• “…ndani ya wiki moja, majeshi ya Uganda na wapiganaji wa M23 watakuwa Kisangani, kwa amri ya Rais Yoweri Museveni, Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Uganda (UPDF)…” - Muhoozi Kainerugaba, Mkuu wa Majeshi ya Uganda .

    “…ndani ya wiki moja, majeshi ya Uganda na wapiganaji wa M23 watakuwa Kisangani, kwa amri ya Rais Yoweri Museveni, Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Uganda (UPDF)…” - Muhoozi Kainerugaba, Mkuu wa Majeshi ya Uganda 🇺🇬.
    0 Comments ·0 Shares ·102 Views
  • Read more
    Rais wa Nchi ya Iran 🇮🇷, Ayatollah Ali Khamenei, amesema kuwa vitisho vya Nchi ya Marekani 🇺🇸 dhidi ya Taifa lake havisaidii lolote na havitaleta matokeo yoyote kama Rais Donald Tramp anavyofikiria. Kiongozi huyo amesema hayo baada ya Rais Trump kuonya uwezekano wa hatua za kijeshi kuchukuliwa dhidi ya Iran. "Wamarekani wanapaswa kuelewa kwamba vitisho havitafanikiwa wanapokabiliana na Iran. Wao (Marekani) na wengine wanapaswa kufahamu kuwa wakifanya lolote baya dhidi ya taifa la Iran, watajibiwa kwa nguvu kubwa." alisema Rais Khemenei Mnamo Machi 7, Rais Trump alisema kuwa alimwandikia barua Rais Khamenei, akimtaka kuanzisha mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran, huku akionya kuwa kuna uwezekano wa kuchukua hatua za kijeshi iwapo Iran itakataa. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, alisema Alhamisi wiki hii kuwa barua hiyo ilikuwa zaidi ya tishio, ingawa pia ilionesha uwezekano wa mazungumzo. "Tunachunguza kwa kina maudhui ya barua hiyo, na tutajibu rasmi katika siku chache zijazo” alisema Waziri huyo Kulingana na ripoti ya tovuti ya habari ya Marekani, Axios, ikimnukuu Afisa wa Serikali ya Trump na vyanzo vingine vikisema, barua hiyo inaweka muda wa miezi miwili wa kufikia makubaliano mapya ya nyuklia. Hata hivyo, haijabainishwa ni lini muda huo utaanza au kuisha. Kwa muda mrefu, Rais Khamenei amepuuza wito wa Rais Trump wa mazungumzo ya moja kwa moja, akisema kuwa Rais huyo wa Marekani anajaribu kudanganya ulimwengu kwa kuonesha kuwa Marekani iko tayari kwa mazungumzo huku Iran ikionekana kutotaka kushiriki. Ikumbukwe kwamba Trump ambaye alianza muhula wake wa pili Januari 2025, amerudisha sera yake ya shinikizo la juu dhidi ya Iran. Wakati wa kipindi chake cha kwanza, Trump aliiondoa Marekani kwenye makubaliano ya kihistoria ya nyuklia ya 2015 kati ya Iran na mataifa yenye nguvu ulimwenguni na akairejeshea Tehran vikwazo vikubwa vya kiuchumi.
    0 Comments ·0 Shares ·157 Views
  • Read more
    "Msimu uliyopita Zamalek aligomea mechi dhidi ya Al Ahly, Mamlaka za soka nchini Misri zikampa ushindi Al Ahly wa mabao mawili na alama zake tatu kisha wakailima Zamalek alama tatu na timu ikashuka mpaka nafasi ya 12 kama sikosei, Bodi na Chama wala hakikuwaza mara mbili, ni kesi kubwa sana kwenye dunia ya soka kukacha mechi. Jana, Al Ahly nae kaleta mbwembwe zile zile za masuala ya Kanuni akagomea mchezo, akasahau kanuni ya kutokea Uwanjani na kucheza mechi ndio kanuni yenye maana zaidi kwenye soka, amejikuta anapoteza alama tatu na mabao matatu kwa Zamalek, Kanuni hii inaweza kusema hivi ila Kanuni nyingine ikawa na maelezo mengine. Nikukumbushe tu Al Ahly aliyeadhibiwa ndio Klabu Tajiri zaidi Afrika, Klabu yenye Mashabiki na Wanachama wengi zaidi Afrika, ndio Klabu ya pili kwa Mataji mengi duniani baada ya Real Madrid, ila huko Misri watu hawatazami makunyanzi, ukileta maksudi, Bodi na Chama cha soka zinakufanyia bahati mbaya, Ahly inatajwa pia ina nguvu kubwa sana CAF, sio ya kufikirika ama nadharia ndio uhalisia ila wamepita nayo mapema tu. Nawakumbusha tena Watu wangu HAKI huenda na WAJIBU, mfano Tanzania kwa mujibu wa Katiba kuandamana ni haki yako ila unapaswa kutoa taarifa kwa Polisi masaa 72 kabla, umeelewa hapo? Ni haki yako ila huja na Wajibu, Kanuni ili ikulinde hakikisha umetekeleza Wajibu, biashara za Mamlaka za soka duniani ni mpira, kutocheza mpira ni kuzitusi, hazikuachi salama. Ni haki yako kuja kufanya mazoezi uwanja wa mechi siku moja kabla ila ni Wajibu wako kunijulisha kuwa nakuja, ili nikuandalie mazingira, huenda narekebisha mfumo wa Umeme? Huenda hali ya usalama sio shwari, huenda nimepulizia dawa za dudu zinaweka kukuathiri, yaani ni HAKI yako ila una WAJIBU wako huu ni mfano tu. Mnasemaje Watu wangu wa nchini Yemen haya hayawahusu sana, huko kwenu Kivyenu vyenu Wayemen😀" - Farhan JR, Mchambuzi.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·256 Views
  • Read more
