• #PART6

    Alipoingia Ikulu Kabila alifuta jina Zaire na kurudisha Congo (Jamhuri ya kidemokrasia). Baadae alifikiria kuiachia Kivu, eneo lenye utajiri mkubwa wa madini adimu duniani. Akasema "to hell with Lemera Agreement" akautupilia mbali mkataba wa Lemera. Akasema Kivu itabaki Congo na madini ya Kivu yatajenga Congo. Full stop. Ashakuwa Rais utamfanya nini?

    Kagame hakuamini macho yake. Alishawaza jinsi ambavyo Rwanda ingekuwa Dubai ya Afrika kwa rasilimali za Congo. Lakini ghafla aligeukwa na mshirika wake Laurent Désiré Kabila. Akamfuata "Godfather" wake mzee Museveni. Mzee akasema kama katugeuka tumpige. Wakatafuta kikundi cha Waasi wakiunge mkono. Wakapata Rassemblement Congolais pour la Démocratie (RCD), kilichoongozwa na Jenerali Ernest Wamba dia Wamba. Kikundi kikapewa silaha na fedha kikaanza kumshughulikia Kabila.

    RCD ikaanza kuchapana na jeshi la Congo (FARDC) ikiwa na backup ya Rwanda na Uganda. Vita vikapamba moto. Rwanda na Uganda nao wakaingiza majeshi Congo kusaidia waasi wa RCD. Kabila akaona anazidiwa, akaomba msaada Angola na Chad. Nchi hizo zikaleta vikosi vyake Congo. Mapigano yakawa makali sana. Eneo la mashariki mwa Congo likageuka machinjioni. Watu walikufa kwa wingi, mpaka maiti zikatapakaa barabarani bila kuzikwa, zikawa zinadonolewa na ndege.

    Hii iliitwa Vita ya Pili ya Congo (1998–2002), iliyokua mbaya zaidi katika historia ya vita zote Afrika. Imebatizwa jina "Vita Kuu ya Afrika". Inakadiriwa watu laki tano walipoteza maisha huku mamilioni wakikimbia nchi. Mapigano yaliendelea, huku vikosi vya Rwanda na Uganda vikichota madini. Katikati ya mapigano mgongano wa kimaslahi ukajitokeza.

    Jasin Stearns, katika kitabu chake Dancing in the Glory of Monsters, anasema Kagame alishindwa kuelewana na "godfather" wake Museveni juu ya mgawanyo wa mali. Hali hiyo ilifanya kikundi cha RCD kipasuke na kuzaliwa vikundi viwili. Cha kwanza kikajiita RCD-Goma kikiongozwa na Kanali Emile Ilunga (hiki kilisaidiwa na Rwanda) na cha pili kikajiita RCD-Kisangani, kikiongozwa na Jenerali Mbusa Nyamwisi (kikisaidiwa na Uganda).
    (Malisa GJ)

    #PART6 Alipoingia Ikulu Kabila alifuta jina Zaire na kurudisha Congo (Jamhuri ya kidemokrasia). Baadae alifikiria kuiachia Kivu, eneo lenye utajiri mkubwa wa madini adimu duniani. Akasema "to hell with Lemera Agreement" akautupilia mbali mkataba wa Lemera. Akasema Kivu itabaki Congo na madini ya Kivu yatajenga Congo. Full stop. Ashakuwa Rais utamfanya nini? Kagame hakuamini macho yake. Alishawaza jinsi ambavyo Rwanda ingekuwa Dubai ya Afrika kwa rasilimali za Congo. Lakini ghafla aligeukwa na mshirika wake Laurent Désiré Kabila. Akamfuata "Godfather" wake mzee Museveni. Mzee akasema kama katugeuka tumpige. Wakatafuta kikundi cha Waasi wakiunge mkono. Wakapata Rassemblement Congolais pour la Démocratie (RCD), kilichoongozwa na Jenerali Ernest Wamba dia Wamba. Kikundi kikapewa silaha na fedha kikaanza kumshughulikia Kabila. RCD ikaanza kuchapana na jeshi la Congo (FARDC) ikiwa na backup ya Rwanda na Uganda. Vita vikapamba moto. Rwanda na Uganda nao wakaingiza majeshi Congo kusaidia waasi wa RCD. Kabila akaona anazidiwa, akaomba msaada Angola na Chad. Nchi hizo zikaleta vikosi vyake Congo. Mapigano yakawa makali sana. Eneo la mashariki mwa Congo likageuka machinjioni. Watu walikufa kwa wingi, mpaka maiti zikatapakaa barabarani bila kuzikwa, zikawa zinadonolewa na ndege. Hii iliitwa Vita ya Pili ya Congo (1998–2002), iliyokua mbaya zaidi katika historia ya vita zote Afrika. Imebatizwa jina "Vita Kuu ya Afrika". Inakadiriwa watu laki tano walipoteza maisha huku mamilioni wakikimbia nchi. Mapigano yaliendelea, huku vikosi vya Rwanda na Uganda vikichota madini. Katikati ya mapigano mgongano wa kimaslahi ukajitokeza. Jasin Stearns, katika kitabu chake Dancing in the Glory of Monsters, anasema Kagame alishindwa kuelewana na "godfather" wake Museveni juu ya mgawanyo wa mali. Hali hiyo ilifanya kikundi cha RCD kipasuke na kuzaliwa vikundi viwili. Cha kwanza kikajiita RCD-Goma kikiongozwa na Kanali Emile Ilunga (hiki kilisaidiwa na Rwanda) na cha pili kikajiita RCD-Kisangani, kikiongozwa na Jenerali Mbusa Nyamwisi (kikisaidiwa na Uganda). (Malisa GJ)
    Like
    2
    · 0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·1K Views
  • 0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·350 Views
  • 0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·346 Views
  • Mo Salah amebakisha mabao 83 kuivunja rekodi ya ufungaji bora wa muda wote ya ligi kuu ya England inayoshikiliwa na muingereza Alan Shearer.

