• Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·125 Views
  • “…ndani ya wiki moja, majeshi ya Uganda na wapiganaji wa M23 watakuwa Kisangani, kwa amri ya Rais Yoweri Museveni, Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Uganda (UPDF)…” - Muhoozi Kainerugaba, Mkuu wa Majeshi ya Uganda .

    “…ndani ya wiki moja, majeshi ya Uganda na wapiganaji wa M23 watakuwa Kisangani, kwa amri ya Rais Yoweri Museveni, Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Uganda (UPDF)…” - Muhoozi Kainerugaba, Mkuu wa Majeshi ya Uganda 🇺🇬.
    0 Comments ·0 Shares ·504 Views
  • Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·144 Views
  • Jeshi la Nchi ya Uganda limesema limewaua Wapiganaji 242 wa kundi la Waasi Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo linalojulikana kama CODECO baada ya kushambulia kambi ya Jeshi hilo la Uganda mpakani mashariki mwa DR Congo mapema wiki hii ambapo madai yamepingwa na Kundi hilo.

    Msemaji wa Jeshi la Uganda, Chris Magezi, amesema mamia ya Wapiganaji wa kundi la CODECO walishambulia kituo cha kijeshi cha Uganda People's Defence Forces (UPDF) katika eneo la Fataki, Mkoani Ituri, siku ya Jumatano na Alhamisi. Jeshi hilo lilijibu mashambulizi hayo mara zote mbili, likiwaangamiza Wapiganaji 31 siku ya kwanza na 211 siku ya pili, Magezi alisema katika chapisho kwenye akaunti yake ya Mtandao wa X Ijumaa usiku na kuongeza kuwa askari mmoja wa UPDF aliuawa na wengine wanne kujeruhiwa.

    Msemaji wa CODECO, Basa Zukpa Gerson, alipinga taarifa ya jeshi Jumamosi, akisema kundi hilo lilipoteza wapiganaji wawili tu na kwamba idadi ya vifo vya Wanajeshi wa UPDF ilikuwa juu zaidi. Chanzo kimoja cha Umoja wa Mataifa ambacho hakikutaka kutajwa jina kilisema Waasi 70 na Wanajeshi wa Uganda 12 waliuawa.

    Kulikuwa na mapigano zaidi kati ya pande hizo mbili asubuhi ya Jumamosi, alisema Msemaji wa CODECO na kiongozi mmoja wa jamii za kiraia wa eneo hilo. Wapiganaji wa CODECO wanasema lengo lao ni kuwalinda Wakulima wa Lendu dhidi ya Wafungaji wa Hema, ambao kihistoria wamekuwa wakigombana kuhusu ardhi.

    Kundi hilo ni moja ya makundi mengi ya Waasi yanayopigania ardhi na rasilimali za madini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambapo Waasi wa M23 wameongeza mashambulizi mwaka huu na kupata mafanikio makubwa. Uganda ilituma wanajeshi DR Congo mwaka 2021 kusaidia Serikali kupambana na kundi lingine la Waasi, Allied Democratic Forces (ADF), ambalo lina uhusiano na Islamic State na linafanya mashambulizi ya kikatili kwenye baadhi ya Vijiji.

