• Kaka 2003 Alitua Malpesa Airpot Milan akiwa amevaa mewani ya mwanafunzi, Nywele zake amechana vizuri kama mwanafunzi, kitu pekee alichokosa ili awe mwanafunzi kamili ni vitabu na lunchbox, "nikasema" Mungu wangu tumefanya nini hiki? hivi huyu ataweza kucheza professional football kwa kiwango kinachotakiwa?

    Sikuwahi kumuona Ricardo Kaka kabla hiyo ndo ilikua mara ya kwanza, hata video yake yoyote sikuiona kwahiyo nilikua na wasiwasi.

    Hatimae siku ilifika Kaka akaja kwenye mazoezi kitu cha kwanza nilichotaka kumuuliza ni "Umewaambia wazazi wako kuwa haujaenda shule leo?", Walinzi wa Milanello(uwanja wa mazoezi) walikua na kila sababu ya kumuuliza iko wapi leseni yako ya udereva kabla ya kumruhusu kuingia ila unajua ni nini kilitokea? Ni hiki...

    Aliposimama uwanjani kwa mara ya kwanza niliskia kwaya na tarumbeta kutoka mbinguni kweli Kaka alikua ni Genius alieteremshwa kutoka mbinguni asante Mungu.

    Alipogusa tu mpira alikua na uwezo wa ajabu niliacha kuongea maana hakuna neno la kuelezea hisia zangu, hakuna neno kwenye kamusi linaloweza kuelezea ni nini niliona.

    Nilimpenda sana Kaka, kweli nilimpenda, sana, Aliweka chini mewani yake akavaa tracksuit na akawa kitu ambacho sikutegemea "mchezaji mwenye viwango vya dunia".

    Hayo ni Maneno aliyoandika Carlo Ancelotti kwenye kitabu chake "The beautiful Game of an Ordinary Genius", akielezea nini kilitokea alipokua kocha wa Ac Milan na walipomsajili Ricardo Izecson dos Santos Leite maarufu Ricardo Kaka.
    Kaka 2003 Alitua Malpesa Airpot Milan akiwa amevaa mewani ya mwanafunzi, Nywele zake amechana vizuri kama mwanafunzi, kitu pekee alichokosa ili awe mwanafunzi kamili ni vitabu na lunchbox, "nikasema" Mungu wangu tumefanya nini hiki? hivi huyu ataweza kucheza professional football kwa kiwango kinachotakiwa? Sikuwahi kumuona Ricardo Kaka kabla hiyo ndo ilikua mara ya kwanza, hata video yake yoyote sikuiona kwahiyo nilikua na wasiwasi. Hatimae siku ilifika Kaka akaja kwenye mazoezi kitu cha kwanza nilichotaka kumuuliza ni "Umewaambia wazazi wako kuwa haujaenda shule leo?", Walinzi wa Milanello(uwanja wa mazoezi) walikua na kila sababu ya kumuuliza iko wapi leseni yako ya udereva kabla ya kumruhusu kuingia ila unajua ni nini kilitokea? Ni hiki... Aliposimama uwanjani kwa mara ya kwanza niliskia kwaya na tarumbeta kutoka mbinguni kweli Kaka alikua ni Genius alieteremshwa kutoka mbinguni asante Mungu. Alipogusa tu mpira alikua na uwezo wa ajabu niliacha kuongea maana hakuna neno la kuelezea hisia zangu, hakuna neno kwenye kamusi linaloweza kuelezea ni nini niliona. Nilimpenda sana Kaka, kweli nilimpenda, sana, Aliweka chini mewani yake akavaa tracksuit na akawa kitu ambacho sikutegemea "mchezaji mwenye viwango vya dunia". Hayo ni Maneno aliyoandika Carlo Ancelotti kwenye kitabu chake "The beautiful Game of an Ordinary Genius", akielezea nini kilitokea alipokua kocha wa Ac Milan na walipomsajili Ricardo Izecson dos Santos Leite maarufu Ricardo Kaka.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·552 Views
  • DOUBLE AGENTS NGULI WANNE KUWAHI KUTOKEA KATIKA ULIMWENGU WA UJASUSI

    Mustakabali wa taifa lolote lile hutegemea pamoja na mambo mengine mifumo ya ulinzi, kwani hii ndio nguzo mhimu katika kuhakikisha ustawi wa maslahi ya taifa husika

    Ni kwa msingi huo basi mataifa yote duniani yameunda vyombo tofauti tofauti vya ulinzi mojawapo ikiwemo idara za ujajusi, mifano ipo mingi, CIA, M16, BND, MOSSAD, TISS n.k!

    Lakini kuwa na taasisi au vyombo hivyo vinahiyaji nguvu kazi, nguvu kazi hii sharti iwe yenye weledi na uzalendo wa kutukuka, kwani kazi wanayoifanya ni kazi nyeti mno na inayozungukwa na mambo mengi sana, hivyo kuteleza kwa namna yoyote ile basi kunaacha madhara makubwa mno! Na kiukweli wapo walioteleza na kuleta madhara yasiyoelezeka, sasa Leo nimeona tuangalie kwa ufupi baadhi ya wanausalama walioteleza na kujikuta walitumia pande mbili au zaidi maarufu kwa jina la *DOUBLE AGENT*

    *Lakini kwanza kabisa double agent ni nani?*

    Tunaweza tukasema ni afisa usalama wa tasisis au serikali ambaye amepewa majukumuu ya kuichunguza taasisi au nchi nyingine lakini wakati huo huo anakuwa tena anafanya kazi hiyo hiyo kwa ajiri ya taasisi au nchi anayopaswa kuichunguza dhidi ya taasisi au nchi iliyomtuma! Wengi wanasem double agent anaweza kuwa matokeo ya tamaa ya pesa, kulazimishwa( baada ya kutishiwa kufanyiwa kitu kibaya), mapenzi tu, yaani mtu anapenda tu kuwa double agent, kupandikizwa kwa makusudi( marekani wamefaidika sana na aina hii hasa Mashariki ya kati) au inaweza kuwa ni sababu ya mitazamo…

    Hawa wafuatao ni baadhi ya double agents nguli kuwahi kutokea na balaa

    *Human Khalid Al-Balawi*

    Huyu jamaa alikuwa daktari kitaaluma na alikuwa raia wa Jordan, alikamatwa na mamlaka za Jordan kipindi akiwa mwanafunzi kwenye chuo kikuu cha Isntanbul nchini Uturuki baada ya kuonekana akiwa na muelekeo wa misimamamo mikali, inasemekana baadae CIA waliingilia na kumshawishi awe double agent kwa ahadi ya kusamehewa. Jamaa alikubali na CIA wakamuandaa kikamilifu kwa kazi hiyo ambapo baada ya kuiva wakampeleka Pakistan na Afghanistan na kumpa jukumuu la kufuatilia nyendo na shughuli za alqaida nchini humo.

