• (F)
    Baada ya uchunguzi wa haraka, polisi walifukua miili kadhaa ya wagonjwa wa Shipman na kugundua kitu cha kutisha—miili yao ilikuwa na kiwango kikubwa cha morphine.

    Shipman alikamatwa na kushtakiwa kwa mauaji ya wagonjwa 15, lakini uchunguzi wa kina ulionesha kuwa huenda alikuwa amewaua zaidi ya watu 250 kwa kipindi cha miaka 23!

    Alifungwa jela mwaka 2000, na mwaka 2004, alipatikana amejinyonga kwenye seli yake.
    (F) Baada ya uchunguzi wa haraka, polisi walifukua miili kadhaa ya wagonjwa wa Shipman na kugundua kitu cha kutisha—miili yao ilikuwa na kiwango kikubwa cha morphine. Shipman alikamatwa na kushtakiwa kwa mauaji ya wagonjwa 15, lakini uchunguzi wa kina ulionesha kuwa huenda alikuwa amewaua zaidi ya watu 250 kwa kipindi cha miaka 23! Alifungwa jela mwaka 2000, na mwaka 2004, alipatikana amejinyonga kwenye seli yake.
    Like
    Love
    2
    0 Comments 0 Shares 74 Views
  • (C)
    Baada ya kifo cha mama yake, Shipman aliamua kuwa daktari. Alijiunga na Chuo Kikuu cha Leeds na baadaye akawa tabibu wa familia.

    Katika mwonekano wa nje, alikuwa mtu mwema, mtu wa familia, mwenye mke na watoto, anayependwa na wagonjwa wake. Lakini ndani yake, alikuwa akijificha kwenye kivuli cha giza na mauaji l.

    Alianza kazi yake kama daktari huko Yorkshire, na ilisemekana kuwa alikuwa mzuri sana kwa wagonjwa wake.

    Hata hivyo, mnamo 1975, alinaswa akiandika dawa za opioid (pethidine) kwa matumizi yake binafsi. Alipatikana na hatia, lakini badala ya kufungwa jela, alipigwa faini na kupoteza kazi kwa muda mfupi.

    Baadaye, alihamia mji wa Hyde na kuanza upya maisha yake kama daktari wa familia.

    Huko ndipo msururu wa vifo vya ajabu ulipoanza.
    (C) Baada ya kifo cha mama yake, Shipman aliamua kuwa daktari. Alijiunga na Chuo Kikuu cha Leeds na baadaye akawa tabibu wa familia. Katika mwonekano wa nje, alikuwa mtu mwema, mtu wa familia, mwenye mke na watoto, anayependwa na wagonjwa wake. Lakini ndani yake, alikuwa akijificha kwenye kivuli cha giza na mauaji l. Alianza kazi yake kama daktari huko Yorkshire, na ilisemekana kuwa alikuwa mzuri sana kwa wagonjwa wake. Hata hivyo, mnamo 1975, alinaswa akiandika dawa za opioid (pethidine) kwa matumizi yake binafsi. Alipatikana na hatia, lakini badala ya kufungwa jela, alipigwa faini na kupoteza kazi kwa muda mfupi. Baadaye, alihamia mji wa Hyde na kuanza upya maisha yake kama daktari wa familia. Huko ndipo msururu wa vifo vya ajabu ulipoanza.
    Like
    1
    0 Comments 0 Shares 80 Views
  • BAADHI YA MAENEO MAARUFU KATIKA BIBLIA YALIVO HII LEO

    01. MLIMA SINAI

    Mlima ambao Mungu aliwapa Waisraeli sheria yake ulikuwa katika jangwa hilo la kale.

    Mara kadhaa Musa alipanda juu ili kupokea maagizo mbalimbali.

    Vibao viwili vya mawe vilichongwa na maandishi ya amri kumi za Mungu mlimani. kwamba uwepo wa Mungu ulifunika kilele na wingu zito na umeme mkali wakati wa uchongaji amri kumi za Mungu
    BAADHI YA MAENEO MAARUFU KATIKA BIBLIA YALIVO HII LEO 01. MLIMA SINAI Mlima ambao Mungu aliwapa Waisraeli sheria yake ulikuwa katika jangwa hilo la kale. Mara kadhaa Musa alipanda juu ili kupokea maagizo mbalimbali. Vibao viwili vya mawe vilichongwa na maandishi ya amri kumi za Mungu mlimani. kwamba uwepo wa Mungu ulifunika kilele na wingu zito na umeme mkali wakati wa uchongaji amri kumi za Mungu
    0 Comments 0 Shares 101 Views
  • KWENU MNAOJIITA WACHAMBUZI KWA KOFIA ZA USHABIKI NA CHUKI BINAFSI

    kuna kipindi Azam Fc iliwapa wachezaji 5 Simba sports club ili Simba ichukue Ubingwa

    Kuna kipindi kwenye mchezo mmoja Saido ntibanzokiza aliachiwa magoli matano kwenye mechi moja ili Amfikie Fiston kalala Mayele

    Kuna kipindi mchezaji wa Coastal Union alikwepa mpira uliopigwa na saido ili uwe goli

    Mzunguko wa kwanza michezo 2 ya kwanza ya Simba sc dhidi ya Tabora United na Fountain Gate fc wachezaji walifungiwa na kuonekana hawana vibali baada ya wote kucheza na Simba vibali vyao vilikuwepo na walicheza vema na kushinda

    Mzunguko huu wa pili vivyo hivyo Tabora United wachezaji wake Muhimu walikuwa majeruhi na wengine hawakuwa na vibali ila mara tu baada ya kucheza na Simba wachezaji wote walipata vibali na waliokuwa wanaumwa walipona

    Yanga sc ambayo jana imetufunga goli 2 kwa moja ni kikosi hiki hiki kama sikosei ndicho kilichowalamba Tano ni Yanga hii hii ambayo mtoto amezaliwa na amekuwa hajawahi kuona japo Simba ikipata walau Draw dhidi ya yanga kila siku ni vichapo tu

    Nilichogundua mashabiki wengi wa Simba wana wivu sana huwa wanataka wafungwe wao peke yao na Yanga

    Mkiona hapawafai mnaruhusiwa kuhama ligi ila kwa Taarifa za ndaaaaaaani Yanga wamesema popote mtakapohamia na wenyewe watakuja

    Asubuhi mbaya kwenu wabaya wetu
    KWENU MNAOJIITA WACHAMBUZI KWA KOFIA ZA USHABIKI NA CHUKI BINAFSI kuna kipindi Azam Fc iliwapa wachezaji 5 Simba sports club ili Simba ichukue Ubingwa Kuna kipindi kwenye mchezo mmoja Saido ntibanzokiza aliachiwa magoli matano kwenye mechi moja ili Amfikie Fiston kalala Mayele Kuna kipindi mchezaji wa Coastal Union alikwepa mpira uliopigwa na saido ili uwe goli Mzunguko wa kwanza michezo 2 ya kwanza ya Simba sc dhidi ya Tabora United na Fountain Gate fc wachezaji walifungiwa na kuonekana hawana vibali baada ya wote kucheza na Simba vibali vyao vilikuwepo na walicheza vema na kushinda Mzunguko huu wa pili vivyo hivyo Tabora United wachezaji wake Muhimu walikuwa majeruhi na wengine hawakuwa na vibali ila mara tu baada ya kucheza na Simba wachezaji wote walipata vibali na waliokuwa wanaumwa walipona Yanga sc ambayo jana imetufunga goli 2 kwa moja ni kikosi hiki hiki kama sikosei ndicho kilichowalamba Tano ni Yanga hii hii ambayo mtoto amezaliwa na amekuwa hajawahi kuona japo Simba ikipata walau Draw dhidi ya yanga kila siku ni vichapo tu Nilichogundua mashabiki wengi wa Simba wana wivu sana huwa wanataka wafungwe wao peke yao na Yanga Mkiona hapawafai mnaruhusiwa kuhama ligi ila kwa Taarifa za ndaaaaaaani Yanga wamesema popote mtakapohamia na wenyewe watakuja Asubuhi mbaya kwenu wabaya wetu
    0 Comments 0 Shares 111 Views
  • Katika hatua mpya ya mzozo unaoendelea Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo , kundi la Waasi wa M23 likishirikiana na Muungano wa Mto Congo (AFC) limetangaza kuwa Wanajeshi wa zamani wa Jeshi la DR Congo (FARDC) waliokamatwa au kujisalimisha wamehitimu mafunzo ya kiitikadi na mbinu za kijeshi.

