0 Comments
路0 Shares
路11 Views
-
-
-
-
-
Rais wa Marekani , Donald Trump ametupilia mbali madai kwamba Nchi ya Urusi imekataa mapendekezo ya Nchi yake ya Marekani ya kusitisha mapigano Nchini Ukraine . Kiongozi huyo wa Marekani alionyesha kwa ufanisi kuwa ni mapema kujadili kuimarisha vikwazo vya Nchi ya Marekani dhidi ya Urusi.
"Yeye (Rais wa Urusi Vladimir Putin ) hakukataa chochote. Na wana vikwazo," - Donald Trump aliwaambia Waandishi wa habari katika Ikulu ya Marekani (White House), akijibu swali ikiwa Marekani inapaswa kuimarisha vikwazo dhidi ya Urusi kwa sababu madai ya Putin kukataa usitishaji vita Nchini Ukraine.
"Wana takriban vikwazo zaidi kuliko mtu yeyote," aliongeza
Putin na Trump walipiga simu mnamo Machi 18, 2025 wakijadili wazo la kusitisha mapigano kwa siku thelathini katika mzozo wa Ukraine, njia za kuzuia kuongezeka zaidi kwa mvutano na masuala kadhaa ya kimataifa, Kremlin ilisema. Kulingana na maelezo yake ya wito huo, Kiongozi huyo wa Urusi aliunga mkono mpango wa Rais wa Marekani wa kusitisha mapigano ya nishati na miundombinu Nchini Ukraine.
Ikulu ya White House ilisema katika usomaji huo kwamba Viongozi hao wawili pia walikubaliana kuanza mazungumzo ya kiufundi "juu ya utekelezaji wa usitishaji vita wa baharini katika Bahari Nyeusi, usitishaji kamili wa mapigano na amani ya kudumu."
Rais wa Marekani 馃嚭馃嚫, Donald Trump ametupilia mbali madai kwamba Nchi ya Urusi 馃嚪馃嚭 imekataa mapendekezo ya Nchi yake ya Marekani ya kusitisha mapigano Nchini Ukraine 馃嚭馃嚘. Kiongozi huyo wa Marekani alionyesha kwa ufanisi kuwa ni mapema kujadili kuimarisha vikwazo vya Nchi ya Marekani dhidi ya Urusi. "Yeye (Rais wa Urusi Vladimir Putin ) hakukataa chochote. Na wana vikwazo," - Donald Trump aliwaambia Waandishi wa habari katika Ikulu ya Marekani (White House), akijibu swali ikiwa Marekani inapaswa kuimarisha vikwazo dhidi ya Urusi kwa sababu madai ya Putin kukataa usitishaji vita Nchini Ukraine. "Wana takriban vikwazo zaidi kuliko mtu yeyote," aliongeza Putin na Trump walipiga simu mnamo Machi 18, 2025 wakijadili wazo la kusitisha mapigano kwa siku thelathini katika mzozo wa Ukraine, njia za kuzuia kuongezeka zaidi kwa mvutano na masuala kadhaa ya kimataifa, Kremlin ilisema. Kulingana na maelezo yake ya wito huo, Kiongozi huyo wa Urusi aliunga mkono mpango wa Rais wa Marekani wa kusitisha mapigano ya nishati na miundombinu Nchini Ukraine. Ikulu ya White House ilisema katika usomaji huo kwamba Viongozi hao wawili pia walikubaliana kuanza mazungumzo ya kiufundi "juu ya utekelezaji wa usitishaji vita wa baharini katika Bahari Nyeusi, usitishaji kamili wa mapigano na amani ya kudumu."0 Comments 路0 Shares 路42 Views -
Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza rasmi kuondoa hitaji la visa kwa Watanzania wanaoingia Nchini humo, kuanzia tarehe 20 Machi, 2025. Hatua hii ni sehemu ya utekelezaji wa uanachama wa DR Congo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na jitihada za kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kiuchumi kati ya mataifa hayo mawili.
Ikumbukwe kwamba Nchi ya Tanzania ilikuwa imeondoa utaratibu wa malipo ya visa kwa Raia wa DRC tangu Septemba 2, 2023, ikitarajia hatua ya kurudishiwa fadhila. Uamuzi wa sasa wa DR Congo unaimarisha mahusiano ya ujirani mwema na kufungua fursa zaidi za biashara na ushirikiano wa kikanda.
Serikali ya Tanzania imesifu hatua hiyo, ikisisitiza kuwa inalingana na ajenda za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Mkataba wa Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA). Hatua hii inaashiria ushirikiano bora wa kidiplomasia na unaleta unafuu mkubwa kwa Wafanyabiashara na wasafiri wa pande zote mbili.
Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 馃嚚馃嚛 imetangaza rasmi kuondoa hitaji la visa kwa Watanzania wanaoingia Nchini humo, kuanzia tarehe 20 Machi, 2025. Hatua hii ni sehemu ya utekelezaji wa uanachama wa DR Congo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na jitihada za kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kiuchumi kati ya mataifa hayo mawili. Ikumbukwe kwamba Nchi ya Tanzania 馃嚬馃嚳 ilikuwa imeondoa utaratibu wa malipo ya visa kwa Raia wa DRC tangu Septemba 2, 2023, ikitarajia hatua ya kurudishiwa fadhila. Uamuzi wa sasa wa DR Congo unaimarisha mahusiano ya ujirani mwema na kufungua fursa zaidi za biashara na ushirikiano wa kikanda. Serikali ya Tanzania imesifu hatua hiyo, ikisisitiza kuwa inalingana na ajenda za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Mkataba wa Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA). Hatua hii inaashiria ushirikiano bora wa kidiplomasia na unaleta unafuu mkubwa kwa Wafanyabiashara na wasafiri wa pande zote mbili.0 Comments 路0 Shares 路34 Views -
Nchi ya Ufaransa imepinga vikali kauli ya Waziri wa Ulinzi wa Israel , Israel Katz, aliyedokeza uwezekano wa Israel kutwaa baadhi ya maeneo ya Ukanda wa Gaza iwapo Kundi la Hamas haitowaachia huru mateka waliosalia. Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Jean-Noel Barrot, amesema kuwa Ufaransa inapinga aina yoyote ya unyakuzi wa ardhi ya Palestina, iwe Gaza au Ukingo wa Magharibi. Kauli hiyo inakuja wakati ambapo Israel imezidisha mashambulizi yake Gaza, hali iliyosababisha maelfu ya wakazi wa maeneo ya Al-Salatin, Al-Karama, na Al-Awda kusini mwa Gaza kuamriwa kuyahama makazi yao kabla ya mashambulizi mapya.
Katika tukio jingine, Jeshi la Israel lilidungua makombora mawili yaliyofyatuliwa na Hamas kuelekea mji wa Ashkelon, ambapo Hamas ilidai kuwa shambulio hilo ni jibu kwa mashambulizi dhidi ya raia wa Gaza. Waziri wa Ulinzi wa Israel ameapa kuendeleza mashambulizi ya angani, majini, na ardhini hadi mateka wote waachiliwe na Hamas ishindwe kabisa.
Hatua hizi za Israel zimezua ukosoaji mkubwa kimataifa. Uturuki imelaani shambulio la Israel dhidi ya hospitali iliyojengwa na nchi hiyo huko Gaza, huku Rais wa Urusi , Vladimir Putin, akielezea kusikitishwa kwake na mashambulizi hayo.
Nchi ya Ufaransa 馃嚝馃嚪 imepinga vikali kauli ya Waziri wa Ulinzi wa Israel 馃嚠馃嚤, Israel Katz, aliyedokeza uwezekano wa Israel kutwaa baadhi ya maeneo ya Ukanda wa Gaza iwapo Kundi la Hamas haitowaachia huru mateka waliosalia. Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Jean-Noel Barrot, amesema kuwa Ufaransa inapinga aina yoyote ya unyakuzi wa ardhi ya Palestina, iwe Gaza au Ukingo wa Magharibi. Kauli hiyo inakuja wakati ambapo Israel imezidisha mashambulizi yake Gaza, hali iliyosababisha maelfu ya wakazi wa maeneo ya Al-Salatin, Al-Karama, na Al-Awda kusini mwa Gaza kuamriwa kuyahama makazi yao kabla ya mashambulizi mapya. Katika tukio jingine, Jeshi la Israel lilidungua makombora mawili yaliyofyatuliwa na Hamas kuelekea mji wa Ashkelon, ambapo Hamas ilidai kuwa shambulio hilo ni jibu kwa mashambulizi dhidi ya raia wa Gaza. Waziri wa Ulinzi wa Israel ameapa kuendeleza mashambulizi ya angani, majini, na ardhini hadi mateka wote waachiliwe na Hamas ishindwe kabisa. Hatua hizi za Israel zimezua ukosoaji mkubwa kimataifa. Uturuki 馃嚬馃嚪 imelaani shambulio la Israel dhidi ya hospitali iliyojengwa na nchi hiyo huko Gaza, huku Rais wa Urusi 馃嚪馃嚭, Vladimir Putin, akielezea kusikitishwa kwake na mashambulizi hayo.0 Comments 路0 Shares 路25 Views -
Rais wa Nchi ya Iran , Ayatollah Ali Khamenei, amesema kuwa vitisho vya Nchi ya Marekani dhidi ya Taifa lake havisaidii lolote na havitaleta matokeo yoyote kama Rais Donald Tramp anavyofikiria. Kiongozi huyo amesema hayo baada ya Rais Trump kuonya uwezekano wa hatua za kijeshi kuchukuliwa dhidi ya Iran.
