Upgrade to Pro

  • SAKATA LA JASUSI SERGEI SKRIPAL NA MWANAE NI UTEKELEZAJI WA OPERATION SARLISBURY ILIYOTEKELEZWA NA RUSSIA, KIMSIMGI NI VITA KATI YA URUSI NA NATO KUJIBU MAPIGO YA UCHAGUZI WA MAREKANI MWAKA 2016.

    Na mhariri wako Comred Mbwana Allyamtu

    Sakata la jaribio la mauaji ya jasusi au mpelelezi, ndumilakuwili wa Urusi na Uingereza, Sergei Skripal na binti yake Yulia katika kitongoji cha Salisbury jijini London nchini Uingereza linachukua sura mpya kila siku.

    Wawili hao walipatikana wakiwa hawajitambui katika eneo la maduka liitwalo Maltings mwanzoni mwa Machi.

    Taarifa kutoka kwa polisi wa Uingereza ambao hushughulikia matukio ya kigaidi wanaamini kuwa jasusi huyo na mwanaye, walivuta hewa iliyokuwa na kemikali yenye sumu iitwayo novichok.

    Kemikali hii hushambulia mfumo wa mfahamu na inasemekana ilitengenezwa katika maabara moja huko Urusi na ilitumika wakati wa Vita vya Pili vya Dunia mwaka 1935 hadi 1945. Kemikali hiyo iliachwa mlangoni mwa nyumba ambayo amekuwa akiishi jasusi huyo na mwanaye katika eneo hilo la Salisbury.

    Mashirika makubwa ya habari nchini Uingereza yameipa umuhimu habari hii ambapo Machi 30, yalitangaza kuwa binti wa Skripal, Yulia hakuwa katika hali tete kiafya.

    Kufuatia tukio hilo Serikali ya Uingereza chini ya Waziri Mkuu, Theresa May iliitupia lawama Serikali ya Urusi kwa kuhusika na uovu huo na ili kuonyesha kuwa imechukia iliamua kuwafukuza wanadiplomasia wa Urusi wapatao 23.

    Urusi imekanusha kuhusika na uovu huo na ikaahidi kuwa kwa kila hukumu itakayotolewa nayo itajibu kwa ukubwa huohuo au zaidi ya hapo, na ikajibu kwa kutoa hukumu ya kisasi kwa kuwafukuza wanadiplomasia 23 wa Uingereza na kufunga kituo cha Lugha na Utamaduni cha Uingereza, British Council na imeitaka Uingereza kuwaondoa wanadiplomasia wake wengine wapatao 50 katika kipindi cha mwezi mmoja.
    Ili kuonyesha mshikamano na Uingereza nchi nyingine za Ulaya Magharibi na Australia zimewafukuza wanadiplomasia wa Urusi wanaofikia 150 huku Marekani ikiongoza kwa kufunga ubalozi mdogo wa Urusi katika Jiji la Seattle na kuwafukuza wanadiplomasia 60 kutoka nchi hiyo.

    Urusi nayo haikubaki kimya, Waziri wa Mambo ya Nje, Sergei Lavrov ametangaza kuwafukuza wanadiplomasia 60 wa Marekani na vilevile kufunga ubalozi wa Marekani katika mji wa Saint Petersburg na kuahidi kuwa kila nchi iliyohusika na kufukuza wanadiplomasia wake itaadhibiwa vilivyo.

    Kwa ujumla nchi karibu 23 na Umoja wa Kujihami wa nchi za Ulaya Magharibi (Nato) kote ulimwenguni zimeonyesha kukerwa na vitendo vya Urusi kwa kuingilia mambo ya ndani ya nchi tofautitofauti, kama vile kuvamia Ukraine na kulichukua jimbo la Krimea, kuitungua ndege ya Malaysia na kuingilia uchaguzi Mkuu wa Marekani mwaka 2016.
    Siyo mara ya kwanza nchi hizi kuingia katika mzozo wa kidiplomasia kwani mwaka 1986 Ronald Reagan aliyekuwa Rais wa Marekani, aliamuru wanadiplomasia 80 wa Shirikisho la Urusi (USSR) wafukuzwe nchini humo na mwaka 2016, Rais Barak Obama aliwatimua wanadiplomasia 35 kutoka nchi hiyo kwa tuhuma za kudukua kompyuta za chama cha Democratic kwa nia ya kumhujumu mgombea wake wa Rais, Hillary Clinton.