    Katika taarifa ya Kundi la M23 kwenye mtandao wao wa X leo Februari 18, picha zilionyesha Wanajeshi hao wakiwa na sare na silaha rasmi za wanamgambo hao. Ujumbe uliambatana na chapisho hilo ulieleza:

    "Wanajeshi wa zamani wa FARDC, waliokamatwa au kujisalimisha, wamemaliza mafunzo ya kiitikadi na mbinu huko Rumangabo Mjini Goma chini ya AFC/M23. Sasa wakiwa na vifaa kamili na wanaolipwa, wametumwa Lubero, ambako wanashiriki kikamilifu muungano wa serikali."

    Wakati huo huo, Uganda imetangaza kuwa vikosi vyake vya kijeshi vimeanza kuelekea Bunia, DRC, ikiwa ni siku chache baada ya Jeshi la Uganda kutoa muda wa saa 24 kwa Askari waliopo eneo hilo kujisalimisha.

    Taarifa nyingine kuwa, hapo jana Kundi la Waasi hao wa M23 wamefanikiwa kuteka eneo la Kamanyola na sasa hivi wanajipanga kuelekea Uvira, Fizi kisha Mkoa wa Tanganyika (Kalemie) kabla ya kwenda Mjini Lubumbashi. Kwa mujibu wa Wananchi wa Kamanyala wanasema kuwa Kundi la Wapiganaji wa Wazalendo ambao wanapigana kwa upande wa Serikali waliibwa Silaha zao kisha wakakimbia na kuwaachia M23 kuichukua Kamanyola.

    Katika hatua mpya ya mzozo unaoendelea Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 馃嚚馃嚛, kundi la Waasi wa M23 likishirikiana na Muungano wa Mto Congo (AFC) limetangaza kuwa Wanajeshi wa zamani wa Jeshi la DR Congo (FARDC) waliokamatwa au kujisalimisha wamehitimu mafunzo ya kiitikadi na mbinu za kijeshi. Katika taarifa ya Kundi la M23 kwenye mtandao wao wa X leo Februari 18, picha zilionyesha Wanajeshi hao wakiwa na sare na silaha rasmi za wanamgambo hao. Ujumbe uliambatana na chapisho hilo ulieleza: "Wanajeshi wa zamani wa FARDC, waliokamatwa au kujisalimisha, wamemaliza mafunzo ya kiitikadi na mbinu huko Rumangabo Mjini Goma chini ya AFC/M23. Sasa wakiwa na vifaa kamili na wanaolipwa, wametumwa Lubero, ambako wanashiriki kikamilifu muungano wa serikali." Wakati huo huo, Uganda imetangaza kuwa vikosi vyake vya kijeshi vimeanza kuelekea Bunia, DRC, ikiwa ni siku chache baada ya Jeshi la Uganda kutoa muda wa saa 24 kwa Askari waliopo eneo hilo kujisalimisha. Taarifa nyingine kuwa, hapo jana Kundi la Waasi hao wa M23 wamefanikiwa kuteka eneo la Kamanyola na sasa hivi wanajipanga kuelekea Uvira, Fizi kisha Mkoa wa Tanganyika (Kalemie) kabla ya kwenda Mjini Lubumbashi. Kwa mujibu wa Wananchi wa Kamanyala wanasema kuwa Kundi la Wapiganaji wa Wazalendo ambao wanapigana kwa upande wa Serikali waliibwa Silaha zao kisha wakakimbia na kuwaachia M23 kuichukua Kamanyola.
    0 Comments 0 Shares 162 Views
  • “Ukiwa Mwandishi wa Habari una vitu viwili muhimu vya kuchunga navyo ni Ulimi wako na Mikono yako, unapaswa kufahamu unaongea nini ama unaandika kitu gani, nyuma ya mauaji ya Kimbari yalikuwa ni matamshi ya Watangazaji pia ambao walieneza chuki, kwasasa kuna kazi mbili za hatari nazo ni Ualimu na Waandishi wa Habari, hawa wanaweza kutengeneza taifa la Wajinga ama Waelevu.

    Nataka kusema nini? Nataka kusema juu ya kelele na shutuma za Yanga na Singida bado hakuna aliyetupa picha kamili zaidi ni kuwa Mashabiki wanalalamika kwa hisia, Waandishi tunalalamika kwa hisia ila hakuna anayekuja mbele kutoa usahihi, inaitwa Proving beyond reasonable doubt! Nimeona Wadau wanasema TFF haifanyi chochote, lakini wewe umewapa tip gani? Taasisi haifanyi maamuzi kwa hisia, the corporate world works differently from streets.

    Bado kizazi chetu cha Uandishi kuna kitu kinamiss ni INVESTIGATIVE JOURNALISM, binafsi nakiri wazi TUMEFELI sana eneo hili, yaani sote tunalaumu Singida kufanya rotation tunaita kupanga matokeo, tangu lini duniani kubadili kikosi chako ni kupanga matokeo? Ikitokea Coastal kabadili kikosi, ikitokea Simba kabadili ama AZAM? Yani timu inalaumiwa kwa kutumia Wachezaji wake?

    Tunaweza kuwa na hoja ila mpaka sasa hazina mashiko zaidi tunaonekana tunalalama ila tukipelekwa Mahakamani hakuna ambaye atathibitisha chochote, kama kufungwa ni kupanga matokeo mara ya mwisho Simba kumfunga Yanga ndani ya dakika 90 ni lini? Kama kufungwa ni kupanga matokeo lini Singida kamfunga Simba? Kama kufungwa ni kupanga lini Namungo kamfunga Simba lini?

    Sisi WAANDISHI tuna homework tunapaswa kufanya, tutaharibu fikra za Watanzania! Wenzetu Ulaya walipoibua kashfa ya Casciopoli pale Italia walikuja na data, hata UEFA Heated Balls Scandal watu walikuwa na data! Yanga wakisema waende kisheria nani anaweza kuja na hoja za kueleweka? Kama hakuna taarifa sahihi, mifano hai basi tunaongelea hisia, TFF atareact endapo atajitokea Mtu akaattack matter not the subject" - Farhan JR, Mchambuzi.

