VIONGOZI YANGA SC SIO HALALI, WANACHAMA 2 WALISHINDA KESI MWEZI AGOSTI MWAKA 2023.
Wanachama wawili wa Yanga SC JUMA MAGOMA (pichani) na GEOFREY MWAIPOPO walishinda kesi waliyofungua katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar mwaka jana mwezi Agosti. Kesi yao ilikuwa dhidi ya Baraza la wadhamini la klabu hiyo kuikabidhi klabu kwa mtu wasiyemjua wala asiyekuwa Mwanachama wakati kesi inafunguliwa mwezi Mei mwaka 2022 siku moja kabla ya uchaguzi mkuu wa klabu uliomuweka madarakani Rais wa Yanga Eng Hersi Said. Awali walifungua kesi hiyo Mahakama ya Wilaya ya Ilala iliyopo Kinyerezi jijini Dar, kabla ya kushauriwa kuihamishia katika Mahakama ya Kisutu.
Walipinga kutumika kwa katiba ya mwaka 2020 ambayo ilitumika kwenye uchaguzi Mkuu uliouweka uongozi uliopo madarakani wakisema katiba hiyo sio halali. Inasemekana RITA waliitwa kutoa ushahidi na wakasema wanaifahamu katiba ya mwaka 2011ambayo ipo ofisini kwao na hiyo ya mwaka 2020 hawaitambui.
Baada ya kupata hukumu yao mwezi Agosti mwaka 2023 JUMA MAGOMA NA GEOFREY MWAIPOPO wameona hakuna utekelezaji wa hukumu hiyo hata baada ya kuwasilisha kwa wahusika wakaamua kufungua kesi ya kukazia hukumu ambapo itatolewa maamuzi mwezi Agosti tarehe 5 mwaka 2024, ili hukumu hiyo ianze kufanya kazi. Ambapo inategemewa Mkutano Mkuu wa Yanga kuitwa ambao utajumuisha WANACHAMA WOTE HAI sio wawakilishi wa matawi pekee (kama ilivyo sasa) na kwenda kwenye uchaguzi mkuu wa uchaguzi wa viongozi wa klabu kwa kufuata katiba ya mwaka 2011. Kama hili litatokea manake Eng Hersi na timu yake watakuwa wameondoshwa madarakani kwakuwa watakuwa wameingia isivyo halali.