na songa mbele huenda njia uliyo nayo ndiyo itakayo kutoa kamwe usijaribu kuishi maisha wanayoishi wengine kumbuka maisha ni vile unavyoamua kuishi wewe na si mwingine anavoishi. Unapoona wengine wanafanikiwa basi jitume na wewe uweze kufanikiwa, kubwa ni kuongeza juhudi katika kazi zako. Rafiki yako akinunua gari leo, furahi, kumbuka wakati utakaponunua la kwako litakuwa jipya zaidi kuliko la kwake na utatamba kwa wakati huo kiasi cha wao kukuonea wivu pia. Hakuna washindi wa kudumu katika maisha, ila kuna washindi kwa muda. Maisha siyo mashindano, usishindane na yoyote, kumbuka, kuwa maisha ni kama kitabu kwamba tunasoma kitabu kimoja lakini kurasa tofauti katika muda tofauti na kila mtu anafanikiwa kwa nafasi na wakati wake, inategemea unaanda mazingira yapi ya kufanikiwa... Usiruhusu woga ndani yako kuuwa ndoto ndani yako, baki ukichochea matamanio yako pia jaribu kuthubutu kufanya usiwe mtu wa kuogopa hasara katika jambo la mafanikio kwani bila changamoto huwezi kutoboa. Ni nini unatamani Leo...!? Andika kwa sababu siku moja dunia itatamani kukusoma, na itakuwa ni sehemu ya historia yako ya mafanikio. Hakuna mahali usipoweza kufika isipokuwa juani tu, jiamini, fanyia kazi malengo yako, tambua changamoto na zisikukatize tamaa. Usiumie kwa kuona wenzako wanafanikiwa, kumbuka anga ni pana sana na kila ndege anaweza kupaa bila kumgusa mwenzake. Thamini kila jambo dogo ambalo linakujia katika maisha. Chini ya dunia kila kitu kinawezekana ukiamua epuka kupoteza muda mwingi kuumizwa na vitu visivyo na msingi katika maisha yako na pindi litokeapo jambo ambalo unaona litakurudisha nyuma basi weka pembeni jambo hilo kisha elekeza akili katika njia ya kutafuta mafanikio ipo siku utafanikiwa na mambo yote yataenda sawa. Nahitimisha kwa kusema "Katika harakati za mafanikio kuna vitu vingi sana ambavyo huwa tunatamani viende kwa pamoja lakini kwa bahati mbaya kuna vingine huangukia njiani hivyo basi vyote ambavyo vinaonekana kukukwamisha fanya kuviweka kando kwa muda kisha chukua hata moja katika vingi hivyo lipeleke hadi mwisho kisha anza kuyarudia haya mengine baada ya mafanikio.
    ·584 Views
  • Tom Cruz

    "𝗔𝗭𝗔𝗠 𝗛𝗜𝗜 𝗡𝗜 𝗣𝗥𝗢𝗣𝗔𝗚𝗔𝗡𝗗𝗔 𝗠𝗡𝗔𝗧𝗔𝗞𝗔 𝗞𝗨𝗜𝗡𝗭𝗜𝗦𝗛𝗔

    Nimevumilia Nimeshindwa Kwakweli😮‍💨Ila Azam Kwan Mna Nia Gan Na yangaIko wap Siri kati yenu Na Wateja Wenu

    Inachekesha sana huu Mjadala wa sindano.

    Na ukitaka kujua hii ni Ajenda Maalum ya ‘Azam FC’ kutaka kuichafua BRAND ya YANGA kwa kutengeneza Propaganda za Kipuuzi, Fatilia hizi hoja hapa chini

    1: Ile Video imetolewa na inaonekana ni baada ya mechi, Yani mtendaji wa Azam akifanya usafi kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.

    2:Ni video ya Lini? Mechi gani? Hakuna Taarifa hii, Hata mpuuzi mmoja aliyesambaza hakuweka huu ujinga hakutoa hizi Taarifa Kinachoonekana pale na kufanya wapuuzi wengi kuihusisha yanga ni chupa za maji za GSM, Tujiulize hapa

    3:Ni Timu ngapi za Ligi Kuu zinatumia Maji ya GSM? Ni Yanga pekee wanaodhaminiwa na GSM ndio wamecheza pale, kwanini Yanga?

    4:Mtu akiwaza kwamba hapa pia kuna Vita ya Kibiashara kati ya GSM WATER NA MAJI YA UHAI? kutakuwa na Tatizo? Huyu mfanya usafi wa Azam anaweza kuwa amechukua chupa za maji ya GSM kwa ajili ya kuichafua Brand ya GSM na Yanga kwa ujumla?

    5:Sio kwamba Azam wanatengeneza hii michezo ya kitoto na kurekodi video kisha kuzisambaza?

    Ishu nyingine ni zile sindano.

    Kuna haja gani ya Timu kuwa na madaktari kama sindano zinaonekana tatizo?

    Wachezaji wakiumia hawatibiwi? Zile Ambulance ni za nini pia kama huduma ya afya ya wachezaji ni tatizo. Huu ni Upuuzi sana.

    Zile sindano pale kwenye video zimeonekana ni mbili, kama ni ajenda ya kuongeza nguvu, ndio Yanga wawaongeze nguvu wachezaji wawili tu? Au Sindano wameshare??

    Tuacheni Propaganda za Kipuuzi, Tuchezeni mpira.