    “Ukiwa Mwandishi wa Habari una vitu viwili muhimu vya kuchunga navyo ni Ulimi wako na Mikono yako, unapaswa kufahamu unaongea nini ama unaandika kitu gani, nyuma ya mauaji ya Kimbari yalikuwa ni matamshi ya Watangazaji pia ambao walieneza chuki, kwasasa kuna kazi mbili za hatari nazo ni Ualimu na Waandishi wa Habari, hawa wanaweza kutengeneza taifa la Wajinga ama Waelevu. Nataka kusema nini? Nataka kusema juu ya kelele na shutuma za Yanga na Singida bado hakuna aliyetupa picha kamili zaidi ni kuwa Mashabiki wanalalamika kwa hisia, Waandishi tunalalamika kwa hisia ila hakuna anayekuja mbele kutoa usahihi, inaitwa Proving beyond reasonable doubt! Nimeona Wadau wanasema TFF haifanyi chochote, lakini wewe umewapa tip gani? Taasisi haifanyi maamuzi kwa hisia, the corporate world works differently from streets. Bado kizazi chetu cha Uandishi kuna kitu kinamiss ni INVESTIGATIVE JOURNALISM, binafsi nakiri wazi TUMEFELI sana eneo hili, yaani sote tunalaumu Singida kufanya rotation tunaita kupanga matokeo, tangu lini duniani kubadili kikosi chako ni kupanga matokeo? Ikitokea Coastal kabadili kikosi, ikitokea Simba kabadili ama AZAM? Yani timu inalaumiwa kwa kutumia Wachezaji wake? Tunaweza kuwa na hoja ila mpaka sasa hazina mashiko zaidi tunaonekana tunalalama ila tukipelekwa Mahakamani hakuna ambaye atathibitisha chochote, kama kufungwa ni kupanga matokeo mara ya mwisho Simba kumfunga Yanga ndani ya dakika 90 ni lini? Kama kufungwa ni kupanga matokeo lini Singida kamfunga Simba? Kama kufungwa ni kupanga lini Namungo kamfunga Simba lini? Sisi WAANDISHI tuna homework tunapaswa kufanya, tutaharibu fikra za Watanzania! Wenzetu Ulaya walipoibua kashfa ya Casciopoli pale Italia walikuja na data, hata UEFA Heated Balls Scandal watu walikuwa na data! Yanga wakisema waende kisheria nani anaweza kuja na hoja za kueleweka? Kama hakuna taarifa sahihi, mifano hai basi tunaongelea hisia, TFF atareact endapo atajitokea Mtu akaattack matter not the subject" - Farhan JR, Mchambuzi.
    0 Comments 0 Shares 217 Views
  • Zakazakazi azidi kumshushia nondo Amri Kiemba.

    MUONGO!

    Amri Kiemba alicheza Simba kwa misimu mitano na nusu, kuanzia 2009/10 hadi Disemba 2014.

    Katika kipindi hicho, Azam FC na Simba zilikutana mara 10, Simba ikishinda mara tano na Azam FC mara tatu, na mara mbili sare...angalia picha ya pili.

    Katika hizo mara tano ambazo Simba ilishinda, mbili ni za msimu wa 2009/10.

    24/10/2009
    Simba 1-0 Azam FC

    14/3/2010
    Azam FC 0-2 Simba

    Huu ulikuwa msimu ambao Simba ilikuwa kwenye ubora mkubwa sana na ikamaliza ligi bila kupoteza hata mchezo mmoja.

    Walishinda mechi zote za mzunguko wa kwanza, wakaja kupata sare mbili tu mzunguko wa pili, dhidi ya Kagera Sugar na African Lyon.

    Kwa ubora huo, huwezi kuilamu Azam FC ilhali timu zote zilifungwa...kiungwana unawasifia Simba kwamba walikuwa kwenye ubora wa hali ya juu.

    Lakini baada ya msimu huo, Azam FC na Simba zililingana matokeo hadi Kiemba alipoondoka Simba kwenda Azam FC.

    Swali ni je, Kiemba anapata wapi uhalali wa kutilia shaka maandalizi yaliyoleta matokeo kama haya?

    Msimu wa 2013/14, Azam FC ikawa kwenye ubora mkubwa na kumaliza ligi bila kupoteza hata mchezo mmoja, ikiwemo kushinda nje ndani dhidi ya Simba ya Kiemba na maandalizi yao ya hali ya juu.

    28/10/2013
    Simba 1-2 Azam FC

    30/3/2014
    Azam FC 2-1 Simba

    Baada ya mechi hizi Kiemba akaenda Azam FC...na mechi yake ya kwanza ikaisha kwa sare ya 1-1.

    Ni vipi Kiemba hakuridhika na maandalizi ya Azam FC yaliyoleta sare lakini aliridhika na maandalizi ya Simba yaliyowafanya wafungwe nje ndani msimu mmoja tu nyuma yake?

    Msimu mmoja kabla Kiemba hajasajiliwa Simba, Azam FC ilishinda 2-0 na mashabiki wa Simba wakaenda kushusha kinyesi nyumbani kwa mwenyekiti wao Hassan Dalali.

    Ina maana maandalizi ya Azam FC yangekuwa hafifu yangewatoa kinyesi Simba kweli?

    Azam FC ilikuwa inaifunga Simba kabla yeye hajaenda, na ikaifunga akiwemo...kwa maandalizi yale yale...halafu anakuja hadharani leo, miaka zaidi ya 10 na kusema aliona maandalizi hafifu...sasa walikuwa wanashindaje kwa maandalizi hafifu?

    Ni mbaya sana kumuita mtu muongo...lakini Kiemba kwenye hili itoshe tu kusema kwamba WEWE NI MUONGO!

    Zakazakazi azidi kumshushia nondo Amri Kiemba. MUONGO! Amri Kiemba alicheza Simba kwa misimu mitano na nusu, kuanzia 2009/10 hadi Disemba 2014. Katika kipindi hicho, Azam FC na Simba zilikutana mara 10, Simba ikishinda mara tano na Azam FC mara tatu, na mara mbili sare...angalia picha ya pili. Katika hizo mara tano ambazo Simba ilishinda, mbili ni za msimu wa 2009/10. 24/10/2009 Simba 1-0 Azam FC 14/3/2010 Azam FC 0-2 Simba Huu ulikuwa msimu ambao Simba ilikuwa kwenye ubora mkubwa sana na ikamaliza ligi bila kupoteza hata mchezo mmoja. Walishinda mechi zote za mzunguko wa kwanza, wakaja kupata sare mbili tu mzunguko wa pili, dhidi ya Kagera Sugar na African Lyon. Kwa ubora huo, huwezi kuilamu Azam FC ilhali timu zote zilifungwa...kiungwana unawasifia Simba kwamba walikuwa kwenye ubora wa hali ya juu. Lakini baada ya msimu huo, Azam FC na Simba zililingana matokeo hadi Kiemba alipoondoka Simba kwenda Azam FC. Swali ni je, Kiemba anapata wapi uhalali wa kutilia shaka maandalizi yaliyoleta matokeo kama haya? Msimu wa 2013/14, Azam FC ikawa kwenye ubora mkubwa na kumaliza ligi bila kupoteza hata mchezo mmoja, ikiwemo kushinda nje ndani dhidi ya Simba ya Kiemba na maandalizi yao ya hali ya juu. 28/10/2013 Simba 1-2 Azam FC 30/3/2014 Azam FC 2-1 Simba Baada ya mechi hizi Kiemba akaenda Azam FC...na mechi yake ya kwanza ikaisha kwa sare ya 1-1. Ni vipi Kiemba hakuridhika na maandalizi ya Azam FC yaliyoleta sare lakini aliridhika na maandalizi ya Simba yaliyowafanya wafungwe nje ndani msimu mmoja tu nyuma yake? Msimu mmoja kabla Kiemba hajasajiliwa Simba, Azam FC ilishinda 2-0 na mashabiki wa Simba wakaenda kushusha kinyesi nyumbani kwa mwenyekiti wao Hassan Dalali. Ina maana maandalizi ya Azam FC yangekuwa hafifu yangewatoa kinyesi Simba kweli? Azam FC ilikuwa inaifunga Simba kabla yeye hajaenda, na ikaifunga akiwemo...kwa maandalizi yale yale...halafu anakuja hadharani leo, miaka zaidi ya 10 na kusema aliona maandalizi hafifu...sasa walikuwa wanashindaje kwa maandalizi hafifu? Ni mbaya sana kumuita mtu muongo...lakini Kiemba kwenye hili itoshe tu kusema kwamba WEWE NI MUONGO!
    0 Comments 0 Shares 135 Views
  • Zakazakazi amjibu Amri Kiemba.

    TUONGEE KWA FACT

    Ni kweli kwamba Amri Kiemba alicheza Azam FC kwa mkopo wa miezi 6 akitokea Simba, 2014/15.

