DOUBLE AGENTS NGULI WANNE KUWAHI KUTOKEA KATIKA ULIMWENGU WA UJASUSI
Mustakabali wa taifa lolote lile hutegemea pamoja na mambo mengine mifumo ya ulinzi, kwani hii ndio nguzo mhimu katika kuhakikisha ustawi wa maslahi ya taifa husika
Ni kwa msingi huo basi mataifa yote duniani yameunda vyombo tofauti tofauti vya ulinzi mojawapo ikiwemo idara za ujajusi, mifano ipo mingi, CIA, M16, BND, MOSSAD, TISS n.k!
Lakini kuwa na taasisi au vyombo hivyo vinahiyaji nguvu kazi, nguvu kazi hii sharti iwe yenye weledi na uzalendo wa kutukuka, kwani kazi wanayoifanya ni kazi nyeti mno na inayozungukwa na mambo mengi sana, hivyo kuteleza kwa namna yoyote ile basi kunaacha madhara makubwa mno! Na kiukweli wapo walioteleza na kuleta madhara yasiyoelezeka, sasa Leo nimeona tuangalie kwa ufupi baadhi ya wanausalama walioteleza na kujikuta walitumia pande mbili au zaidi maarufu kwa jina la *DOUBLE AGENT*
*Lakini kwanza kabisa double agent ni nani?*
Tunaweza tukasema ni afisa usalama wa tasisis au serikali ambaye amepewa majukumuu ya kuichunguza taasisi au nchi nyingine lakini wakati huo huo anakuwa tena anafanya kazi hiyo hiyo kwa ajiri ya taasisi au nchi anayopaswa kuichunguza dhidi ya taasisi au nchi iliyomtuma! Wengi wanasem double agent anaweza kuwa matokeo ya tamaa ya pesa, kulazimishwa( baada ya kutishiwa kufanyiwa kitu kibaya), mapenzi tu, yaani mtu anapenda tu kuwa double agent, kupandikizwa kwa makusudi( marekani wamefaidika sana na aina hii hasa Mashariki ya kati) au inaweza kuwa ni sababu ya mitazamo…
Hawa wafuatao ni baadhi ya double agents nguli kuwahi kutokea na balaa
*Human Khalid Al-Balawi*
Huyu jamaa alikuwa daktari kitaaluma na alikuwa raia wa Jordan, alikamatwa na mamlaka za Jordan kipindi akiwa mwanafunzi kwenye chuo kikuu cha Isntanbul nchini Uturuki baada ya kuonekana akiwa na muelekeo wa misimamamo mikali, inasemekana baadae CIA waliingilia na kumshawishi awe double agent kwa ahadi ya kusamehewa. Jamaa alikubali na CIA wakamuandaa kikamilifu kwa kazi hiyo ambapo baada ya kuiva wakampeleka Pakistan na Afghanistan na kumpa jukumuu la kufuatilia nyendo na shughuli za alqaida nchini humo.
Human aliifanya kazi hiyo kwa uaminifu mkubwa mno na akafanikiwa kuwashawishi CIA ambao walionekana kumwamini 100%. Kumbe hawakujua kuwa aliqaida walikuwa tayari wamembadilisha na alikuwa akifanya nao kazi.
Siku moja akawaeleza kuwa alikuwa na taarifa muhimu kuhusu kiongozi wa juu wa alqaida bwana Ayman- Al-Zawahili na akawapa masharti kuwa angependa taarifa hizo azifikishe kwa viongozi wakuu wa CIA katika eneo hilo, kwakuwa walikuwa wanamtafuta sana Zawahili hawakusita kumkubalia na kumuagiza afike kwenye Ofisi za CIA eneo la Khost Afghanistan, Khalid alifika kwa kuchelewa na kutokana na kimuhe muhe cha taarifa waliyokuwa wanakwenda kuipokea basi wakasahau hadi kumkagua, kumbe jamaa alikuwa amevaa mabomu, baada ya kufika ndani kwa wakubwa jamaa alijilipua na kuua maafisa kadhaa wa ngazi za juu wa CIA katika eneo hilo.
*Arthur Owens*
Arthur alikuwa mwingereza kutoka kisiwa cha Wales na kabla ya vita ya dunia ya pili alikuwa akifanya kazi kama mkandarasi na alikuwa akifanya serikali zote mbili, Ujerumani na England, baada ya vita kuanza aliajiriwa kama mhandisi kwenye meli vita za England akifanya kazi kama fundi betri, baadae Wajerumani walianza kumuomba awape taarifa hasa kuhusu meli vita za England na yeye bila hiana akifanya kazi hiyo, baadae alijiunga nao rasmi na akawa anafanya kazi nao huku pesa na wanawake wazuri yakiwa ndo malipo kwa kazi yake hiyo tukufu.
Baadae alirudi England na kujipeleka moja kwa moja kwa M15 na kuwaeleza ukweli wake na wajerumani, M16 walimpokea na kumtumia ambapo aliwasaidia kufichua zaidi maofisa 120 wa kijeruman nchini England na wakamtumia kuwalisha Wajerumani hao habari za uongo na zile zisixokuwa na athari kubwa kwao.
