Upgrade to Pro

  • MAMA YANGU NDIYE MALKIA WA NGUVU

    “Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.”
    — Kutoka 20:12 (Biblia Takatifu)

    Hongera Uliye Na Mama ,Hongera Wewe Ambaye Mama Yako Yupo.

    Polee Wewe Ambaye Una Mdharau Mama Yako
    Polee Wale Ambao Mama Zao Wakiugua Wanaweka Vikao Vya Kuchagua Aende Kukaa Kwa Nani.

    Poleni Ninyi Mnaoishi Mijini Katika Mahekalu ,Na Mama Zenu Wako Vijijini Wanaishi Katika Majumba Ambayo Paa Zake Zinauliza Niue Nisiue.

    Poleni Ninyi Ambao Mmetenga Bajeti Za Kwenda Kutanua Katika Ma club Kila Weekend Wakati Mama Zenu Wanashindia Mihogo Na Chunga La Kuchemsha Jana.

    Poleni Ninyi Ambao Mnatembelea Magari Makali Na Kuhonga Michepuko Lakini Mama Zenu Huko Vijijini Hamja Wanunulia Hata Bodaboda.

    Poleni Ninyi Ambao Mkiombwa Fedha Na Mama Zetu Mnakasirika Lakini Ya Kununulia Mkojo Wa Firauni Kwenye Ma Bar Na Kufurahia Na Marafiki Zipo.

    Poleni Ninyi Mabinti Ambao Hamzungumzi Na Mama Zenu Yapata Mwaka Wa Tano Sasa Sababu Tu Ya Maonyo Yao Yamewakwaza.

    Nawapongeza Ninyi Nyote Wenye Mahusiano Mazuri Na Mama Zetu Maana Mmetambua Thamani Ya Mama Zenu

    Mungu Awabariki Sana Na Maana Mmetenda Jambo Jema Na Tena Lenye Kumpendeza Mungu

    _Mambo Ya Walawi 19:3[Biblia Takatifu]
    “Kila mtu na amche mama yake, na baba yake, nanyi mtazitunza Sabato zangu; mimi ndimi
    Bwana, Mungu wenu.”

    Mama Yako Ndiyo Kila Kitu Katika Maisha Yako Maana Alivumulia Yote Kakubeba Tumboni Mwake Miezi Tisa,Alivumulia Shida Zote Nyakati Za Kukuzaa Alikabiliana Na Kifo Ana Kwa Ana Lakini Kwa Maombi Yake Ukazaliwa.

    Akakulea Kwa Mapenzi Yote Ambayo Mama Anastahili Kufanya Kwa Mtoto Wake ,Hata Ulipo Mnyea Hakuukata Kiganja Cha Mkono Wake Sababu Wewe Ni Mtoto Wake.

    Alichana Nguo Zake Akakubali Yeye Abaki Mtupu Ili Wewe Uweze Kusitirika ,Alikufunika Kwa Khanga Yake Moja Ili Usipate Baridi Kali Lakini Yeye Alikubaliwa Kupigwa Na Baridi.