    Mwisho, Yanga wawe macho sana na Azam .. Wanaweza kuonekana ni watu wema kwa kanzu wanazovaa, kumbe moyoni ni Mashetani wenye malengo ya kuidhoofisha Yanga"
    Tom Cruz ✍️ "𝗔𝗭𝗔𝗠 𝗛𝗜𝗜 𝗡𝗜 𝗣𝗥𝗢𝗣𝗔𝗚𝗔𝗡𝗗𝗔 𝗠𝗡𝗔𝗧𝗔𝗞𝗔 𝗞𝗨𝗜𝗡𝗭𝗜𝗦𝗛𝗔 Nimevumilia Nimeshindwa Kwakweli😮‍💨Ila Azam Kwan Mna Nia Gan Na yanga😭Iko wap Siri kati yenu Na Wateja Wenu🥵 Inachekesha sana huu Mjadala wa sindano. Na ukitaka kujua hii ni Ajenda Maalum ya ‘Azam FC’ kutaka kuichafua BRAND ya YANGA kwa kutengeneza Propaganda za Kipuuzi, Fatilia hizi hoja hapa chini 1: Ile Video imetolewa na inaonekana ni baada ya mechi, Yani mtendaji wa Azam akifanya usafi kwenye vyumba vya kubadilishia nguo. 2:Ni video ya Lini? Mechi gani? Hakuna Taarifa hii, Hata mpuuzi mmoja aliyesambaza hakuweka huu ujinga hakutoa hizi Taarifa Kinachoonekana pale na kufanya wapuuzi wengi kuihusisha yanga ni chupa za maji za GSM, Tujiulize hapa 3:Ni Timu ngapi za Ligi Kuu zinatumia Maji ya GSM? Ni Yanga pekee wanaodhaminiwa na GSM ndio wamecheza pale, kwanini Yanga? 4:Mtu akiwaza kwamba hapa pia kuna Vita ya Kibiashara kati ya GSM WATER NA MAJI YA UHAI? kutakuwa na Tatizo? Huyu mfanya usafi wa Azam anaweza kuwa amechukua chupa za maji ya GSM kwa ajili ya kuichafua Brand ya GSM na Yanga kwa ujumla? 5:Sio kwamba Azam wanatengeneza hii michezo ya kitoto na kurekodi video kisha kuzisambaza? Ishu nyingine ni zile sindano. Kuna haja gani ya Timu kuwa na madaktari kama sindano zinaonekana tatizo? Wachezaji wakiumia hawatibiwi? Zile Ambulance ni za nini pia kama huduma ya afya ya wachezaji ni tatizo. Huu ni Upuuzi sana. Zile sindano pale kwenye video zimeonekana ni mbili, kama ni ajenda ya kuongeza nguvu, ndio Yanga wawaongeze nguvu wachezaji wawili tu? Au Sindano wameshare?? Tuacheni Propaganda za Kipuuzi, Tuchezeni mpira. Mwisho, Yanga wawe macho sana na Azam .. Wanaweza kuonekana ni watu wema kwa kanzu wanazovaa, kumbe moyoni ni Mashetani wenye malengo ya kuidhoofisha Yanga"
    Love
    1
    1 Σχόλια ·467 Views
  • Simba ina habari njema juu ya beki wake wa kati, Abdulrazack Hamza ambaye alipata majeraha muda mfupi baada ya kujiunga na kambi ya timu ya Taifa Stars’ hivi karibuni kwa ajili ya maandalizi ya mechi 2 dhidi ya DR Congo za kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika (Afcon) 2025.

    Baada ya matibabu ambayo ameyapata chini ya uangalizi wa jopo la madaktari wa Simba, beki huyo yupo katika maendeleo mazuri kiafya na leo Jumatatu ataungana na wenzake kikosini kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya Yanga.
    #paulswai
    Simba ina habari njema juu ya beki wake wa kati, Abdulrazack Hamza ambaye alipata majeraha muda mfupi baada ya kujiunga na kambi ya timu ya Taifa Stars’ hivi karibuni kwa ajili ya maandalizi ya mechi 2 dhidi ya DR Congo za kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika (Afcon) 2025. Baada ya matibabu ambayo ameyapata chini ya uangalizi wa jopo la madaktari wa Simba, beki huyo yupo katika maendeleo mazuri kiafya na leo Jumatatu ataungana na wenzake kikosini kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya Yanga. #paulswai
    Like
    1
    ·492 Views
  • SIMBASC YAPATA PIGO JISHUA MUTALE NJE WIKI MBILI

    Daktari wa Simba, Edwin Kagabo amethibitisha kuwa kiungo mshambuliaji Joshua Mutale atakuwa nje ya uwanja kwa wiki mbili kuuguza majeraha.
    .
    Mutale alipata maumivu ya nyama za paja katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Tabora United uliopigwa katika Uwanja wa KMC Agosti 18.
    .
    Dkt. Kagabo amesema Mutale hajapata majeraha makubwa lakini ili kumlinda asiumie zaidi atakuwa nje ya uwanja kwa muda huo.
    SIMBASC YAPATA PIGO JISHUA MUTALE NJE WIKI MBILI Daktari wa Simba, Edwin Kagabo amethibitisha kuwa kiungo mshambuliaji Joshua Mutale 🇿🇲 atakuwa nje ya uwanja kwa wiki mbili kuuguza majeraha. . Mutale alipata maumivu ya nyama za paja katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Tabora United uliopigwa katika Uwanja wa KMC Agosti 18. . Dkt. Kagabo amesema Mutale hajapata majeraha makubwa lakini ili kumlinda asiumie zaidi atakuwa nje ya uwanja kwa muda huo.
    Love
    Like
    4
    1 Σχόλια ·378 Views

  • Dkt. Kagabo azungumzia Hali ya Mutale

    Daktari wa timu, Edwin Kagabo amesema jeraha alilopata kiungo mshambuliaji Joshua Mutale sio kubwa na tayari ameanza matibabu.

    Mon, Aug 19

    Mutale alipata maumivu ya nyama za paja katika mchezo wa jana wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Tabora United na kutolewa dakika ya 31.

    Dkt. Kagabo amesema Mutale amepata changamoto ya nyama za paja (hamstring muscles) lakini hali yake sio mbaya sana.