Mwaka 1941 Arthur na mwenzake mmoja walikamatwa na wajerumani lakini cha ajabu mwenzake alinyongwa huku yeye akiachwa hali iliyowatia wasiwasi England na alivyorudi walimkamata na kumtia kolokoloni hadi baada ya vita, baadae aliwalazimisha England wamlipe fedha kwa maadai ya kumfunga bila makosa na kama watagoma basi ataweka hadharani kila kitu, England walinywea na hadi anakufa hakuwahi kusema chochote.
*Kim Philby*
Kim Philby alikuwa ni afisa wa idara ya usalama ya England, yeye na wenzake wanne walitengeza a spy ring iliyopewa jina la the Combridge five, na wakifanya kazi kwa niaba ya KGB, ni kipindi ambacho wote watano walikuwa wakisoma chuoni hapo, wenzake walikuwa ni pamoja na Donald MacLean, Guy borguess na Anthony Brunt ambapo mtu wa tano kwenye kundi hilo hadi Leo hajawahi kujulikana! Kimsingi Borguess ndiye aliyemsajili Kim na wakati huyo tayari yeye alikuwa ni double agent.
Kilichomsukuma Kim ilikuwa ni imani yake katika falsafa za kijamaa, pamoja na kuwa double agent lakini Kim anasemwa kama mtu aliyefanya kazi kwa weledi mkubwa sana na alipata kutunukiwa nishani kadhaa kwa utumishi uliotukuka kabla ya kuja kumgundua kuwa alikuwa akifanya kazi na KGB, wakati wenzake wanakamatwa yeye alikuwa ameshaacha kazi na alikuwa Lebanon na hakurudi tena England Bali aliekea Jamhuri ya Usovieti ambako alipewa kazi kwenye idara kadhaa za ulinzi, alifariki mwaka 1988 akiwa huko huko Usovieti, Kim aliandika kitabu alichokipa jina la *My secret war* akieleza namna alivyopambana na ubepari.
*Juan Pujol Garsia*
Garsia alikuwa mhisipania ambaye maisha yake yalionekana kutokua na muelekeo kwani kwenye umri wa miaka 32 alikuwa ameshindwa karibia kila kitu, shule, biashara na hata familia, vyote alikuwa amejaribu na vikamshinda.
Baadae wakati wa vita kuu ya pili ya dunia aliamua kwenda kuomba kazi kwenye idara za usalama za England na Marekani lakini aligonga mwamba kwa madai mtu ambaye hakuwa na uwezo hata wa kufuga kuku angeweje kufanya kazi nyeti kama hii tena katika wakati tete. Baada ya kukataliwa akaona isiwe taabu akaenda zake kwa Wajerumani na kujifanya mmoja wa wanazi kindakindaki wa Hitler, manazi baadae walimuamini na kumpa kazi ambapo walimpangia kwenda England! Alielekea huko akipitia Porto Ureno na alianza kazi kwa kukusanya habari kwenye magazeti na redio, baadae alianza kupiga hatua kwa kusajili watu mhimu kutoka wazara ya habari na mawasiliano pamoja na masekretari kwenye wizara mbalimbali, baadae pia alifanikiwa kuingia hadi jeshini na jusajili watu huko.
Garsia alikuja kuumbuliwa na double agent wa kijerumani ambaye aliwatonya England juu ya uwepo wake nchini humo.
Baada ya kubumbuluka Garsia akijipeleka mwenyewe kwa M15 ambapo walikubali kuendelea kutumia mara hii wakimtumia kuwalisha habari za uongo.
Garsia anakumbukwa sana kutokana na kazi tukufu aliyoifanya wakati majeshi ya muungano wa England, Canada, Marekani na baadhi ya wanajeshi wa Ufaransa yalipoanza oparesheni ya kukomboa maeneo yaliyokuwa yamekamatwa na Ujerumani na hasa katika uvamizi wa eneo la Normandy, baada ya wanajeshi wa muungano kuelekea katika eneo hilo wajerumani walipata intelejensia na wakawa wametuma vikosi kwenda kupambana na majeshi ya muungano huku vikosi vingine vikiwekwa tayari nchini ubelgiji, lakini Garsia kwa ujasiri wa hali ya juu akamtumia telegraphy na kumwambia hakukuwa na mashambulizi yoyote katika eneo hilo na kwamba habari alizokuwa amepewa Hitler ulikuwa ni uongo, kwakuwa Hitler alikuwa anamuamini sana basi akaiamini taarifa hii na akaviamrisha vikosi vyake vilivyokuwa njiani kurejea na vile vilivyokuwa ubelgiji kuendelea kubaki.
Wengi wanachukulia hatua hii kama mwanzo wa majeshi ya muungano kuanza kujizatiti kwani hadi hapo Ujerumani ilikuwa tayari imekamata karibu ulaya nzima na ndio maana Garsia anachukuliwa kama double agent aliyefanya kazi ya kutukuka, lakini pia anatajwa kama double agent aliyetunukiwa tunzo nyingi mno kutoka pande zote yaani Ujerumani na England, baada ya vita Garsia alikwenda zake Amerika kusini ambapo alifungua maktaba na kumalizia maisha yake huko.
OUR MOTTO
========
KIJANA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USITUMIKE VIBAYA KUICHAFUA NCHI YAKO.