    Alisajiliwa dirisha dogo lililofunguliwa Disemba 15, 2014, na walikuja wawili, yeye na Saad Kawemba kama mtendaji mku (CEO).

    Akiwa Azam FC, Kiemba alikutana na mechi mbili dhidi ya Simba,

    24/01/2015
    Azam FC 1-1 Simba

    Hii mechi ndiyo ile ambayo Aggrey Morris alimfanyia madhambi Okwi hadi akapoteza fahamu...akaenda kuzindukia hospitali.

    02/05/2015
    Simba 2-1 Azam FC

    Hii mechi kwa asilimia kubwa iliamuliwa na kadi nyekundu ya Salum Abubakar dakika 38, na kuumia kwa Frank Domayo dakika chache baadaye.

    Lakini hadi wakati huo, Azam FC ilikuwa imeushika mchezo hasa. Kipindi cha pili Simba wakapata goli, Azam FC ikiwa pungufu ikasawazisha...dakika za jioni Simba wakapata bao la pili.

    Hii ilikuwa mechi ya kwanza ya Simba kuifunga Azam FC tangu Oktoba 27, 2012 kwenye ile mechi ambayo Azam FC ilisimamisha wachezaji wanne ikiwatuhumu kuihujumu timu.

    Wachezaji hawa ni Agrey Morris, Erasto Nyoni, Dida na Said Morad...na walisimamishwa hadi Aprili 2013. Yaani timu ifanye maandalizi finyu halafu isimamishe wachezaji wanne kwa takribani miezi 6?

    Simba baada ya kushinda mchezo huo, hawakushinda tena ndiyo hadi 2015...na 2016...tena hadi 2018.

    Kuanzia 2013 hadi 2017 Simba walishinda mechi mbili tu dhidi ya Azam...halafu Kiemba anasema alikuwa haoni maandalizi...maandalizi gani?

    Kama adui yako anakufa kwa asali, kwanini umpige bunduki?

    Kiemba alikuwa Simba ambayo ilifungwa mfululizo na Azam FC kwa miaka mitatu...walikuwa wanajiandaaje huko?

    Kiemba anaheshimika sana, lakini huu ushuhuda wake wa kupika unamvunjia heshima.

    Eti maandalizi dhidi ya Yanga yalikuwa tofauti. Ok...akiwa Azam FC, Kiemba alikutana na mechi mbili dhidi ya Yanga.

    28/12/2014
    Yanga 2-2 Azam FC

    06/05/2015
    Azam FC 2-1 Yanga

    Hii mechi ndiyo ile ya siku ya mvua nyingi, Yanga wameshakuwa mabingwa.

    Coutinho anataka kupiga faulo, Ngassa anamnyang'anya mpira.

    Kwa wanaokumbuka, wataikumbuka mechi hii.

    Huu ulikuwa mchezo wa kwanza Azam FC kuifunga Yanga tangu 2013, lakini katika kipindi hicho, Simba akichomoka kwa Azam, ni sare!

    Zakazakazi amjibu Amri Kiemba. TUONGEE KWA FACT Ni kweli kwamba Amri Kiemba alicheza Azam FC kwa mkopo wa miezi 6 akitokea Simba, 2014/15. Alisajiliwa dirisha dogo lililofunguliwa Disemba 15, 2014, na walikuja wawili, yeye na Saad Kawemba kama mtendaji mku (CEO). Akiwa Azam FC, Kiemba alikutana na mechi mbili dhidi ya Simba, 24/01/2015 Azam FC 1-1 Simba Hii mechi ndiyo ile ambayo Aggrey Morris alimfanyia madhambi Okwi hadi akapoteza fahamu...akaenda kuzindukia hospitali. 02/05/2015 Simba 2-1 Azam FC Hii mechi kwa asilimia kubwa iliamuliwa na kadi nyekundu ya Salum Abubakar dakika 38, na kuumia kwa Frank Domayo dakika chache baadaye. Lakini hadi wakati huo, Azam FC ilikuwa imeushika mchezo hasa. Kipindi cha pili Simba wakapata goli, Azam FC ikiwa pungufu ikasawazisha...dakika za jioni Simba wakapata bao la pili. Hii ilikuwa mechi ya kwanza ya Simba kuifunga Azam FC tangu Oktoba 27, 2012 kwenye ile mechi ambayo Azam FC ilisimamisha wachezaji wanne ikiwatuhumu kuihujumu timu. Wachezaji hawa ni Agrey Morris, Erasto Nyoni, Dida na Said Morad...na walisimamishwa hadi Aprili 2013. Yaani timu ifanye maandalizi finyu halafu isimamishe wachezaji wanne kwa takribani miezi 6? Simba baada ya kushinda mchezo huo, hawakushinda tena ndiyo hadi 2015...na 2016...tena hadi 2018. Kuanzia 2013 hadi 2017 Simba walishinda mechi mbili tu dhidi ya Azam...halafu Kiemba anasema alikuwa haoni maandalizi...maandalizi gani? Kama adui yako anakufa kwa asali, kwanini umpige bunduki? Kiemba alikuwa Simba ambayo ilifungwa mfululizo na Azam FC kwa miaka mitatu...walikuwa wanajiandaaje huko? Kiemba anaheshimika sana, lakini huu ushuhuda wake wa kupika unamvunjia heshima. Eti maandalizi dhidi ya Yanga yalikuwa tofauti. Ok...akiwa Azam FC, Kiemba alikutana na mechi mbili dhidi ya Yanga. 28/12/2014 Yanga 2-2 Azam FC 06/05/2015 Azam FC 2-1 Yanga Hii mechi ndiyo ile ya siku ya mvua nyingi, Yanga wameshakuwa mabingwa. Coutinho anataka kupiga faulo, Ngassa anamnyang'anya mpira. Kwa wanaokumbuka, wataikumbuka mechi hii. Huu ulikuwa mchezo wa kwanza Azam FC kuifunga Yanga tangu 2013, lakini katika kipindi hicho, Simba akichomoka kwa Azam, ni sare!
    0 Comments 0 Shares 101 Views
  • "Kwa mijadala ambayo nimeitazama inaendelea baada ya mchezo wa Yanga na Singida Black Stars inaonyesha kuwa asilimia kubwa ya watu walikuwa na matokeo ya Singida kushinda kwenye mechi hiyo.

    Kikawaida mwalimu anaweza kupanga kikosi kulingana na mahitaji ya mchezo husika na namna ambavyo amewasoma wapinzani na sio mchezaji bora anaweza kuanza kwenye mechi.

    Kinachoendelea kwasasa ni kuzinyima uhuru hizi timu za madaraja ya chini kuamua wachezaji zitakazowatumia kwenye michezo yake dhidi ya Simba na Yanga.

    Hii pia ni aina moja wapo ya kudumaza soka letu. Yanga kwenye ubora wao kila timu imepata ilichokitegemea, kila timu imevuna ilichokipanda.Ili timu isiwe imepanga matokeo lazima iifunge Yanga? Na ikifungwa tu basi imepanga matokeo?

    Tuwape uhuru makocha wa kuamua nyota watakaocheza kwenye michezo husika kulingana na mbinu za wapinzani wao." - Lameck Shabahanga Mwandishi wa habari.