    MTUNZI WA JINA LA 'TANZANIA' AFARIKI Hicho ni kipande cha gazeti la The Nationalist la Oktoba 30, 1964. Habari kubwa kwenye gazeti hili na Nchi kwa ujumla ni jina jipya la TANZANIA. Ni kwamba baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wa April 26, 1964, jina la nchi mpya lilikuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Lakini jina hili lilikuwa refu sana na kuwa kero kwa Watumiaji. Serikali kupitia wizara ya habari na utalii chini ya waziri Dkt. Idrisa Abdul Wakili, ikaanzisha mchakato wa kutafuta jina jipya litakalokuwa fupi na rahisi. Ikatoa tangazo kupitia gazeti la Tanganyika Standard, ambalo sasa ni Daily News, kuwataka Watanzania wenye kuweza kubuni jina jipya la Nchi kufanya hivyo. Ndipo kijana wa miaka 18 kutoka Morogoro, Mohamed Iqbal Dar, Mwanafunzi wa Sekondari ya Aga Khan Morogoro, akaliona tangazo hilo na kushiriki. Akatunga jina la Tanzania na kulituma kwenye anwani iliyotangazwa. Baada ya muda kupita, akapata barua kutoka serikalini ikimtaja na kumpongeza yeye kama mmoja wa Washindi 16 na wakatakiwa kufika ofisi za wizara. Kwa pamoja watu hawa walitakiwa kugawana zawadi ya shilingi 200, wakati huo shilingi moja ilikuwa sawa na dola 8 za Marekani. Siku ilipofika, watu wawili tu walijitokeza; yeye Mohamed Iqbal Dar na Yusufal Pir Mohamed. Lakini huyo mwenzake hakuwa na ile barua ya kutajwa kama mshindi na kupongezwa... Serikali ikashindwa kumthibitisha hivyo kumtangaza Mohamed Iqbal Dar kama Mshindi pekee. Ndipo Jumatano ya Oktoba 29, 1964 serikali ikatangaza rasmi kwamba jina jipya la nchi ni Tanzania na gazeti la The Nationalist likaichapisha habari hii kubwa, Alhamisi ya Oktoba 30, 1964. Jina la Tanzania likaanza kutumika rasmi Novemba Mosi, 1964. - Alitungaje jina? TAN - kutoka Tanganyika ZAN - kutoka Zanzibar I - kutoka jina lake la Iqbal. A - kutoka dini yake ya Ahmadiya. Hii pia ikawa rahisi zaidi kwake kwani majina ya nchi nyingi za Afrika yaliishia na A kama Ethiopia, Zambia, Gambia nk. - Ni nani huyu Mohamed Iqbal Dar? Ni mtoto wa Dkt. Dar, ambaye alikuja Tanzania mwaka 1930 kutoka India. Alifikia Tanga, na ndiko alikozaliwa Mohamed, hakafu akahamia Morogoro. Mohamed amefarikia huko Birmingham Nchini Uingereza 🇬🇧.
    Like
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·455 Views
  • Read more
    Nikueleze kwa kifupi sana kiini cha mgogoro. Kabla ya mwaka 1991 Ukraine ilikua sehemu ya Urusi kupitia muungano wa kisovieti wa USSR. Baada ya USSR kufa ndipo taifa la Ukraine likazaliwa pamoja na mataifa mengine 14 yaliyokua majimbo ya Urusi. Lakini usisahau mwaka 1949 umoja wa kujihami wa nchi za magharibi (NATO) ulianzishwa dhidi ya Urusi (USSR). Makubaliano yao ni kwamba ikiwa Urusi itamgusa mmoja wao basi wote watamvamia. Marekani akiwa kinara. Kuanguka kwa USSR kukafanya mataifa 15 mapya kuzaliwa. Baadhi ya Mataifa hayo yakawa na hofu kuwa Urusi inaweza kurudi kuyakalia kimabavu. Kwahiyo yakaomba kujiunga NATO kwa usalama wao. Estonia, Latvia na Lithuania zikapata uanachana wa NATO chap kwa haraka. Ukraine ilipoomba uanachama Urusi ikakataa, kwa sababu ya strategic position ya Ukraine ambayo inaiweka Urusi hatarini. Ukraine ilipokosa uanachama NATO ikamua kujilinda kwa kusuka mpango wa nyuklia. Marekani na Urusi zikashtuka. Kwa kutambua hatari ya nyuklia zikamsihi sana Ukraine aachane na mpango huo. Mwaka 1994 ukaandaliwa mkataba uitwao Budapest memorundum, huko Hungary. Mkataba huo ulihusisha nchi 4. Urusi na Ukraine zilisaini kwamba hakuna atakayemvamia mwenzake. Marekani na Uingereza zikasaini kwamba atakayemvamia mwenzake watampiga bila huruma. Pia Marekani na Uingereza zitagharamia fedha na vifaa vyote vya vita. Mkataba ukasainiwa na Ukraine ikasitisha mpango wake wa nyuklia. Lakini Mwaka 2014 Urusi ikaivamia Ukraine na kuchukua jimbo lake la Crimea kimabavu. Marekani na Uingereza hazikuipiga Urusi kama mkataba wa Budapest unavyosema. Ukraine akalalamika lakini akapuuzwa. Kwenye vita inayoendelea sasa, Urusi ameshajitwalia majimbo manne Donetsk, Luhansk, Zaporizhzhia na Kherson lakini Marekani na Uingereza ziko kimya. Ukraine inaona imesalitiwa. Mkataba wa Budapest ulikua kiini macho. Laiti Ukraine ingekataa kusaini na kuendelea na mpango wake wa nyuklia, leo Urusi isingethubutu kuigusa. Lakini Waliomdanganya sasa wamemgeuka na wanamfokea. Ukraine ingeyajua maneno ya Mzee Jomo Kenyatta "Learn to fight your own battle" isingeachana na mpango wake wa nyuklia mwaka 1994. Wangejifunza kupigana vita yao wenyewe bila kutegemea mtu.! (Malisa GJ)