    "Mutale alipata maumivu ya nyama za paja na tayari ameanza matibabu ya awali na uchanguzi kuhusu ukubwa wa tatizo utakamilika baada ya saa 48 ingawa inaonekana sio kubwa," amesema Dk. Kagabo. #paulswai
    Dkt. Kagabo azungumzia Hali ya Mutale Daktari wa timu, Edwin Kagabo amesema jeraha alilopata kiungo mshambuliaji Joshua Mutale sio kubwa na tayari ameanza matibabu. Mon, Aug 19 Mutale alipata maumivu ya nyama za paja katika mchezo wa jana wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Tabora United na kutolewa dakika ya 31. Dkt. Kagabo amesema Mutale amepata changamoto ya nyama za paja (hamstring muscles) lakini hali yake sio mbaya sana. "Mutale alipata maumivu ya nyama za paja na tayari ameanza matibabu ya awali na uchanguzi kuhusu ukubwa wa tatizo utakamilika baada ya saa 48 ingawa inaonekana sio kubwa," amesema Dk. Kagabo. #paulswai
    Like
    Love
    5
    2 Σχόλια ·341 Views
  • MEDICAL ASSISTANT

    Tsh5000

     άλλο
    Dar es Salaam· Νέο · Σε απόθεμα

    KARIBUNI KWA DAKTARI BINGWA UWEZE KUPATA HUDUMA BOZA NA ZENYE UNAFUU ZAIDI. AHSANTE.
    KARIBUNI KWA DAKTARI BINGWA UWEZE KUPATA HUDUMA BOZA NA ZENYE UNAFUU ZAIDI. AHSANTE.
    Like
    Love
    2
    ·759 Views
  • Mi mtoto wa maskini, mkulima uko kijijini handeni...//

    kutokana na kukosa ada, nilifukuzwa shuleni....//

    sababu ya umasikini, ndoto yangu ya kua rubani ilipotea...//

    mwana nilikaa chini..nikawaza, vipi nitajikomboa....//

    nilikaa nikafikiria sana, mpaka kichwa kiliniuma...//

    jibu pekee lilokuja, ni kwenda kutafuta dar es salama...//

    Bila kuaga wazazi, niliiba pesa za marejesho ya bi mkubwa...//

    Sikujali yangu mavazi, nikalivamia gari sai baba....//

    nikafika dar..tatizo likawa sina pa kula wala pa kulala....//

    safari yangu nilifika salama, nikiwa stendi ubungo, likatokea tukio sikia....//

    ishu ilikua sista kaibiwa na wajuba, mwana nikapambania kurudisha mali zake...//

    kwa bahati nzuri nikazipata, kwa furaha yule sista alinishukuru na kunipeleka nyumbani kwake....//

    alikua anaishi alone, jumba kubwa la kifahari.....//

    alikua msomi, alifanya kazi muhimbili kama daktari....//

    mungu akikupa...akuandikii barua, nimeamini maneno ya enzi...//

    yaani kama masihara, yule dada akanitaka kimapenzi....//

    mwana sikufikiria, haraka nikakubali ombi lake....//

    ikapangwa siku ya harusi, ili niwe mume wake.....//

    nikawapa tarifa wazazi, kua nimepata mwali na soon nitaoa....//

    nafurahi walifurahi, walinambia kila hatua waliniombea....//

    nilipata baraka za wazazi, mpambanaki nikaoa...//

    ndoa yetu ilikua ya kawaida, ila nashukuru ilifanikiwa....//

    kama utani aiseee, saivi ni namiliki maduka kariakooo....//

    ukiniona ni pedesheee, usikate tamaa wanangu tupambane mpaka mwisho..//
    Mi mtoto wa maskini, mkulima uko kijijini handeni...// kutokana na kukosa ada, nilifukuzwa shuleni....// sababu ya umasikini, ndoto yangu ya kua rubani ilipotea...// mwana nilikaa chini..nikawaza, vipi nitajikomboa....// nilikaa nikafikiria sana, mpaka kichwa kiliniuma...// jibu pekee lilokuja, ni kwenda kutafuta dar es salama...// Bila kuaga wazazi, niliiba pesa za marejesho ya bi mkubwa...// Sikujali yangu mavazi, nikalivamia gari sai baba....// nikafika dar..tatizo likawa sina pa kula wala pa kulala....// safari yangu nilifika salama, nikiwa stendi ubungo, likatokea tukio sikia....// ishu ilikua sista kaibiwa na wajuba, mwana nikapambania kurudisha mali zake...// kwa bahati nzuri nikazipata, kwa furaha yule sista alinishukuru na kunipeleka nyumbani kwake....// alikua anaishi alone, jumba kubwa la kifahari.....// alikua msomi, alifanya kazi muhimbili kama daktari....// mungu akikupa...akuandikii barua, nimeamini maneno ya enzi...// yaani kama masihara, yule dada akanitaka kimapenzi....// mwana sikufikiria, haraka nikakubali ombi lake....// ikapangwa siku ya harusi, ili niwe mume wake.....// nikawapa tarifa wazazi, kua nimepata mwali na soon nitaoa....// nafurahi walifurahi, walinambia kila hatua waliniombea....// nilipata baraka za wazazi, mpambanaki nikaoa...// ndoa yetu ilikua ya kawaida, ila nashukuru ilifanikiwa....// kama utani aiseee, saivi ni namiliki maduka kariakooo....// ukiniona ni pedesheee, usikate tamaa wanangu tupambane mpaka mwisho..//
    ·219 Views
  • Support haraKATI temana na KATI panaUA
    Ukimwi haTARI hakuponyi dakTARI tambUA
    Kupendwa bahatI kuolewa zalI acha kuzingUA
    Nimekuweka ndanI waheshimu wazazI wamenilea nikakUA
    Ukitii masharTI nitakupenda kwa dhaTI kicheche sita mjUA
    Support haraKATI temana na KATI panaUA Ukimwi haTARI hakuponyi dakTARI tambUA Kupendwa bahatI kuolewa zalI acha kuzingUA Nimekuweka ndanI waheshimu wazazI wamenilea nikakUA Ukitii masharTI nitakupenda kwa dhaTI kicheche sita mjUA
    ·445 Views
  • Its so cuty like malaiKA,,nimwonapo naburudiKA..