    Human aliifanya kazi hiyo kwa uaminifu mkubwa mno na akafanikiwa kuwashawishi CIA ambao walionekana kumwamini 100%. Kumbe hawakujua kuwa aliqaida walikuwa tayari wamembadilisha na alikuwa akifanya nao kazi.

    Siku moja akawaeleza kuwa alikuwa na taarifa muhimu kuhusu kiongozi wa juu wa alqaida bwana Ayman- Al-Zawahili na akawapa masharti kuwa angependa taarifa hizo azifikishe kwa viongozi wakuu wa CIA katika eneo hilo, kwakuwa walikuwa wanamtafuta sana Zawahili hawakusita kumkubalia na kumuagiza afike kwenye Ofisi za CIA eneo la Khost Afghanistan, Khalid alifika kwa kuchelewa na kutokana na kimuhe muhe cha taarifa waliyokuwa wanakwenda kuipokea basi wakasahau hadi kumkagua, kumbe jamaa alikuwa amevaa mabomu, baada ya kufika ndani kwa wakubwa jamaa alijilipua na kuua maafisa kadhaa wa ngazi za juu wa CIA katika eneo hilo.

    *Arthur Owens*

    Arthur alikuwa mwingereza kutoka kisiwa cha Wales na kabla ya vita ya dunia ya pili alikuwa akifanya kazi kama mkandarasi na alikuwa akifanya serikali zote mbili, Ujerumani na England, baada ya vita kuanza aliajiriwa kama mhandisi kwenye meli vita za England akifanya kazi kama fundi betri, baadae Wajerumani walianza kumuomba awape taarifa hasa kuhusu meli vita za England na yeye bila hiana akifanya kazi hiyo, baadae alijiunga nao rasmi na akawa anafanya kazi nao huku pesa na wanawake wazuri yakiwa ndo malipo kwa kazi yake hiyo tukufu.

    Baadae alirudi England na kujipeleka moja kwa moja kwa M15 na kuwaeleza ukweli wake na wajerumani, M16 walimpokea na kumtumia ambapo aliwasaidia kufichua zaidi maofisa 120 wa kijeruman nchini England na wakamtumia kuwalisha Wajerumani hao habari za uongo na zile zisixokuwa na athari kubwa kwao.

    Mwaka 1941 Arthur na mwenzake mmoja walikamatwa na wajerumani lakini cha ajabu mwenzake alinyongwa huku yeye akiachwa hali iliyowatia wasiwasi England na alivyorudi walimkamata na kumtia kolokoloni hadi baada ya vita, baadae aliwalazimisha England wamlipe fedha kwa maadai ya kumfunga bila makosa na kama watagoma basi ataweka hadharani kila kitu, England walinywea na hadi anakufa hakuwahi kusema chochote.

    *Kim Philby*

    Kim Philby alikuwa ni afisa wa idara ya usalama ya England, yeye na wenzake wanne walitengeza a spy ring iliyopewa jina la the Combridge five, na wakifanya kazi kwa niaba ya KGB, ni kipindi ambacho wote watano walikuwa wakisoma chuoni hapo, wenzake walikuwa ni pamoja na Donald MacLean, Guy borguess na Anthony Brunt ambapo mtu wa tano kwenye kundi hilo hadi Leo hajawahi kujulikana! Kimsingi Borguess ndiye aliyemsajili Kim na wakati huyo tayari yeye alikuwa ni double agent.

    Kilichomsukuma Kim ilikuwa ni imani yake katika falsafa za kijamaa, pamoja na kuwa double agent lakini Kim anasemwa kama mtu aliyefanya kazi kwa weledi mkubwa sana na alipata kutunukiwa nishani kadhaa kwa utumishi uliotukuka kabla ya kuja kumgundua kuwa alikuwa akifanya kazi na KGB, wakati wenzake wanakamatwa yeye alikuwa ameshaacha kazi na alikuwa Lebanon na hakurudi tena England Bali aliekea Jamhuri ya Usovieti ambako alipewa kazi kwenye idara kadhaa za ulinzi, alifariki mwaka 1988 akiwa huko huko Usovieti, Kim aliandika kitabu alichokipa jina la *My secret war* akieleza namna alivyopambana na ubepari.

    *Juan Pujol Garsia*

    Garsia alikuwa mhisipania ambaye maisha yake yalionekana kutokua na muelekeo kwani kwenye umri wa miaka 32 alikuwa ameshindwa karibia kila kitu, shule, biashara na hata familia, vyote alikuwa amejaribu na vikamshinda.

    Baadae wakati wa vita kuu ya pili ya dunia aliamua kwenda kuomba kazi kwenye idara za usalama za England na Marekani lakini aligonga mwamba kwa madai mtu ambaye hakuwa na uwezo hata wa kufuga kuku angeweje kufanya kazi nyeti kama hii tena katika wakati tete. Baada ya kukataliwa akaona isiwe taabu akaenda zake kwa Wajerumani na kujifanya mmoja wa wanazi kindakindaki wa Hitler, manazi baadae walimuamini na kumpa kazi ambapo walimpangia kwenda England! Alielekea huko akipitia Porto Ureno na alianza kazi kwa kukusanya habari kwenye magazeti na redio, baadae alianza kupiga hatua kwa kusajili watu mhimu kutoka wazara ya habari na mawasiliano pamoja na masekretari kwenye wizara mbalimbali, baadae pia alifanikiwa kuingia hadi jeshini na jusajili watu huko.

    Garsia alikuja kuumbuliwa na double agent wa kijerumani ambaye aliwatonya England juu ya uwepo wake nchini humo.

    Baada ya kubumbuluka Garsia akijipeleka mwenyewe kwa M15 ambapo walikubali kuendelea kutumia mara hii wakimtumia kuwalisha habari za uongo.

    Garsia anakumbukwa sana kutokana na kazi tukufu aliyoifanya wakati majeshi ya muungano wa England, Canada, Marekani na baadhi ya wanajeshi wa Ufaransa yalipoanza oparesheni ya kukomboa maeneo yaliyokuwa yamekamatwa na Ujerumani na hasa katika uvamizi wa eneo la Normandy, baada ya wanajeshi wa muungano kuelekea katika eneo hilo wajerumani walipata intelejensia na wakawa wametuma vikosi kwenda kupambana na majeshi ya muungano huku vikosi vingine vikiwekwa tayari nchini ubelgiji, lakini Garsia kwa ujasiri wa hali ya juu akamtumia telegraphy na kumwambia hakukuwa na mashambulizi yoyote katika eneo hilo na kwamba habari alizokuwa amepewa Hitler ulikuwa ni uongo, kwakuwa Hitler alikuwa anamuamini sana basi akaiamini taarifa hii na akaviamrisha vikosi vyake vilivyokuwa njiani kurejea na vile vilivyokuwa ubelgiji kuendelea kubaki.