    Mweshimu Mama Yako Maana Ndiye Kiumbe Pekee Duniani Ambacho Hubeba Maumivu Ya Mtoto Wake**
    *#Jose Bambo#*
    MAMA YANGU NDIYE MALKIA WA NGUVU “Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.” — Kutoka 20:12 (Biblia Takatifu) Hongera Uliye Na Mama ,Hongera Wewe Ambaye Mama Yako Yupo. Polee Wewe Ambaye Una Mdharau Mama Yako Polee Wale Ambao Mama Zao Wakiugua Wanaweka Vikao Vya Kuchagua Aende Kukaa Kwa Nani. Poleni Ninyi Mnaoishi Mijini Katika Mahekalu ,Na Mama Zenu Wako Vijijini Wanaishi Katika Majumba Ambayo Paa Zake Zinauliza Niue Nisiue. Poleni Ninyi Ambao Mmetenga Bajeti Za Kwenda Kutanua Katika Ma club Kila Weekend Wakati Mama Zenu Wanashindia Mihogo Na Chunga La Kuchemsha Jana. Poleni Ninyi Ambao Mnatembelea Magari Makali Na Kuhonga Michepuko Lakini Mama Zenu Huko Vijijini Hamja Wanunulia Hata Bodaboda. Poleni Ninyi Ambao Mkiombwa Fedha Na Mama Zetu Mnakasirika Lakini Ya Kununulia Mkojo Wa Firauni Kwenye Ma Bar Na Kufurahia Na Marafiki Zipo. Poleni Ninyi Mabinti Ambao Hamzungumzi Na Mama Zenu Yapata Mwaka Wa Tano Sasa Sababu Tu Ya Maonyo Yao Yamewakwaza. Nawapongeza Ninyi Nyote Wenye Mahusiano Mazuri Na Mama Zetu Maana Mmetambua Thamani Ya Mama Zenu Mungu Awabariki Sana Na Maana Mmetenda Jambo Jema Na Tena Lenye Kumpendeza Mungu _Mambo Ya Walawi 19:3[Biblia Takatifu] “Kila mtu na amche mama yake, na baba yake, nanyi mtazitunza Sabato zangu; mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.” Mama Yako Ndiyo Kila Kitu Katika Maisha Yako Maana Alivumulia Yote Kakubeba Tumboni Mwake Miezi Tisa,Alivumulia Shida Zote Nyakati Za Kukuzaa Alikabiliana Na Kifo Ana Kwa Ana Lakini Kwa Maombi Yake Ukazaliwa. Akakulea Kwa Mapenzi Yote Ambayo Mama Anastahili Kufanya Kwa Mtoto Wake ,Hata Ulipo Mnyea Hakuukata Kiganja Cha Mkono Wake Sababu Wewe Ni Mtoto Wake. Alichana Nguo Zake Akakubali Yeye Abaki Mtupu Ili Wewe Uweze Kusitirika ,Alikufunika Kwa Khanga Yake Moja Ili Usipate Baridi Kali Lakini Yeye Alikubaliwa Kupigwa Na Baridi. Mweshimu Mama Yako Maana Ndiye Kiumbe Pekee Duniani Ambacho Hubeba Maumivu Ya Mtoto Wake** *#Jose Bambo#*
    Like
    1
    ·620 Views
  • Usivutiwe na muonekano wake wa nje,maana hujui ndani yake Kuna nini

    Usivutiwe na upole wake maana hujui nafsi yake inawaza nini


    Usidanganyike na ucheshi wake hujui moyo wake una mshauri nini

    Usivutiwe na utajiri alionao maana hujui amepitia mangapi Katika maisha yake

    Yule usiye mtegemea na kumdhania Katika maisha yako, ndiye anaweza kuwa msaada wakati wa shida yako

    Yule umuonaye hana u muhimu Katika maisha yako na asiyefaa kusimama mbele ya macho yako, ipo siku ndiye atakaye kuwa malaika wako wa nuru siku yakikukuta

    Usidhani wewe ni bora kuliko wengine,jifunze kuheshimu wengine maana hujui ni nani atakaye kufadhili siku yakikufika

    Fikiria kabla ya kutenda kisha tafakari kabla ya kuamua kitu chochote, maana hatima yako haipo mikononi mwako
    *#Jose Bambo #*




    Usivutiwe na muonekano wake wa nje,maana hujui ndani yake Kuna nini Usivutiwe na upole wake maana hujui nafsi yake inawaza nini Usidanganyike na ucheshi wake hujui moyo wake una mshauri nini Usivutiwe na utajiri alionao maana hujui amepitia mangapi Katika maisha yake Yule usiye mtegemea na kumdhania Katika maisha yako, ndiye anaweza kuwa msaada wakati wa shida yako Yule umuonaye hana u muhimu Katika maisha yako na asiyefaa kusimama mbele ya macho yako, ipo siku ndiye atakaye kuwa malaika wako wa nuru siku yakikukuta Usidhani wewe ni bora kuliko wengine,jifunze kuheshimu wengine maana hujui ni nani atakaye kufadhili siku yakikufika Fikiria kabla ya kutenda kisha tafakari kabla ya kuamua kitu chochote, maana hatima yako haipo mikononi mwako *#Jose Bambo #*
    Like
    1
    1 Comments ·307 Views
  • Like
    1
    ·225 Views
More Stories