• Like
    1
    · 0 Commentarios ·0 Acciones ·150 Views
  • MTUNZI WA JINA LA 'TANZANIA' AFARIKI

    Hicho ni kipande cha gazeti la The Nationalist la Oktoba 30, 1964. Habari kubwa kwenye gazeti hili na Nchi kwa ujumla ni jina jipya la TANZANIA. Ni kwamba baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wa April 26, 1964, jina la nchi mpya lilikuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Lakini jina hili lilikuwa refu sana na kuwa kero kwa Watumiaji.

    Serikali kupitia wizara ya habari na utalii chini ya waziri Dkt. Idrisa Abdul Wakili, ikaanzisha mchakato wa kutafuta jina jipya litakalokuwa fupi na rahisi. Ikatoa tangazo kupitia gazeti la Tanganyika Standard, ambalo sasa ni Daily News, kuwataka Watanzania wenye kuweza kubuni jina jipya la Nchi kufanya hivyo. Ndipo kijana wa miaka 18 kutoka Morogoro, Mohamed Iqbal Dar, Mwanafunzi wa Sekondari ya Aga Khan Morogoro, akaliona tangazo hilo na kushiriki.

    Akatunga jina la Tanzania na kulituma kwenye anwani iliyotangazwa. Baada ya muda kupita, akapata barua kutoka serikalini ikimtaja na kumpongeza yeye kama mmoja wa Washindi 16 na wakatakiwa kufika ofisi za wizara. Kwa pamoja watu hawa walitakiwa kugawana zawadi ya shilingi 200, wakati huo shilingi moja ilikuwa sawa na dola 8 za Marekani.

    Siku ilipofika, watu wawili tu walijitokeza; yeye Mohamed Iqbal Dar na Yusufal Pir Mohamed. Lakini huyo mwenzake hakuwa na ile barua ya kutajwa kama mshindi na kupongezwa... Serikali ikashindwa kumthibitisha hivyo kumtangaza Mohamed Iqbal Dar kama Mshindi pekee. Ndipo Jumatano ya Oktoba 29, 1964 serikali ikatangaza rasmi kwamba jina jipya la nchi ni Tanzania na gazeti la The Nationalist likaichapisha habari hii kubwa, Alhamisi ya Oktoba 30, 1964. Jina la Tanzania likaanza kutumika rasmi Novemba Mosi, 1964.

    - Alitungaje jina?

    TAN - kutoka Tanganyika
    ZAN - kutoka Zanzibar
    I - kutoka jina lake la Iqbal.
    A - kutoka dini yake ya Ahmadiya. Hii pia ikawa rahisi zaidi kwake kwani majina ya nchi nyingi za Afrika yaliishia na A kama Ethiopia, Zambia, Gambia nk.

    - Ni nani huyu Mohamed Iqbal Dar?