    Tabasamu flani huwezi eleZEA,,akitembea mwendo,pozi ongeZEA..

    Jina falzana mzuri kila idara,,daktari bila zana white colour..

    Kiuno cha swala thamani ya dola,,nyuma kombola nyumbani angolla..

    Wapi nianzie ili nimfate,,kipi nimpatie il nimpate..
    Its so cuty like malaiKA,,nimwonapo naburudiKA.. Tabasamu flani huwezi eleZEA,,akitembea mwendo,pozi ongeZEA.. Jina falzana mzuri kila idara,,daktari bila zana white colour.. Kiuno cha swala thamani ya dola,,nyuma kombola nyumbani angolla.. Wapi nianzie ili nimfate,,kipi nimpatie il nimpate..
    Like
    2
    ·127 Views
  • Branding !

    Mganga - Daktari
    Mmbea - Mtangazaji
    Muongo - Mwanasiasa
    Muuza madawa - Pharmacist
    Majambazi - Watoza ushuru
    Branding ! Mganga - Daktari Mmbea - Mtangazaji Muongo - Mwanasiasa Muuza madawa - Pharmacist Majambazi - Watoza ushuru
    Like
    Love
    Yay
    6
    1 Σχόλια ·166 Views
  • Je wajua?
    MUHAMMED IQBAL DAR ndiye aliyebuni jina la nchi ya TANZANIA?
    Muhammed Iqbal Dar ni mtanzania mwenye asili ya India mzaliwa wa mkoani Tanga mwaka 1944, dini yake ni Muislamu dhehebu la Ahmadiya, baba yake aitwaye Dokta Tufail Ahmad Dar alikuwa ni daktari wa binadamu aliyehamia Tanzania kutoka India mwaka 1930 na walikuwa wakiishi mkoani Morogoro.
    Mwandishi wa kituo cha Redio Safari ya mkoani Mtwara aitwae Alphonce Tonny Kapelah aliwahi kumhoji Muhammed ana kwa ana na ndipo Muhammed alianza kuhadithia jinsi alivyoweza kubuni jina TANZANIA kama ifuatavyo;
    Mnamo mwaka 1964 Tanganyika na Zanzibar zilipoungana serikali waliita muungano huo jina la "Republic of Tanganyika & Zanzibar" jina ambalo lilikuwa refu sana hivyo serikali ikatoa tangazo kwa raia kutoa mapendekezo ya majina ili kupata jina moja zuri litakalobeba maana ya Tanganyika na Zanzibar kwa pamoja na atakaeshinda atapewa zawadi ya Tsh 200, Mohammed anasema siku moja alikuwa maktaba akisoma gazeti la Tanganyika Standard ambalo kwa sasa linaitwa Daily News akaona tangazo hilo ndipo akaamua ashiriki shindano hilo, akachukua karatasi kisha akaandika maneno BISMILLAH RAHMAN RAHIM kisha akaandika TANGANYIKA kisha akaandika ZANZIBAR alafu akaandika jina lake IQBAL kisha akaandika dhehebu la dini yake AHMADIYA kisha akaomba Mungu amjaalie apate jina zuri litakalofaa, baada ya hapo akaandika herufi tatu za mwanzo kwenye neno TANGANYIKA akaunganisha na herufi tatu nyingine za mwanzo kutoka kwenye neno ZANZIBAR (TAN+ZAN) akapata neno TANZAN lakini akaona hili neno bado halijakamilika kuitwa muungano huo, akaweka herufi moja ya mwanzo kutoka kwenye jina lake IQBAL (TAN+ZAN+I) kisha akaongeza na herufi moja ya mwanzo ya neno AHMADIYA (TAN+ZAN+I+A) akapata neno TANZANIA kisha akahisi huenda hili likawa jina sahihi akaamua kufanya utafiti akagundua nchi nyingi za Afrika majina yake yanaishia na herufi IA nchi kama ETHIOPIA, ZAMBIA, NIGERIA, TUNISIA, SOMALIA, GAMBIA, NAMIBIA, LIBERIA, MAURITANIA ndipo akaona hili ndio jina sahihi.
    Baada ya hapo akatuma jina hilo kwa kamati ya kuratibu shindano hilo kisha alikaa miezi kadhaa baadae akapokea barua iliyoeleza kuwa ameshinda shindano hilo na aende ili apewe zawadi yake kisha akapewa pongezi, Muhammed alienda lakini kuna mtu mwingne aitwae Yusufal Pir Mohammed na yeye pia alienda akidai yeye ndie aliyeshinda lakini alipoambiwa aonyeshe barua ya uthibitisho na pongezi kama ya Muhammed hakuwa nayo hivyo Muhammed alipewa cheki yake ya Tsh 200 na zawadi ya ngao, Muhammed pia alisema kwamba washiriki walioshiriki shindano hilo walikuwa 16 lakini alishinda yeye.
    Kwa wakati huo ambao Muhammed alikuwa anahojiwa na Alphonce Muhammed alikuwa anaishi nchini Uingereza mjini Birmingham.
    Ahsante
    Je wajua? MUHAMMED IQBAL DAR ndiye aliyebuni jina la nchi ya TANZANIA? Muhammed Iqbal Dar ni mtanzania mwenye asili ya India mzaliwa wa mkoani Tanga mwaka 1944, dini yake ni Muislamu dhehebu la Ahmadiya, baba yake aitwaye Dokta Tufail Ahmad Dar alikuwa ni daktari wa binadamu aliyehamia Tanzania kutoka India mwaka 1930 na walikuwa wakiishi mkoani Morogoro. Mwandishi wa kituo cha Redio Safari ya mkoani Mtwara aitwae Alphonce Tonny Kapelah aliwahi kumhoji Muhammed ana kwa ana na ndipo Muhammed alianza kuhadithia jinsi alivyoweza kubuni jina TANZANIA kama ifuatavyo; Mnamo mwaka 1964 Tanganyika na Zanzibar zilipoungana serikali waliita muungano huo jina la "Republic of Tanganyika & Zanzibar" jina ambalo lilikuwa refu sana hivyo serikali ikatoa tangazo kwa raia kutoa mapendekezo ya majina ili kupata jina moja zuri litakalobeba maana ya Tanganyika na Zanzibar kwa pamoja na atakaeshinda atapewa zawadi ya Tsh 200, Mohammed anasema siku moja alikuwa maktaba akisoma gazeti la Tanganyika Standard ambalo kwa sasa linaitwa Daily News akaona tangazo hilo ndipo akaamua ashiriki shindano hilo, akachukua karatasi kisha akaandika maneno BISMILLAH RAHMAN RAHIM kisha akaandika TANGANYIKA kisha akaandika ZANZIBAR alafu akaandika jina lake IQBAL kisha akaandika dhehebu la dini yake AHMADIYA kisha akaomba Mungu amjaalie apate jina zuri litakalofaa, baada ya hapo akaandika herufi tatu za mwanzo kwenye neno TANGANYIKA akaunganisha na herufi tatu nyingine za mwanzo kutoka kwenye neno ZANZIBAR (TAN+ZAN) akapata neno TANZAN lakini akaona hili neno bado halijakamilika kuitwa muungano huo, akaweka herufi moja ya mwanzo kutoka kwenye jina lake IQBAL (TAN+ZAN+I) kisha akaongeza na herufi moja ya mwanzo ya neno AHMADIYA (TAN+ZAN+I+A) akapata neno TANZANIA kisha akahisi huenda hili likawa jina sahihi akaamua kufanya utafiti akagundua nchi nyingi za Afrika majina yake yanaishia na herufi IA nchi kama ETHIOPIA, ZAMBIA, NIGERIA, TUNISIA, SOMALIA, GAMBIA, NAMIBIA, LIBERIA, MAURITANIA ndipo akaona hili ndio jina sahihi. Baada ya hapo akatuma jina hilo kwa kamati ya kuratibu shindano hilo kisha alikaa miezi kadhaa baadae akapokea barua iliyoeleza kuwa ameshinda shindano hilo na aende ili apewe zawadi yake kisha akapewa pongezi, Muhammed alienda lakini kuna mtu mwingne aitwae Yusufal Pir Mohammed na yeye pia alienda akidai yeye ndie aliyeshinda lakini alipoambiwa aonyeshe barua ya uthibitisho na pongezi kama ya Muhammed hakuwa nayo hivyo Muhammed alipewa cheki yake ya Tsh 200 na zawadi ya ngao, Muhammed pia alisema kwamba washiriki walioshiriki shindano hilo walikuwa 16 lakini alishinda yeye. Kwa wakati huo ambao Muhammed alikuwa anahojiwa na Alphonce Muhammed alikuwa anaishi nchini Uingereza mjini Birmingham. Ahsante
    Like
    Love
    Yay
    4
    ·499 Views
  • *AFYA YA MACHO.*