    Kwa sasa Salah yupo nafasi ya 6 akiwa na mabao 178, na anayo nafasi ya kupanda hadi nafasi ya 5 na kumshusha Sergio Kun-Aguero mwenye mabao 184, endapo atafunga mabao 7 katika mechi 15 zilizobaki. Na kama itakuwa hivyo basi atakuwa amebakisha mabao 76 ili kuvunja kabisa ya muda wote.

    Kwa rekodi ya ufungaji ya Salah, atahitaji misimu angalau minne kuifikia rekodi hii. Hii ni kwa sababu tangu ajiunge Liverpool 2016/18 amekuwa na wastani wa kufunga mabao 22 kwa msimu.

    2024/25 - 21
    2023/24 - 18
    2022/23 - 19
    2021/22 - 23
    2020/21 - 22
    2019/20 - 19
    2018/19 - 22
    2017/18 - 32

    Mkataba wa Mo Salah utaisha mwishoni mwa msimu huu na mazungumzo ya mkataba mpya yanasuasua. Salah mwenye miaka 32 amesema anatamani kubaki Liverpool, akini apewe mkataba wa miaka mitatu hadi 2028.

    Ila wamiliki wa klabu hiyo, kampuni ya FSG, wanasita kutoa mkataba mrefu namna hiyo kwa hofu ya umri wake.

    Mo Salah amebakisha mabao 83 kuivunja rekodi ya ufungaji bora wa muda wote ya ligi kuu ya England inayoshikiliwa na muingereza Alan Shearer. Kwa sasa Salah yupo nafasi ya 6 akiwa na mabao 178, na anayo nafasi ya kupanda hadi nafasi ya 5 na kumshusha Sergio Kun-Aguero mwenye mabao 184, endapo atafunga mabao 7 katika mechi 15 zilizobaki. Na kama itakuwa hivyo basi atakuwa amebakisha mabao 76 ili kuvunja kabisa ya muda wote. Kwa rekodi ya ufungaji ya Salah, atahitaji misimu angalau minne kuifikia rekodi hii. Hii ni kwa sababu tangu ajiunge Liverpool 2016/18 amekuwa na wastani wa kufunga mabao 22 kwa msimu. 2024/25 - 21 2023/24 - 18 2022/23 - 19 2021/22 - 23 2020/21 - 22 2019/20 - 19 2018/19 - 22 2017/18 - 32 Mkataba wa Mo Salah utaisha mwishoni mwa msimu huu na mazungumzo ya mkataba mpya yanasuasua. Salah mwenye miaka 32 amesema anatamani kubaki Liverpool, akini apewe mkataba wa miaka mitatu hadi 2028. Ila wamiliki wa klabu hiyo, kampuni ya FSG, wanasita kutoa mkataba mrefu namna hiyo kwa hofu ya umri wake.
    Like
    3
    · 0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·734 Views
  • 0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·330 Views
  • 0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·310 Views
  • 0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·344 Views
  • 0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·305 Views
  • 0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·259 Views
  • 0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·314 Views