    Wengi wanachukulia hatua hii kama mwanzo wa majeshi ya muungano kuanza kujizatiti kwani hadi hapo Ujerumani ilikuwa tayari imekamata karibu ulaya nzima na ndio maana Garsia anachukuliwa kama double agent aliyefanya kazi ya kutukuka, lakini pia anatajwa kama double agent aliyetunukiwa tunzo nyingi mno kutoka pande zote yaani Ujerumani na England, baada ya vita Garsia alikwenda zake Amerika kusini ambapo alifungua maktaba na kumalizia maisha yake huko.

    OUR MOTTO
    ========
    KIJANA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USITUMIKE VIBAYA KUICHAFUA NCHI YAKO.
    DOUBLE AGENTS NGULI WANNE KUWAHI KUTOKEA KATIKA ULIMWENGU WA UJASUSI Mustakabali wa taifa lolote lile hutegemea pamoja na mambo mengine mifumo ya ulinzi, kwani hii ndio nguzo mhimu katika kuhakikisha ustawi wa maslahi ya taifa husika Ni kwa msingi huo basi mataifa yote duniani yameunda vyombo tofauti tofauti vya ulinzi mojawapo ikiwemo idara za ujajusi, mifano ipo mingi, CIA, M16, BND, MOSSAD, TISS n.k! Lakini kuwa na taasisi au vyombo hivyo vinahiyaji nguvu kazi, nguvu kazi hii sharti iwe yenye weledi na uzalendo wa kutukuka, kwani kazi wanayoifanya ni kazi nyeti mno na inayozungukwa na mambo mengi sana, hivyo kuteleza kwa namna yoyote ile basi kunaacha madhara makubwa mno! Na kiukweli wapo walioteleza na kuleta madhara yasiyoelezeka, sasa Leo nimeona tuangalie kwa ufupi baadhi ya wanausalama walioteleza na kujikuta walitumia pande mbili au zaidi maarufu kwa jina la *DOUBLE AGENT* *Lakini kwanza kabisa double agent ni nani?* Tunaweza tukasema ni afisa usalama wa tasisis au serikali ambaye amepewa majukumuu ya kuichunguza taasisi au nchi nyingine lakini wakati huo huo anakuwa tena anafanya kazi hiyo hiyo kwa ajiri ya taasisi au nchi anayopaswa kuichunguza dhidi ya taasisi au nchi iliyomtuma! Wengi wanasem double agent anaweza kuwa matokeo ya tamaa ya pesa, kulazimishwa( baada ya kutishiwa kufanyiwa kitu kibaya), mapenzi tu, yaani mtu anapenda tu kuwa double agent, kupandikizwa kwa makusudi( marekani wamefaidika sana na aina hii hasa Mashariki ya kati) au inaweza kuwa ni sababu ya mitazamo… Hawa wafuatao ni baadhi ya double agents nguli kuwahi kutokea na balaa *Human Khalid Al-Balawi* Huyu jamaa alikuwa daktari kitaaluma na alikuwa raia wa Jordan, alikamatwa na mamlaka za Jordan kipindi akiwa mwanafunzi kwenye chuo kikuu cha Isntanbul nchini Uturuki baada ya kuonekana akiwa na muelekeo wa misimamamo mikali, inasemekana baadae CIA waliingilia na kumshawishi awe double agent kwa ahadi ya kusamehewa. Jamaa alikubali na CIA wakamuandaa kikamilifu kwa kazi hiyo ambapo baada ya kuiva wakampeleka Pakistan na Afghanistan na kumpa jukumuu la kufuatilia nyendo na shughuli za alqaida nchini humo. Human aliifanya kazi hiyo kwa uaminifu mkubwa mno na akafanikiwa kuwashawishi CIA ambao walionekana kumwamini 100%. Kumbe hawakujua kuwa aliqaida walikuwa tayari wamembadilisha na alikuwa akifanya nao kazi. Siku moja akawaeleza kuwa alikuwa na taarifa muhimu kuhusu kiongozi wa juu wa alqaida bwana Ayman- Al-Zawahili na akawapa masharti kuwa angependa taarifa hizo azifikishe kwa viongozi wakuu wa CIA katika eneo hilo, kwakuwa walikuwa wanamtafuta sana Zawahili hawakusita kumkubalia na kumuagiza afike kwenye Ofisi za CIA eneo la Khost Afghanistan, Khalid alifika kwa kuchelewa na kutokana na kimuhe muhe cha taarifa waliyokuwa wanakwenda kuipokea basi wakasahau hadi kumkagua, kumbe jamaa alikuwa amevaa mabomu, baada ya kufika ndani kwa wakubwa jamaa alijilipua na kuua maafisa kadhaa wa ngazi za juu wa CIA katika eneo hilo. *Arthur Owens* Arthur alikuwa mwingereza kutoka kisiwa cha Wales na kabla ya vita ya dunia ya pili alikuwa akifanya kazi kama mkandarasi na alikuwa akifanya serikali zote mbili, Ujerumani na England, baada ya vita kuanza aliajiriwa kama mhandisi kwenye meli vita za England akifanya kazi kama fundi betri, baadae Wajerumani walianza kumuomba awape taarifa hasa kuhusu meli vita za England na yeye bila hiana akifanya kazi hiyo, baadae alijiunga nao rasmi na akawa anafanya kazi nao huku pesa na wanawake wazuri yakiwa ndo malipo kwa kazi yake hiyo tukufu. Baadae alirudi England na kujipeleka moja kwa moja kwa M15 na kuwaeleza ukweli wake na wajerumani, M16 walimpokea na kumtumia ambapo aliwasaidia kufichua zaidi maofisa 120 wa kijeruman nchini England na wakamtumia kuwalisha Wajerumani hao habari za uongo na zile zisixokuwa na athari kubwa kwao. Mwaka 1941 Arthur na mwenzake mmoja walikamatwa na wajerumani lakini cha ajabu mwenzake alinyongwa huku yeye akiachwa hali iliyowatia wasiwasi England na alivyorudi walimkamata na kumtia kolokoloni hadi baada ya vita, baadae aliwalazimisha England wamlipe fedha kwa maadai ya kumfunga bila makosa na kama watagoma basi ataweka hadharani kila kitu, England walinywea na hadi anakufa hakuwahi kusema chochote. *Kim Philby* Kim Philby alikuwa ni afisa wa idara ya usalama ya England, yeye na wenzake wanne walitengeza a spy ring iliyopewa jina la the Combridge five, na wakifanya