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·523 Views
  • Read more
    Privaldinho ✍️ CEO wa Getafe si anachambua. Sasa na mimi nianze kuchambua. Nimetazama vikosi vya Singida mechi 4 za nyuma Makipa Vs Kagera - Metacha Vs JKT - Amas Vs KMC - Masalanga Vs Yanga - Masalanga Ndani ya mechi nne makipa watatu Beki ya kushoto Imoro amecheza mechi 2 kati ya 5, vs Makolo, Mechi za Kagera na KMC akacheza Malonga. Vs JKT akacheza Imoro, vs Yanga akacheza Gadiel. Mechi 5 mabeki wa kushoto 3. Mechi ya JKT mabeki wa kati alikuwa Assink na Kennedy (Tra bi ta hakuwepo), jana ameanzia benchi. Mechi ya KMC alianza Tra bita na Kennedy. Tra bi ta alitolewa dkk 46 akaingia Assink beki mpya ambaye ameanza jana. Mechi ya Kagera Kennedy hakucheza wakaanza Tra bita na Manyama, vs makolo Kennedy na tra bi na vs Ken Gold, Kennedy na Manyama. Maana yake, kuna Manyama, Tra, Kennedy na ongezeko la beki mpya Assink kutoka Ghana aliyecheza jana. Kiufupi hakuna mwenye uhakika wa namba eneo hilo. Viungo wa kati Vs Yanga (Damaro, Nashon, Gego) Chukwu akabadilishiwa majukumu) Vs JKT (Chukwu, Nashon, Arthur) Vs KMC (Damaro, Athur, Tchakei) Vs Kagera (Damaro, Chukwu, Athur) vs Kolo (Damaro, Gego, Keyekeh) Vs Ken Gold (Damaro, Gego, Keyekeh) Yanga vs Singida wameanza na viungo wakabaji kiasilia 3. Damaro aliyecheza mechi 5/6, Gego aliyeanza mechi 3/3 na kutokea sub mechi 2. NB: Eneo la ushambuliaji, Tchakae hajacheza vs JKT na Yanga. Jana wamelalamika hajacheza ila hawajajiuliza kwanini hakucheza vs JKt Vs Yanga - Pokou Rupia Adebayor (Sowah Sub) Vs JKT - Lyanga, Sowah, Pokou (Rupia top scorer out) Vs KMC - Sowah, Rupia, Pokou (timu ikakosa balance, nyuma yao yupo Tchake (luxury player) wakapoteza mechi.) Hii ni kwa wale mnafirikia Sowah na Rupia kuanza pamoja away. KMC waliongoza umiliki wa mchezo. Kidogo kipindi cha pili Singida walibadilika baada ya sub ya Rupia, Pokou na Tchakei, akaingia Gego na Tchukwu Vs Kagera -Sowah, Rupia, Tchakei (matokeo 2-2, kwa mara nyingine wanakuwa vulnerable kudefend. Mbaya zaidi wakiwa nyumbani. Vs Kolo - Tchakei, Rupia Athur Vs Ken Gold - Tchakei, Rupia, Adebayor Vs Prisons - Lyanga, Rupia Tchakei Ni wachache sana wenye uhakika wa namba. Agenda ya kikosi kubadilika sio habari mpya kwao labda kama wewe ni mgeni wa JIJI
    0 Comments ·0 Shares ·600 Views
  • Read more
    Zakazakazi azidi kumshushia nondo Amri Kiemba. MUONGO! Amri Kiemba alicheza Simba kwa misimu mitano na nusu, kuanzia 2009/10 hadi Disemba 2014. Katika kipindi hicho, Azam FC na Simba zilikutana mara 10, Simba ikishinda mara tano na Azam FC mara tatu, na mara mbili sare...angalia picha ya pili. Katika hizo mara tano ambazo Simba ilishinda, mbili ni za msimu wa 2009/10. 24/10/2009 Simba 1-0 Azam FC 14/3/2010 Azam FC 0-2 Simba Huu ulikuwa msimu ambao Simba ilikuwa kwenye ubora mkubwa sana na ikamaliza ligi bila kupoteza hata mchezo mmoja. Walishinda mechi zote za mzunguko wa kwanza, wakaja kupata sare mbili tu mzunguko wa pili, dhidi ya Kagera Sugar na African Lyon. Kwa ubora huo, huwezi kuilamu Azam FC ilhali timu zote zilifungwa...kiungwana unawasifia Simba kwamba walikuwa kwenye ubora wa hali ya juu. Lakini baada ya msimu huo, Azam FC na Simba zililingana matokeo hadi Kiemba alipoondoka Simba kwenda Azam FC. Swali ni je, Kiemba anapata wapi uhalali wa kutilia shaka maandalizi yaliyoleta matokeo kama haya? Msimu wa 2013/14, Azam FC ikawa kwenye ubora mkubwa na kumaliza ligi bila kupoteza hata mchezo mmoja, ikiwemo kushinda nje ndani dhidi ya Simba ya Kiemba na maandalizi yao ya hali ya juu. 28/10/2013 Simba 1-2 Azam FC 30/3/2014 Azam FC 2-1 Simba Baada ya mechi hizi Kiemba akaenda Azam FC...na mechi yake ya kwanza ikaisha kwa sare ya 1-1. Ni vipi Kiemba hakuridhika na maandalizi ya Azam FC yaliyoleta sare lakini aliridhika na maandalizi ya Simba yaliyowafanya wafungwe nje ndani msimu mmoja tu nyuma yake? Msimu mmoja kabla Kiemba hajasajiliwa Simba, Azam FC ilishinda 2-0 na mashabiki wa Simba wakaenda kushusha kinyesi nyumbani kwa mwenyekiti wao Hassan Dalali. Ina maana maandalizi ya Azam FC yangekuwa hafifu yangewatoa kinyesi Simba kweli? Azam FC ilikuwa inaifunga Simba kabla yeye hajaenda, na ikaifunga akiwemo...kwa maandalizi yale yale...halafu anakuja hadharani leo, miaka zaidi ya 10 na kusema aliona maandalizi hafifu...sasa walikuwa wanashindaje kwa maandalizi hafifu? Ni mbaya sana kumuita mtu muongo...lakini Kiemba kwenye hili itoshe tu kusema kwamba WEWE NI MUONGO!
