• Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu Msanii wa muziki wa zamani Ferdnand Ndikuriyo (27) maarufu Chuma cha Chuma kutoka Nchini Burundi , kutumikia kifungo cha miaka mitatu (3) Jela na kulipa faini ya Shilingi 500,000 baada ya kukutwa na hatia ya kuishi Nchini Tanzania bila kibali.

    Hukumu hiyo imetolewa leo, Februari 5, 2025, na Hakimu Mkazi Mkuu, Yusto Ruboroga, baada ya upande wa mashtaka kuthibitisha shtaka dhidi ya mshtakiwa. Ikumbukwe kwamba Chuma cha Chuma alikamatwa kwa kosa hilo Septemba 18, 2024, katika eneo la Las Vegas Casino, Upanga Wilayani Ilala, Jijini Dar es Salaam.

    Hakimu Ruboroga alisema kuwa mshtakiwa ni Mkosaji wa mara ya pili (2) na kwamba anahitaji kupewa adhabu kali ili iwe fundisho kwake na kwa Watu wengine wanaojihusisha na vitendo kama hivyo vya kuingia Nchini Tanzania bila vibali (uhamiaji haramu).

    Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu Msanii wa muziki wa zamani Ferdnand Ndikuriyo (27) maarufu Chuma cha Chuma kutoka Nchini Burundi 🇧🇮, kutumikia kifungo cha miaka mitatu (3) Jela na kulipa faini ya Shilingi 500,000 baada ya kukutwa na hatia ya kuishi Nchini Tanzania 🇹🇿 bila kibali. Hukumu hiyo imetolewa leo, Februari 5, 2025, na Hakimu Mkazi Mkuu, Yusto Ruboroga, baada ya upande wa mashtaka kuthibitisha shtaka dhidi ya mshtakiwa. Ikumbukwe kwamba Chuma cha Chuma alikamatwa kwa kosa hilo Septemba 18, 2024, katika eneo la Las Vegas Casino, Upanga Wilayani Ilala, Jijini Dar es Salaam. Hakimu Ruboroga alisema kuwa mshtakiwa ni Mkosaji wa mara ya pili (2) na kwamba anahitaji kupewa adhabu kali ili iwe fundisho kwake na kwa Watu wengine wanaojihusisha na vitendo kama hivyo vya kuingia Nchini Tanzania bila vibali (uhamiaji haramu).
    0 Comments ·0 Shares ·88 Views
  • Rais wa Marekani , Donald Trump amesaini amri ya utendaji kuiondoa rasmi Nchi ya Marekani kutoka Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa (UNHRC) na Shirika la Misaada na Kazi la Umoja wa Mataifa kwa Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA).

    Aidha, ameagiza mapitio ya ushiriki wa Marekani katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO). Hatua hiyo ilifanyika Februari 4, 2025, ambapo kipande cha video fupi kilichowekwa kwenye mtandao wa X wa Rais Trump kilionyesha Katibu wa Wafanyakazi wa Ikulu ya White House, Will Scharf, akimkabidhi Rais agizo hilo kwa ajili ya kutia saini.

    "Kwa kuzingatia hatua nyingi zilizochukuliwa na mashirika kadhaa ya Umoja wa Mataifa ambazo zimeonyesha upendeleo mkubwa wa chuki dhidi ya Marekani, tuna agizo la utendaji lililotayarishwa kwa ajili yako ambalo lingeiondoa Marekani kutoka UNHRC na UNRWA, huku pia likipitia upya ushiriki wetu katika UNESCO." amesema Will Scharf kama sababu ya Donald Trump kuamua kujiondoa kwenye Mashirika hayo.

    Ameongeza kuwa agizo hilo pia linaelekeza ukaguzi wa kina wa ushiriki wa Marekani katika Umoja wa Mataifa kwa ujumla, hususan kuhusu tofaudi kubwa za ufadhili zinazotolewa na Marekani ikilinganishwa na mataifa mengine ambayo "hayatendei haki Marekani".

    Rais wa Marekani 🇺🇸, Donald Trump amesaini amri ya utendaji kuiondoa rasmi Nchi ya Marekani kutoka Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa (UNHRC) na Shirika la Misaada na Kazi la Umoja wa Mataifa kwa Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA). Aidha, ameagiza mapitio ya ushiriki wa Marekani katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO). Hatua hiyo ilifanyika Februari 4, 2025, ambapo kipande cha video fupi kilichowekwa kwenye mtandao wa X wa Rais Trump kilionyesha Katibu wa Wafanyakazi wa Ikulu ya White House, Will Scharf, akimkabidhi Rais agizo hilo kwa ajili ya kutia saini. "Kwa kuzingatia hatua nyingi zilizochukuliwa na mashirika kadhaa ya Umoja wa Mataifa ambazo zimeonyesha upendeleo mkubwa wa chuki dhidi ya Marekani, tuna agizo la utendaji lililotayarishwa kwa ajili yako ambalo lingeiondoa Marekani kutoka UNHRC na UNRWA, huku pia likipitia upya ushiriki wetu katika UNESCO." amesema Will Scharf kama sababu ya Donald Trump kuamua kujiondoa kwenye Mashirika hayo. Ameongeza kuwa agizo hilo pia linaelekeza ukaguzi wa kina wa ushiriki wa Marekani katika Umoja wa Mataifa kwa ujumla, hususan kuhusu tofaudi kubwa za ufadhili zinazotolewa na Marekani ikilinganishwa na mataifa mengine ambayo "hayatendei haki Marekani".
    0 Comments ·0 Shares ·133 Views
  • Msanii wa Nigeria , Wizkid achangia kumpa Bob Marley tuzo yake akiwa ni Marehemu.