"Wamarekani wanapaswa kuelewa kwamba vitisho havitafanikiwa wanapokabiliana na Iran. Wao (Marekani) na wengine wanapaswa kufahamu kuwa wakifanya lolote baya dhidi ya taifa la Iran, watajibiwa kwa nguvu kubwa." alisema Rais Khemenei
Mnamo Machi 7, Rais Trump alisema kuwa alimwandikia barua Rais Khamenei, akimtaka kuanzisha mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran, huku akionya kuwa kuna uwezekano wa kuchukua hatua za kijeshi iwapo Iran itakataa. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, alisema Alhamisi wiki hii kuwa barua hiyo ilikuwa zaidi ya tishio, ingawa pia ilionesha uwezekano wa mazungumzo.
"Tunachunguza kwa kina maudhui ya barua hiyo, na tutajibu rasmi katika siku chache zijazo” alisema Waziri huyo
Kulingana na ripoti ya tovuti ya habari ya Marekani, Axios, ikimnukuu Afisa wa Serikali ya Trump na vyanzo vingine vikisema, barua hiyo inaweka muda wa miezi miwili wa kufikia makubaliano mapya ya nyuklia. Hata hivyo, haijabainishwa ni lini muda huo utaanza au kuisha. Kwa muda mrefu, Rais Khamenei amepuuza wito wa Rais Trump wa mazungumzo ya moja kwa moja, akisema kuwa Rais huyo wa Marekani anajaribu kudanganya ulimwengu kwa kuonesha kuwa Marekani iko tayari kwa mazungumzo huku Iran ikionekana kutotaka kushiriki.
Ikumbukwe kwamba Trump ambaye alianza muhula wake wa pili Januari 2025, amerudisha sera yake ya shinikizo la juu dhidi ya Iran. Wakati wa kipindi chake cha kwanza, Trump aliiondoa Marekani kwenye makubaliano ya kihistoria ya nyuklia ya 2015 kati ya Iran na mataifa yenye nguvu ulimwenguni na akairejeshea Tehran vikwazo vikubwa vya kiuchumi.
Rais wa Nchi ya Iran 馃嚠馃嚪, Ayatollah Ali Khamenei, amesema kuwa vitisho vya Nchi ya Marekani 馃嚭馃嚫 dhidi ya Taifa lake havisaidii lolote na havitaleta matokeo yoyote kama Rais Donald Tramp anavyofikiria. Kiongozi huyo amesema hayo baada ya Rais Trump kuonya uwezekano wa hatua za kijeshi kuchukuliwa dhidi ya Iran. "Wamarekani wanapaswa kuelewa kwamba vitisho havitafanikiwa wanapokabiliana na Iran. Wao (Marekani) na wengine wanapaswa kufahamu kuwa wakifanya lolote baya dhidi ya taifa la Iran, watajibiwa kwa nguvu kubwa." alisema Rais Khemenei Mnamo Machi 7, Rais Trump alisema kuwa alimwandikia barua Rais Khamenei, akimtaka kuanzisha mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran, huku akionya kuwa kuna uwezekano wa kuchukua hatua za kijeshi iwapo Iran itakataa. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, alisema Alhamisi wiki hii kuwa barua hiyo ilikuwa zaidi ya tishio, ingawa pia ilionesha uwezekano wa mazungumzo. "Tunachunguza kwa kina maudhui ya barua hiyo, na tutajibu rasmi katika siku chache zijazo” alisema Waziri huyo Kulingana na ripoti ya tovuti ya habari ya Marekani, Axios, ikimnukuu Afisa wa Serikali ya Trump na vyanzo vingine vikisema, barua hiyo inaweka muda wa miezi miwili wa kufikia makubaliano mapya ya nyuklia. Hata hivyo, haijabainishwa ni lini muda huo utaanza au kuisha. Kwa muda mrefu, Rais Khamenei amepuuza wito wa Rais Trump wa mazungumzo ya moja kwa moja, akisema kuwa Rais huyo wa Marekani anajaribu kudanganya ulimwengu kwa kuonesha kuwa Marekani iko tayari kwa mazungumzo huku Iran ikionekana kutotaka kushiriki. Ikumbukwe kwamba Trump ambaye alianza muhula wake wa pili Januari 2025, amerudisha sera yake ya shinikizo la juu dhidi ya Iran. Wakati wa kipindi chake cha kwanza, Trump aliiondoa Marekani kwenye makubaliano ya kihistoria ya nyuklia ya 2015 kati ya Iran na mataifa yenye nguvu ulimwenguni na akairejeshea Tehran vikwazo vikubwa vya kiuchumi.0 Comments 路0 Shares 路47 Views -