    0 Comments ·0 Shares ·467 Views
  • Read more
    KUTOKA SINGIDA BLACK STARS ✍️ HII NI KWENU WACHAMBUZI WOTE WENYE USHABIKI KULIKO UCHAMBUZI Singida Black stars Sc ni Timu yenye utaratibu wake na mipango yake juu ya kuiongoza Timu yake kwa misingi yake Timu yetu haipangiwi na wala hatupelekeshwi na maneno ya mitandaoni katika kuiendesha Timu Yetu, Tunaomba Mfahamu kuwa kila mchezaji Tuliyemsajili anatufaa na anafaa kuipambania Nembo ya Timu yetu Katika kikosi chetu chenye jumla ya wachezaji 33 wote wakiwa wazima wa Afya na Fitness nzuri kocha wetu na Benchi letu la Ufundi lina uhuru wa Kumchagua Mchezaji yeyote akaanza katika kikosi cha kwanza katika mchezo wowote Rejea michezo Yetu Mitatu ya nyuma kabla ya mchezo wa jana dhidi ya Yanga sc Tulicheza michezo 3 dhidi ya Kagera Sugar, KMC Fc, na JKT Tanzania Katika mchezo wetu dhidi ya Kagera sugar tulianzisha wachezaji wengi wa kimataifa na Tulipata sare ya goli 2-2 mchezo uliofuata tukacheza dhidi ya KMC FC na wachezaji wengi wa kimataifa walianza pia tukafungwa goli 2 bila Benchi la ufundi kikafanya mabadiliko kadhaa kwenye mchezo uliofuata dhidi ya JKT Tanzania Na tukapata ushindi kwenye moja ya Viwanja ambavyo Timu zote za ligi kuu hakuna iliyopata ushindi Baada ya Benchi la Ufundi kuridhika na vipaji vya wachezaji wetu wa ndani waliotupa Ushindi wa mchezo wa JKT Tanzania wakaridhishwa kwamba wachezaji wale wanafaa baadhi yao kuanza kwenye mchezo dhidi ya Yanga, kwa upande wa Timu yetu Tumefurahi Timu ilicheza vizuri kwa nidhamu ya hali ya juu na mchezo ukaisha kwa goal 2-1 Sasa baada ya mchezo ule wameibuka watu wanaojiita wachambuzi kwa vivuli vya ushabiki wao na roho zao mbaya na umaskini uliowajaa wanataka kutupangia Kikosi chetu kitu Ambacho kwetu hakikubaliki hata kidogo Ni mfano uone mwanaume Ameoa wake 4 alafu wewe jirani yake unataka kumpangia kwamba Leo kalale kwa mwanamke huyu na utapikiwa na huyu hilo haliwezekani Abadani SISI HATUPANGIWI MAISHA NA VITAKATAKA KAMA NYINYI
    0 Comments ·0 Shares ·683 Views
  • Read more
    Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya Nchi ya Uganda 🇺🇬 (UPDF), Jenerali Muhoozi Kainerugaba, amesema Uganda inatoa saa (24) vikosi vyote vilivyopo katika Mji wa Bunia Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩 kuacha kuuwa Raia wa kabila la Bahima (ambalo asili yake ni kutoka Nchini Uganda) lasivyo Jeshi lake litashambulia Mji huo. Kainerugaba ametoa kauli hiyo Februari 15 katika mtandao wake wa X. Huku akielezwa kuwa na historia ya kuchapisha maoni ya uchochezi kuhusu sera za kigeni mara kwa mara. Alisema ana mamlaka ya Rais Yoweri Museveni, ambaye pia ni Baba yake Mzazi ambako hata hivyo, alipotafutwa Msemaji wa Jeshi la Uganda alisema hawezi kuzungumzia suala hilo. Hata hivyo, kabla ya kusasisha ujumbe huo kwenye mtandao wa X, Jenerali huyo alikuwa alieleza bila kutoa ushahidi, kwamba Watu kutoka kabila la Bahima walikuwa wakiuawa huko Nchini DR Congo.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·360 Views
  • Read more
    Rais wa Nchi ya Liberia 🇱🇷, Joseph Boakai amewasimamisha kazi zaidi ya Maafisa 450 wa Serikali yake akiwemo Waziri anayesimamia bajeti pamoja na Mabalozi kwa kushindwa kutangaza mali zao ndani ya muda uliowekwa. Uamuzi huo unafuatia agizo la Rais huyo lililotolewa Novemba 27, 2024, ambalo lilitoa muda wa nyongeza wa siku kumi (10) kwa Maafisa hao kutekeleza agizo hilo lakini wakashindwa kufanya hivyo. Maafisa hao wamesimamishwa kazi kwa muda wa mwezi mmoja bila mshahara au hadi watakapowasilisha tamko la mali zao kama inavyotakiwa.
    0 Comments ·0 Shares ·214 Views
  • Read more
    #PART3 Dogo alianza kupiga picha na maadui wa baba yake. Unajua maana yake? Kijana wako, damu yako mwenyewe, anashirikiana na watu waliotaka kukuangusha. Hii haikuwa tu ishu ya "Hana time na baba yake," hii ilikuwa ni chuki ya makusudi. Na chuki hiyo haikutoka kwa mtoto mwenyewe, bali ilitengenezwa na mama yake. Mama ambaye baada ya kuachwa alitaka pesa nyingi kutoka kwa 50 Cent lakini ikashindikana. Mama ambaye hakuwa na njia ya kumkomoa baba, akaamua kutumia mtoto kama silaha. Na mtoto, bila kujua anatumika kama chess piece, akaingia kwenye mchezo wa mama. Huu ni ukweli mchungu. Katika ndoa au mahusiano yanayovunjika, asilimia kubwa ya wanawake hutumia watoto kama njia ya kulipiza kisasi. Ni wachache sana watakaoruhusu baba wa mtoto wao aendelee kuwa na uhusiano mzuri na mwanawe baada ya kutengana.
    0 Comments ·0 Shares ·524 Views
  • Read more
    #PART2 Na kweli, wakampigia kura, Obama akaingia madarakani. Mwaka wa kwanza ukapita. Mwaka wa pili ukapita. Mwaka wa tatu ukapita. Gereza bado liko palepale. Kila alipoulizwa juu ya ahadi yake, alitoa majibu yasiyoeleweka. Ndani ya miaka yake minane madarakani, Guantanamo Bay liliendelea kuwepo. Ndipo Wamarekani wakagundua kitu. Hata Rais hana nguvu juu ya gereza hili. Wakati Trump akaingia madarakani, yeye hakutumia Guantanamo kama njia ya kuombea kura. Hakusema atalifunga. Hakusema atalifungua. Lakini alipoingia, akatoa amri ya kuhamisha wafungwa zaidi ya 30,000. Lengo lake lilikuwa moja tu. "Tuhakikishe gereza linajaa wale ambao kweli wanastahili kuwepo humo."