    Pamoja na mafanikio makubwa aliyoyapata akiwa hai, Mwanamziki nguli Duniani, Raia wa Jamaica , Bob Marley hakuwahi kushinda tuzo ya Grammy katika maisha yake, lakini miaka michache iliopita familia yake walimtafuta Msanii kutoka Nchini Nigeria, Wizkid kwa ajili ya kufanya Collabo na Bob Marley ili waweze kuifanya upya kazi ya Bob Marley "One love, Music inspired by the Film, Album.

    Baada ya albamu hiyo kutoka ambapo Wizkid ameifanya upya imeshinda albamu bora ya mwaka ya Reggae 2025 kwenye tuzo za Grammy na kuweka rekodi ya kuwa tuzo ya kwanza ya Grammy ya Bob Marley huku shukurani kubwa amepewa Wizkid.

    Aidha, Wizkid amepokea cheti kutoka kwenye Uongozi wa Grammy na barua ya shukurani kutoka kwa familia ya Marley kwa kuifanya heshima ya baba yao kuendelea kuwepo Duniani na kumsaidia Mwanamziki huyo Mkongwe wa muziki wa Reggae kushinda Grammy yake ya kwanza.

    Msanii wa Nigeria 🇳🇬, Wizkid achangia kumpa Bob Marley tuzo yake akiwa ni Marehemu. Pamoja na mafanikio makubwa aliyoyapata akiwa hai, Mwanamziki nguli Duniani, Raia wa Jamaica 🇯🇲, Bob Marley hakuwahi kushinda tuzo ya Grammy katika maisha yake, lakini miaka michache iliopita familia yake walimtafuta Msanii kutoka Nchini Nigeria, Wizkid kwa ajili ya kufanya Collabo na Bob Marley ili waweze kuifanya upya kazi ya Bob Marley "One love, Music inspired by the Film, Album. Baada ya albamu hiyo kutoka ambapo Wizkid ameifanya upya imeshinda albamu bora ya mwaka ya Reggae 2025 kwenye tuzo za Grammy na kuweka rekodi ya kuwa tuzo ya kwanza ya Grammy ya Bob Marley huku shukurani kubwa amepewa Wizkid. Aidha, Wizkid amepokea cheti kutoka kwenye Uongozi wa Grammy na barua ya shukurani kutoka kwa familia ya Marley kwa kuifanya heshima ya baba yao kuendelea kuwepo Duniani na kumsaidia Mwanamziki huyo Mkongwe wa muziki wa Reggae kushinda Grammy yake ya kwanza.
    0 Comments ·0 Shares ·173 Views
  • Klabu zinazofanya vizuri katika Ligi Kuu zao barani Afrika kwa Wiki (14) zilizopita.

    3. Simba SC
    8. Yanga SC

    Klabu zinazofanya vizuri katika Ligi Kuu zao barani Afrika kwa Wiki (14) zilizopita. 3. Simba SC 8. Yanga SC
    0 Comments ·0 Shares ·58 Views
  • Rais wa Marekani , Donald Trump, ameshitua Watu Duniani baada ya kutangaza nia yake ya kuchukua udhibiti wa Ukanda wa Gaza ulioharibiwa na vita na kuufanyia maendeleo ya kiuchumi baada ya Wapalestina kuhamishiwa maeneo mengine. Hatua hiyo inaweza kubadili sera za Marekani za miongo kadhaa kuhusu mgogoro wa Israel na Palestina.

    Katika mkutano wa pamoja na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, Rais huyo alitangaza mpango huu bila kutoa maelezo ya kina.

    Kabla ya tangazo hilo, Trump alipendekeza kuwa zaidi ya Wapalestina milioni mbili (2) wa Gaza wahamishiwe Nchi jirani. Alikitaja kisiwa hicho kidogo, ambacho kwa sasa kina makubaliano dhaifu ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas, kuwa “eneo la kubomolewa.”

    Pendekezo hili linakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Washirika na Wapinzani wa Marekani. Pia linaibua maswali kuhusu ikiwa Saudi Arabia itashiriki katika juhudi mpya za Marekani za kuleta uhusiano wa kawaida kati ya Israel na mataifa ya Kiarabu.

