• (B)
    Dr. Harold Frederick Shipman alizaliwa mnamo 1946 huko Nottingham, Uingereza.

    Alikua katika familia yenye maisha ya kawaida, lakini kitu kimoja kilimtofautisha na watoto wengine—upendo wake kwa mama yake.

    Mama yake, Vera, alikuwa kila kitu kwake. Lakini alipofikisha miaka 17, alishuhudia kitu ambacho pengine kingemuumba kuwa mtu wa kutisha zaidi katika historia ya madaktari.

    Mama yake aligunduliwa kuwa na saratani ya mapafu.

    Katika miezi ya mwisho ya ugonjwa wake, alikuwa akipewa dawa za kupunguza maumivu—morphine—na Harold kijana aliona jinsi dawa hizo zilivyomfanya mama yake awe mtulivu kabla ya kufariki.

    Ilikuwa ni tukio lililobadilisha maisha yake.

    Lakini hakuna aliyefikiria kwamba tukio hili lingekuwa chanzo cha wimbi la vifo visivyoelezeka.
    (B) Dr. Harold Frederick Shipman alizaliwa mnamo 1946 huko Nottingham, Uingereza. Alikua katika familia yenye maisha ya kawaida, lakini kitu kimoja kilimtofautisha na watoto wengine—upendo wake kwa mama yake. Mama yake, Vera, alikuwa kila kitu kwake. Lakini alipofikisha miaka 17, alishuhudia kitu ambacho pengine kingemuumba kuwa mtu wa kutisha zaidi katika historia ya madaktari. Mama yake aligunduliwa kuwa na saratani ya mapafu. Katika miezi ya mwisho ya ugonjwa wake, alikuwa akipewa dawa za kupunguza maumivu—morphine—na Harold kijana aliona jinsi dawa hizo zilivyomfanya mama yake awe mtulivu kabla ya kufariki. Ilikuwa ni tukio lililobadilisha maisha yake. Lakini hakuna aliyefikiria kwamba tukio hili lingekuwa chanzo cha wimbi la vifo visivyoelezeka.
    Like
    2
    · 0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·121 Views
  • (C)
    Baada ya kifo cha mama yake, Shipman aliamua kuwa daktari. Alijiunga na Chuo Kikuu cha Leeds na baadaye akawa tabibu wa familia.

    Katika mwonekano wa nje, alikuwa mtu mwema, mtu wa familia, mwenye mke na watoto, anayependwa na wagonjwa wake. Lakini ndani yake, alikuwa akijificha kwenye kivuli cha giza na mauaji l.

    Alianza kazi yake kama daktari huko Yorkshire, na ilisemekana kuwa alikuwa mzuri sana kwa wagonjwa wake.

    Hata hivyo, mnamo 1975, alinaswa akiandika dawa za opioid (pethidine) kwa matumizi yake binafsi. Alipatikana na hatia, lakini badala ya kufungwa jela, alipigwa faini na kupoteza kazi kwa muda mfupi.

    Baadaye, alihamia mji wa Hyde na kuanza upya maisha yake kama daktari wa familia.

    Huko ndipo msururu wa vifo vya ajabu ulipoanza.
    (C) Baada ya kifo cha mama yake, Shipman aliamua kuwa daktari. Alijiunga na Chuo Kikuu cha Leeds na baadaye akawa tabibu wa familia. Katika mwonekano wa nje, alikuwa mtu mwema, mtu wa familia, mwenye mke na watoto, anayependwa na wagonjwa wake. Lakini ndani yake, alikuwa akijificha kwenye kivuli cha giza na mauaji l. Alianza kazi yake kama daktari huko Yorkshire, na ilisemekana kuwa alikuwa mzuri sana kwa wagonjwa wake. Hata hivyo, mnamo 1975, alinaswa akiandika dawa za opioid (pethidine) kwa matumizi yake binafsi. Alipatikana na hatia, lakini badala ya kufungwa jela, alipigwa faini na kupoteza kazi kwa muda mfupi. Baadaye, alihamia mji wa Hyde na kuanza upya maisha yake kama daktari wa familia. Huko ndipo msururu wa vifo vya ajabu ulipoanza.
    Like
    1
    · 0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·84 Views
  • (D)
    Shipman alikuwa daktari wa kuaminika. Wagonjwa wake walimpenda kwa sababu alikuwa mwenye huruma, na alikuwa akiwatembelea hata majumbani kwao.

    Lakini ilianza kuonekana kuwa wagonjwa wake walikuwa wakifa kwa wingi kuliko kawaida.

    Walikuwa wakifa kwa "mashambulizi ya moyo" au "udhaifu wa uzee." Hakukuwa na ishara ya mateso—ilikuwa ni kama waliaga dunia kwa utulivu.

    Mara nyingi, alikuwa daktari pekee aliyekuwepo wakati wa vifo hivyo.

    Hakuna aliyeshuku lolote, hasa kwa sababu wengi wa waliokufa walikuwa wazee.

    Lakini jambo la ajabu ni kwamba, tofauti na madaktari wengine ambao hujaribu kuwaokoa wagonjwa wao hadi dakika ya mwisho, Shipman hakuwahi kujaribu kuwapigania—hakuwahi kupiga simu kwa ambulansi.