    *Daniel S.W.*

    Macho ni kiungo Muhimu sana kwa kuona. Asilimia kubwa ya taarifa kwa sisi wanadamu tunazipata kwa kupitia macho.

    Lakini wengi hazituzingatii Afya ya macho yapokuwa tunayatumia mpaka pale ambapo tatizo linakuwa kubwa na ndio tunakumbuka kwenda kwa Madaktari.

    WHO inasema kuna takbrani watu billioni 2.2 wenye matatizo ya macho au Upofu. Na kati ya Hao watu Billioni 1 wana matatizo ya Macho ambayo yangeweza yatibu mapema *¹*

    Matatizo ya macho ni matatizo ambayo yanawaathiri watu wengi. Na hata kama hauna tatizo unajukumu la kuhakikisha usalama wa macho yako upo katika viwango vizuri.

    Kwanza kabisa tambua kuwa Jicho linahitaji mambo yafuatayo.

    *Vitamin A*. Vitamin Hii inahitajika sana kwaajili ya kuzalisha rhodopsin ambazo ni seli Muhimu sana ndani ya jicho zinazosaidia kuona. Na pia Vitamin A inasaidia sana kufanya jicho liwe na hali ya unyevu wakati wote.

    *Carotenoids*. Hizi ni vichembechembe vinavyofanya matunda yawe na rangi. Hivi husaidia katika kuondoa sumusumu kwenye jicho.

    *Vitamin C na E.* Hizi pia zinasaidi katika kulinda jicho dhidi ya sumusumu. Hizi vitamin zinapatikana sana kwenye matunda, nafaka, na Mboga mboga.

    Tuendelee kujifunza ili tuweze zingatia macho yetu.
    *AFYA YA MACHO.* *Daniel S.W.* Macho ni kiungo Muhimu sana kwa kuona. Asilimia kubwa ya taarifa kwa sisi wanadamu tunazipata kwa kupitia macho. Lakini wengi hazituzingatii Afya ya macho yapokuwa tunayatumia mpaka pale ambapo tatizo linakuwa kubwa na ndio tunakumbuka kwenda kwa Madaktari. WHO inasema kuna takbrani watu billioni 2.2 wenye matatizo ya macho au Upofu. Na kati ya Hao watu Billioni 1 wana matatizo ya Macho ambayo yangeweza yatibu mapema *¹* Matatizo ya macho ni matatizo ambayo yanawaathiri watu wengi. Na hata kama hauna tatizo unajukumu la kuhakikisha usalama wa macho yako upo katika viwango vizuri. Kwanza kabisa tambua kuwa Jicho linahitaji mambo yafuatayo. *Vitamin A*. Vitamin Hii inahitajika sana kwaajili ya kuzalisha rhodopsin ambazo ni seli Muhimu sana ndani ya jicho zinazosaidia kuona. Na pia Vitamin A inasaidia sana kufanya jicho liwe na hali ya unyevu wakati wote. *Carotenoids*. Hizi ni vichembechembe vinavyofanya matunda yawe na rangi. Hivi husaidia katika kuondoa sumusumu kwenye jicho. *Vitamin C na E.* Hizi pia zinasaidi katika kulinda jicho dhidi ya sumusumu. Hizi vitamin zinapatikana sana kwenye matunda, nafaka, na Mboga mboga. Tuendelee kujifunza ili tuweze zingatia macho yetu.
    Love
    Like
    8
    6 Σχόλια ·429 Views
  • SIRI IMEFICHUKA
    UJUE UGONJWA WA (PID)
    (Pelvic Inflammatory Disease)
    Kwa manufaa zaidi usisite kusoma hadi mwisho....