    0 Comments ·0 Shares ·419 Views
  • Read more
    #PART10 March 23, 2009 Mkataba wa amani uitwao "March 23 Agreement" ukasainiwa huko Goma, kati ya serikali ya Congo na Waasi wa CNDP, wasuluhishi wakiwa mzee Mkapa na mzee Obasanjo. Mapigano yakasitishwa Ntaganda na askari wa CNDP wakaingizwa kwenye jeshi la Congo (FARDC). Kukawepo na miaka mitatu ya amani, vita ikakoma kabisa. Lakini ghafla, April 04, mwaka 2012 Bosco Ntaganda alitangaza kujitoa kwenye jeshi la Congo (FARDC) pamoja na baadhi ya askari waliokuwa wanamgambo wa CNDP. Ntaganda alidai Serikali ya Congo imeshindwa kutekeleza mkataba wa amani wa Machi 23, 2009. Alisema Makataba huo uliweka masharti ya kutowabughudhi askari 600 wa CNDP waliokataa kujiunga na jeshi la Congo. Lakini serikali ya Congo iliwashughulikia. Baadhi walikamatwa na wengine kuuawa. Pia alidai serikali ya Congo imeshindwa kuwalinda Watutsi (Banyamulenge) waishio mashariki mwa nchi hiyo. Ntaganda akatangaza kuanzisha kikundi kipya cha waasi kiitwacho M23. Alidai kutumia jina hilo ili kuikumbusha serikali ya Congo kuheshimu mkataba wa amani wa Machi 23, 2009. Kundi la M23 likapata wafuasi wengi hasa askari wa zamani wa CNDP na Banyamulenge wa Kivu. Mapigano yakaanza upya. Rwanda na Uganda zikashutumiwa kuunga mkono waasi hao, lakini zikakataa. Hata hivyo Rwanda ililaumiwa kwa kuruhusu M23 kuwa na kambi za kijeshi katika miji ya Gisenyi na Rusizi. Pia Rwanda ilihusishwa na mgogoro huo kwa sababu Ntaganda hakuwa Mkongomani, bali Mnyarwanda aliyezaliwa na kukulia Rwanda. Ametumikia jeshi la Rwanda kwa miaka mingi, kabla ya kuhamia Congo kupigania haki za Banyamulenge. Baada ya mwaka mmoja wa mapigano makali, vikosi vya M23 vikazidiwa nguvu na jeshi la serikali. Machi 18, 2013, Bosco Ntaganda akakimbilia Rwanda na akaenda mwenyewe kujisalimisha kwenye ubalozi wa Marekani mjini Kigali. Akasafirishwa kwenda The Heague kwenye mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai (ICC). Mwaka 2015 kesi yake ikaanza kusikilizwa, na mwaka 2019 akapatikana na hatia katika makosa 18, yakiwemo ubakaji, mauaji ya raia wasio na hatia, na kutumikisha watoto jeshini. Akahukumiwa kifungo cha miaka 30 jela, adhabu ambayo anaitumikia hadi sasa. (Malisa GJ)
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·797 Views
  • Read more
    #PART9 Baada ya miaka mitatu ya utulivu, ghafla 2006 Jenerali Laurent Nkunda, aliasi jeshi kwa madai serikali imeshindwa kutekeleza Mkataba wa Amani wa SunCity. Ikumbukwe kabla ya kujiunga na Jeshi, alikua mpiganaji wa RCD - Goma, kundi lililoungwa mkono na Rwanda. Baada ya mkataba wa Suncity waasi wote waliingizwa jeshini akiwemo Nkunda. Lakini Juni 29, 2006, Nkunda akaasi jeshi na kuunda kundi la Congrès National pour la Défense du Peuple (CNDP). Madai yake: - Askari wa vikundi vya waasi walioingizwa jeshini hawakupewa vyeo. - Serikali ya Congo kushindwa kuwatanbua Watutsi (Banyamulenge) waishio mashariki mwa nchi hiyo kama raia wa Congo. - Serikali ya Congo kushindwa kuwakamata wanamgambo wa kihutu wa FDLR (Intarahanwe) waliojificha Congo baada ya kufanya mauaji ya kimbari Rwanda 1994. Nkunda akasema lengo la kuanzisha kundi la waasi la CNDP ni kupigania haki za Watutsi waishio mashariki mwa Congo (Banyamulenge) na kukabiliana na wanamgambo wa Kihutu wa FDLR. Nkunda akaungwa mkono na Rwanda na Uganda, akapewa silaha, vita ikaanza upyaaaaa (tamka kwa sauti ya mbunge Bwege). CNDP ikaua raia wengi wenye asili ya Kihutu ikiwatumu kuwa wafuasi wa FDLR. Serikali ya Burundi ikiongozwa na Piere Nkurunzinza (Mhutu) ikaingiza jeshi Congo kupambana na CNDP ili kulinda raia wake waliokua Congo. Kwa miaka mitatu kukawa na mapigano makali sana mashariki mwa Congo. January 2009 Waasi wa CNDP wakazidiwa. Laurent Nkunda akakimbilia Rwanda. Alipofika akakamatwa na kuwekwa kizuizini. Mpaka leo, bado anashikiliwa bila kufikishwa mahakamani. Jenerali Bosco Ntaganda, Mtutsi (Banyamulenge) wa Kivu akateuliwa kuongoza CNDP. Akafanya vitendo vingi vya kikatili kwa raia kuliko mtangulizi wake, kama ubakaji, mauaji ya halaiki, na kutumikisha watoto jeshini. Machi 23, 2009 serikali ya Congo na CNDP wakasaini Mkataba wa Amani, ulioitwa "March 23 Agreement" wenye masharti yafuatayo: - Kusitisha mapigano kwa pande zote. - Kuingiza askari wa CNDP kwenye jeshi la Congo. - Kutowashtaki askari wa CNDP kwa makosa waliyofanya wakati wa vita. - Wananchi wa Kivu wanufaike na rasilimali zao - Kulinda haki za binadamu Kivu (Malisa GJ)
    0 Comments ·0 Shares ·784 Views
  • Read more
