Nchi ya Uchina imeweka rekodi mpya ya Dunia kwa kutangaza na kuliwasha "Jua lake Bandia" kwa zaidi ya dakika (17) lenye joto la (milioni 100°C): Hii ni rekodi mpya ya Dunia baada ya kuvunja rekodi ya awali ya sekunde (403) iliyotokea mwaka 2023.
Ufanisi huu ulifanywa na Watafiti kutoka Taasisi ya Fizikia ya Plasmas (ASIPP) na Taasisi ya Sayansi za Fizikia kutoka Hefei iliyopo katika jimbo la Anhui Nchini China.
"Reactor" ya EAST ni sehemu ya jitihada zinazofanywa na Wanasayansi wa Kichina kukuza nishati ya "fusion". Hatua hii inawakilisha maendeleo makubwa katika utafiti wa nishati ya "fusion" ambapo kigezo cha sekunde 1000 cha kufanya kazi kinachukuliwa kama kipimo cha uwezo wa kuitumia.
Lengo kuu la mradi huu ni kutoa chanzo cha nishati safi kisichokuwa na kikomo na kusaidia uchunguzi wa anga za nje za mfumo wa jua.
Nchi ya Uchina 🇨🇳 imeweka rekodi mpya ya Dunia kwa kutangaza na kuliwasha "Jua lake Bandia" kwa zaidi ya dakika (17) lenye joto la (milioni 100°C): Hii ni rekodi mpya ya Dunia baada ya kuvunja rekodi ya awali ya sekunde (403) iliyotokea mwaka 2023.