    Jeshi la Nchi ya Uganda 🇺🇬 limesema limewaua Wapiganaji 242 wa kundi la Waasi Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩 linalojulikana kama CODECO baada ya kushambulia kambi ya Jeshi hilo la Uganda mpakani mashariki mwa DR Congo mapema wiki hii ambapo madai yamepingwa na Kundi hilo. Msemaji wa Jeshi la Uganda, Chris Magezi, amesema mamia ya Wapiganaji wa kundi la CODECO walishambulia kituo cha kijeshi cha Uganda People's Defence Forces (UPDF) katika eneo la Fataki, Mkoani Ituri, siku ya Jumatano na Alhamisi. Jeshi hilo lilijibu mashambulizi hayo mara zote mbili, likiwaangamiza Wapiganaji 31 siku ya kwanza na 211 siku ya pili, Magezi alisema katika chapisho kwenye akaunti yake ya Mtandao wa X Ijumaa usiku na kuongeza kuwa askari mmoja wa UPDF aliuawa na wengine wanne kujeruhiwa. Msemaji wa CODECO, Basa Zukpa Gerson, alipinga taarifa ya jeshi Jumamosi, akisema kundi hilo lilipoteza wapiganaji wawili tu na kwamba idadi ya vifo vya Wanajeshi wa UPDF ilikuwa juu zaidi. Chanzo kimoja cha Umoja wa Mataifa ambacho hakikutaka kutajwa jina kilisema Waasi 70 na Wanajeshi wa Uganda 12 waliuawa. Kulikuwa na mapigano zaidi kati ya pande hizo mbili asubuhi ya Jumamosi, alisema Msemaji wa CODECO na kiongozi mmoja wa jamii za kiraia wa eneo hilo. Wapiganaji wa CODECO wanasema lengo lao ni kuwalinda Wakulima wa Lendu dhidi ya Wafungaji wa Hema, ambao kihistoria wamekuwa wakigombana kuhusu ardhi. Kundi hilo ni moja ya makundi mengi ya Waasi yanayopigania ardhi na rasilimali za madini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambapo Waasi wa M23 wameongeza mashambulizi mwaka huu na kupata mafanikio makubwa. Uganda ilituma wanajeshi DR Congo mwaka 2021 kusaidia Serikali kupambana na kundi lingine la Waasi, Allied Democratic Forces (ADF), ambalo lina uhusiano na Islamic State na linafanya mashambulizi ya kikatili kwenye baadhi ya Vijiji.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·624 Views
  • Love
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·367 Views
  • Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·145 Views
  • Like
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·139 Views
  • Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·146 Views
  • 0 Comments ·0 Shares ·138 Views
  • "Najisikia vibaya namna watu wanavyoniona na kuanza kuniita Yesu, wanafikia hata kutundika picha zangu katika nyumba zao, mimi ni mwigizaji tu, mimi ni mtu" - Jonathan Roumie(50), mwigizaji wa Marekani

    Aidha, Jonathan Roumie katika mahojiano amesema maisha yake binafsi alikuwa na hali mbaya kiuchumi hakuwa na uhakika siku inayofuata atakula nini, alikuwa mwigizaji ila kiuchumi alikuwa bado hajafanikiwa. Baada ya mambo kuzidi kuwa magumu siku moja ni kama alikuwa anamuomba Mungu kuhusu hali anayopitia ili mambo yake yakae sawa

    Baada ya miezi kama mitatu ndio akapata nafasi ya kuigiza kama Yesu katika series ya "The Chosen" iliyoanza kuoneshwa 2017 ambayo imejipatia umaarufu mkubwa sana hadi sasa imetazamwa na watu zaidi ya milioni 250 na misimu mipya inafuata huku ikipongezwa kwa kinachoonekana kuigizwa

    Umaarufu wa uhusika wake kama Yesu umempa umaarufu mkubwa na fursa nyingi ikiwemo katika mikutano na makongamano makubwa ya kidini na app za dini ya kikiristo

    Jonathan ambaye ni mkatoliki, alipoulizwa na New York Times, je ni tukio gani gumu analokumbuka ambalo alishakutana nalo baada ya kuigiza kama Yesu, amejibu kwa kusema kuna kipindi alikuwa katika mkutano kwenye uwanja wenye watu takribani 40,000 baadaye alishuka stejini akaenda kwenye chumba fulani uwanjani hapo, mmoja wa walinzi alikuja akamwambia nje kuna mwanamke ana mtoto kwenye kiti cha magurudumu anaomba kusalimiana na wewe

    Jonathan alitoka akaonana na mwanamke husika na mwanae ambaye kwa ufupi alieleza jinsi Yesu alivyoponya mtu katika hiyo series ya "The Chosen" na kusema angependa mwanae pia apone yaani akimtaka Jonathan amponye mtoto wake. Ilibidi Jonathan amueleze ukweli kwamba yeye sio mponyaji wala mhubiri bali ni mwigizaji tu.