    #PART6 Alipoingia Ikulu Kabila alifuta jina Zaire na kurudisha Congo (Jamhuri ya kidemokrasia). Baadae alifikiria kuiachia Kivu, eneo lenye utajiri mkubwa wa madini adimu duniani. Akasema "to hell with Lemera Agreement" akautupilia mbali mkataba wa Lemera. Akasema Kivu itabaki Congo na madini ya Kivu yatajenga Congo. Full stop. Ashakuwa Rais utamfanya nini? Kagame hakuamini macho yake. Alishawaza jinsi ambavyo Rwanda ingekuwa Dubai ya Afrika kwa rasilimali za Congo. Lakini ghafla aligeukwa na mshirika wake Laurent Désiré Kabila. Akamfuata "Godfather" wake mzee Museveni. Mzee akasema kama katugeuka tumpige. Wakatafuta kikundi cha Waasi wakiunge mkono. Wakapata Rassemblement Congolais pour la Démocratie (RCD), kilichoongozwa na Jenerali Ernest Wamba dia Wamba. Kikundi kikapewa silaha na fedha kikaanza kumshughulikia Kabila. RCD ikaanza kuchapana na jeshi la Congo (FARDC) ikiwa na backup ya Rwanda na Uganda. Vita vikapamba moto. Rwanda na Uganda nao wakaingiza majeshi Congo kusaidia waasi wa RCD. Kabila akaona anazidiwa, akaomba msaada Angola na Chad. Nchi hizo zikaleta vikosi vyake Congo. Mapigano yakawa makali sana. Eneo la mashariki mwa Congo likageuka machinjioni. Watu walikufa kwa wingi, mpaka maiti zikatapakaa barabarani bila kuzikwa, zikawa zinadonolewa na ndege. Hii iliitwa Vita ya Pili ya Congo (1998–2002), iliyokua mbaya zaidi katika historia ya vita zote Afrika. Imebatizwa jina "Vita Kuu ya Afrika". Inakadiriwa watu laki tano walipoteza maisha huku mamilioni wakikimbia nchi. Mapigano yaliendelea, huku vikosi vya Rwanda na Uganda vikichota madini. Katikati ya mapigano mgongano wa kimaslahi ukajitokeza. Jasin Stearns, katika kitabu chake Dancing in the Glory of Monsters, anasema Kagame alishindwa kuelewana na "godfather" wake Museveni juu ya mgawanyo wa mali. Hali hiyo ilifanya kikundi cha RCD kipasuke na kuzaliwa vikundi viwili. Cha kwanza kikajiita RCD-Goma kikiongozwa na Kanali Emile Ilunga (hiki kilisaidiwa na Rwanda) na cha pili kikajiita RCD-Kisangani, kikiongozwa na Jenerali Mbusa Nyamwisi (kikisaidiwa na Uganda). (Malisa GJ)
    Like
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·798 Views
  • Read more
    #PART5 Eneo la Kivu ni eneo la kimkakati sana na mabepari wote duniani wanalitolea macho kutokana na utajiri wake. Kivu ina madini ya Coltan ambayo yanatumika kutengeneza simu na laptop. 80% ya coltan yote duniani inatoka Congo (unaweza kugoogle kama huamini). Yani kwa kifupi bila Congo hakuna smartphones wala laptop duniani. Kivu pia kuna madini ya tin yanayotumika kutengenezea solder za kuchomelea vifaa vya kielektroniki kama radio, TV, simu, nk. Kuna madini ya Tungsten yanayotumika kutengenezea silaha. Na pia kuna Cobalt inayotumika kutengeneza betri mbalimbali zikiwemo za magari. Kama haitoshi Kivu kuna dhahabu nyingi mno. Eneo la Kivu ni eneo lenye dhahabu nyingi zaidi duniani ambayo bado haijachimbwa (The most unexplored gold site globally). Kagame aliona fursa. Wakati huo Rwanda ilikuwa imetoka kwenye vita na machafuko ya muda mrefu. Akataka rasilimali za jirani. Lakini atazipataje wakati yeye na Mobutu hawaelewani? Akakaamua kumuunga mkono mzee Laurent Kabila. Lakini akaweka masharti. Nikikusaidia kumng'oa Mobutu, eneo la Kivu Kusini, lenye Watutsi wengi (Banyamulenge), litajitenga na Congo na kuwa nchi inayojitegemea. Alishapiga hesabu za mbali za kuifanya Kivu kuwa sehemu ya Rwanda baada ya kujitenga DRC. Kabila akasema poa tu. Ashapigana miaka 30 msituni bila mafanikio? Sasa kapata "kamserereko" ka kwenda Ikulu akatae? Kagame nyuma yake walikuwepo Ufaransa na Uingereza akasema twende kwa maandishi. Mkataba ukasainiwa mji mdogo wa Lemera, Kivu Kusini. AFDL ikapewa support ya silaha na pesa, ikaamsha dude kupigana na majeshi ya serikali (FARDC). Wakati Mobutu anajaribu kupambana na AFDL, vikaibuka vikundi vingine vya waasi zaidi ya 40 kupigana na majeshi ya serikali. Vita ikiwa imepamba moto, Rwanda ikajitosa rasmi kupigana na serikali ya Mobutu kwa kisingizio cha kuwatafuta wanamgambo wa Intarahamwe waliokimbilia Congo. Uganda nayo ikaingiza jeshi kuwatafuta waasi wa LRA. Mobutu kaona "nini cha kufia" akadaka chopa akatokomea zake Moroco. Kesho yake tar.17 Mei 1997, Laurent Kabila akatangazwa Rais mpya wa Congo. Vita hii ikabatizwa jina vita vya kwanza vya Congo (1996-1997). (Malisa GJ)
    Like
    2
    · 1 Comments ·0 Shares ·970 Views
  • Read more
    muda mwingi yeye yeye utamkuta anaiongoza camera drone (ndege isiyo na rubani) au anakuwa na peni na karatasi yako muda mwingi anaandika baadhi ya vitu huyu ndo mfungua code wa kocha fadlu davies , huyu ndo anampa mifumo na uwezo wa timu inayotarajiwa kucheza na SIMBA , huyu ndo humpa udhaifu na ubora wa timu pinzani inayotarajiwa kucheza na SIMBA huyu ndo anajifungia ndani na kocha fadlu kumpa mrejesho wa perfomance ya mchezaji mmoja mmoja wa SIMBA baada ya kumalizika mazoezi Ni bwanamdogo sana ila uwezo wake unatisha sana ukizungumzia mafanikio ya RAJA CASABLANCA msimu uliopita basi moja kati ya waliochangia ni huyu jamaa na raja ikamaliza msimu uliopita ligi ya moroco wakiwa mabingwa na walimaliza msimu bila kufungwa (unbeaten) anaitwa MUEEZKAJEE ni mchambuzi wa video wa SIMBA SPORTS CLUB ( video &perfomance analysis) ni kijana mzaliwa wa africa kusini ila uwezo mkubwa sana , hata ile siku anaenda kuuambia uongozi wa RAJA kuwa anaondoka na anamfata kocha fadlu viongozi wa RAJA waliumia sana wote kwa pamoja walikuwa raja na msimu uliopita na wakaipa ubingwa namsimu huu wapo SIMBA wanaendelea kuwapa furaha wanasimba. 👍👍👍👍🦁🦁🦁🦁 #paulswai
    Like
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·797 Views
  • Read more