    Mwaka 2006 Skripal alihukumiwa kifungo cha miaka 13, nchini Urusi katika kesi ambayo iliendeshwa katika mahakama ya siri, alipewa haki ya ukimbizi na ukazi nchini Uingereza mwaka 2010 baada ya makubaliano ya kubadilishana wafungwa katika mtindo ambao ulitumika enzi za vita baridi kuhusiana na shughuli za kijasusi.

    Kulingana na nyaraka za kumbukumbu ambazo vyombo vya habari vya Uingereza vilizipata kutoka makumbusho ya taifa ya Uingereza mwaka 2015, zinaonyesha kuwa Serikali ya Urusi imekuwa ikiichunguza Uingereza muda mrefu lakini kisa kinachojulikana sana ni kile kilichopewa jina la Cambridge Four, ambapo kitengo cha ujasusi cha shirikisho la Urusi (USSR), KGB, katika miaka ya 1930 kabla ya vita vya pili vya dunia kiligundua kuwa Serikali ya Uingereza ilikuwa ikitumia Chuo Kikuu cha Cambridge kama sehemu maalumu ya kuwapata majasusi wachanga wakiwa masomoni. KGB waliwafuata wanafunzi wanne wa wakati huo ambao ni Anthony Blunt, Donald Duart Maclean, Kim Phillby na Guy Burgess.
    Wasomi hao ambao kwa bahati nzuri kwao KGB walipomaliza masomo yao waliingia kufanya kazi katika Mashirika ya Ujasusi ya Uingereza, MI5 na MI6, na wakawa ni majasusi ndumilakuwili.

    Walifanya kazi yao hadi mwaka 1964 ambapo Anthony Blunt ambaye alikuwa akifanya kazi katika Shirika la Ujasusi wa ndani, MI5, alikiri kuwa jasusi ndumilakuwili ili asishtakiwe na habari hiyo ilikuja kutolewa na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza wakati huo, Magreth Thatcher alipokuwa akihutubia Bunge mwaka 1979. Donald Duart Maclean, Kim Phillby na Guy Burgess wao walitimkia Urusi na Serikali ya Uingereza ikawa imekubali yaiishe.

    Kwa hiyo Urusi imekuwa hailali usingizi wakati wote wa miaka ya vita baridi kati ya nchi za Ulaya Mashariki na Magharibi miaka ya 1945 hadi mwanzoni mwa miaka ya 1990, imekuwa ikiingiza wapelelezi wake maeneo mbalimbali katika nchi hizo ili kupata habari nyeti kuhusiana na masuala mbalimbali katika nyanja za uchumi, biashara hasa ya silaha na teknolojia yake na hivi karibuni kuingilia mambo ya siasa za uchaguzi huko Marekani.
    Ukiangalia kisa cha safari hii hakina tofauti sana kile alichofanyiwa Jasusi mwingine wa Urusi Novemba 2006, Alexander Litvinenko ambaye aliwekewa kemikali iitwayo Polonium 210 katika kikombe cha chai katika mgahawa mmoja jijini London.

    Litvinenko alitoroka Urusi baada ya kutofautiana na wenzake katika shirika la kijasusi la nchi hiyo FSB, ambapo aliutuhumu uongozi wa juu wa nchi hiyo kuigeuza nchi hiyo kuwa Taifa la kimafia. akiwa nchini Uingereza, alifanya kazi kama mwandishi wa habari, vitabu na mshauri wa mambo ya usalama.
    Akiwa Uingereza aliandika vitabu viwili, Blowing up Russia: Terror from within na Lubyanka Criminal Group ambapo aliituhumu idara hiyo ya kijasusi kwa vitendo vya mauaji na matumizi ya mabomu na mauaji ya mwandishi wa habari, Anna Politkovskaya kwa amri kutoka kwa Rais wa nchi hiyo, Vladimir Putin.