    "Kwa mijadala ambayo nimeitazama inaendelea baada ya mchezo wa Yanga na Singida Black Stars inaonyesha kuwa asilimia kubwa ya watu walikuwa na matokeo ya Singida kushinda kwenye mechi hiyo. Kikawaida mwalimu anaweza kupanga kikosi kulingana na mahitaji ya mchezo husika na namna ambavyo amewasoma wapinzani na sio mchezaji bora anaweza kuanza kwenye mechi. Kinachoendelea kwasasa ni kuzinyima uhuru hizi timu za madaraja ya chini kuamua wachezaji zitakazowatumia kwenye michezo yake dhidi ya Simba na Yanga. Hii pia ni aina moja wapo ya kudumaza soka letu. Yanga kwenye ubora wao kila timu imepata ilichokitegemea, kila timu imevuna ilichokipanda.Ili timu isiwe imepanga matokeo lazima iifunge Yanga? Na ikifungwa tu basi imepanga matokeo? Tuwape uhuru makocha wa kuamua nyota watakaocheza kwenye michezo husika kulingana na mbinu za wapinzani wao." - Lameck Shabahanga Mwandishi wa habari.
    0 Comments 0 Shares 117 Views
  • "Wakati tunazilaumu Simba Sports na Azam Football Club Kuukosa Ubingwa,tukumbuke pia Mazingira Yao Magumu ya Kushindana

    Parameters za Simba Sports na Azam Fc Kuchukua Ubingwa zimebadilika Kabisa na ni tofauti Washindani wenzao Kwenye Ligi

    Kuna hoja Lazy sana eti Mbona Simba Sports alicheza na Tabora United Dhaifu?

    Kwenye Mechi zote 2 Tabora wana uwezo wa Ku justifie Kwanini walichezesha Vikosi vile na ukawaelewa vizuri tu.

    Mechi ya Kwanza n issue ya Vibali,na mechi ya Pili Heritier Makambo alikuwa na Kadi 3 za njano. Yacouba Sogne alikuwa ni Majeruhi..

    Kuna hoja Lazy nyingine Kwamba mbona Kikosi bora cha Singida Black Stars Kilifungwa 2-0 na KMC ambayo ilifungwa 6-1 na Yanga?

    Kwanza Kwenye hiyo hoja hapo wote tumekubaliana Kwamba Singida Black Stars wamepanga Kikosi Dhaifu

    Pili, Sisi hatusemi Singida Black Stars angepanga Kikosi bora lazima angeshinda dhidi ya Yanga au asingepoteza mechi

    Mbona ile Mechi ya Kwanza Kule Amani Complex Zanzibar Singida Black Stars waliweka Full Mkoko na bado Yanga alishinda 1-0 bao la Paccome ?

    Swali ni Sababu ipi ya Singida Black Stars Kubadilisha wachezaji 6 Kutoka Kwenye Kikosi Kilichomfunga Jkt Tanzania 1-0?

    Mbaya zaidi Kuna wachezaji walichezeshwa Kabisa nje ya Maeneo ya ya asili na wachezaji wenye nafasi zao wakiwa bench

    Singida black stars Dhaifu ilipigwa 2-0 Kipindi Cha Kwanza na Stars bora ilishinda 1-0 Kipindi cha Pili.

    Ligi yetu tukufu inachezewa na watu ambao hawana nia njema na Mpira wetu na Kama tusipotwanga sasa hivi tutakuja Kuula Mbichi" - Wilson Orumo, Mchambuzi.

    "Wakati tunazilaumu Simba Sports na Azam Football Club Kuukosa Ubingwa,tukumbuke pia Mazingira Yao Magumu ya Kushindana Parameters za Simba Sports na Azam Fc Kuchukua Ubingwa zimebadilika Kabisa na ni tofauti Washindani wenzao Kwenye Ligi Kuna hoja Lazy sana eti Mbona Simba Sports alicheza na Tabora United Dhaifu? Kwenye Mechi zote 2 Tabora wana uwezo wa Ku justifie Kwanini walichezesha Vikosi vile na ukawaelewa vizuri tu. Mechi ya Kwanza n issue ya Vibali,na mechi ya Pili Heritier Makambo alikuwa na Kadi 3 za njano. Yacouba Sogne alikuwa ni Majeruhi.. Kuna hoja Lazy nyingine Kwamba mbona Kikosi bora cha Singida Black Stars Kilifungwa 2-0 na KMC ambayo ilifungwa 6-1 na Yanga? Kwanza Kwenye hiyo hoja hapo wote tumekubaliana Kwamba Singida Black Stars wamepanga Kikosi Dhaifu Pili, Sisi hatusemi Singida Black Stars angepanga Kikosi bora lazima angeshinda dhidi ya Yanga au asingepoteza mechi Mbona ile Mechi ya Kwanza Kule Amani Complex Zanzibar Singida Black Stars waliweka Full Mkoko na bado Yanga alishinda 1-0 bao la Paccome ? Swali ni Sababu ipi ya Singida Black Stars Kubadilisha wachezaji 6 Kutoka Kwenye Kikosi Kilichomfunga Jkt Tanzania 1-0? Mbaya zaidi Kuna wachezaji walichezeshwa Kabisa nje ya Maeneo ya ya asili na wachezaji wenye nafasi zao wakiwa bench Singida black stars Dhaifu ilipigwa 2-0 Kipindi Cha Kwanza na Stars bora ilishinda 1-0 Kipindi cha Pili. Ligi yetu tukufu inachezewa na watu ambao hawana nia njema na Mpira wetu na Kama tusipotwanga sasa hivi tutakuja Kuula Mbichi" - Wilson Orumo, Mchambuzi.
    0 Comments 0 Shares 131 Views

  • KUTOKA SINGIDA BLACK STARS

    HII NI KWENU WACHAMBUZI WOTE WENYE USHABIKI KULIKO UCHAMBUZI

    Singida Black stars Sc ni Timu yenye utaratibu wake na mipango yake juu ya kuiongoza Timu yake kwa misingi yake

    Timu yetu haipangiwi na wala hatupelekeshwi na maneno ya mitandaoni katika kuiendesha Timu Yetu, Tunaomba Mfahamu kuwa kila mchezaji Tuliyemsajili anatufaa na anafaa kuipambania Nembo ya Timu yetu

    Katika kikosi chetu chenye jumla ya wachezaji 33 wote wakiwa wazima wa Afya na Fitness nzuri kocha wetu na Benchi letu la Ufundi lina uhuru wa Kumchagua Mchezaji yeyote akaanza katika kikosi cha kwanza katika mchezo wowote

    Rejea michezo Yetu Mitatu ya nyuma kabla ya mchezo wa jana dhidi ya Yanga sc Tulicheza michezo 3 dhidi ya Kagera Sugar, KMC Fc, na JKT Tanzania

    Katika mchezo wetu dhidi ya Kagera sugar tulianzisha wachezaji wengi wa kimataifa na Tulipata sare ya goli 2-2 mchezo uliofuata tukacheza dhidi ya KMC FC na wachezaji wengi wa kimataifa walianza pia tukafungwa goli 2 bila Benchi la ufundi kikafanya mabadiliko kadhaa kwenye mchezo uliofuata dhidi ya JKT Tanzania Na tukapata ushindi kwenye moja ya Viwanja ambavyo Timu zote za ligi kuu hakuna iliyopata ushindi

    Baada ya Benchi la Ufundi kuridhika na vipaji vya wachezaji wetu wa ndani waliotupa Ushindi wa mchezo wa JKT Tanzania wakaridhishwa kwamba wachezaji wale wanafaa baadhi yao kuanza kwenye mchezo dhidi ya Yanga, kwa upande wa Timu yetu Tumefurahi Timu ilicheza vizuri kwa nidhamu ya hali ya juu na mchezo ukaisha kwa goal 2-1

    Sasa baada ya mchezo ule wameibuka watu wanaojiita wachambuzi kwa vivuli vya ushabiki wao na roho zao mbaya na umaskini uliowajaa wanataka kutupangia Kikosi chetu kitu Ambacho kwetu hakikubaliki hata kidogo

