SHERIA YA URAIA NA UHALALI WA WACHEZAJI WA SINGIDA BIG STARS & SIMBA KUPEWA URAIA WA TANZANIA
Ijumaa, Januari 24, 2025
1. Usuli
Jana, Januari 23, 2025, Idara ya Uhamiaji ilieleza kuwa wachezaji watatu (3) wa Singida Big Stars (EK Keyeke, JA Bada & MD Camara) wamepewa uraia tajnisi wa Tanzania kwa mujibu wa vifungu vya 9 & 23 vya Sheria ya Uraia Sura ya 357.
Kabla jogoo halijawika, klabu ya Simba nayo jana hiyohiyo ikaomba wachezaji wake 9 wa kigeni nao wapewe uraia wa Tanzania.
2. Wageni Kupewa Uraia kwasababu ya Mbungi Si Jambo Geni
Si jambo geni kwa wageni kupewa uraia kwasababu ya mbungi. Mfano mzuri ni nchi ya Tunisia.
Tunisia ilimpa uraia Mbrazil Jose Clayton mwaka 1998 na akaichezea Tunisia michuano ya FIFA (kombe la dunia nchini Ufaransa).
Tunisia pia ilimpa uraia raia wa Brazil, Franchine Silva dos Santos, mwaka 2000 na akaichezea Tunisia michuano ya FIFA.
Toka mwaka jana 2024, wananchi wa Tunisia wanashinikiza Mbrazil mwingine, Rodrigo Rodriguez, apewe uraia wa Tunisia. Mshambuliaji huyo wa Esperance de Tunis ni moto wa kuotea mbali.
Kwa mujibu wa sheria za Tunia, ili mgeni aweze kupewa uraia ni lazma awe amekaa Tunisia si chini ya miaka 5. Hata hivyo, Waziri ameruhusiwa kumpa mgeni uraia iwapo huyo mwombaji _"has provided great services to the country"_.
3. Wachezaji 3 wa Singida Black Stars
3.1 Emmanuel Kwame Keyeke
Huyu raia wa Ghana ni fundi. Ni fundi kwelikweli. Ndiye Mchezaji Bora wa Ligi ya ndani ya Ghana 2023/24.
Toka asajiliwe Julai 2024 na Singida Black Stars _amekiwasha_ kwelikweli. Ametwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi mara Nne !
3.2 Josephat Athur Bada
Singida Black Stars ilimsajili Julai 2024 kiungo huyu raia wa Ivory Coast baada ya kuizidi ujanja Ismailia ya Masri.
3.3 Mohammed Damaro Camara
Kiungo huyu alisajiliwa Julai 2024.
4. Kifungu cha 9 & 23
4.1 Kifungu cha 9 cha Sheria ya Uraia kinaeleza:
4.1.1 Kifungu cha 9(1) kinaeleza kuwa mgeni yeyote mwenye miaka 18 au zaidi aweza kuomba uraia kwa Waziri wa Mambo ya Ndani na ataweza kupewa uraia tajnisi iwapo ametimiza masharti ya Jedwali la Pili.
4.2 Kifungu cha 23 kinaeleza kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani hatalazimika kutoa sababu yoyote baada ya kukubali au kukataa maombi ya uraia na uamuzi huo wa Waziri utakuwa wa mwisho na hautaweza kukatiwa rufaa wala kupingwa mahakamani.
4.3 Jedwali la Pili
Jedwali la Pili limeweka masharti kadhaa. Sharti moja linaeleza : _"The applicant must have an adequate knowledge of Kiswahili or the English language"_.
5. Maswali chechefu:
5.1 Je, wachezaji Josephat Athur Bada na Mohammed Damaro Camara ambao wanazungumza kifaransa tu wamewezaje kukidhi kigezo cha kuwa na _*"ADEQUATE* knowledge"_ ya Kiswahili au Kiingereza ndani ya miezi 6 tu ?
5.2 Je, Waziri wa Mambo ya Ndani anafahamu kuwa Kisheria ingawa Sheria inaeleza kuwa _"Uamuzi wa Waziri ni wa Mwisho"_, haimaanishi kuwa Waziri akisigina Sheria, uamuzi hauwezi kupingwa? Yapo maamuzi mengi ya Mahakama Kuu yaelezeayo msimamo huu kuntu wa sheria mf :
5.2.1 Tanzania Air Services Ltd Vs Minister for Labour (1996) TLR 217
_*"The decision that the Minister's decision is final and conclusive does not mean that the decision cannot be reviewed by the High court. Indeed no appeal against such decision but an aggrieved party may come to the High court and ask for prerogative orders"*_.
5.2.2 Ben Kahale Vs AG*, Misc. Civil cause 23/2019:
_*"Our understanding is that when the decision of the Minister is final, it doesn't oust jurisdiction of the court as final authority in dispensation of justice. We say so because the decision may still be subject to Judicial review"*_.
5.2 Je, kwanini Uomgozi wa Simba ndio uliowaombea wachezaji wake 9 uraia badala ya kila Mchezaji kuomba kama walivyofanya wale wachezaji 3 wa Singida Black Stars? Iweje timu kongwe kama Simba izidiwe uelewa na Singida Black Stars kuhusu mchakato huu ? Simba imekiri kwenye barua yao _"Tunaomba ofisi yako iridhie maombi yetu na kutupa utaratibu husika..."_
5.3 Je, iwapo tutakuwa tunamwaga tu uraia kwa kila Mchezaji mgeni, haitatuathiri mbeleni ? Ikumbukwe kuwa lengo kubwa la kusajili wageni ni kwavile hakuna wachezaji wa ndani wenye ubora wa kutosha. Je, kila Mchezaji mgeni ana ubora wa kutosha?