    Litvinenko akiwa mahututi kitandani hospitalini jijini London aliwatamkia ndugu zake kuwa alikuwa na uhakika kuwa Rais wa Urusi, Vladimir Putin ndiye aliyeamuru auawe.
    Serikali ya Uingereza ya wakati huo chini ya Waziri Mkuu, Tony Blair ilifanya upelelezi na kugundua kuwa jasusi huyo siku chache kabla ya kupata mkasa huo alikuwa ametembelewa na jasusi mwingine mstaafu wa FSB ambaye kwa sasa ni mfanyabiashara, Andrey Lugovoy.
    Serikali ya Uingereza iliitaka Urusi imsalimishe kwake ili afanyiwe mahojiano lakini Urusi ilikataa kwa maelezo kuwa Katiba ya nchi hiyo inakataza raia wake kupelekwa nchi nyingine kufanyiwa mashtaka ya jinai. Uhusiano kati ya nchi hizo mbili ulififia kwa muda.

    Serikali ya Uingereza kwa matukio yote haya imekuwa ikiituhumu serikali ya Urusi kwa kile inachoeleza kuwa kemikali hizo haziwezi kuwa mikononi mwa mtu binafsi bila kuwa na kibari cha mamlaka za juu za nchi hiyo.

    Wakati Kim Phillby alipokimbilia Urusi baada ya kushtukia kuwa wenzake walikuwa wanaelekea kumgundua kuwa ni ndumilakuwili, Ofisa mmoja wa ngazi ya juu ndani ya KGB wakati huo alimsifu kuwa alikuwa jasusi mwenye thamani kubwa wa karne iliyopita.

    Urusi imekuwa ikitoa ulinzi wa kiwango cha juu kwa majasusi ndumilakuwili ambao wamefanikiwa kuingia nchini humo baada ya mambo kwenda kombo huko kwao.

    Marekani nayo haikuwahi kupona kwa taasisi zake za kijasusi kuingiliwa na wenzao wa Urusi. Mwaka 2001 Shirika la Ujasusi wa Ndani, FBI, lilimkamata Robert Hanssen ambaye alikuwa mtumishi wake kwa kupeleka taarifa za siri za nchi hiyo kwa Urusi tangu mwaka 1979 kwa kulipwa fedha na almasi.