    Ni mfano uone mwanaume Ameoa wake 4 alafu wewe jirani yake unataka kumpangia kwamba Leo kalale kwa mwanamke huyu na utapikiwa na huyu hilo haliwezekani Abadani SISI HATUPANGIWI MAISHA NA VITAKATAKA KAMA NYINYI
    KUTOKA SINGIDA BLACK STARS 鉁嶏笍 HII NI KWENU WACHAMBUZI WOTE WENYE USHABIKI KULIKO UCHAMBUZI Singida Black stars Sc ni Timu yenye utaratibu wake na mipango yake juu ya kuiongoza Timu yake kwa misingi yake Timu yetu haipangiwi na wala hatupelekeshwi na maneno ya mitandaoni katika kuiendesha Timu Yetu, Tunaomba Mfahamu kuwa kila mchezaji Tuliyemsajili anatufaa na anafaa kuipambania Nembo ya Timu yetu Katika kikosi chetu chenye jumla ya wachezaji 33 wote wakiwa wazima wa Afya na Fitness nzuri kocha wetu na Benchi letu la Ufundi lina uhuru wa Kumchagua Mchezaji yeyote akaanza katika kikosi cha kwanza katika mchezo wowote Rejea michezo Yetu Mitatu ya nyuma kabla ya mchezo wa jana dhidi ya Yanga sc Tulicheza michezo 3 dhidi ya Kagera Sugar, KMC Fc, na JKT Tanzania Katika mchezo wetu dhidi ya Kagera sugar tulianzisha wachezaji wengi wa kimataifa na Tulipata sare ya goli 2-2 mchezo uliofuata tukacheza dhidi ya KMC FC na wachezaji wengi wa kimataifa walianza pia tukafungwa goli 2 bila Benchi la ufundi kikafanya mabadiliko kadhaa kwenye mchezo uliofuata dhidi ya JKT Tanzania Na tukapata ushindi kwenye moja ya Viwanja ambavyo Timu zote za ligi kuu hakuna iliyopata ushindi Baada ya Benchi la Ufundi kuridhika na vipaji vya wachezaji wetu wa ndani waliotupa Ushindi wa mchezo wa JKT Tanzania wakaridhishwa kwamba wachezaji wale wanafaa baadhi yao kuanza kwenye mchezo dhidi ya Yanga, kwa upande wa Timu yetu Tumefurahi Timu ilicheza vizuri kwa nidhamu ya hali ya juu na mchezo ukaisha kwa goal 2-1 Sasa baada ya mchezo ule wameibuka watu wanaojiita wachambuzi kwa vivuli vya ushabiki wao na roho zao mbaya na umaskini uliowajaa wanataka kutupangia Kikosi chetu kitu Ambacho kwetu hakikubaliki hata kidogo Ni mfano uone mwanaume Ameoa wake 4 alafu wewe jirani yake unataka kumpangia kwamba Leo kalale kwa mwanamke huyu na utapikiwa na huyu hilo haliwezekani Abadani SISI HATUPANGIWI MAISHA NA VITAKATAKA KAMA NYINYI
    0 Comments 0 Shares 150 Views
  • KUWA MAKINI UNAYEMSHIRIKISHA SIRI ZAKO...

    Nenda kwenye mitandao ya kijamii uone jinsi wanaume waliokomaa wenye ndevu na wanawake wakubwa wenye mawigi ya bei wanavyojidhalilisha. Unapoona jinsi watu wanavyoshiriki mambo ya faragha kwenye maeneo ya umma, utaelewa kwa nini mambo fulani yanakusudiwa kuwa siri. Kutoka kona moja hadi nyingine, kwa nia ya kumrudia aliyewaudhi, watu wanashuka sana, na hawajali jinsi chochote watakachofichua kitawaathiri katika siku zijazo, wanachojali ni kumpiga yule wanayehisi kukanyagwa kwenye vidole vyao. Kuanzia mazungumzo yaliyovuja, video kuvuja, hadi mazungumzo ya faragha, nilichojifunza ni kwamba sio kila mtu anayetabasamu na wewe ana uwezo wa kutunza siri zako. Mitandao ya kijamii imetufundisha somo hili kwa njia ya kikatili zaidi. Tumeona marafiki waliopendana mara moja, mahusiano ya mara moja-tamu, ushirikiano wa mara moja-imara ukiporomoka katika ushindani mkali, na siri zilizomwagika kama maji machafu mitaani. Tumeona maungamo ya kibinafsi yakigeuzwa kuwa fedheha hadharani, na uaminifu mkubwa ukivunjwa na chapisho moja, maoni moja, kufichuliwa mara moja. Watu wengine wana kuhara kwa mdomo. Hawajui jinsi ya kushikilia kile walichoambiwa kwa ujasiri. Hawaoni siri kuwa takatifu; wanaziona kama silaha, kimya kwa sasa, lakini tayari kuachiliwa wakati mawimbi yanabadilika. Na mawimbi hubadilika kila wakati.

    Hakuna kitu kibaya kwa kuwaamini watu, lakini kuna kitu hatari kwa kuamini kwa urahisi sana. Maisha yametufundisha kuwa sio kila anayekusikiliza anakusikiliza kwa mapenzi, wengine wanakusanya data. Wengine wanangojea, kwa subira, kwa wakati sahihi wa kutumia maneno yako dhidi yako. Rafiki leo anaweza kuwa mgeni kesho. Mpenzi leo anaweza kuwa adui wiki ijayo. Huyo mwenzako, huyo jamaa, huyo mtu unayemtajia wakati wote ni mtamu, wanaweza kuficha siri yako wakati mambo yanaharibika? Wengi hawawezi. Wengi hawataweza. Kwa hivyo, weka siri zako, siri. Ikiwa huwezi kuiweka mwenyewe, kwa nini unapaswa kutarajia mtu mwingine? Ikiwa kina kina sana kwako kubeba peke yako, kuwa mwangalifu unaiweka mikononi mwa nani. Baadhi ya watu ni wadogo. Hawaachi tu na kuondoka; lazima wachafue weupe wako kabla hawajaondoka. Ni lazima wakuvute kwenye matope, lazima wafichue kile kilichokusudiwa kuwa kitakatifu, lazima watumie wanachokijua kukuletea aibu. Na ndio maana lazima uwe na hekima. Zingatia kile unachoshiriki wakati jua linawaka katika urafiki wako. Kuwa mwangalifu kile unachosema wakati kila kitu ni cha kimapenzi na cha kupendeza. Kwa sababu upendo ni mtamu, lakini watu wengine wanapoanguka kutoka kwa upendo, hugeuka kuwa mbwa mwitu.

    Wapende watu, lakini usiwe mjinga. Sio kila anayekusikia atakulinda. Na misimu inapobadilika, uhusiano unapovunjika, urafiki unapoisha, utatamani ungejiwekea mambo fulani. Uwe mwenye busara. Uwe na hekima. Zuia nyeupe yako isichafuke.