kazi kwa niaba ya KGB, ni kipindi ambacho wote watano walikuwa wakisoma chuoni hapo, wenzake walikuwa ni pamoja na Donald MacLean, Guy borguess na Anthony Brunt ambapo mtu wa tano kwenye kundi hilo hadi Leo hajawahi kujulikana! Kimsingi Borguess ndiye aliyemsajili Kim na wakati huyo tayari yeye alikuwa ni double agent. Kilichomsukuma Kim ilikuwa ni imani yake katika falsafa za kijamaa, pamoja na kuwa double agent lakini Kim anasemwa kama mtu aliyefanya kazi kwa weledi mkubwa sana na alipata kutunukiwa nishani kadhaa kwa utumishi uliotukuka kabla ya kuja kumgundua kuwa alikuwa akifanya kazi na KGB, wakati wenzake wanakamatwa yeye alikuwa ameshaacha kazi na alikuwa Lebanon na hakurudi tena England Bali aliekea Jamhuri ya Usovieti ambako alipewa kazi kwenye idara kadhaa za ulinzi, alifariki mwaka 1988 akiwa huko huko Usovieti, Kim aliandika kitabu alichokipa jina la *My secret war* akieleza namna alivyopambana na ubepari. *Juan Pujol Garsia* Garsia alikuwa mhisipania ambaye maisha yake yalionekana kutokua na muelekeo kwani kwenye umri wa miaka 32 alikuwa ameshindwa karibia kila kitu, shule, biashara na hata familia, vyote alikuwa amejaribu na vikamshinda. Baadae wakati wa vita kuu ya pili ya dunia aliamua kwenda kuomba kazi kwenye idara za usalama za England na Marekani lakini aligonga mwamba kwa madai mtu ambaye hakuwa na uwezo hata wa kufuga kuku angeweje kufanya kazi nyeti kama hii tena katika wakati tete. Baada ya kukataliwa akaona isiwe taabu akaenda zake kwa Wajerumani na kujifanya mmoja wa wanazi kindakindaki wa Hitler, manazi baadae walimuamini na kumpa kazi ambapo walimpangia kwenda England! Alielekea huko akipitia Porto Ureno na alianza kazi kwa kukusanya habari kwenye magazeti na redio, baadae alianza kupiga hatua kwa kusajili watu mhimu kutoka wazara ya habari na mawasiliano pamoja na masekretari kwenye wizara mbalimbali, baadae pia alifanikiwa kuingia hadi jeshini na jusajili watu huko. Garsia alikuja kuumbuliwa na double agent wa kijerumani ambaye aliwatonya England juu ya uwepo wake nchini humo. Baada ya kubumbuluka Garsia akijipeleka mwenyewe kwa M15 ambapo walikubali kuendelea kutumia mara hii wakimtumia kuwalisha habari za uongo. Garsia anakumbukwa sana kutokana na kazi tukufu aliyoifanya wakati majeshi ya muungano wa England, Canada, Marekani na baadhi ya wanajeshi wa Ufaransa yalipoanza oparesheni ya kukomboa maeneo yaliyokuwa yamekamatwa na Ujerumani na hasa katika uvamizi wa eneo la Normandy, baada ya wanajeshi wa muungano kuelekea katika eneo hilo wajerumani walipata intelejensia na wakawa wametuma vikosi kwenda kupambana na majeshi ya muungano huku vikosi vingine vikiwekwa tayari nchini ubelgiji, lakini Garsia kwa ujasiri wa hali ya juu akamtumia telegraphy na kumwambia hakukuwa na mashambulizi yoyote katika eneo hilo na kwamba habari alizokuwa amepewa Hitler ulikuwa ni uongo, kwakuwa Hitler alikuwa anamuamini sana basi akaiamini taarifa hii na akaviamrisha vikosi vyake vilivyokuwa njiani kurejea na vile vilivyokuwa ubelgiji kuendelea kubaki. Wengi wanachukulia hatua hii kama mwanzo wa majeshi ya muungano kuanza kujizatiti kwani hadi hapo Ujerumani ilikuwa tayari imekamata karibu ulaya nzima na ndio maana Garsia anachukuliwa kama double agent aliyefanya kazi ya kutukuka, lakini pia anatajwa kama double agent aliyetunukiwa tunzo nyingi mno kutoka pande zote yaani Ujerumani na England, baada ya vita Garsia alikwenda zake Amerika kusini ambapo alifungua maktaba na kumalizia maisha yake huko. OUR MOTTO ======== KIJANA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USITUMIKE VIBAYA KUICHAFUA NCHI YAKO.
    0 Comments ·0 Shares ·707 Views
  • HIVI UNAJUA: Facebook ni huduma ya mitandao ya kijamii ambayo iliundwa na mwanafunzi wa Harvard Mark Zuckerberg mwaka wa 2004. Hapo awali iliundwa kama chombo cha mtandao kwa wanafunzi wa Harvard, ilienea haraka kwa shule nyingine na hatimaye ilifunguliwa kwa umma mwaka wa 2006. Facebook sasa, kwa sana. ukingo mpana, mtandao mkubwa zaidi wa kijamii duniani kote . Kufikia robo ya tatu ya 2021, Facebook ilikuwa na zaidi ya watumiaji bilioni 2.9 wanaofanya kazi kila mwezi na jumla ya watumiaji bilioni 3.58 wanaopata bidhaa zozote za msingi za kampuni hiyo Facebook, WhatsApp, Instagram na Messenger kila mwezi.
    HIVI UNAJUA: Facebook ni huduma ya mitandao ya kijamii ambayo iliundwa na mwanafunzi wa Harvard Mark Zuckerberg mwaka wa 2004. Hapo awali iliundwa kama chombo cha mtandao kwa wanafunzi wa Harvard, ilienea haraka kwa shule nyingine na hatimaye ilifunguliwa kwa umma mwaka wa 2006. Facebook sasa, kwa sana. ukingo mpana, mtandao mkubwa zaidi wa kijamii duniani kote . Kufikia robo ya tatu ya 2021, Facebook ilikuwa na zaidi ya watumiaji bilioni 2.9 wanaofanya kazi kila mwezi na jumla ya watumiaji bilioni 3.58 wanaopata bidhaa zozote za msingi za kampuni hiyo Facebook, WhatsApp, Instagram na Messenger kila mwezi.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·341 Views
  • IFAHAMU SHULE YA BEI KUBWA ZAIDI DUNIANI.