    Alikuwa akiwapatia sindano ya morphine katika dozi kubwa—sawa na aliyowahi kuona ikitumiwa kwa mama yake alipokuwa kijana. Na ndani ya dakika chache, walikuwa wakiondoka duniani kimyakimya
    (D) Shipman alikuwa daktari wa kuaminika. Wagonjwa wake walimpenda kwa sababu alikuwa mwenye huruma, na alikuwa akiwatembelea hata majumbani kwao. Lakini ilianza kuonekana kuwa wagonjwa wake walikuwa wakifa kwa wingi kuliko kawaida. Walikuwa wakifa kwa "mashambulizi ya moyo" au "udhaifu wa uzee." Hakukuwa na ishara ya mateso—ilikuwa ni kama waliaga dunia kwa utulivu. Mara nyingi, alikuwa daktari pekee aliyekuwepo wakati wa vifo hivyo. Hakuna aliyeshuku lolote, hasa kwa sababu wengi wa waliokufa walikuwa wazee. Lakini jambo la ajabu ni kwamba, tofauti na madaktari wengine ambao hujaribu kuwaokoa wagonjwa wao hadi dakika ya mwisho, Shipman hakuwahi kujaribu kuwapigania—hakuwahi kupiga simu kwa ambulansi. Alikuwa akiwapatia sindano ya morphine katika dozi kubwa—sawa na aliyowahi kuona ikitumiwa kwa mama yake alipokuwa kijana. Na ndani ya dakika chache, walikuwa wakiondoka duniani kimyakimya
    Like
    1
    · 0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·99 Views
  • (E)
    Kwa miaka mingi, Shipman aliendelea na mauaji yake bila kugundulika.

    Lakini mnamo 1998, alifanya kosa moja kubwa—alijaribu kughushi wosia wa mgonjwa wake mmoja, Kathleen Grundy.

    Kathleen alikuwa mama mwenye afya njema mwenye umri wa miaka 81. Alipoaga dunia ghafla, binti yake, Angela Woodruff, alishangazwa na jinsi kifo hicho kilivyotokea bila onyo.

    Lakini mshangao mkubwa zaidi ulikuja alipogundua kuwa mama yake alikuwa ameandika wosia mpya, ukisema kuwa mali yake yote iende kwa daktari wake—Harold Shipman!

    Huo ulikuwa ushahidi wa kwanza wa kweli kwamba huyu hakuwa daktari wa kawaida—alikuwa muuaji.
    (E) Kwa miaka mingi, Shipman aliendelea na mauaji yake bila kugundulika. Lakini mnamo 1998, alifanya kosa moja kubwa—alijaribu kughushi wosia wa mgonjwa wake mmoja, Kathleen Grundy. Kathleen alikuwa mama mwenye afya njema mwenye umri wa miaka 81. Alipoaga dunia ghafla, binti yake, Angela Woodruff, alishangazwa na jinsi kifo hicho kilivyotokea bila onyo. Lakini mshangao mkubwa zaidi ulikuja alipogundua kuwa mama yake alikuwa ameandika wosia mpya, ukisema kuwa mali yake yote iende kwa daktari wake—Harold Shipman! Huo ulikuwa ushahidi wa kwanza wa kweli kwamba huyu hakuwa daktari wa kawaida—alikuwa muuaji.
    Like
    1
    · 0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·81 Views
  • (F)
    Baada ya uchunguzi wa haraka, polisi walifukua miili kadhaa ya wagonjwa wa Shipman na kugundua kitu cha kutisha—miili yao ilikuwa na kiwango kikubwa cha morphine.

    Shipman alikamatwa na kushtakiwa kwa mauaji ya wagonjwa 15, lakini uchunguzi wa kina ulionesha kuwa huenda alikuwa amewaua zaidi ya watu 250 kwa kipindi cha miaka 23!

    Alifungwa jela mwaka 2000, na mwaka 2004, alipatikana amejinyonga kwenye seli yake.
    (F) Baada ya uchunguzi wa haraka, polisi walifukua miili kadhaa ya wagonjwa wa Shipman na kugundua kitu cha kutisha—miili yao ilikuwa na kiwango kikubwa cha morphine. Shipman alikamatwa na kushtakiwa kwa mauaji ya wagonjwa 15, lakini uchunguzi wa kina ulionesha kuwa huenda alikuwa amewaua zaidi ya watu 250 kwa kipindi cha miaka 23! Alifungwa jela mwaka 2000, na mwaka 2004, alipatikana amejinyonga kwenye seli yake.
    Like
    Love
    2
    · 0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·79 Views
  • Issue ya Harold Shipman ilitikisa ulimwengu wa kitabibu.

    Ilizua hofu na maswali mengi—je, kuna wauaji wengine waliyojificha kwenye taaluma ya tiba?

    Serikali ya Uingereza ilibadilisha sheria za matibabu, na hospitali nyingi duniani ziliboresha mifumo yao ili kuhakikisha hakuna daktari mwingine anayeweza kufanya alichofanya Shipman.
    Issue ya Harold Shipman ilitikisa ulimwengu wa kitabibu. Ilizua hofu na maswali mengi—je, kuna wauaji wengine waliyojificha kwenye taaluma ya tiba? Serikali ya Uingereza ilibadilisha sheria za matibabu, na hospitali nyingi duniani ziliboresha mifumo yao ili kuhakikisha hakuna daktari mwingine anayeweza kufanya alichofanya Shipman.
    Like
    Love
    2
    · 0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·92 Views
  • Life quotes
    Life quotes
    Like
    1
    · 0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·57 Views
  • Usisahau kunifollow,kulike na kucomment asante
    Usisahau kunifollow,kulike na kucomment asante
    Like
    1
    · 0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·28 Views
  • Naomba mnifollow wadau na like zenu na comments ni za muhimu sana
    Naomba mnifollow wadau na like zenu na comments ni za muhimu sana
    Like
    1
    · 0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·56 Views
  • #Comment,#like and #follow meplease
    #Comment,#like and #follow meplease
    Like
    1
    · 0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·40 Views