    KUWA MAKINI UNAYEMSHIRIKISHA SIRI ZAKO... Nenda kwenye mitandao ya kijamii uone jinsi wanaume waliokomaa wenye ndevu na wanawake wakubwa wenye mawigi ya bei wanavyojidhalilisha. Unapoona jinsi watu wanavyoshiriki mambo ya faragha kwenye maeneo ya umma, utaelewa kwa nini mambo fulani yanakusudiwa kuwa siri. Kutoka kona moja hadi nyingine, kwa nia ya kumrudia aliyewaudhi, watu wanashuka sana, na hawajali jinsi chochote watakachofichua kitawaathiri katika siku zijazo, wanachojali ni kumpiga yule wanayehisi kukanyagwa kwenye vidole vyao. Kuanzia mazungumzo yaliyovuja, video kuvuja, hadi mazungumzo ya faragha, nilichojifunza ni kwamba sio kila mtu anayetabasamu na wewe ana uwezo wa kutunza siri zako. Mitandao ya kijamii imetufundisha somo hili kwa njia ya kikatili zaidi. Tumeona marafiki waliopendana mara moja, mahusiano ya mara moja-tamu, ushirikiano wa mara moja-imara ukiporomoka katika ushindani mkali, na siri zilizomwagika kama maji machafu mitaani. Tumeona maungamo ya kibinafsi yakigeuzwa kuwa fedheha hadharani, na uaminifu mkubwa ukivunjwa na chapisho moja, maoni moja, kufichuliwa mara moja. Watu wengine wana kuhara kwa mdomo. Hawajui jinsi ya kushikilia kile walichoambiwa kwa ujasiri. Hawaoni siri kuwa takatifu; wanaziona kama silaha, kimya kwa sasa, lakini tayari kuachiliwa wakati mawimbi yanabadilika. Na mawimbi hubadilika kila wakati. Hakuna kitu kibaya kwa kuwaamini watu, lakini kuna kitu hatari kwa kuamini kwa urahisi sana. Maisha yametufundisha kuwa sio kila anayekusikiliza anakusikiliza kwa mapenzi, wengine wanakusanya data. Wengine wanangojea, kwa subira, kwa wakati sahihi wa kutumia maneno yako dhidi yako. Rafiki leo anaweza kuwa mgeni kesho. Mpenzi leo anaweza kuwa adui wiki ijayo. Huyo mwenzako, huyo jamaa, huyo mtu unayemtajia wakati wote ni mtamu, wanaweza kuficha siri yako wakati mambo yanaharibika? Wengi hawawezi. Wengi hawataweza. Kwa hivyo, weka siri zako, siri. Ikiwa huwezi kuiweka mwenyewe, kwa nini unapaswa kutarajia mtu mwingine? Ikiwa kina kina sana kwako kubeba peke yako, kuwa mwangalifu unaiweka mikononi mwa nani. Baadhi ya watu ni wadogo. Hawaachi tu na kuondoka; lazima wachafue weupe wako kabla hawajaondoka. Ni lazima wakuvute kwenye matope, lazima wafichue kile kilichokusudiwa kuwa kitakatifu, lazima watumie wanachokijua kukuletea aibu. Na ndio maana lazima uwe na hekima. Zingatia kile unachoshiriki wakati jua linawaka katika urafiki wako. Kuwa mwangalifu kile unachosema wakati kila kitu ni cha kimapenzi na cha kupendeza. Kwa sababu upendo ni mtamu, lakini watu wengine wanapoanguka kutoka kwa upendo, hugeuka kuwa mbwa mwitu. Wapende watu, lakini usiwe mjinga. Sio kila anayekusikia atakulinda. Na misimu inapobadilika, uhusiano unapovunjika, urafiki unapoisha, utatamani ungejiwekea mambo fulani. Uwe mwenye busara. Uwe na hekima. Zuia nyeupe yako isichafuke.
    Love
    1
    0 Comments 0 Shares 133 Views
  • TSHISEKEDI JIFUNZE KWA NETANYAHU

    "Mnakumbuka kauli ya Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kwamba hata iweje hata zungumza na Hamas ?
    Tena Netanyahu akajitapa akisema kamwe Israel haitazungumza na magaidi, Netanyahu alisema hayo akijua fika ana sapoti kubwa ya Marekani inayompa nguvu na uwezo wa kila aina unaohitajika wa kijeshi!!

    Lakini mwisho wa siku Netanyahu alikaa chini na Hamas na kuzungumza baada ya hapo mateka pamoja na wafungwa wanaachiwa amani imerudi kiasi Gaza

    Somo kwa Tshisekedi kaa chini uzungumze na M23 vinginevyo unaenda kutengeneza serikali ndani ya serikali, jeshi la Congo ni ungaa halina uwezo wa kukabiliana na M23, Tshisekedi unatoa wapi kiburi cha kukataa kuzungumza na M23?

    Washirika wa Congo nao kila siku vikao vingii lakini hatua za kukabiliana na M23 zimekuwa chache!! Tshisekedi kubali mazungumzo na M23 jifunze kwa Netanyahu!!!" - Zungu, Mtangazaji na Mchambuzi wa Siasa.

    TSHISEKEDI JIFUNZE KWA NETANYAHU "Mnakumbuka kauli ya Waziri mkuu wa Israel馃嚠馃嚤 Benjamin Netanyahu kwamba hata iweje hata zungumza na Hamas ? Tena Netanyahu akajitapa akisema kamwe Israel haitazungumza na magaidi, Netanyahu alisema hayo akijua fika ana sapoti kubwa ya Marekani inayompa nguvu na uwezo wa kila aina unaohitajika wa kijeshi!! Lakini mwisho wa siku Netanyahu alikaa chini na Hamas na kuzungumza baada ya hapo mateka pamoja na wafungwa wanaachiwa amani imerudi kiasi Gaza Somo kwa Tshisekedi kaa chini uzungumze na M23 vinginevyo unaenda kutengeneza serikali ndani ya serikali, jeshi la Congo ni ungaa halina uwezo wa kukabiliana na M23, Tshisekedi unatoa wapi kiburi cha kukataa kuzungumza na M23? Washirika wa Congo nao kila siku vikao vingii lakini hatua za kukabiliana na M23 zimekuwa chache!! Tshisekedi kubali mazungumzo na M23 jifunze kwa Netanyahu!!!" - Zungu, Mtangazaji na Mchambuzi wa Siasa.
    Like
    1
    0 Comments 0 Shares 106 Views
  • Aliacha historria (John Jones) ni onyo kali kwa wale wanaopenda mapango.

    Kamwe usipite kwenye sehemu nyembamba sana bila uhakika wa kutoka.

    Hakikisha unakuwa na vifaa vya kutosha vya usalama.

    Usijaribu kupita kwenye njia usizozifahamu vizuri.

    Na zaidi ya yote, uhai ni wa thamani kuliko ujasiri.

    Nutty Putty Cave inabaki kuwa kaburi lililofungwa, na watu wengi wakiogopa hata kufikiria juu yake.
    Aliacha historria (John Jones) ni onyo kali kwa wale wanaopenda mapango. Kamwe usipite kwenye sehemu nyembamba sana bila uhakika wa kutoka. Hakikisha unakuwa na vifaa vya kutosha vya usalama. Usijaribu kupita kwenye njia usizozifahamu vizuri. Na zaidi ya yote, uhai ni wa thamani kuliko ujasiri. Nutty Putty Cave inabaki kuwa kaburi lililofungwa, na watu wengi wakiogopa hata kufikiria juu yake.
    Like
    1
    0 Comments 0 Shares 123 Views
  • Baada ya masaa 28 ya mapambano, John Jones alikufa rasmi mnamo 25 Novemba 2009.

    Waokoaji walihitimisha kuwa haikuwa salama kujaribu kuutoa mwili wake.

    Waliamua kufunga pango hilo milele, ili kuzuia vifo vingine.

    Nutty Putty Cave sasa imefungwa, na mwili wa John Jones umebaki ndani milele—kaburi lake likiwa sehemu ileile aliyokufa.

    Ni moja ya vifo vya kusikitisha na vya kutisha zaidi katika historia ya upimaji wa mapango.
    Baada ya masaa 28 ya mapambano, John Jones alikufa rasmi mnamo 25 Novemba 2009. Waokoaji walihitimisha kuwa haikuwa salama kujaribu kuutoa mwili wake. Waliamua kufunga pango hilo milele, ili kuzuia vifo vingine. Nutty Putty Cave sasa imefungwa, na mwili wa John Jones umebaki ndani milele—kaburi lake likiwa sehemu ileile aliyokufa. Ni moja ya vifo vya kusikitisha na vya kutisha zaidi katika historia ya upimaji wa mapango.
    Love
    1
    0 Comments 0 Shares 78 Views
  • #funny #socialpop
    #funny #socialpop
    0 Comments 0 Shares 153 Views 0
  • Marais wa Urusi , V. Putin na yule wa Marekani , D.Trump walizungumza leo hii kwa muda saa moja na nusu kuhusu kumaliza vita Nchini Ukraine , kuboresha uhusiano kati ya Marekani na Urusi, na uwezekano wa kubadilishana Wafungwa.