    Ni mtoto wa Dkt. Dar, ambaye alikuja Tanzania mwaka 1930 kutoka India. Alifikia Tanga, na ndiko alikozaliwa Mohamed, hakafu akahamia Morogoro. Mohamed amefarikia huko Birmingham Nchini Uingereza .
    MTUNZI WA JINA LA 'TANZANIA' AFARIKI Hicho ni kipande cha gazeti la The Nationalist la Oktoba 30, 1964. Habari kubwa kwenye gazeti hili na Nchi kwa ujumla ni jina jipya la TANZANIA. Ni kwamba baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wa April 26, 1964, jina la nchi mpya lilikuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Lakini jina hili lilikuwa refu sana na kuwa kero kwa Watumiaji. Serikali kupitia wizara ya habari na utalii chini ya waziri Dkt. Idrisa Abdul Wakili, ikaanzisha mchakato wa kutafuta jina jipya litakalokuwa fupi na rahisi. Ikatoa tangazo kupitia gazeti la Tanganyika Standard, ambalo sasa ni Daily News, kuwataka Watanzania wenye kuweza kubuni jina jipya la Nchi kufanya hivyo. Ndipo kijana wa miaka 18 kutoka Morogoro, Mohamed Iqbal Dar, Mwanafunzi wa Sekondari ya Aga Khan Morogoro, akaliona tangazo hilo na kushiriki. Akatunga jina la Tanzania na kulituma kwenye anwani iliyotangazwa. Baada ya muda kupita, akapata barua kutoka serikalini ikimtaja na kumpongeza yeye kama mmoja wa Washindi 16 na wakatakiwa kufika ofisi za wizara. Kwa pamoja watu hawa walitakiwa kugawana zawadi ya shilingi 200, wakati huo shilingi moja ilikuwa sawa na dola 8 za Marekani. Siku ilipofika, watu wawili tu walijitokeza; yeye Mohamed Iqbal Dar na Yusufal Pir Mohamed. Lakini huyo mwenzake hakuwa na ile barua ya kutajwa kama mshindi na kupongezwa... Serikali ikashindwa kumthibitisha hivyo kumtangaza Mohamed Iqbal Dar kama Mshindi pekee. Ndipo Jumatano ya Oktoba 29, 1964 serikali ikatangaza rasmi kwamba jina jipya la nchi ni Tanzania na gazeti la The Nationalist likaichapisha habari hii kubwa, Alhamisi ya Oktoba 30, 1964. Jina la Tanzania likaanza kutumika rasmi Novemba Mosi, 1964. - Alitungaje jina? TAN - kutoka Tanganyika ZAN - kutoka Zanzibar I - kutoka jina lake la Iqbal. A - kutoka dini yake ya Ahmadiya. Hii pia ikawa rahisi zaidi kwake kwani majina ya nchi nyingi za Afrika yaliishia na A kama Ethiopia, Zambia, Gambia nk. - Ni nani huyu Mohamed Iqbal Dar? Ni mtoto wa Dkt. Dar, ambaye alikuja Tanzania mwaka 1930 kutoka India. Alifikia Tanga, na ndiko alikozaliwa Mohamed, hakafu akahamia Morogoro. Mohamed amefarikia huko Birmingham Nchini Uingereza 🇬🇧.
    Like
    2
    · 0 Commentarios ·0 Acciones ·944 Views
  • Serikali ya Kinshasa (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ) imetangaza kuwa Bidhaa (Biashara) kutoka Miji ya Goma na Bukavu ambayo ni Miji inayopatikana Mashariki mwa DR Congo kulipa ushuru wa kuingia kwenye Mikoa mingine ambayo inasimamiwa na Serekali ya Kinshasa.

    Miji ya Goma na Bukavu inadhibitiwa na Waasi wa kundi la M23 na inachukuliwa kama Nchi nyingine ndani ya DR Congo huku Serekali ya Kinshasa ikizitaka Nchi nyingine Duniani kutotambua Miji hiyo kama sehemu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

    Waasi wa kundi la M23 wamesema kuwa wapo kwenye hatua za mwisho ya kutangaza Viongozi wao katika Miji hiyo ambapo wanasema kuwa wataanda uchaguzi ili kuwapata Viongozi wataongoza Miji hiyo ambayo ipo chini ya Uongozi wao.

    Hata hatua nyingine, Serekali ya Kinshasa imetangaza rasmi Mji wa Uvira kuwa ndiyo Mji Mkuu wa Serekali ya Mkoa wa Sud-Kivu na Makazi ya muda ya Gavana wa Mkoa huo wa Sud-Kivu baada ya Mji wa Bukavu kuvamiwa na kudhibitiwa na Waasi wa M23.

