Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Goma wafunguliwa upya baada ya kufungwa kwa mwaka mzima.
Goma, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Goma umefunguliwa rasmi leo Alhamisi, baada ya kufungwa kwa karibu mwaka mzima kufuatia kukamatwa kwa Mji na Waasi wa AFC/M23.
Ndege ya kwanza kuwasili katika Uwanja huo ilikuwa Helikopta ya MONUSCO, iliyomleta Kiongozi wa muda wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa, Vivian van de Perre. Ziara yake inalenga kuthibitisha msaada wa Umoja wa Mataifa katika mchakato wa amani unaoendelea kati ya serikali ya Congo na Waasi.
Akiwa na Waandishi wa habari, van de Perre alisema: "Tumekuja hapa kuthibitisha dhamira ya MONUSCO katika kuunga mkono mchakato wa amani unaoendelea kati ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kundi la AFC/M23."
Aliongeza kuwa: "Nina mpango wa kukutana na pande zote husika ili kuendeleza mfumo wa ufuatiliaji na ukaguzi wa mapatano ya kusitisha mapigano."
Ziara hii inatekelezwa chini ya azimio la 2808 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, linalowekwa ili MONUSCO isaidie utekelezaji wa mapatano ya amani na kuhakikisha usalama wa Raia.
Ufunguaji upya wa Uwanja huu ni ishara ya matumaini kwa Wakazi wa Nord-Kivu, na ni hatua muhimu katika juhudi za kimataifa za kurejesha utulivu na usalama katika eneo lililoathiriwa na mizozo ya kivita.
Toa maoni yako
#Habari

0 Comments
0 Shares
8 Views