My sister, uzuri wako sio kama kitu cha kukiweka parade ili watu wakione na kukikubali, then wewe uridhike kutokana na hilo pekee.
Huu Ulimwengu sio jumba la makumbusho kwamba uzunguke huku na huko kuvuta attention ya watu ili wakuone na kukukubali as if wewe ni kivutio cha utalii then ndio ujione umefanikiwa kwa hilo.
Uzuri wako sio kama hifadhi ya Gombe, watalii walipe waje waone sokwe wanavoruka ruka, na kuondoka zao. Sio kama hifadhi ya Serengeti au grumeti watalii waje waone Nyumbu wanavyohama kutoka upande huu kwenda upande mwengine. Walipe dola zao na kuondoka.
Ni bora zaidi uthaminiwe na mwanaume mmoja, kuliko kutamaniwa na dazani ya useless horny men.
Ndio uwe mzuri, lakini mzuri kwa ajili yako peke yako..na sio kwa ajili ya ulimwengu. Hauwezi kushindana na ulimwengu kwa ku-base kwenye uzuri, makalio, shape, etc..ulimwengu unao wanawake wa aina hiyo wengi sana na ambao hawana wanaweza wakapata kwa artificial ways.
Lakini roho nzuri, utu wema, tabia iliyo njema nani anaweza ku-fake? Beautiful mind nani anaweza kuipata? Sio vizuri hata kidogo kupiga picha za nusu uchi na kuziweka mitandaoni ili upate comments na likes za kutosha. Sio vema hata kidogo kuvaa nguo za mitego kwa minajili ya kusumbua vichwa vya wanaume wakware.
Hata kama una-hustle, unajitafutia riziki yako kwa mikono yako wewe mwenyewe, vaa vizuri, ishi maisha mazuri yatakayowapendeza na kuwabariki wengine...ishi maisha ambayo watu watapenda kukusikia jinsi unavyoongea kuliko wanavyopenda kukuona ukiwa unatembea nusu uchi, kuna kitu Mwenyezi Mungu amekiweka kwenye ulimi wako...wewe ni mzuri zaidi ya sura na shepu yako.
My wisdom, "The female brain itself is a highly intuitive emotion-processing machine, which when put to practice in the progress of the society, would do much more than any man can with all his analytical perspectives"