    Shule ya bei kubwa zaidi Duniani inaitwa Instut Le Rosey ambayo ipo Switzerland, ada ya Mwanafunzi mmoja kwa mwaka sio chini ya USD 117,434 ambayo kwa Tsh. ni kama Milioni 272 Unaambiwa ukiachia mazingira mazuri.

    Shule ipo karibu na Ziwa, ina madarasa 50, Maabara 8 za Sayansi, Theater na kila asubuhi Wanafunzi hupata breki ya kula chocolate

    Ukiacha masomo, Wanafunzi hufundishwa kucheza golf, kutumia farasi, wanacho chumba maalum kwa ajili ya muziki na studio kwa ajili ya sanaa nyingine Wanafunzi wanaweza kujifunza kwa lugha mbili ambazo ni Kiingereza na Kifaransa ambapo pamoja na kwamba ni Shule ya bei ghali lakini wanausambaza upendo mwingi kwa Afrika ambako wamejenga Shule kwenye nchi ya Mali
    IFAHAMU SHULE YA BEI KUBWA ZAIDI DUNIANI. Shule ya bei kubwa zaidi Duniani inaitwa Instut Le Rosey ambayo ipo Switzerland, ada ya Mwanafunzi mmoja kwa mwaka sio chini ya USD 117,434 ambayo kwa Tsh. ni kama Milioni 272 Unaambiwa ukiachia mazingira mazuri. Shule ipo karibu na Ziwa, ina madarasa 50, Maabara 8 za Sayansi, Theater na kila asubuhi Wanafunzi hupata breki ya kula chocolate Ukiacha masomo, Wanafunzi hufundishwa kucheza golf, kutumia farasi, wanacho chumba maalum kwa ajili ya muziki na studio kwa ajili ya sanaa nyingine Wanafunzi wanaweza kujifunza kwa lugha mbili ambazo ni Kiingereza na Kifaransa ambapo pamoja na kwamba ni Shule ya bei ghali lakini wanausambaza upendo mwingi kwa Afrika ambako wamejenga Shule kwenye nchi ya Mali
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·470 Views
  • Jamani siyo mm ni jibu la mwanafunzi
    Jamani siyo mm🙏🙏 ni jibu la mwanafunzi👇
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·120 Views
  • MWALIMU NA MWANAFUNZI.

    Mtoto: Mwalimu mimi nataka nisome darasa la nne kwani hili la3 halinifai.

    Mwalimu: Kwa nini unasema hivyo?

    Mtoto: Nina akili…

    Basi mwalimu akamueleza mkuu wa shule na mkuu kaitisha interview kwa dogo. Maswali ni haya….

    Mwalimu: Kwenye ndege kuna matofali 20 tukitoa moja tukalidondosha chini yatabaki mangapi?

    Dogo: Yatabaki 19.

    Mwalimu: Nipe hatua za kumuweka tembo kwenye friji.

    Dogo: Unafungua friji unamuweka tembo kisha unafunga.

    Mwalimu: Nipe hatua za kumuweka nyani kwenye friji.

    Dogo: Unafungua friji unamtoa tembo ulemuweka..unamueka nyani kisha unafunga friji.

    Mwalimu: Kuna sherehe ya siku ya kuzaliwa kwa simba, wanyama wote wameenda kasoro mmoja. Ni nani na kwa nini?

    Dogo: Ni nyani kwa sababu tumemuweka kwenye friji.

    Mwalimu: Bibi kizee amevuka mto unaokuwaga na mamba na viboko wakali, aliwezaje?

    Dogo: Aliweza kwani mamba na viboko nao walienda kwenye sherehe ya kuzaliwa kwa simba.

    Mwalimu: Ingawa bibi kizee alivuka mto, baadae alikufa. Unadhani ni kwanini alikufa?

    Dogo: Alidondokewa na lile tofali tulotoa kwenye ndege na kutupa chini.

    Mwalimu mkuu: Huyu dogo akasome chuo kikuu….


    NIMEAMUA KUONDOKA NAE ATANIFAHA SANA
    MWALIMU NA MWANAFUNZI. Mtoto: Mwalimu mimi nataka nisome darasa la nne kwani hili la3 halinifai. Mwalimu: Kwa nini unasema hivyo? Mtoto: Nina akili… Basi mwalimu akamueleza mkuu wa shule na mkuu kaitisha interview kwa dogo. Maswali ni haya…. Mwalimu: Kwenye ndege kuna matofali 20 tukitoa moja tukalidondosha chini yatabaki mangapi? Dogo: Yatabaki 19. Mwalimu: Nipe hatua za kumuweka tembo kwenye friji. Dogo: Unafungua friji unamuweka tembo kisha unafunga. Mwalimu: Nipe hatua za kumuweka nyani kwenye friji. Dogo: Unafungua friji unamtoa tembo ulemuweka..unamueka nyani kisha unafunga friji. Mwalimu: Kuna sherehe ya siku ya kuzaliwa kwa simba, wanyama wote wameenda kasoro mmoja. Ni nani na kwa nini? Dogo: Ni nyani kwa sababu tumemuweka kwenye friji. Mwalimu: Bibi kizee amevuka mto unaokuwaga na mamba na viboko wakali, aliwezaje? Dogo: Aliweza kwani mamba na viboko nao walienda kwenye sherehe ya kuzaliwa kwa simba. Mwalimu: Ingawa bibi kizee alivuka mto, baadae alikufa. Unadhani ni kwanini alikufa? Dogo: Alidondokewa na lile tofali tulotoa kwenye ndege na kutupa chini. Mwalimu mkuu: Huyu dogo akasome chuo kikuu…. 😆😆😆😆😆😆😆😆 😁😁😁😂😂😂NIMEAMUA KUONDOKA NAE ATANIFAHA SANA
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·284 Views
  • Usikubali kuanguka na kuendelea kukaa chini huku una UWEZO mkubwa ndani yako. Hakuna aliyewahi kufanikiwa moja kwa moja tena pasipo kupitia maanguko mengi. Kila mtu unayemwona amefanikiwa leo hii ni matokeo ya kuwa chini mara nyingi alikokutana nako.