    Ugonjwa Wa Pid Ni Nini?

    Ugonjwa wa pid ni maambukizi katika viungo vya uzazi vya mwanamke.
    Maambukizi haya kutokea ikiwa bakteria wanaoambukiza kwa njia ya kujamiiana watasambaa kutoka kwenye uke kwenda kwenye mji wa mimba (Uterus), mirija ya uzazi (Fallopian tubes) na kwenye ovari (ambapo mayai ya mwanamke hupatikana).

    SABABU YA UGONJWA WA PID NI NINI?

    Ugonjwa wa pid husababishwa na magonjwa ya zinaa kama vile kisonono (gonorrhea) na pangusa (chlamydia).
    Mwili wa mwanamke unapokuwa na afya njema, mlango wa kizazi huwa na uwezo mkubwa wa kuzuia bakteria wasiweze kuingia katika viungo vya ndani vya uzazi kutoka ukeni.
    Hata hivyo wakati mlango wa kizazi unapokuwa wazi na kuruhusu magonjwa ya zinaa kuingia hasa kisonono (gonorrhea) na pangusa (chlamydia), mlango wa kizazi hupata maambukizi na kisha hupoteza uwezo wake na hivyo kuruhusu maambukizi na bakteria kuingia na kufika juu kwenye viungo vya uzazi.

    JINSI MWANAMKE ANAVYO AMBUKIZWA PID

    Kuna njia kadhaa ambazo mwanamke anaweza kuambukizwa ugonjwa wa pid. Njia hizo ni pamoja na:
    A) Kama  Una Ugonjwa Wa Zinaa Na Hujatibiwa.
    B) Kufanya Ngono Zembe Isiyosalama (Yaani Kulala Na Wanaume Tofauti Tofauti).
    C) Kuwa Na Mpenzi Ambaye Ana Wanawake Wengi Nje. 
    D) Kama Umeshawai Kuwa Na Historia Ya Kuugua Pid Kabla. 
    E) Maambukizi Ya Nje Ya Uzazi Mara Baada Ya Kutoa Mimba Kwa Njia Zisizo Salama (Post Abortion) Au Mara Baada Ya Mimba Kutoka (Miscarriage).
    F) Maambukizi Ya Nje Ya Uzazi Hasa Kipindi Mara Baada Ya Kujifungua (Postpartum Period).
    G) Kutumia Vipandikizi Vya Ndani Ya Mfuko Wa Uzazi (IUCD) Kama Njia Mojawapo Ya Uzazi Wa Mpango.
    H) Kuambukizwa Kupitia Damu Iliyo Na Vimelea Vya Pid. 
    I) Kutuma Sana Vidole Wakati Wa Kusafisha Uke (Excess Vaginal Douching).

    DALILI ZA PID KWA MWANAMKE

     Zipo dalili kadhaa za ugonjwa wa pid kwa mwanamke, miongoni mwa dalili hizo ni pamoja na;
    A) Kuhisi Maumivu Ya Tumbo Hasa Maeneo Ya Chini Ya Kitovu.
    B) Kupata Maumivu Ya Mgongo.
    C) Kupata Utoko Mchafu Sehemu Za Siri, Utoko Huu Huambatana Na Harufu Mbaya.
    D) Kuhisi Maumivu Wakati Wa Kukojoa.
    E) Kupata Maumivu/Kutokwa Na Damu Wakati Wa Tendo La Ndoa. 
    F) Kutokwa Damu Bila Mpangilio Wakati Wa Hedhi.
    G) Kupata Homa.
    H) Wakati Fulani Kuhisi Kichefuchefu Kama Mwanamke Mjamzito Na kutapika.


    MADHARA YA PID

    PID ambayo haikupata tiba inaweza kusababisha makovu na vifuko vyenye maji yenye wadudu kwenye mkondo wa njia ya uzazi ya mwanamke, vitu hivi vinaweza kusababisha madhara ya kudumu kwenye viungo vya uzazi. Madhara yanayoweza kutokea ni pamoja na;

    A) Mimba kutunga nje ya mirija ya uzazi (Ectopic Pregnancy).

    PID ndiyo sababu ya mimba kutunga nje ya kizazi, mimba huweza kutunga nje ya kizazi endapo PID imesababisha makovu ndani ya mirija ya uzazi. Makovu haya husababisha yai lililopevushwa kushindwa kusafiri ndani ya mirija ya uzazi kuelekea kwenye nyumba ya mirija ya uzazi. Mimba nje ya uzazi husababisha utokaji wa damu usiowakawaida unaoweza kukatisha maisha ya mwanamke.

    B) Ugumba.

    Uharibifu wa viungo vya uzazi huweza kusababisha ugumba, kushindwa kupata ujauzito. Kadri unavyozidi kupata PID mara nyingi zaidi ndivyo hatari ya ugumba inavyozidi, kuchelewa kupata tiba ya PID kuongeza hatari ya ugumba.

    C) Maumivu Sugu Ya Nyonga.

    PID inaweza kusababisha maumivu ya nyonga yanayoweza kudumu miaka mingi. Makovu ndani ya mirija ya uzazi na viungo vingine vya uzazi huweza kuleta maumivu wakati wa kujamiiana na wakati yai hudondoshwa (ovulation).

    D) Tubo Ovarian Abscess.

    PID huweza kusababisha kutunga kwa usaha na kufanya majipu ndani ya mirija ya uzazi na ovari, ingawa huweza kuota ndani ya nyumba ya uzazi na shingo ya kizazi kama tiba haitatolewa, unaweza kupata maambukizi hatarishi kwa maisha.