    Kwa sehemu kubwa shughuli za ujasusi zimekuwa zikifanywa kwa njia ya teknolojia (Artificial Intelligence) ambapo mitambo ya kompyuta na setelaiti na kamera zenye nguvu za kunasa picha hutumika na pale ambapo haiwezekani, inabidi kutumia binadamu (human intelligence) ili kupata habari ambazo ni siri na mataifa karibu yote duniani yameuweka ujasusi kama ni kosa la uhaini kwa yeyote atakayejihusisha nao.
    SAKATA LA JASUSI SERGEI SKRIPAL NA MWANAE NI UTEKELEZAJI WA OPERATION SARLISBURY ILIYOTEKELEZWA NA RUSSIA, KIMSIMGI NI VITA KATI YA URUSI NA NATO KUJIBU MAPIGO YA UCHAGUZI WA MAREKANI MWAKA 2016. Na mhariri wako Comred Mbwana Allyamtu Sakata la jaribio la mauaji ya jasusi au mpelelezi, ndumilakuwili wa Urusi na Uingereza, Sergei Skripal na binti yake Yulia katika kitongoji cha Salisbury jijini London nchini Uingereza linachukua sura mpya kila siku. Wawili hao walipatikana wakiwa hawajitambui katika eneo la maduka liitwalo Maltings mwanzoni mwa Machi. Taarifa kutoka kwa polisi wa Uingereza ambao hushughulikia matukio ya kigaidi wanaamini kuwa jasusi huyo na mwanaye, walivuta hewa iliyokuwa na kemikali yenye sumu iitwayo novichok. Kemikali hii hushambulia mfumo wa mfahamu na inasemekana ilitengenezwa katika maabara moja huko Urusi na ilitumika wakati wa Vita vya Pili vya Dunia mwaka 1935 hadi 1945. Kemikali hiyo iliachwa mlangoni mwa nyumba ambayo amekuwa akiishi jasusi huyo na mwanaye katika eneo hilo la Salisbury. Mashirika makubwa ya habari nchini Uingereza yameipa umuhimu habari hii ambapo Machi 30, yalitangaza kuwa binti wa Skripal, Yulia hakuwa katika hali tete kiafya. Kufuatia tukio hilo Serikali ya Uingereza chini ya Waziri Mkuu, Theresa May iliitupia lawama Serikali ya Urusi kwa kuhusika na uovu huo na ili kuonyesha kuwa imechukia iliamua kuwafukuza wanadiplomasia wa Urusi wapatao 23. Urusi imekanusha kuhusika na uovu huo na ikaahidi kuwa kwa kila hukumu itakayotolewa nayo itajibu kwa ukubwa huohuo au zaidi ya hapo, na ikajibu kwa kutoa hukumu ya kisasi kwa kuwafukuza wanadiplomasia 23 wa Uingereza na kufunga kituo cha Lugha na Utamaduni cha Uingereza, British Council na imeitaka Uingereza kuwaondoa wanadiplomasia wake wengine wapatao 50 katika kipindi cha mwezi mmoja. Ili kuonyesha mshikamano na Uingereza nchi nyingine za Ulaya Magharibi na Australia zimewafukuza wanadiplomasia wa Urusi wanaofikia 150 huku Marekani ikiongoza kwa kufunga ubalozi mdogo wa Urusi katika Jiji la Seattle na kuwafukuza wanadiplomasia 60 kutoka nchi hiyo. Urusi nayo haikubaki kimya, Waziri wa Mambo ya Nje, Sergei Lavrov ametangaza kuwafukuza wanadiplomasia 60 wa Marekani na vilevile kufunga ubalozi wa Marekani katika mji wa Saint Petersburg na kuahidi kuwa kila nchi iliyohusika na kufukuza wanadiplomasia wake itaadhibiwa vilivyo. Kwa ujumla nchi karibu 23 na Umoja wa Kujihami wa nchi za Ulaya Magharibi (Nato) kote ulimwenguni zimeonyesha kukerwa na vitendo vya Urusi kwa kuingilia mambo ya ndani ya nchi tofautitofauti, kama vile kuvamia Ukraine na kulichukua jimbo la Krimea, kuitungua ndege ya Malaysia na kuingilia uchaguzi Mkuu wa Marekani mwaka 2016. Siyo mara ya kwanza nchi hizi kuingia katika mzozo wa kidiplomasia kwani mwaka 1986 Ronald Reagan aliyekuwa Rais wa Marekani, aliamuru wanadiplomasia 80 wa Shirikisho la Urusi (USSR) wafukuzwe nchini humo na mwaka 2016, Rais Barak Obama aliwatimua wanadiplomasia 35 kutoka nchi hiyo kwa tuhuma za kudukua kompyuta za chama cha Democratic kwa nia ya kumhujumu mgombea wake wa Rais, Hillary Clinton. Mwaka 2006 Skripal alihukumiwa kifungo cha miaka 13, nchini Urusi katika kesi ambayo iliendeshwa katika mahakama ya siri, alipewa haki ya ukimbizi na ukazi nchini Uingereza mwaka 2010 baada ya makubaliano ya kubadilishana wafungwa katika mtindo ambao ulitumika enzi za vita baridi kuhusiana na shughuli za kijasusi. Kulingana na nyaraka za kumbukumbu ambazo vyombo vya habari vya Uingereza vilizipata kutoka makumbusho ya taifa ya Uingereza mwaka 2015, zinaonyesha kuwa Serikali ya Urusi imekuwa ikiichunguza Uingereza muda mrefu lakini kisa kinachojulikana sana ni kile kilichopewa jina la Cambridge Four, ambapo kitengo cha ujasusi cha shirikisho la Urusi (USSR), KGB, katika miaka ya 1930 kabla ya vita vya pili vya dunia kiligundua kuwa Serikali ya Uingereza ilikuwa ikitumia Chuo Kikuu cha Cambridge kama sehemu maalumu