    Tofauti ni kuwa, watu waliofanikiwa wakianguka mahali hawachelewi kuinuka na wanatumia anguko lao kama sehemu ya kujiboresha zaidi kwenye safari ya maisha yao. Hii ni tofauti sana na watu wanaoshindwa katika maisha, wao wakianguka wanabaki chini wakisubiri watu wengine wawainue au kuwatia moyo, wakilia na kusononeka kwamba kwa nini wameanguka. Nataka nikuambie hata mwanafunzi wa Yesu aliyejulikana kwa jina la Petro aliwahi kuanguka kwa kuamkana Yesu mara tatu lakini alipogundua amekosea, aliinuka akatubu kisha akaendelea na safari yake dhidi ya kusudi aliloitiwa.

    Usikubali kuanguka kwenye eneo lolote kwenye maisha yako ukakubali kubaki chini pasipo kuinuka. Acha kubaki ulipo ukijilaumu na kujisemea mengi mabaya dhidi yako. Acha kuendelea kulaumu wengine kwa anguko lako. Kumbuka mwenye jukumu la maisha yako 100% ni wewe mwenyewe, hivyo inakupasa kuinuka binafsi hapo ulipo pasipo kusubiri kuinuliwa na mtu mwingine. Unahitaji KUJITIA NGUVU na kuinuka ili uweze kuifaata ndoto yako na kuifanikisha.

    Kama umeanguka kwenye masomo inuka na rudi shule tena kuendelea na masomo yako ili kufanya vizuri zaidi. Kama umeanguka kwenye biashara hakikisha unarudi kwenye biashara yako ili kuleta matokeo mapya yatakayobadilisha biashara yako. Usijikatie tamaa kwa sababu ya kushindwa mara moja. Kushindwa si kushindwa ila kukubali kushindwa ndio kushindwa. Inuka maana uwezo mkubwa wa kushinda upo ndani yako. Amini wewe ni mshindi.

    Believe It's Possible!

    #ishindotoyako
    Usikubali kuanguka na kuendelea kukaa chini huku una UWEZO mkubwa ndani yako. Hakuna aliyewahi kufanikiwa moja kwa moja tena pasipo kupitia maanguko mengi. Kila mtu unayemwona amefanikiwa leo hii ni matokeo ya kuwa chini mara nyingi alikokutana nako. Tofauti ni kuwa, watu waliofanikiwa wakianguka mahali hawachelewi kuinuka na wanatumia anguko lao kama sehemu ya kujiboresha zaidi kwenye safari ya maisha yao. Hii ni tofauti sana na watu wanaoshindwa katika maisha, wao wakianguka wanabaki chini wakisubiri watu wengine wawainue au kuwatia moyo, wakilia na kusononeka kwamba kwa nini wameanguka. Nataka nikuambie hata mwanafunzi wa Yesu aliyejulikana kwa jina la Petro aliwahi kuanguka kwa kuamkana Yesu mara tatu lakini alipogundua amekosea, aliinuka akatubu kisha akaendelea na safari yake dhidi ya kusudi aliloitiwa. Usikubali kuanguka kwenye eneo lolote kwenye maisha yako ukakubali kubaki chini pasipo kuinuka. Acha kubaki ulipo ukijilaumu na kujisemea mengi mabaya dhidi yako. Acha kuendelea kulaumu wengine kwa anguko lako. Kumbuka mwenye jukumu la maisha yako 100% ni wewe mwenyewe, hivyo inakupasa kuinuka binafsi hapo ulipo pasipo kusubiri kuinuliwa na mtu mwingine. Unahitaji KUJITIA NGUVU na kuinuka ili uweze kuifaata ndoto yako na kuifanikisha. Kama umeanguka kwenye masomo inuka na rudi shule tena kuendelea na masomo yako ili kufanya vizuri zaidi. Kama umeanguka kwenye biashara hakikisha unarudi kwenye biashara yako ili kuleta matokeo mapya yatakayobadilisha biashara yako. Usijikatie tamaa kwa sababu ya kushindwa mara moja. Kushindwa si kushindwa ila kukubali kushindwa ndio kushindwa. Inuka maana uwezo mkubwa wa kushinda upo ndani yako. Amini wewe ni mshindi. Believe It's Possible! #ishindotoyako
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·326 Views
  • Mwanafunzi akikutwa na simu, mpe aivunje mwenyewe. Itamuumiza sana, hatorudia tena
    Mwanafunzi akikutwa na simu, mpe aivunje mwenyewe. Itamuumiza sana, hatorudia tena
    Like
    Love
    6
    · 4 Comments ·0 Shares ·318 Views ·94
  • 🖥 Computer Kama Bunduki

    Mwanafunzi mwenye kipaji kutoka Thailand ametengeneza casing ya kipekee kwa ajili ya kompyuta yake ya michezo, inayofanana na bunduki ya kisasa ya mtafuta shabaha. Alikusanya mashine hii kwa ajili ya shindano la Cooler Master, ambapo washiriki wanashindania taji la casing ya kipekee zaidi.

    Ingawa sifa kamili za kompyuta hiyo hazijafichuliwa, inajulikana kuwa zina ubora wa juu kabisa. Mtengenezaji huyu ametumia $2700 (sawa na takriban TZS 6,345,000) kwa ajili ya kuunda Computer hii. Ikiwa atashinda shindano hilo, atapata zawadi ya $5000 (takriban TZS 11,750,000).

    #Hora_Tech
    #Computer #Thailand #mwanafunzi
    🖥 Computer Kama Bunduki 😱 Mwanafunzi mwenye kipaji kutoka Thailand ametengeneza casing ya kipekee kwa ajili ya kompyuta yake ya michezo, inayofanana na bunduki ya kisasa ya mtafuta shabaha. Alikusanya mashine hii kwa ajili ya shindano la Cooler Master, ambapo washiriki wanashindania taji la casing ya kipekee zaidi. 💾 Ingawa sifa kamili za kompyuta hiyo hazijafichuliwa, inajulikana kuwa zina ubora wa juu kabisa. Mtengenezaji huyu ametumia $2700 (sawa na takriban TZS 6,345,000) kwa ajili ya kuunda Computer hii. Ikiwa atashinda shindano hilo, atapata zawadi ya $5000 (takriban TZS 11,750,000). ➤ #Hora_Tech #Computer #Thailand #mwanafunzi
    Like
    Love
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·850 Views
  • Mwalimu Afurahi kukutana na MWANAFUNZI wake wa SEKONDARY!

    Dr. MWIGULU NCHMBA!