    MADHARA YA PID KWA MJAMZITO

    Yafuatayo ni madhara yanayoweza kutokea kwa mama mjamzito endapo atashindwa kupata tiba ya pid mapema;
    1) Kujifungua kabla ya wakati au ujauzito kuharibika.
    2) Kujifungua mtoto mwenye maambukizi na wakati mwingine hufariki muda mchache baada ya Kujifungua au kujifungua mtoto mfu.
    3) Kuziba kwa mirija ya uzazi.

    JINSI YA KUJIZUIA KUPATA PID

    Kuna njia kadhaa za kuzuia ugonjwa wa pid.
    Njia hizi ni pamoja na;
    A) Kuwai Kuwaona Wataalamu Wa Afya Mara Dalili Za Ugonjwa Zinapoanza Kujitokeza Au Pindi Tu Unapogundua Kuwa Mpenzi Wako Ana Dalili Za Magonjwa Ya Zinaa Au Anatembea Na Wanawake Wengi.
    B) Kufanya Vipimo Mara Kwa Mara Hasa Vipimo Vya Uzazi, Pamoja Na Vipimo Vya Maambukizi Ya Magonjwa Yanayosambazwa Ka Njia Ya Ngono (STI) Hususani Kwa Mgonjwa Wa Chlamydia, Ufanye Vipimo Kila Mwaka Mara Moja.
    C) Kutofanya ngono mara baada ya kujifungua, mimba kutoka au mara baada ya kutoa mimba ili kuhakikisha njia ya shingo ya uzazi imefunga vyema.
    D) Njia Hakiki Ya Kujizuia Na Maambukizi Haya Ni Kuacha Ngono Zembe

    MATIBABU YA PID

    -MATIBABU YA HOSPITALI
    Matibabu ya pid kwa kutumia dawa yataondoa mara moja maambukizi yanayosababishwa na pid lakini hakuna njia ya kukarabati makovu au uharibifu kwenye njia ya viungo vya uzazi uliotokana na pid. Matibabu ya pid Hospitalini yaweza kuwa:

    A) Antibiotics Za Kutibu Pid.

    Daktari atakuandikia dawa inayoendana na chanzo cha tatizo lako.Utasubiri siku kadhaa kuona kama dawa ulizopewa zinafanya kazi.
    Dawa za Pid zinazotolewa na daktari ni pamoja na; Metronidazole tabs, doxycycline tabs na cefixime tabs

    B) Kumtibu Mpenzi Wako.

    Kuzuia maambukizi yafaa mpenzi wako afanyiwe uchunguzi na atibiwe.

    C) Kuacha Kushiriki Ngono Kwa Muda.

    -MATIBABU YA KUDUMU.
    Kutokana na kutumia bidhaa bora za BF-SUMA mtu utapata tiba sahihi ya kumaliza kabisa maambukizi ya PID kwa kuua vimelea vya magonjwa, kutobu majeraha na kurekebisha mfumo mzima wa uzazi wa mwanamke.