    NAKUKUMBUSHA MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOKWENDA KUNUNUA WANAWAKE WANAOJIUZA (DADA POA) `````````````````````````````````` Soma kwa makini kilichoandikwa acha kukurupuka kuacha comment..hii ni kwa ajili ya Elimu. Mambo haya pengine ni ya aibu na hayasemeki kwa urahisi tena hayafurahishi kusemwa hadharani. Lakini leo nitayasema kwa uchache kwa nia ya kujenga na wala sikusudii kuhamasisha uzinzi wala biashara hiyo 1. Usiende na nguo ambazo unazitumia katika shughuli zako za uzalishaji, iwe ni kazi ya kuajiriwa au kujiajiri. Na kama utaenda nazo basi ukimaliza usizitumie tena katika shughuli zako hizo baadhi yao Wana nuksi 2. Usiende na pesa nyingi ikiwa utaenda katika makazi yao. Kama bei ya kumnunua ni Tsh 5,000 basi nenda na walau 10,000 tu 3. Usifike na kuchagua papo hapo. Bali fika na usimame umbali kidogo utakaokuruhusu kuwaona vizuri na kuchagua umtakae. Usiwakaribie kabla hujachagua ukiwa mbali. 4. Chagua dada poa ambaye ngozi yake bado inanuru, pia zingatia umri wake usiwe mdogo sana wala usiwe mkubwa sana. 5. Usimuulize ulize maswali personal, wala usiombe namba zake za simu ikiwa ndio mara yako ya kwanza au ya pili kupata huduma yake. 6. Bila shaka hatakuruhusu kumnyonya romance, labda utoe dau kubwa. Hata uvutiwe naye kwa kiwango kipi, kamwe usikutanishe mdomo wako na wake, wala ulimi wako na wake kukwepa magonjwa kama hepatitis A,B,C. 7. Usiwe na vitu vingi na wala usivue suruali yote wakati wa tendo (short time) Na Kama umemchukua kwa full time ili umtumie usiku mzima. Basi asubuhi isikukute naye kahaba huyo. Hakikisha unaondoka kabla jogoo wa asubuhi hajawika au aondoke kabla ya jogoo wa alfajiri hajawika jitahidi sana mjukuu wangu mchweo yasikukute na Dada poa maana nyota njema huonekana asubuhi 8. Usimpeleke malaya katika geto au nyumba yako unayoitumia wewe na mkeo, wanao wakuwazaa au ndugu zako. 9. Usimdhulumu Dada poa malipo yake. Mpe kadiri ya mapatano yenu mlivyoelewana 10. Usitumie ulimi wako kumlamba mahala popote HUYO Dada poa 11. Usionyeshe ubora wa nguvu zako Kwa Dada poa pindi ufanyapo naye mapenzi. Kwa maana huwezi shindana na dada poa, na wala huwezi onyesha nguvu zako kwake. Utakuja ujifie 12. Usitumie Dawa za kusisimua kuongeza nguvu za kiume au urijali ufanyapo mapenzi na Dada poa Huwezi pata sifa popote Kwa kufanya hivyo. Ni afadhali utumie mbinu hizo kwa mkeo wa ndoa. Utasifiiwa na hakuna atakayekulaumu. 13. Usiogope magonjwa ya zinaa Kama UKIMWI n.k ufanyapo mapenzi na Dada poa isipokuwa ogopa dhambi ya uzinzi unayoifanya. 14. Usikae chini alafu Dada poa aje juu yako, bali wewe ndio uwe juu Kwa mitindo yote mtakayoitumia. Kwa sababu mwanaume ndiye anapaswa kuwa juu. Na Kama kuna mwanamke anayestahili kuwa juu basi ni Mkeo uliyemuoa ukamuacha nyumbani hii ni kwasababu za kiusalama zaidi. 15. Utakapofika mshindo, usiache shahawa zako kwenye kondomu kiholela. Ikiwezekana ondoka nazo ukazitupie mbele Kwa mbele, uwa wanazitumia kwenye uganga wa kienyeji kuvutia Watu madukani huku wewe unafirisika hela haikai mfukoni. 16. Usiwekeane ahadi na nadhiri na Dada poa. Usimuahidi ahadi yoyote kwa maana wengi wao wamejawa na hila za falme za giza 17. Usiguse Jambo lolote nyumbani kwako utakaporudi kabla haujajitakasa. Usimkumbatie Mkeo, wala watoto wako, wala wajukuu wako utokapo kufanya uzinzi na kahaba 18. Usije ukajisahau ukazaa na dada poa ilhali unajua unamke. 19. Usifanye mapenzi na dada poa taa zikiwa zimezimwa, kama huna D mbili huwezi kuelewa hapa 😂 20. Usifanye mapenzi na dada poa ukiwa haupo timamu kiakili, aidha ukiwa umelewa pombe au kutumia vilevi vingine vinavyoathiri ubongo 21. Kama vile usivyomjua vizuri huyo dada poa nawe asikujue vizuri. Jitahidi kudanganya karibu kila kitu hasa mambo yanayohusu familia yako, na kazi yako. 22. Usiende kununua dada poa kama hujiwezi Kwa self-defence na kupigana. Hii itakusaidia Kama itatokea dharura za yeye kukufanyia uhuni kwa kukuuza Kwa ving'asti kwa kukusingizia haujamlipa au umemlipa Pungufu ilhali ulimlipa mlivyokubaliana 23. Kama amekufurahisha Sana unaweza mpa bonus Kwa kuifanya roho yako ijisikie Raha. 24. Ikiwa umenunua dada poa kwa Tsh 30,000/= basi hakikisha NYUMBANI siku hiyo umeacha mara mbili ya hiyo 25. Ikiwa utaundiwa zengwe na kukamatwa na huyo dada poa basi suluhisha uwezavyo ishu isifike nyumbani kwa familia yako. Mwisho usinunue dada poa eneo ambalo ni mbali na barabara. Eneo ambalo limejitenga sana usiende kununua, utakuja kunishukuru Kama hakuna ulazima wa kununua dada poa mwaka huu nakushauri acha kwani sio kitu kizuri kiroho kwani miili yao mingi imebeba laana, mikosi na mabalaa kwa kua wanalala na kitu mtu mwenye kila aina ya changamoto kwa sababu tu ya pesa huu ndio ushauri wangu kwako `````````````````````````````````````````` Acha maoni yako soma kwa umakini...🙏
    Love
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·917 Views
  • Read more
    Idara ya Sheria ya Marekani imewafukuza kazi zaidi ya maafisa muhimu kumi na mbili waliokuwa wakifanya kazi katika timu ya Mwendesha Mashtaka Maalum Jack Smith, iliyokuwa ikimshitaki Rais Donald Trump. Uamuzi huo umefuata baada ya Kaimu Mwanasheria Mkuu, James McHenry kusema kwamba maafisa hao hawawezi kuaminiwa katika kutekeleza ajenda ya Rais Trump kwa uaminifu.
