Upgrade to Pro

Kuna siku nilikutana na mdada fulani hivi kwenye ofisi x.
Wakati huo nilikuwa nafuatilia huko jambo fulani hivi.
Wote tulikuwa mapokezi na mimi nilikuwa nimeshahudumiwa kwa hivi nilikuwa nasubiri kuitwa mahali nilipokuwa naelekea.

Yeye katika shida yake aliyokuwa amefika ili asaidiwe kuitatua aliulizwa maswali haya;

1. Una baba? Akajibu sina, simfahamu hata sijui yuko wapi, kwani hata sijawahi kumwona.

2. Una mama? Akajibu mama pia simfahamu maana alifariki ningali mdogo sana.

3. Sasa kabila lako ni lipi? Akajibu hata kabila silijui kwa kuwa simfahamu baba, kwa kuwa nimekulia kwa bibi mzaa mama nitataja kabila lake.

Na maswali mengi yaliyofuatia.
Mimi kilichonishangaza na kunishawishi nijiulize maswali mengi ni hiyo namba moja.

Swali ambalo binti ameulizwa kama ana baba akajibu hata hamfahamu. Kiuhalisia wanaume wengi tumekuwa tukiyakimbia majukumu yetu sana. Fikiria mtu anajua kabisa kuwa alimpa mwanamke ujauzito, hata kama haikuwa wakati sahihi badala ya kuonesha japo ushirikiano na mwanamke huyo anamkimbia.

Mwanamke anakuwa na maumivu mengi, maumivu ya kukimbiwa na mtu aliyempenda, maumivu ya kutukanwa kuwa amepatia ujauzito nyumbani, maumivu ya kubezwa, maumivu ya ujauzito kama mama, uchovu na kila aina ya kejeli.
Katika nyakati zile ambazo wanatuhtaji sana tunawakimbia.

Matokeo yake ambalo hatuombei mama akipata shida wakati wa kujifungua akafariki, mtoto anabaki mpweke, haonji upendo wa yeyote. Anaingia kwenye ulimwengu wa mahangaiko peke yake na huku baba yake upo bize na mambo mengine.
Nafikiri tuwe na huruma nao, tusiwatelekeze watoto ambao ndio taifa la kesho.

Poleni sana wanawake kwa yanayowakumba.

Kuna siku nilikutana na mdada fulani hivi kwenye ofisi x. Wakati huo nilikuwa nafuatilia huko jambo fulani hivi. Wote tulikuwa mapokezi na mimi nilikuwa nimeshahudumiwa kwa hivi nilikuwa nasubiri kuitwa mahali nilipokuwa naelekea. Yeye katika shida yake aliyokuwa amefika ili asaidiwe kuitatua aliulizwa maswali haya; 1. Una baba? Akajibu sina, simfahamu hata sijui yuko wapi, kwani hata sijawahi kumwona. 2. Una mama? Akajibu mama pia simfahamu maana alifariki ningali mdogo sana. 3. Sasa kabila lako ni lipi? Akajibu hata kabila silijui kwa kuwa simfahamu baba, kwa kuwa nimekulia kwa bibi mzaa mama nitataja kabila lake. Na maswali mengi yaliyofuatia. Mimi kilichonishangaza na kunishawishi nijiulize maswali mengi ni hiyo namba moja. Swali ambalo binti ameulizwa kama ana baba akajibu hata hamfahamu. Kiuhalisia wanaume wengi tumekuwa tukiyakimbia majukumu yetu sana. Fikiria mtu anajua kabisa kuwa alimpa mwanamke ujauzito, hata kama haikuwa wakati sahihi badala ya kuonesha japo ushirikiano na mwanamke huyo anamkimbia. Mwanamke anakuwa na maumivu mengi, maumivu ya kukimbiwa na mtu aliyempenda, maumivu ya kutukanwa kuwa amepatia ujauzito nyumbani, maumivu ya kubezwa, maumivu ya ujauzito kama mama, uchovu na kila aina ya kejeli. Katika nyakati zile ambazo wanatuhtaji sana tunawakimbia. Matokeo yake ambalo hatuombei mama akipata shida wakati wa kujifungua akafariki, mtoto anabaki mpweke, haonji upendo wa yeyote. Anaingia kwenye ulimwengu wa mahangaiko peke yake na huku baba yake upo bize na mambo mengine. Nafikiri tuwe na huruma nao, tusiwatelekeze watoto ambao ndio taifa la kesho. Poleni sana wanawake kwa yanayowakumba. 🤡🤡🤡
Like
1
·149 Views