ya kuwapata majasusi wachanga wakiwa masomoni. KGB waliwafuata wanafunzi wanne wa wakati huo ambao ni Anthony Blunt, Donald Duart Maclean, Kim Phillby na Guy Burgess. Wasomi hao ambao kwa bahati nzuri kwao KGB walipomaliza masomo yao waliingia kufanya kazi katika Mashirika ya Ujasusi ya Uingereza, MI5 na MI6, na wakawa ni majasusi ndumilakuwili. Walifanya kazi yao hadi mwaka 1964 ambapo Anthony Blunt ambaye alikuwa akifanya kazi katika Shirika la Ujasusi wa ndani, MI5, alikiri kuwa jasusi ndumilakuwili ili asishtakiwe na habari hiyo ilikuja kutolewa na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza wakati huo, Magreth Thatcher alipokuwa akihutubia Bunge mwaka 1979. Donald Duart Maclean, Kim Phillby na Guy Burgess wao walitimkia Urusi na Serikali ya Uingereza ikawa imekubali yaiishe. Kwa hiyo Urusi imekuwa hailali usingizi wakati wote wa miaka ya vita baridi kati ya nchi za Ulaya Mashariki na Magharibi miaka ya 1945 hadi mwanzoni mwa miaka ya 1990, imekuwa ikiingiza wapelelezi wake maeneo mbalimbali katika nchi hizo ili kupata habari nyeti kuhusiana na masuala mbalimbali katika nyanja za uchumi, biashara hasa ya silaha na teknolojia yake na hivi karibuni kuingilia mambo ya siasa za uchaguzi huko Marekani. Ukiangalia kisa cha safari hii hakina tofauti sana kile alichofanyiwa Jasusi mwingine wa Urusi Novemba 2006, Alexander Litvinenko ambaye aliwekewa kemikali iitwayo Polonium 210 katika kikombe cha chai katika mgahawa mmoja jijini London. Litvinenko alitoroka Urusi baada ya kutofautiana na wenzake katika shirika la kijasusi la nchi hiyo FSB, ambapo aliutuhumu uongozi wa juu wa nchi hiyo kuigeuza nchi hiyo kuwa Taifa la kimafia. akiwa nchini Uingereza, alifanya kazi kama mwandishi wa habari, vitabu na mshauri wa mambo ya usalama. Akiwa Uingereza aliandika vitabu viwili, Blowing up Russia: Terror from within na Lubyanka Criminal Group ambapo aliituhumu idara hiyo ya kijasusi kwa vitendo vya mauaji na matumizi ya mabomu na mauaji ya mwandishi wa habari, Anna Politkovskaya kwa amri kutoka kwa Rais wa nchi hiyo, Vladimir Putin. Litvinenko akiwa mahututi kitandani hospitalini jijini London aliwatamkia ndugu zake kuwa alikuwa na uhakika kuwa Rais wa Urusi, Vladimir Putin ndiye aliyeamuru auawe. Serikali ya Uingereza ya wakati huo chini ya Waziri Mkuu, Tony Blair ilifanya upelelezi na kugundua kuwa jasusi huyo siku chache kabla ya kupata mkasa huo alikuwa ametembelewa na jasusi mwingine mstaafu wa FSB ambaye kwa sasa ni mfanyabiashara, Andrey Lugovoy. Serikali ya Uingereza iliitaka Urusi imsalimishe kwake ili afanyiwe mahojiano lakini Urusi ilikataa kwa maelezo kuwa Katiba ya nchi hiyo inakataza raia wake kupelekwa nchi nyingine kufanyiwa mashtaka ya jinai. Uhusiano kati ya nchi hizo mbili ulififia kwa muda. Serikali ya Uingereza kwa matukio yote haya imekuwa ikiituhumu serikali ya Urusi kwa kile inachoeleza kuwa kemikali hizo haziwezi kuwa mikononi mwa mtu binafsi bila kuwa na kibari cha mamlaka za juu za nchi hiyo. Wakati Kim Phillby alipokimbilia Urusi baada ya kushtukia kuwa wenzake walikuwa wanaelekea kumgundua kuwa ni ndumilakuwili, Ofisa mmoja wa ngazi ya juu ndani ya KGB wakati huo alimsifu kuwa alikuwa jasusi mwenye thamani kubwa wa karne iliyopita. Urusi imekuwa ikitoa ulinzi wa kiwango cha juu kwa majasusi ndumilakuwili ambao wamefanikiwa kuingia nchini humo baada ya mambo kwenda kombo huko kwao. Marekani nayo haikuwahi kupona kwa taasisi zake za kijasusi kuingiliwa na wenzao wa Urusi. Mwaka 2001 Shirika la Ujasusi wa Ndani, FBI, lilimkamata Robert Hanssen ambaye alikuwa mtumishi wake kwa kupeleka taarifa za siri za nchi hiyo kwa Urusi tangu mwaka 1979 kwa kulipwa fedha na almasi. Kwa sehemu kubwa shughuli za ujasusi zimekuwa zikifanywa kwa njia ya teknolojia (Artificial Intelligence) ambapo mitambo ya kompyuta na setelaiti na kamera zenye nguvu za kunasa picha hutumika na pale ambapo haiwezekani, inabidi kutumia binadamu (human intelligence) ili kupata habari ambazo ni siri na mataifa karibu yote duniani yameuweka ujasusi kama ni kosa la uhaini kwa yeyote atakayejihusisha nao.
    ·336 Views
  • Chombo cha Habari cha Al Jazeera kimepigwa marufuku nchini DRC baada ya kufanya mahojiano na Bertrand Bisimwa, kiongozi wa kundi la waasi la M23 ambalo limechukua udhibiti katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo.