    Serikali ya Kinshasa (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩) imetangaza kuwa Bidhaa (Biashara) kutoka Miji ya Goma na Bukavu ambayo ni Miji inayopatikana Mashariki mwa DR Congo kulipa ushuru wa kuingia kwenye Mikoa mingine ambayo inasimamiwa na Serekali ya Kinshasa. Miji ya Goma na Bukavu inadhibitiwa na Waasi wa kundi la M23 na inachukuliwa kama Nchi nyingine ndani ya DR Congo huku Serekali ya Kinshasa ikizitaka Nchi nyingine Duniani kutotambua Miji hiyo kama sehemu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Waasi wa kundi la M23 wamesema kuwa wapo kwenye hatua za mwisho ya kutangaza Viongozi wao katika Miji hiyo ambapo wanasema kuwa wataanda uchaguzi ili kuwapata Viongozi wataongoza Miji hiyo ambayo ipo chini ya Uongozi wao. Hata hatua nyingine, Serekali ya Kinshasa imetangaza rasmi Mji wa Uvira kuwa ndiyo Mji Mkuu wa Serekali ya Mkoa wa Sud-Kivu na Makazi ya muda ya Gavana wa Mkoa huo wa Sud-Kivu baada ya Mji wa Bukavu kuvamiwa na kudhibitiwa na Waasi wa M23.
    Like
    1
    · 0 Commentarios ·0 Acciones ·426 Views
  • Nchi ya Ujerumani imepanda kusitisha misaada kwa Nchi ya Rwanda kutokana na kujihusisha kwao na Kundi la Waasi wa M23 ambao limefanikiwa kuiteka Miji ya Goma na Bukavu Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo . Tayari Rwanda imeshafahamishwa na Ujerumani kuhusu mpango huo.

    Aidha, Nchi ya Rwanda imekuwa ikinufaika na misaada kutoka Nchini Ujerumani inayokadiriwa kufikia thamani ya wastani wa Dola za Kimarekani milioni 53 kwa mwaka ambayo imekuwa ikitolewa katika nyanja mbalimbali ikiwemo uchumi, uzalishaji wa chanjo na mabadiliko ya tabia Nchi.

    Nchi ya Ujerumani 🇩🇪 imepanda kusitisha misaada kwa Nchi ya Rwanda 🇷🇼 kutokana na kujihusisha kwao na Kundi la Waasi wa M23 ambao limefanikiwa kuiteka Miji ya Goma na Bukavu Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩. Tayari Rwanda imeshafahamishwa na Ujerumani kuhusu mpango huo. Aidha, Nchi ya Rwanda imekuwa ikinufaika na misaada kutoka Nchini Ujerumani inayokadiriwa kufikia thamani ya wastani wa Dola za Kimarekani milioni 53 kwa mwaka ambayo imekuwa ikitolewa katika nyanja mbalimbali ikiwemo uchumi, uzalishaji wa chanjo na mabadiliko ya tabia Nchi.
    Like
    1
    · 0 Commentarios ·0 Acciones ·485 Views
  • Love
    1
    · 0 Commentarios ·0 Acciones ·279 Views
  • Alhamdulillah MASHALLAH

    napokea iftari kwa AJILI ya ndugu ndugu zetu mayatima wajane mafakir


    Tunaomba swadaka ya kufturisha ndugu waislam wenzetu katika funga hii
    Swadaka ni tiba swadaka ni ibada kubwa zaidi
    ibada

    SUKARI KG 100
    TAMBI
    MCHELE KG 200
    NGANO KG 100

    CHANGIA SADAKA KIDOGO KWA PALE ULIPO BARIKIWA ALLAH ATAKULIPA

    0655987549
    TIGOPESA
    MOZA MOHAMED

    SWADAKA NDIO IBADA KUBWA ZAIDI
    Alhamdulillah MASHALLAH 🤲 napokea iftari kwa AJILI ya ndugu ndugu zetu mayatima wajane mafakir Tunaomba swadaka ya kufturisha ndugu waislam wenzetu katika funga hii Swadaka ni tiba swadaka ni ibada kubwa zaidi ibada SUKARI KG 100 TAMBI MCHELE KG 200 NGANO KG 100 CHANGIA SADAKA KIDOGO KWA PALE ULIPO BARIKIWA ALLAH ATAKULIPA 0655987549 TIGOPESA MOZA MOHAMED SWADAKA NDIO IBADA KUBWA ZAIDI
    Love
    2
    · 0 Commentarios ·0 Acciones ·797 Views
  • Ukuu wa Muumba
    Ukuu wa Muumba 🙏🙏🙏🙏
    0 Commentarios ·0 Acciones ·273 Views
  • Orodha ya Watayarishaji bora kwenye historia ya muziki wa Tanzania.