    0 Comments ·0 Shares ·239 Views
  • Read more
    SHERIA YA URAIA NA UHALALI WA WACHEZAJI WA SINGIDA BIG STARS & SIMBA KUPEWA URAIA WA TANZANIA Ijumaa, Januari 24, 2025 1. Usuli Jana, Januari 23, 2025, Idara ya Uhamiaji ilieleza kuwa wachezaji watatu (3) wa Singida Big Stars (EK Keyeke, JA Bada & MD Camara) wamepewa uraia tajnisi wa Tanzania kwa mujibu wa vifungu vya 9 & 23 vya Sheria ya Uraia Sura ya 357. Kabla jogoo halijawika, klabu ya Simba nayo jana hiyohiyo ikaomba wachezaji wake 9 wa kigeni nao wapewe uraia wa Tanzania. 2. Wageni Kupewa Uraia kwasababu ya Mbungi Si Jambo Geni Si jambo geni kwa wageni kupewa uraia kwasababu ya mbungi. Mfano mzuri ni nchi ya Tunisia. Tunisia ilimpa uraia Mbrazil Jose Clayton mwaka 1998 na akaichezea Tunisia michuano ya FIFA (kombe la dunia nchini Ufaransa). Tunisia pia ilimpa uraia raia wa Brazil, Franchine Silva dos Santos, mwaka 2000 na akaichezea Tunisia michuano ya FIFA. Toka mwaka jana 2024, wananchi wa Tunisia wanashinikiza Mbrazil mwingine, Rodrigo Rodriguez, apewe uraia wa Tunisia. Mshambuliaji huyo wa Esperance de Tunis ni moto wa kuotea mbali. Kwa mujibu wa sheria za Tunia, ili mgeni aweze kupewa uraia ni lazma awe amekaa Tunisia si chini ya miaka 5. Hata hivyo, Waziri ameruhusiwa kumpa mgeni uraia iwapo huyo mwombaji _"has provided great services to the country"_. 3. Wachezaji 3 wa Singida Black Stars 3.1 Emmanuel Kwame Keyeke Huyu raia wa Ghana ni fundi. Ni fundi kwelikweli. Ndiye Mchezaji Bora wa Ligi ya ndani ya Ghana 2023/24. Toka asajiliwe Julai 2024 na Singida Black Stars _amekiwasha_ kwelikweli. Ametwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi mara Nne ! 3.2 Josephat Athur Bada Singida Black Stars ilimsajili Julai 2024 kiungo huyu raia wa Ivory Coast baada ya kuizidi ujanja Ismailia ya Masri. 3.3 Mohammed Damaro Camara Kiungo huyu alisajiliwa Julai 2024. 4. Kifungu cha 9 & 23 4.1 Kifungu cha 9 cha Sheria ya Uraia kinaeleza: 4.1.1 Kifungu cha 9(1) kinaeleza kuwa mgeni yeyote mwenye miaka 18 au zaidi aweza kuomba uraia kwa Waziri wa Mambo ya Ndani na ataweza kupewa uraia tajnisi iwapo ametimiza masharti ya Jedwali la Pili. 4.2 Kifungu cha 23 kinaeleza kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani hatalazimika kutoa sababu yoyote baada ya kukubali au kukataa maombi ya uraia na uamuzi huo wa Waziri utakuwa wa mwisho na hautaweza kukatiwa rufaa wala kupingwa mahakamani. 4.3 Jedwali la Pili Jedwali la Pili limeweka masharti kadhaa. Sharti moja linaeleza : _"The applicant must have an adequate knowledge of Kiswahili or the English language"_. 5. Maswali chechefu: 5.1 Je, wachezaji Josephat Athur Bada na Mohammed Damaro Camara ambao wanazungumza kifaransa tu wamewezaje kukidhi kigezo cha kuwa na _*"ADEQUATE* knowledge"_ ya Kiswahili au Kiingereza ndani ya miezi 6 tu ? 5.2 Je, Waziri wa Mambo ya Ndani anafahamu kuwa Kisheria ingawa Sheria inaeleza kuwa _"Uamuzi wa Waziri ni wa Mwisho"_, haimaanishi kuwa Waziri akisigina Sheria, uamuzi hauwezi kupingwa? Yapo maamuzi mengi ya Mahakama Kuu yaelezeayo msimamo huu kuntu wa sheria mf : 5.2.1 Tanzania Air Services Ltd Vs Minister for Labour (1996) TLR 217 _*"The decision that the Minister's decision is final and conclusive does not mean that the decision cannot be reviewed by the High court. Indeed no appeal against such decision but an aggrieved party may come to the High court and ask for prerogative orders"*_. 5.2.2 Ben Kahale Vs AG*, Misc. Civil cause 23/2019: _*"Our understanding is that when the decision of the Minister is final, it doesn't oust jurisdiction of the court as final authority in dispensation of justice. We say so because the decision may still be subject to Judicial review"*_. 5.2 Je, kwanini Uomgozi wa Simba ndio uliowaombea wachezaji wake 9 uraia badala ya kila Mchezaji kuomba kama walivyofanya wale wachezaji 3 wa Singida Black Stars? Iweje timu kongwe kama Simba izidiwe uelewa na Singida Black Stars kuhusu mchakato huu ? Simba imekiri kwenye barua yao _"Tunaomba ofisi yako iridhie maombi yetu na kutupa utaratibu husika..."_ 5.3 Je, iwapo tutakuwa tunamwaga tu uraia kwa kila Mchezaji mgeni, haitatuathiri mbeleni ? Ikumbukwe kuwa lengo kubwa la kusajili wageni ni kwavile hakuna wachezaji wa ndani wenye ubora wa kutosha. Je, kila Mchezaji mgeni ana ubora wa kutosha?
    Love
    Like
    Haha
    4
    · 2 Comments ·0 Shares ·1K Views
More Results