    Vyombo vya Habari vimeripoti kuwa, Waziri wa sheria wa Congo ametoa tishio la adhabu ya kifo kwa waandishi wa habari na wengine wanaoripoti kuhusu waasi wa M23, ingawa hakuna sheria rasmi inayopiga marufuku vyombo vya habari kuripoti kuhusu makundi ya waasi.
    Chombo cha Habari cha Al Jazeera kimepigwa marufuku nchini DRC baada ya kufanya mahojiano na Bertrand Bisimwa, kiongozi wa kundi la waasi la M23 ambalo limechukua udhibiti katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo. Vyombo vya Habari vimeripoti kuwa, Waziri wa sheria wa Congo ametoa tishio la adhabu ya kifo kwa waandishi wa habari na wengine wanaoripoti kuhusu waasi wa M23, ingawa hakuna sheria rasmi inayopiga marufuku vyombo vya habari kuripoti kuhusu makundi ya waasi.
    ·92 Views
  • Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limethibitisha kumshikilia aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA na Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Dkt. Wilbrod Slaa kwa ajili ya mahojiano ya baadhi ya mambo.

    Kamanda Jumanne Muliro ambaye hakuweka wazi sababu za kumshikilia, amesema mahojiano yanakwenda vizuri, hivyo wanaangalia mifumo ya kisheria itakayowaelekeza nini cha kufanya.
    Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limethibitisha kumshikilia aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA na Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Dkt. Wilbrod Slaa kwa ajili ya mahojiano ya baadhi ya mambo. Kamanda Jumanne Muliro ambaye hakuweka wazi sababu za kumshikilia, amesema mahojiano yanakwenda vizuri, hivyo wanaangalia mifumo ya kisheria itakayowaelekeza nini cha kufanya.
    Like
    1
    1 Comments ·110 Views
  • Haji Manara aomba radhi kwa Jeshi la Polisi la Magereza baada ya Haji kumfokea na kumkejeli (na kumdharau) mmoja wa Askari wake baada ya mchezo wa klabu ya Yanga SC dhidi ya klabu ya Tanzania Prisons. Haji Manara alitaka kufanya mahojiano na Waandishi wa habari lakini Askari huyo wa Magereza akamtata Haji Manara asifanye mahojiano hayo sehemu ambayo alitaka kufanya kwa sababu ilikuwa sio mahali sahihi kwa ajili ya kufanya mahojiano.