    Kwa huduma na ushauri wasiliana na mtaalam wa afya kupitia,,,
    0745693900
    #tiba#pid #afya #bfsuma
    🚨🚨🚨SIRI IMEFICHUKA🚨🚨🚨 UJUE UGONJWA WA (PID) (Pelvic Inflammatory Disease) Kwa manufaa zaidi usisite kusoma hadi mwisho.... 💫Ugonjwa Wa Pid Ni Nini? Ugonjwa wa pid ni maambukizi katika viungo vya uzazi vya mwanamke. Maambukizi haya kutokea ikiwa bakteria wanaoambukiza kwa njia ya kujamiiana watasambaa kutoka kwenye uke kwenda kwenye mji wa mimba (Uterus), mirija ya uzazi (Fallopian tubes) na kwenye ovari (ambapo mayai ya mwanamke hupatikana). 💫SABABU YA UGONJWA WA PID NI NINI? Ugonjwa wa pid husababishwa na magonjwa ya zinaa kama vile kisonono (gonorrhea) na pangusa (chlamydia). Mwili wa mwanamke unapokuwa na afya njema, mlango wa kizazi huwa na uwezo mkubwa wa kuzuia bakteria wasiweze kuingia katika viungo vya ndani vya uzazi kutoka ukeni. Hata hivyo wakati mlango wa kizazi unapokuwa wazi na kuruhusu magonjwa ya zinaa kuingia hasa kisonono (gonorrhea) na pangusa (chlamydia), mlango wa kizazi hupata maambukizi na kisha hupoteza uwezo wake na hivyo kuruhusu maambukizi na bakteria kuingia na kufika juu kwenye viungo vya uzazi. 💫JINSI MWANAMKE ANAVYO AMBUKIZWA PID Kuna njia kadhaa ambazo mwanamke anaweza kuambukizwa ugonjwa wa pid. Njia hizo ni pamoja na: A) Kama  Una Ugonjwa Wa Zinaa Na Hujatibiwa. B) Kufanya Ngono Zembe Isiyosalama (Yaani Kulala Na Wanaume Tofauti Tofauti). C) Kuwa Na Mpenzi Ambaye Ana Wanawake Wengi Nje.  D) Kama Umeshawai Kuwa Na Historia Ya Kuugua Pid Kabla.  E) Maambukizi Ya Nje Ya Uzazi Mara Baada Ya Kutoa Mimba Kwa Njia Zisizo Salama (Post Abortion) Au Mara Baada Ya Mimba Kutoka (Miscarriage). F) Maambukizi Ya Nje Ya Uzazi Hasa Kipindi Mara Baada Ya Kujifungua (Postpartum Period). G) Kutumia Vipandikizi Vya Ndani Ya Mfuko Wa Uzazi (IUCD) Kama Njia Mojawapo Ya Uzazi Wa Mpango. H) Kuambukizwa Kupitia Damu Iliyo Na Vimelea Vya Pid.  I) Kutuma Sana Vidole Wakati Wa Kusafisha Uke (Excess Vaginal Douching). 💫DALILI ZA PID KWA MWANAMKE  Zipo dalili kadhaa za ugonjwa wa pid kwa mwanamke, miongoni mwa dalili hizo ni pamoja na; A) Kuhisi Maumivu Ya Tumbo Hasa Maeneo Ya Chini Ya Kitovu. B) Kupata Maumivu Ya Mgongo. C) Kupata Utoko Mchafu Sehemu Za Siri, Utoko Huu Huambatana Na Harufu Mbaya. D) Kuhisi Maumivu Wakati Wa Kukojoa. E) Kupata Maumivu/Kutokwa Na Damu Wakati Wa Tendo La Ndoa.  F) Kutokwa Damu Bila Mpangilio Wakati Wa Hedhi. G) Kupata Homa. H) Wakati Fulani Kuhisi Kichefuchefu Kama Mwanamke Mjamzito Na kutapika. 💫MADHARA YA PID PID ambayo haikupata tiba inaweza kusababisha makovu na vifuko vyenye maji yenye wadudu kwenye mkondo wa njia ya uzazi ya mwanamke, vitu hivi vinaweza kusababisha madhara ya kudumu kwenye viungo vya uzazi. Madhara yanayoweza kutokea ni pamoja na; A) Mimba kutunga nje ya mirija ya uzazi (Ectopic Pregnancy). PID ndiyo sababu ya mimba kutunga nje ya kizazi, mimba huweza kutunga nje ya kizazi endapo PID imesababisha makovu ndani ya mirija ya uzazi. Makovu haya husababisha yai lililopevushwa kushindwa kusafiri ndani ya mirija ya uzazi kuelekea kwenye nyumba ya mirija ya uzazi. Mimba nje ya uzazi husababisha utokaji wa damu usiowakawaida unaoweza kukatisha maisha ya mwanamke. B) Ugumba. Uharibifu wa viungo vya uzazi huweza kusababisha ugumba, kushindwa kupata ujauzito. Kadri unavyozidi kupata PID mara nyingi zaidi ndivyo hatari ya ugumba inavyozidi, kuchelewa kupata tiba ya PID kuongeza hatari ya ugumba. C) Maumivu Sugu Ya Nyonga. PID inaweza kusababisha maumivu ya nyonga yanayoweza kudumu miaka mingi. Makovu ndani ya mirija ya uzazi na viungo vingine vya uzazi huweza kuleta maumivu wakati wa kujamiiana na wakati yai hudondoshwa (ovulation). D) Tubo Ovarian Abscess. PID huweza kusababisha kutunga kwa usaha na kufanya majipu ndani ya mirija ya uzazi na ovari, ingawa huweza kuota ndani ya nyumba ya uzazi na shingo ya kizazi kama tiba haitatolewa, unaweza kupata maambukizi hatarishi kwa maisha. 💫MADHARA YA PID KWA MJAMZITO Yafuatayo ni madhara yanayoweza kutokea kwa mama mjamzito endapo atashindwa kupata tiba ya pid mapema; 1) Kujifungua kabla ya wakati au ujauzito kuharibika. 2) Kujifungua mtoto mwenye maambukizi na wakati mwingine hufariki muda mchache baada ya Kujifungua au kujifungua mtoto mfu. 3) Kuziba kwa mirija ya uzazi. 💫JINSI YA KUJIZUIA KUPATA PID Kuna njia kadhaa za kuzuia ugonjwa wa pid. Njia hizi ni pamoja na; A) Kuwai Kuwaona Wataalamu Wa Afya Mara Dalili Za Ugonjwa Zinapoanza Kujitokeza Au Pindi Tu Unapogundua Kuwa Mpenzi Wako Ana Dalili Za Magonjwa Ya Zinaa Au Anatembea Na Wanawake Wengi. B) Kufanya Vipimo Mara Kwa Mara Hasa Vipimo Vya Uzazi, Pamoja Na Vipimo Vya Maambukizi Ya Magonjwa Yanayosambazwa Ka Njia Ya Ngono (STI) Hususani Kwa Mgonjwa Wa Chlamydia, Ufanye Vipimo Kila Mwaka Mara Moja. C) Kutofanya ngono mara baada ya kujifungua, mimba kutoka au mara baada ya kutoa mimba ili kuhakikisha njia ya shingo ya uzazi imefunga vyema. D) Njia Hakiki Ya Kujizuia Na Maambukizi Haya Ni Kuacha Ngono Zembe 💫MATIBABU YA PID 💧-MATIBABU YA HOSPITALI Matibabu ya pid kwa kutumia dawa yataondoa mara moja maambukizi yanayosababishwa na pid lakini hakuna njia ya kukarabati makovu au uharibifu kwenye njia ya viungo vya uzazi uliotokana na pid. Matibabu ya pid Hospitalini yaweza kuwa: A) Antibiotics Za Kutibu Pid. Daktari atakuandikia dawa inayoendana na chanzo cha tatizo lako.Utasubiri siku kadhaa kuona kama dawa ulizopewa zinafanya kazi. Dawa za Pid zinazotolewa na daktari ni pamoja na; Metronidazole tabs, doxycycline tabs na cefixime tabs B) Kumtibu Mpenzi Wako. Kuzuia maambukizi yafaa mpenzi wako afanyiwe uchunguzi na atibiwe. C) Kuacha Kushiriki Ngono Kwa Muda. 💧-MATIBABU YA KUDUMU. Kutokana na kutumia bidhaa bora za BF-SUMA mtu utapata tiba sahihi ya kumaliza kabisa maambukizi ya PID kwa kuua vimelea vya magonjwa, kutobu majeraha na kurekebisha mfumo mzima wa uzazi wa mwanamke. Kwa huduma na ushauri wasiliana na mtaalam wa afya kupitia,,, 📞0745693900 #tiba#pid #afya #bfsuma
    Like
    Love
    8
    ·693 Views
Αναζήτηση αποτελεσμάτων