    1. P Funk
    2. Master Jay
    3. Miika Mwamba
    4. Bonny Love
    5. Prof Ludigo

    6. Bizzman
    7. Enrico
    8. Marco Chali
    9. Hermy B
    10. Lamar

    11. Man Walter
    12. Alain Mapigo
    13. Said Comorean
    14. Ambrose Dunga
    15. Pancho Latino

    16. J Ryder
    17. T Touch
    18. Kameta
    19. Mona Gangster
    20. Shaddy Clever

    21. Complex
    22. Manecky
    23. Abbah
    24. KGT
    25. Bob Junior

    26. Mensen Selekta
    27. Duke
    28. S2Kezzy
    29. Laizer
    30. Abby Daddy

    31. Bonga
    32. Emma The Boy
    33. Nahreel
    34. Mangustino
    35. Kidbway

    36. Shirko
    37. Fundi Samuel
    38. Ali Baucha.

    Panga orodha yako Watayarishaji wa tano bora wa muda wote.
    Orodha ya Watayarishaji bora kwenye historia ya muziki wa Tanzania. 1. P Funk 2. Master Jay 3. Miika Mwamba 4. Bonny Love 5. Prof Ludigo 6. Bizzman 7. Enrico 8. Marco Chali 9. Hermy B 10. Lamar 11. Man Walter 12. Alain Mapigo 13. Said Comorean 14. Ambrose Dunga 15. Pancho Latino 16. J Ryder 17. T Touch 18. Kameta 19. Mona Gangster 20. Shaddy Clever 21. Complex 22. Manecky 23. Abbah 24. KGT 25. Bob Junior 26. Mensen Selekta 27. Duke 28. S2Kezzy 29. Laizer 30. Abby Daddy 31. Bonga 32. Emma The Boy 33. Nahreel 34. Mangustino 35. Kidbway 36. Shirko 37. Fundi Samuel 38. Ali Baucha. Panga orodha yako Watayarishaji wa tano bora wa muda wote.
    Like
    1
    · 0 Commentarios ·0 Acciones ·819 Views
  • Like
    1
    · 0 Commentarios ·0 Acciones ·124 Views
  • "Kwamba TFF impige mvua ya miaka miwili Kijana wake Ally Kamwe? Nimeona taarifa kwa Ndugu yangu Mkomwa, nimewaza sana kwamba TFF kama Taasisi yetu tunayoiamini ifikie maamuzi kama haya? Labda wacha tusubiri taarifa rasmi, lakini kama ni kweli basi inafikirisha sana.

    Kamwe ametiwa hatiani kwa kosa liloitwa la UDHALILISHAJI, kwamba udhalilishaji aliofanya ni kupost “Leo Mjadala redioni 90% ni kuhusu Makolo na Waamuzi” hapo ndipo wakamtia hatiani kwa kudharirisha, lakini nimewaza sana, Ally ni wa kwanza kulaumu? Hao Makolo ni nani? Wanashiriki ligi gani? Ni timu gani? Bado inafikirisha sana, kwamba kuna timu inachezeshwa na Marefa wetu inaitwa Makolo?

    Tufanye ni kosa lakini ije na adhabu ya miaka miwili? Nakumbuka kuna Msemaji alifanya kosa kama hili alifungiwa miezi mitatu, je utofauti wake na Ally ni upi? Miaka miwili imetokana na nini? Je ni TFF tu au kuna Mtu ndani pale au nje yupo nyuma ya mchezo akisukuma kete zake kwa umakini? Ni kosa kubwa kiasi hicho mpaka tumpoteze Kijana wetu kwa miaka miwili?