    Mara baada ya Askari huyo kumkata Haji Manara asifanye mahojiano eneo lile, Haji aligoma na kutoa maneno yasiofaa kwa Askari huyo huku akimvimbua na kumwambia kuwa yeye ni Askari Magereza tu, hawezi kumfanya chochote kile.

    "Kwa heshma na Unyenyekevu mkubwa naomba nirudie tena kwa maandishi kuliomba radhi Jeshi la Magereza,Askari na Wote waliotharika na Sakata la Juzi,,,
    Hakuna Maneno yanayotosha kuzidi neno samahani,ukizingatia hapo awali tulikuwa tunaongea maneno ya kishabiki,,,
    Heshma yangu kwa Taasisi hii na nyingine za Dola haiwezi kuwa na mbadala wa kuomba sana Taaaisi hii muhimu Radhi kwa Viongozi wa Jeshi na Askari wake wote,,

    Asanteni sana " - Haji Manara, Shabiki wa klabu ya Yanga SC.
    Haji Manara aomba radhi kwa Jeshi la Polisi la Magereza baada ya Haji kumfokea na kumkejeli (na kumdharau) mmoja wa Askari wake baada ya mchezo wa klabu ya Yanga SC dhidi ya klabu ya Tanzania Prisons. Haji Manara alitaka kufanya mahojiano na Waandishi wa habari lakini Askari huyo wa Magereza akamtata Haji Manara asifanye mahojiano hayo sehemu ambayo alitaka kufanya kwa sababu ilikuwa sio mahali sahihi kwa ajili ya kufanya mahojiano. Mara baada ya Askari huyo kumkata Haji Manara asifanye mahojiano eneo lile, Haji aligoma na kutoa maneno yasiofaa kwa Askari huyo huku akimvimbua na kumwambia kuwa yeye ni Askari Magereza tu, hawezi kumfanya chochote kile. "Kwa heshma na Unyenyekevu mkubwa naomba nirudie tena kwa maandishi kuliomba radhi Jeshi la Magereza,Askari na Wote waliotharika na Sakata la Juzi,,, Hakuna Maneno yanayotosha kuzidi neno samahani,ukizingatia hapo awali tulikuwa tunaongea maneno ya kishabiki,,, Heshma yangu kwa Taasisi hii na nyingine za Dola haiwezi kuwa na mbadala wa kuomba sana Taaaisi hii muhimu Radhi kwa Viongozi wa Jeshi na Askari wake wote,, Asanteni sana 🙏🙏🙏" - Haji Manara, Shabiki wa klabu ya Yanga SC.
    ·137 Views
  • “Maandalizi ambayo tunaendelea kuyafanya tutakuwa na mchezo mzuri.”- Nahodha Mohamed Hussein.

    Mahojiano kamili ingia Simba App.

    #paulswai
    “Maandalizi ambayo tunaendelea kuyafanya tutakuwa na mchezo mzuri.”- Nahodha Mohamed Hussein. Mahojiano kamili ingia Simba App. #paulswai
    Love
    Like
    4
    ·201 Views
  • 𝐔𝐏𝐃𝐀𝐓𝐄𝐒 || Mahojiano ya Meneja wa habari na mawasiliano wa Simba SC na waandishi wa habari kabla ya kuondoka Nchini kuelekea Libya

    Mwandishi : "Suala la Lameck Lawi limeishaje?"

    Ahmed : "Lameck Lawi ni mchezaji HALALI wa Simba SC, HALALI kabisa zingatia neno Halali kabisa"

    Mwandishi : Mbona hatumuoni katika Kikosi chenu na mlimtambulisha?

    Ahmed : " Suala lake lipo katika kamati na mtapatiwa majibu soon"

    Mwandishi : "Kwanini mmekua na sintofahamu nyingi za mikataba kwa wachezaji wazawa safari hii?"

    Ahmed : " Hiyo ndio maana halisi ya UBAYA UBWELA"

    Mwandishi : "Kwa Yusufu Kagoma, Awesu?"