    Jonathan akamueleza wafanye maombi wote ilichukua kama dakika moja, walipomaliza maombi wakafurahi na kushukuru kisha Jonathan akarudi alipokuwa huku akitokwa na machozi akihisi amewaangusha matarajio waliyokuwa nayo kwake ila amesema ni bora waujue ukweli kuwa yeye sio Yesu wala mponyaji bali ni mwigizaji tu

    Ukiacha hayo ya uhusika wake wa Yesu na dini, Jonathan Roumie amegusia pia kwamba alishafika Tanzania na Rwanda sababu kuna watoto kadhaa wanaoishi katika mazingira magumu huwa anawasaidia na familia zao

    Jonathan Roumie pia ameweka wazi kwamba anatamani watu pia wawe wanamuona katika nyuma ya pazia(behind the scene) anayopitia katika kujiandaa na uigizaji wake kama Yesu ili watu wengine waelewe wajue kumtofautisha katika maisha halisi na kisanaa

    KUMBUKA, zipo filamu nyingine miaka ya nyuma kuhusu Yesu zilizohusisha waigizaji wengine kabla ya sasa Jonathan Roumie kupata umaarufu na uhusika wa Yesu katika series maarufu ya "The Chosen"
    (Swahili Word)

    "Najisikia vibaya namna watu wanavyoniona na kuanza kuniita Yesu, wanafikia hata kutundika picha zangu katika nyumba zao, mimi ni mwigizaji tu, mimi ni mtu" - Jonathan Roumie(50), mwigizaji wa Marekani Aidha, Jonathan Roumie katika mahojiano amesema maisha yake binafsi alikuwa na hali mbaya kiuchumi hakuwa na uhakika siku inayofuata atakula nini, alikuwa mwigizaji ila kiuchumi alikuwa bado hajafanikiwa. Baada ya mambo kuzidi kuwa magumu siku moja ni kama alikuwa anamuomba Mungu kuhusu hali anayopitia ili mambo yake yakae sawa Baada ya miezi kama mitatu ndio akapata nafasi ya kuigiza kama Yesu katika series ya "The Chosen" iliyoanza kuoneshwa 2017 ambayo imejipatia umaarufu mkubwa sana hadi sasa imetazamwa na watu zaidi ya milioni 250 na misimu mipya inafuata huku ikipongezwa kwa kinachoonekana kuigizwa Umaarufu wa uhusika wake kama Yesu umempa umaarufu mkubwa na fursa nyingi ikiwemo katika mikutano na makongamano makubwa ya kidini na app za dini ya kikiristo Jonathan ambaye ni mkatoliki, alipoulizwa na New York Times, je ni tukio gani gumu analokumbuka ambalo alishakutana nalo baada ya kuigiza kama Yesu, amejibu kwa kusema kuna kipindi alikuwa katika mkutano kwenye uwanja wenye watu takribani 40,000 baadaye alishuka stejini akaenda kwenye chumba fulani uwanjani hapo, mmoja wa walinzi alikuja akamwambia nje kuna mwanamke ana mtoto kwenye kiti cha magurudumu anaomba kusalimiana na wewe Jonathan alitoka akaonana na mwanamke husika na mwanae ambaye kwa ufupi alieleza jinsi Yesu alivyoponya mtu katika hiyo series ya "The Chosen" na kusema angependa mwanae pia apone yaani akimtaka Jonathan amponye mtoto wake. Ilibidi Jonathan amueleze ukweli kwamba yeye sio mponyaji wala mhubiri bali ni mwigizaji tu. Jonathan akamueleza wafanye maombi wote ilichukua kama dakika moja, walipomaliza maombi wakafurahi na kushukuru kisha Jonathan akarudi alipokuwa huku akitokwa na machozi akihisi amewaangusha matarajio waliyokuwa nayo kwake ila amesema ni bora waujue ukweli kuwa yeye sio Yesu wala mponyaji bali ni mwigizaji tu Ukiacha hayo ya uhusika wake wa Yesu na dini, Jonathan Roumie amegusia pia kwamba alishafika Tanzania na Rwanda sababu kuna watoto kadhaa wanaoishi katika mazingira magumu huwa anawasaidia na familia zao Jonathan Roumie pia ameweka wazi kwamba anatamani watu pia wawe wanamuona katika nyuma ya pazia(behind the scene) anayopitia katika kujiandaa na uigizaji wake kama Yesu ili watu wengine waelewe wajue kumtofautisha katika maisha halisi na kisanaa KUMBUKA, zipo filamu nyingine miaka ya nyuma kuhusu Yesu zilizohusisha waigizaji wengine kabla ya sasa Jonathan Roumie kupata umaarufu na uhusika wa Yesu katika series maarufu ya "The Chosen" (Swahili Word)
    Love
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·1K Views