    - Hatua ya Marekani kuchukua ushawishi wa moja kwa moja Gaza itapingana na msimamo wa muda mrefu wa Washington na Jumuiya ya kimataifa, ambao unaona Gaza kama sehemu ya Taifa la baadaye la Palestina pamoja na Ukingo wa Magharibi.

    "Marekani itachukua Ukanda wa Gaza, na tutafanya nao kazi nzuri sana. Tutakuwa na umiliki wake na kuhakikisha tunasafisha mabomu na silaha zote hatari zilizobaki."

    "Tutaendeleza Gaza, kuunda maelfu ya ajira, na kuifanya iwe sehemu ambayo Mashariki ya Kati yote itajivunia. Ninaona umiliki wa muda mrefu na ninaamini italeta utulivu mkubwa katika eneo hilo." amesema Donald Trump.

    “nyumbani kwa watu wa dunia.” Aliielezea Gaza kama eneo lenye uwezo wa kuwa “Riviera ya Mashariki ya Kati.” - Donald Trump baada ya kuulizwa nani ataishi Gaza baada ya kuitengeneza

    Trump hakujibu moja kwa moja kuhusu mamlaka au mchakato wa kuchukua eneo hilo la Gaza baada ya kuulizwa Marekani ina mamlaka gani ya kuichukua Gaza, ambalo lina urefu wa maili 25 (km 45) na upana wa hadi maili 6 (km 10) na historia ya vurugu. Serikali za awali za Marekani, ikiwemo ile ya Trump katika muhula wake wa kwanza, ziliepuka kutuma Wanajeshi Gaza.

    Rais wa Marekani 🇺🇸, Donald Trump, ameshitua Watu Duniani baada ya kutangaza nia yake ya kuchukua udhibiti wa Ukanda wa Gaza ulioharibiwa na vita na kuufanyia maendeleo ya kiuchumi baada ya Wapalestina kuhamishiwa maeneo mengine. Hatua hiyo inaweza kubadili sera za Marekani za miongo kadhaa kuhusu mgogoro wa Israel na Palestina. Katika mkutano wa pamoja na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, Rais huyo alitangaza mpango huu bila kutoa maelezo ya kina. Kabla ya tangazo hilo, Trump alipendekeza kuwa zaidi ya Wapalestina milioni mbili (2) wa Gaza wahamishiwe Nchi jirani. Alikitaja kisiwa hicho kidogo, ambacho kwa sasa kina makubaliano dhaifu ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas, kuwa “eneo la kubomolewa.” Pendekezo hili linakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Washirika na Wapinzani wa Marekani. Pia linaibua maswali kuhusu ikiwa Saudi Arabia itashiriki katika juhudi mpya za Marekani za kuleta uhusiano wa kawaida kati ya Israel na mataifa ya Kiarabu. - Hatua ya Marekani kuchukua ushawishi wa moja kwa moja Gaza itapingana na msimamo wa muda mrefu wa Washington na Jumuiya ya kimataifa, ambao unaona Gaza kama sehemu ya Taifa la baadaye la Palestina pamoja na Ukingo wa Magharibi. "Marekani itachukua Ukanda wa Gaza, na tutafanya nao kazi nzuri sana. Tutakuwa na umiliki wake na kuhakikisha tunasafisha mabomu na silaha zote hatari zilizobaki." "Tutaendeleza Gaza, kuunda maelfu ya ajira, na kuifanya iwe sehemu ambayo Mashariki ya Kati yote itajivunia. Ninaona umiliki wa muda mrefu na ninaamini italeta utulivu mkubwa katika eneo hilo." amesema Donald Trump. “nyumbani kwa watu wa dunia.” Aliielezea Gaza kama eneo lenye uwezo wa kuwa “Riviera ya Mashariki ya Kati.” - Donald Trump baada ya kuulizwa nani ataishi Gaza baada ya kuitengeneza Trump hakujibu moja kwa moja kuhusu mamlaka au mchakato wa kuchukua eneo hilo la Gaza baada ya kuulizwa Marekani ina mamlaka gani ya kuichukua Gaza, ambalo lina urefu wa maili 25 (km 45) na upana wa hadi maili 6 (km 10) na historia ya vurugu. Serikali za awali za Marekani, ikiwemo ile ya Trump katika muhula wake wa kwanza, ziliepuka kutuma Wanajeshi Gaza.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·146 Views
  • 0 Comments ·0 Shares ·61 Views
  • 0 Comments ·0 Shares ·60 Views
  • Like
    1
    · 1 Comments ·0 Shares ·26 Views
  • Chukua hiyooo
    Chukua hiyooo 🙄🙄🙄
    Love
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·42 Views ·0
  • Jamaa azingatiwee
    Jamaa azingatiwee 😂😂😂😂
    Love
    Wow
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·42 Views ·0