    Ahmed : "Ubaya ubwela tu"

    Mwandishi : "Inaonekana hamfuati taratibu za kusaini wachezaji"

    Ahmed : "Kusema ukweli Simba tuko smart sana na mikataba na tunajua tunachokifanya ila kuna watu wanajitoa akili"

    Ahmed Ally akizungumza na Waandishi Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere
    #paulswai
    🚨𝐔𝐏𝐃𝐀𝐓𝐄𝐒 || Mahojiano ya Meneja wa habari na mawasiliano wa Simba SC na waandishi wa habari kabla ya kuondoka Nchini kuelekea Libya Mwandishi : "Suala la Lameck Lawi limeishaje?" Ahmed : "Lameck Lawi ni mchezaji HALALI wa Simba SC, HALALI kabisa zingatia neno Halali kabisa" Mwandishi : Mbona hatumuoni katika Kikosi chenu na mlimtambulisha? Ahmed : " Suala lake lipo katika kamati na mtapatiwa majibu soon" Mwandishi : "Kwanini mmekua na sintofahamu nyingi za mikataba kwa wachezaji wazawa safari hii?" Ahmed : " Hiyo ndio maana halisi ya UBAYA UBWELA" Mwandishi : "Kwa Yusufu Kagoma, Awesu?" Ahmed : "Ubaya ubwela tu" Mwandishi : "Inaonekana hamfuati taratibu za kusaini wachezaji" Ahmed : "Kusema ukweli Simba tuko smart sana na mikataba na tunajua tunachokifanya ila kuna watu wanajitoa akili" 🗣️Ahmed Ally akizungumza na Waandishi Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere #paulswai
    Like
    1
    ·479 Views
  • Mgonjwa wa Kwanza wa Neuralink Aeleza Uzoefu Wake

    🎙Katika mahojiano, mgonjwa wa kwanza aliyewekewa kipandikizi cha Neuralink ameeleza uzoefu wake. Mgonjwa huyu, ambaye ni kiwete kutoka shingo kushuka chini, sasa anaweza kudhibiti vifaa kwa nguvu ya mawazo yake. Wakati wa kuwekewa kipandikizi kwa mara ya kwanza, kilitoka kwa sababu wanasayansi hawakuzingatia harakati za ubongo ndani ya kipenyo cha milimita moja, na ilibidi wafanye upasuaji tena.

    Sasa, mgonjwa huyu anaweza kuvinjari TikTok, kuwasiliana kupitia Twitter, kufanya manunuzi mtandaoni, na kucheza michezo ya kompyuta kwa kuunganisha kipandikizi kwenye kompyuta kupitia Bluetooth na programu maalum. Amebainisha kuwa kipandikizi hicho hakileti maumivu wala hali ya kutojisikia vizuri.

    #Hora_Tech
    #Neuralink #mahojiano #Bluetooth
    🧠 Mgonjwa wa Kwanza wa Neuralink Aeleza Uzoefu Wake 🌐 🎙Katika mahojiano, mgonjwa wa kwanza aliyewekewa kipandikizi cha Neuralink ameeleza uzoefu wake. Mgonjwa huyu, ambaye ni kiwete kutoka shingo kushuka chini, sasa anaweza kudhibiti vifaa kwa nguvu ya mawazo yake. Wakati wa kuwekewa kipandikizi kwa mara ya kwanza, kilitoka kwa sababu wanasayansi hawakuzingatia harakati za ubongo ndani ya kipenyo cha milimita moja, na ilibidi wafanye upasuaji tena. 🥸 Sasa, mgonjwa huyu anaweza kuvinjari TikTok, kuwasiliana kupitia Twitter, kufanya manunuzi mtandaoni, na kucheza michezo ya kompyuta kwa kuunganisha kipandikizi kwenye kompyuta kupitia Bluetooth na programu maalum. Amebainisha kuwa kipandikizi hicho hakileti maumivu wala hali ya kutojisikia vizuri. ➤ #Hora_Tech #Neuralink #mahojiano #Bluetooth
    Like
    Love
    2
    ·847 Views