0 Reacties
·0 aandelen
·2 Views
-
-
-
-
-
-
-
Iran yakataa mazungumzo na Trump, yakanusha madai ya uharibifu wa nyuklia.
Katika kile kinachoonekana kuwa kuendelea kwa mvutano wa kidiplomasia kati ya Marekani na Iran, Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, ameibuka hadharani na kukataa pendekezo la Rais wa Marekani, Donald Trump, la kurejea kwenye meza ya mazungumzo.
Akizungumza kupitia vyombo vya habari vya Serikali, Khamenei alisema wazi kuwa pendekezo la Trump halikuwa la kweli, bali ni jaribio la kulazimisha makubaliano kwa njia ya vitisho.
"Trump anasema yeye ni Mtaalamu wa kufanikisha makubaliano, lakini kama makubaliano hayo yanaambatana na shinikizo na matokeo yake tayari yameamuliwa, basi hiyo siyo makubaliano bali ni kulazimisha na vitisho," - Ayatollah Ali Khamenei.
Kauli hiyo ya Khamenei imekuja kufuatia hotuba ya Trump wiki iliyopita, ambapo aliwaambia Wabunge wa Israel kwamba Marekani ingependa kufanikisha makubaliano ya amani na Tehran, hasa baada ya kutangazwa kwa usitishaji mapigano kati ya Israel na Hamas huko Gaza. Katika hotuba hiyo, Trump pia alidai kuwa:
"Marekani imeharibu kabisa maeneo ya nyuklia ya Iran."
Lakini Khamenei alikanusha vikali kauli hiyo, akisema:
"Rais wa Marekani anajivunia kusema kuwa wamebomoa na kuharibu sekta ya nyuklia ya Iran. Vizuri, endeleeni kuota!"
Kauli hizi zinaashiria kuwa uhusiano kati ya Tehran na Washington bado uko katika hali ya sintofahamu, huku Iran ikionekana kuchukua msimamo mkali dhidi ya kile inachokiona kama mbinu za mabeberu.
Kwa sasa, haijafahamika kama juhudi za kidiplomasia zitaendelea, hasa ikizingatiwa kuwa Iran bado inashikilia haki yake ya kuendesha mpango wake wa nyuklia kama nchi huru.
Je, unadhani mvutano huu unaweza kuzua mgogoro mpya wa kimataifa?
Toa maoni yakoIran yakataa mazungumzo na Trump, yakanusha madai ya uharibifu wa nyuklia. Katika kile kinachoonekana kuwa kuendelea kwa mvutano wa kidiplomasia kati ya Marekani na Iran, Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, ameibuka hadharani na kukataa pendekezo la Rais wa Marekani, Donald Trump, la kurejea kwenye meza ya mazungumzo. Akizungumza kupitia vyombo vya habari vya Serikali, Khamenei alisema wazi kuwa pendekezo la Trump halikuwa la kweli, bali ni jaribio la kulazimisha makubaliano kwa njia ya vitisho. "Trump anasema yeye ni Mtaalamu wa kufanikisha makubaliano, lakini kama makubaliano hayo yanaambatana na shinikizo na matokeo yake tayari yameamuliwa, basi hiyo siyo makubaliano bali ni kulazimisha na vitisho," - Ayatollah Ali Khamenei. Kauli hiyo ya Khamenei imekuja kufuatia hotuba ya Trump wiki iliyopita, ambapo aliwaambia Wabunge wa Israel kwamba Marekani ingependa kufanikisha makubaliano ya amani na Tehran, hasa baada ya kutangazwa kwa usitishaji mapigano kati ya Israel na Hamas huko Gaza. Katika hotuba hiyo, Trump pia alidai kuwa: "Marekani imeharibu kabisa maeneo ya nyuklia ya Iran." Lakini Khamenei alikanusha vikali kauli hiyo, akisema: "Rais wa Marekani anajivunia kusema kuwa wamebomoa na kuharibu sekta ya nyuklia ya Iran. Vizuri, endeleeni kuota!" Kauli hizi zinaashiria kuwa uhusiano kati ya Tehran na Washington bado uko katika hali ya sintofahamu, huku Iran ikionekana kuchukua msimamo mkali dhidi ya kile inachokiona kama mbinu za mabeberu. Kwa sasa, haijafahamika kama juhudi za kidiplomasia zitaendelea, hasa ikizingatiwa kuwa Iran bado inashikilia haki yake ya kuendesha mpango wake wa nyuklia kama nchi huru. Je, unadhani mvutano huu unaweza kuzua mgogoro mpya wa kimataifa? Toa maoni yako0 Reacties ·0 aandelen ·51 Views -
0 Reacties ·0 aandelen ·6 Views
-
0 Reacties ·0 aandelen ·32 Views