    Aidha, Putin alimwalika Trump kwenda Mjini Moscow Nchini Urusi na akasema yuko tayari kuwakaribisha Maafisa wa Marekani kwa mazungumzo. Hii ilikuwa simu ya kwanza ya Putin na Rais wa Marekani aliyeko madarakani tangu Februari 2022, alipoongea na Biden muda mfupi kabla ya kutuma Wanajeshi Nchini Ukraine.

    Toa maoni yako
    #MvanoHabari
    #MvanoMtangazaji
    #M33
    Marais wa Urusi 馃嚪馃嚭, V. Putin na yule wa Marekani 馃嚭馃嚫, D.Trump walizungumza leo hii kwa muda saa moja na nusu kuhusu kumaliza vita Nchini Ukraine 馃嚠馃嚤, kuboresha uhusiano kati ya Marekani na Urusi, na uwezekano wa kubadilishana Wafungwa. Aidha, Putin alimwalika Trump kwenda Mjini Moscow Nchini Urusi na akasema yuko tayari kuwakaribisha Maafisa wa Marekani kwa mazungumzo. Hii ilikuwa simu ya kwanza ya Putin na Rais wa Marekani aliyeko madarakani tangu Februari 2022, alipoongea na Biden muda mfupi kabla ya kutuma Wanajeshi Nchini Ukraine. Toa maoni yako #MvanoHabari #MvanoMtangazaji #M33
    0 Comments 0 Shares 312 Views
  • Mahakama ya ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR) imeanza kusikiliza shauri la Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo dhidi ya Nchi ya Rwanda , ambalo limefunguliwa kwenye mahakama hiyo iliyoko Jijini Arusha Nchini Tanzania .

    Aidha, DR Congo ilifungua kesi dhidi ya Rwanda, Agosti 21 2023, ikiituhumu Nchi hiyo kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za kibinadamu. Kupitia kesi namba 007/2023, DR Congo inadai kuwa Nchi ya Rwanda inahusika na mgogoro unaeondelea Mashariki mwa Nchi hiyo hasa Mkoa wa Sud-Kivu.

    Mahakama ya ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR) imeanza kusikiliza shauri la Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 馃嚚馃嚛 dhidi ya Nchi ya Rwanda 馃嚪馃嚰, ambalo limefunguliwa kwenye mahakama hiyo iliyoko Jijini Arusha Nchini Tanzania 馃嚬馃嚳. Aidha, DR Congo ilifungua kesi dhidi ya Rwanda, Agosti 21 2023, ikiituhumu Nchi hiyo kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za kibinadamu. Kupitia kesi namba 007/2023, DR Congo inadai kuwa Nchi ya Rwanda inahusika na mgogoro unaeondelea Mashariki mwa Nchi hiyo hasa Mkoa wa Sud-Kivu.
    Like
    1
    0 Comments 0 Shares 172 Views
  • #allymessi1 #everyone #funny #sosialpop
    #allymessi1 #everyone #funny #sosialpop
    Haha
    1
    0 Comments 0 Shares 241 Views 1
  • Habari iliyobamba kwa sasa kwenye vyombo vya habari ni ndoa ya Stephane Aziz Ki na Hamisa Mobetto, ingawa wapo waliofika mbali na kudai ni kiki tu kwa ajili ya matangazo ya bidhaa fulani na wanatumika tu.

    Baada ya vuta nkuvute ya stori hii hatimaye mama yake Hamisa, Shufaa Rutanga amefunga na anathibitisha kuwepo kwa ndoa hiyo na kuhusu posa ya Aziz Ki, amesema hakuna posa yoyote iliyofika kwake kutoka kwa nyota huyo wa kimataifa wa Burkina Faso ingawa amepokea nyingi kutoka kwa wanaume tofauti wanaotaka kumuoa mwanaye.

    “Sasa ngoja nikuambie ukweli, maana nilikuwa nashindwa kutoa majibu sahihi kutokana na baadhi ya ya vitu kuhusu ndoa hii vilikuwa havijakamilika, sasa vimekamilika na ndoa ipo. Kiukweli namshukuru Mungu maombi yangu kwa mwanagu yameitika, nilikuwa kila kukicha naomba apate mtu sahihi watakayependana ili aolewe, kuwa kwenye ndoa ni heshima kubwa sana" - Mama Mobetto

    Mama Hamisa anasema hekaheka za ndoa hiyo zitaanza Jumamosi Februari 15 na ndiyo siku mahari itatolewa na sherehe itafanyika Februari 19, The Superdome, Masaki, jijini Dar es Salaam.

    “Kutoka moyoni nimewapa baraka zote mkwe wangu AziZ Ki na mwanagu Hamisa na upendo mwingi sana kwake Aziz Ki kwa kupenda watoto wa Hamisa. Hiki ndiyo sababu kuu iliyonifanya nimpende zaidi Aziz Ki, maana kwa hali ya sasa hivi upate mwanamume atakayekubali kuoa mwanamke mwenye watoto ni wachache sana ila Aziz Ki ameonyesha upendo wa dhati kwa mwanangu Hamisa, kapenda boga na maua yake.” - Mama Mobetto

    Wakati huohuo mmoja wa viongozi wa Yanga, amethibitisha ni kweli wawili hao watafunga ndoa Ijumaa na kwasasa Aziz yupo kwenye maandalizi ya Ndoa ingawa atakuwepo kwenye mchezo wa Ijumaa.
    (Mwananchi)

    Habari iliyobamba kwa sasa kwenye vyombo vya habari ni ndoa ya Stephane Aziz Ki na Hamisa Mobetto, ingawa wapo waliofika mbali na kudai ni kiki tu kwa ajili ya matangazo ya bidhaa fulani na wanatumika tu. Baada ya vuta nkuvute ya stori hii hatimaye mama yake Hamisa, Shufaa Rutanga amefunga na anathibitisha kuwepo kwa ndoa hiyo na kuhusu posa ya Aziz Ki, amesema hakuna posa yoyote iliyofika kwake kutoka kwa nyota huyo wa kimataifa wa Burkina Faso ingawa amepokea nyingi kutoka kwa wanaume tofauti wanaotaka kumuoa mwanaye. “Sasa ngoja nikuambie ukweli, maana nilikuwa nashindwa kutoa majibu sahihi kutokana na baadhi ya ya vitu kuhusu ndoa hii vilikuwa havijakamilika, sasa vimekamilika na ndoa ipo. Kiukweli namshukuru Mungu maombi yangu kwa mwanagu yameitika, nilikuwa kila kukicha naomba apate mtu sahihi watakayependana ili aolewe, kuwa kwenye ndoa ni heshima kubwa sana" - Mama Mobetto Mama Hamisa anasema hekaheka za ndoa hiyo zitaanza Jumamosi Februari 15 na ndiyo siku mahari itatolewa na sherehe itafanyika Februari 19, The Superdome, Masaki, jijini Dar es Salaam. “Kutoka moyoni nimewapa baraka zote mkwe wangu AziZ Ki na mwanagu Hamisa na upendo mwingi sana kwake Aziz Ki kwa kupenda watoto wa Hamisa. Hiki ndiyo sababu kuu iliyonifanya nimpende zaidi Aziz Ki, maana kwa hali ya sasa hivi upate mwanamume atakayekubali kuoa mwanamke mwenye watoto ni wachache sana ila Aziz Ki ameonyesha upendo wa dhati kwa mwanangu Hamisa, kapenda boga na maua yake.” - Mama Mobetto Wakati huohuo mmoja wa viongozi wa Yanga, amethibitisha ni kweli wawili hao watafunga ndoa Ijumaa na kwasasa Aziz yupo kwenye maandalizi ya Ndoa ingawa atakuwepo kwenye mchezo wa Ijumaa. (Mwananchi)
    Like
    1
    0 Comments 0 Shares 259 Views
More Results