    Ambae alisoma Shule ya Sekondary ya Iliboru mwa 1994- 1997.
    Mwalimu Afurahi kukutana na MWANAFUNZI wake wa SEKONDARY! Dr. MWIGULU NCHMBA! Ambae alisoma Shule ya Sekondary ya Iliboru mwa 1994- 1997.
    Like
    1
    · 10 Comments ·0 Shares ·389 Views
  • TAFAKARI :

    Kulikuwa na Mwalimu mmoja aliyezoea kumchapa viboko mwanafunzi mmoja mchelewaji shuleni, Mwanafunzi huyo alikuwa ni mtoto wa kimasikini pia mpole sana na mwenye huruma na alikuwa akiishi eneo lenye umbali kiasi mpaka kufika shuleni, kwa hivyo Mwanafunzi yule takriban miaka 3 alikuwa akichelewa kipindi cha kwanza kila siku. Kwa hiyo siku ambazo Mwalimu huyo alikuwa na kipindi cha kwanza darasani kwao Mwanafunzi huyo alikuwa anachapwa kwanza kabla ya kuingia darasani. Hali hii iliendelea kwa muda mrefu, jambo la kushangaza wiki moja ilipita bila yule mwanafunzi kuonekana kabisa shuleni!

    Wiki ililoyofuata yule Mwanafunzi alifika shuleni mapema kabla ya Mwanafunzi mwingine yeyote. Mwalimu yule alishangaa sana alipomwona alifurahi sana alipoingia Darasani alimwita na kumsifia sana mbele ya Darasa kabla ya kumuuliza jambo lo lote.

    "Mwalimu akamwambia yule Mwanafunzi hebu simama akatii amri ya Mwalimu wake akasimama, Mwalimu akawaambia wanafunzi wenzake wampigie makofi kwa sababu leo kawa wa kwanza kufika shuleni. Mwalim akasema kumbe zile fimbo ninazomchapa zimesaidia sana eeeeenh?"

    Wanafunzi walipiga makofi huku wengine wakimcheka na kumdhihaki. Baada ya dakika kadhaa yule Mwanafunzi akamwomba Mwalimu ampe nafasi aseme jambo kidogo ili wapate kujua ni nini anataka kuwaelezea, Mwalimu akamruhusu huku akiwa amemkodolea macho haya tuambie.

    "Kwanza akawaomba radhi kwa kusema Mwalimu pamoja na wanafunzi wenzangu nyote kwa jumla, nakuombeni unisamehe iwapo nilikuwa nikiwaudhi kwa sababu siku zote nilizokuwa nikichelewa kufika shuleni nilikuwa namuuguza Mama yangu mzazi. Baba yangu alifariki kabla sijazaliwa, kwa hivyo sikujaaliwa kumuona nililelewa na Mama yangu tu naye alitengwa na ndugu kutokana na ufukara kwa hakika unyonge ni kitu kibaya sana simjui ndugu ye yote, Mama yangu alipopatwa na Maradhi tulimpeleka hospitalini Mimi ni jirani zetu lakini maradhi yake hayakuonekana. Akaruhusiwa kurudi nyumbani akiwa na Dawa za kutuliza maumivu tu." Kwa sababu hatukuwa na pesa sikuweza kumpeleka popote kwa vipimo zaidi."

    Mara akafuta machozi yaliyoanza kumtiririka kwa wingi mashavuni, na akasema kwa unyonge ewe Mwalimu wangu pamoja na wanafunzi wenzangu.

    "Kwa hivyo kila siku nilitakiwa kufanya usafi wa nyumba kuchota maji, kumsafisha Mama yangu pamoja na kumstiri, kumwandalia chakula chake kabla ya kuondoka kuja hapa shuleni na kazi zingine zote." Akanyamaza kidogo kwa uchungu."

    "Na sikitika kusema leo hii nimewahi kuja Shuleni kwa sababu Mama yangu alifariki wiki moja iliyopita ambayo sikuonekana shuleni nilikuwa nikimalizia msiba wa Mama yangu. Yote ndio mipango yake Mwenyezi Mungu kwa hiyo kilichokuwa kinanichelewesha kimeondoka ndio maana leo nimewahi kufika mapema shuleni."

    Hakuweza kuongea tena kutokana na uchungu, akakaa taratibu kitini huku akilia kwa kwikwi

    Hatimae Darasa zima nalo liligeuka mahala pa msiba kila mmoja akilia pamoja na Mwalimu wao, huku wakimpa pole na kumuomba msamaha kwa jinsi walivyokuwa wakimdhihaki. Naye akawaambia nimekusameheni kwa moyo safi kabisa.

    WITO:

    Msiharakishe kuadhibu wenzenu bila kuwapa nafasi ya kujieleza, sababu huwezi kujua jambo gani linalowasibu bila kuwapa fursa ya kujielezea au kukwambia ili upatikane ufumbuzi wa tatizo.

    Unapo muona mwenzako hayupo sawa kifikra, kiafya, au jambo lo lote muulize kwanza kabla ya kuanza kumshutumu.