    Kwamba tunashindwa kuvumiliana? Kuadhibiana kwa kuhurumiana? Kama ambavyo Wadau wa soka wamekuwa wakiwavumilia Waamuzi? Sikatai amekosea lakini nakataa ukubwa wa adhabu, sitaki kuamini mpaka nione taarifa rasmi ila kama kweli ni miaka miwili basi huenda ikawa adhabu kubwa zaidi kuwahi kutolewa kwa kosa dogo zaidi, inafikirisha, siamini kama taasisi yetu penda ikatoa adhabu kama hii, unless kuwa na Mtu anashawishi.

    Makofi hayamkuzi Mtoto bali yanamuumiza, sheria haipo kusaka haki bali Mshindi, hiyo ni kweli na inafahamika ila Mshindi anapaswa kuwa mpira wa miguu sio Mtu mmoja, kama kweli ni miaka miwili ipo haja ya kupunguza adhabu, kwa maslahi mapana ya mpira kwakuwa Ally ni Kijana wetu, Mtoto wetu ambaye ameutumikia mpira huu kwa mapenzi makubwa sana, itabaki kuwa ni mmoja kati yetu.

    Nachofahamu Chura hawezi kuruka mchana wa jua kali tena nchi kavu kama hakuna kitu kinachomkimbiza" - Farhan JR, Mchambuzi.

    "Kwamba TFF impige mvua ya miaka miwili Kijana wake Ally Kamwe? Nimeona taarifa kwa Ndugu yangu Mkomwa, nimewaza sana kwamba TFF kama Taasisi yetu tunayoiamini ifikie maamuzi kama haya? Labda wacha tusubiri taarifa rasmi, lakini kama ni kweli basi inafikirisha sana. Kamwe ametiwa hatiani kwa kosa liloitwa la UDHALILISHAJI, kwamba udhalilishaji aliofanya ni kupost “Leo Mjadala redioni 90% ni kuhusu Makolo na Waamuzi” hapo ndipo wakamtia hatiani kwa kudharirisha, lakini nimewaza sana, Ally ni wa kwanza kulaumu? Hao Makolo ni nani? Wanashiriki ligi gani? Ni timu gani? Bado inafikirisha sana, kwamba kuna timu inachezeshwa na Marefa wetu inaitwa Makolo? Tufanye ni kosa lakini ije na adhabu ya miaka miwili? Nakumbuka kuna Msemaji alifanya kosa kama hili alifungiwa miezi mitatu, je utofauti wake na Ally ni upi? Miaka miwili imetokana na nini? Je ni TFF tu au kuna Mtu ndani pale au nje yupo nyuma ya mchezo akisukuma kete zake kwa umakini? Ni kosa kubwa kiasi hicho mpaka tumpoteze Kijana wetu kwa miaka miwili? Kwamba tunashindwa kuvumiliana? Kuadhibiana kwa kuhurumiana? Kama ambavyo Wadau wa soka wamekuwa wakiwavumilia Waamuzi? Sikatai amekosea lakini nakataa ukubwa wa adhabu, sitaki kuamini mpaka nione taarifa rasmi ila kama kweli ni miaka miwili basi huenda ikawa adhabu kubwa zaidi kuwahi kutolewa kwa kosa dogo zaidi, inafikirisha, siamini kama taasisi yetu penda ikatoa adhabu kama hii, unless kuwa na Mtu anashawishi. Makofi hayamkuzi Mtoto bali yanamuumiza, sheria haipo kusaka haki bali Mshindi, hiyo ni kweli na inafahamika ila Mshindi anapaswa kuwa mpira wa miguu sio Mtu mmoja, kama kweli ni miaka miwili ipo haja ya kupunguza adhabu, kwa maslahi mapana ya mpira kwakuwa Ally ni Kijana wetu, Mtoto wetu ambaye ameutumikia mpira huu kwa mapenzi makubwa sana, itabaki kuwa ni mmoja kati yetu. Nachofahamu Chura hawezi kuruka mchana wa jua kali tena nchi kavu kama hakuna kitu kinachomkimbiza" - Farhan JR, Mchambuzi.
    Like
    1
    · 0 Commentarios ·0 Acciones ·729 Views