    Tunamuomba Mwenyezi Mungu atujalie tuwe ni wenye kupendana, kuuliza na kusaidiana kwa kila jambo.
    TAFAKARI : Kulikuwa na Mwalimu mmoja aliyezoea kumchapa viboko mwanafunzi mmoja mchelewaji shuleni, Mwanafunzi huyo alikuwa ni mtoto wa kimasikini pia mpole sana na mwenye huruma na alikuwa akiishi eneo lenye umbali kiasi mpaka kufika shuleni, kwa hivyo Mwanafunzi yule takriban miaka 3 alikuwa akichelewa kipindi cha kwanza kila siku. Kwa hiyo siku ambazo Mwalimu huyo alikuwa na kipindi cha kwanza darasani kwao Mwanafunzi huyo alikuwa anachapwa kwanza kabla ya kuingia darasani. Hali hii iliendelea kwa muda mrefu, jambo la kushangaza wiki moja ilipita bila yule mwanafunzi kuonekana kabisa shuleni! Wiki ililoyofuata yule Mwanafunzi alifika shuleni mapema kabla ya Mwanafunzi mwingine yeyote. Mwalimu yule alishangaa sana alipomwona alifurahi sana alipoingia Darasani alimwita na kumsifia sana mbele ya Darasa kabla ya kumuuliza jambo lo lote. "Mwalimu akamwambia yule Mwanafunzi hebu simama akatii amri ya Mwalimu wake akasimama, Mwalimu akawaambia wanafunzi wenzake wampigie makofi kwa sababu leo kawa wa kwanza kufika shuleni. Mwalim akasema kumbe zile fimbo ninazomchapa zimesaidia sana eeeeenh?" Wanafunzi walipiga makofi huku wengine wakimcheka na kumdhihaki. Baada ya dakika kadhaa yule Mwanafunzi akamwomba Mwalimu ampe nafasi aseme jambo kidogo ili wapate kujua ni nini anataka kuwaelezea, Mwalimu akamruhusu huku akiwa amemkodolea macho haya tuambie. "Kwanza akawaomba radhi kwa kusema Mwalimu pamoja na wanafunzi wenzangu nyote kwa jumla, nakuombeni unisamehe iwapo nilikuwa nikiwaudhi kwa sababu siku zote nilizokuwa nikichelewa kufika shuleni nilikuwa namuuguza Mama yangu mzazi. Baba yangu alifariki kabla sijazaliwa, kwa hivyo sikujaaliwa kumuona nililelewa na Mama yangu tu naye alitengwa na ndugu kutokana na ufukara kwa hakika unyonge ni kitu kibaya sana simjui ndugu ye yote, Mama yangu alipopatwa na Maradhi tulimpeleka hospitalini Mimi ni jirani zetu lakini maradhi yake hayakuonekana. Akaruhusiwa kurudi nyumbani akiwa na Dawa za kutuliza maumivu tu." Kwa sababu hatukuwa na pesa sikuweza kumpeleka popote kwa vipimo zaidi." Mara akafuta machozi yaliyoanza kumtiririka kwa wingi mashavuni, na akasema kwa unyonge ewe Mwalimu wangu pamoja na wanafunzi wenzangu. "Kwa hivyo kila siku nilitakiwa kufanya usafi wa nyumba kuchota maji, kumsafisha Mama yangu pamoja na kumstiri, kumwandalia chakula chake kabla ya kuondoka kuja hapa shuleni na kazi zingine zote." Akanyamaza kidogo kwa uchungu." "Na sikitika kusema leo hii nimewahi kuja Shuleni kwa sababu Mama yangu alifariki wiki moja iliyopita ambayo sikuonekana shuleni nilikuwa nikimalizia msiba wa Mama yangu. Yote ndio mipango yake Mwenyezi Mungu kwa hiyo kilichokuwa kinanichelewesha kimeondoka ndio maana leo nimewahi kufika mapema shuleni." Hakuweza kuongea tena kutokana na uchungu, akakaa taratibu kitini huku akilia kwa kwikwi Hatimae Darasa zima nalo liligeuka mahala pa msiba kila mmoja akilia pamoja na Mwalimu wao, huku wakimpa pole na kumuomba msamaha kwa jinsi walivyokuwa wakimdhihaki. Naye akawaambia nimekusameheni kwa moyo safi kabisa. WITO: Msiharakishe kuadhibu wenzenu bila kuwapa nafasi ya kujieleza, sababu huwezi kujua jambo gani linalowasibu bila kuwapa fursa ya kujielezea au kukwambia ili upatikane ufumbuzi wa tatizo. Unapo muona mwenzako hayupo sawa kifikra, kiafya, au jambo lo lote muulize kwanza kabla ya kuanza kumshutumu. Tunamuomba Mwenyezi Mungu atujalie tuwe ni wenye kupendana, kuuliza na kusaidiana kwa kila jambo.
    Like
    3
    · 0 Comments ·0 Shares ·938 Views
  • KWAMFANO WEWE NDIO MWALIMU UNASIMAMIA MTIANI UKACHANA KARATASI YA MWANAFUNZI MMOJA NA WENGINE WOTE WALIOPO CHUMBA CHA MTIANI WAKACHANA NAZAKWAO WEWE KAMA MWALIMU UTAFANYAJE??
    KWAMFANO WEWE NDIO MWALIMU UNASIMAMIA MTIANI UKACHANA KARATASI YA MWANAFUNZI MMOJA NA WENGINE WOTE WALIOPO CHUMBA CHA MTIANI WAKACHANA NAZAKWAO WEWE KAMA MWALIMU UTAFANYAJE??
    Like
    Love
    2
    · 1 Comments ·0 Shares ·356 Views ·25
  • Daraja La Kifo | Majini ni washamba wa kamera kamera ya Samsung Galaxy S4 inapiga picha hadi mizimu

    Bidada anaitwa "Lina" ni Mwanafunzi wa chuo kikuu, amekuwa akivutiwa sana na hadithi ya daraja lililolaaniwa. akiwa na wanafunzi wezake wanafunga safari na kuelekea huko ili kuthibitisha kama ni kweri au ni polojo tu, Wanapowasili kijijini, wanaanza kupeleleza, sasa balaa ni kwamba majini yana onesha umwamba.. yana jidhibitisha kuwa yapo yenyewe.. wanakuja kugundua kuwa hadithi zinazoendelea ni kweli tena ni mbaya zaidi kuliko walivyosimuliwa,🫣 na wanajikuta wao ndio wamekuwa kwenye orodha ya chakura cha usiku huu wakiwindwa na vijukuu vya shetani mwenyewe "Rusifa" Utamu na hofu kamili ya hii movie twende V.I.P Tukatizame

    Telegram 👇🏻👇🏻
    https://t.me/HFilam_Official/1416
    Daraja La Kifo 👹| Majini ni washamba wa kamera 👻📸kamera ya Samsung Galaxy S4 inapiga picha hadi mizimu Bidada anaitwa "Lina" ni Mwanafunzi wa chuo kikuu, amekuwa akivutiwa sana na hadithi ya daraja lililolaaniwa.😳 akiwa na wanafunzi wezake wanafunga safari na kuelekea huko ili kuthibitisha kama ni kweri au ni polojo tu, Wanapowasili kijijini, wanaanza kupeleleza, sasa 😬balaa ni kwamba majini yana onesha umwamba.. yana jidhibitisha kuwa yapo🤡 yenyewe.. wanakuja kugundua kuwa hadithi zinazoendelea ni kweli tena ni mbaya zaidi kuliko walivyosimuliwa,🫣 na wanajikuta wao ndio wamekuwa kwenye orodha ya chakura cha usiku huu wakiwindwa na vijukuu vya shetani mwenyewe "😈Rusifa😈" Utamu na hofu kamili ya hii movie twende V.I.P Tukatizame Telegram 👇🏻👇🏻 https://t.me/HFilam_Official/1416
    Like
    Love
    4
    · 0 Comments ·0 Shares ·949 Views
  • KISWAHILI KIDATO CHA KWANZA

    Tsh15000
    Hiki ni kitabu ambacho kitamsaidia mwanafunzi wa kidato cha kwanza kujifunza kiswahili kwa ufasaha zaidi, pia hata kufaulu katika mitihani yake kwa kiwango cha juu.
    Hiki ni kitabu ambacho kitamsaidia mwanafunzi wa kidato cha kwanza kujifunza kiswahili kwa ufasaha zaidi, pia hata kufaulu katika mitihani yake kwa kiwango cha juu.
    In stock ·New
    MZUMBE
    Like
    Love
    4
    · 1 Comments ·1 Shares ·1K Views