Upgrade to Pro

Je, Ni Sahihi Kuombea Marehemu/Mtu Aliyekufa?

= Mtu akishakufa huwezi tena kumwombea chochote, haifai hata kumwombea apumzike kwa amani au awekwe mahala pema peponi. Hiyo nafasi haipo kabisa maana mara baada ya kufa ni hukumu.

= Mara mtu akifa, hukumu hufanyika halafu wafu huwekwa eneo la mangojeo yaani kuzimu Kwa wenye dhambi na peponi kwa watakatifu wakingojea ujio wa Yesu Kristo. Baada ya hapo kutakuwa na mauti ya pili kwa wenye dhambi, yaani kutupwa kwenye ziwa la moto.

>> Waebrania 9:27
Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu;

= Kwa hiyo, mtu asipotengeneza maisha yake akiwa hai asitarajie kuombewa aende peponi akiisha kufa. Pia waliokufa hata kama waliishi maisha matakatifu hatuwezi kuwaomba watuombee maana tutakuwa tunaomba wafu. Ibada ya wafu ni chukizo kwa Mungu.

>> Kumbukumbu la Torati 18:10-11
10 Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,

11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu.

= Tunao waombezi wawili wakuu kule mbinguni; Yesu Kristo na Roho Mtakatifu.

= Mtu akishakufa mawasiliano hukatwa kati ya walio hai na waliokufa. Hakuna namna unaweza kumwombea chochote ili kubadilisha chochote wala huwezi kumwomba akuombee.

>> Mhubiri 9:5
5 kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.

= Mfano sahihi angalia kwa tajiri na masikini Lazaro;
>>Luka 16: 20-30
19 Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa.

20 Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi,

21 naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake.

22 Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa.

23 Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.

24 Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.

25 Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa.

26 Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.

27 Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu,

28 kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso.

29 Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao.

30 Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu.

31 Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu.
Je, Ni Sahihi Kuombea Marehemu/Mtu Aliyekufa? = Mtu akishakufa huwezi tena kumwombea chochote, haifai hata kumwombea apumzike kwa amani au awekwe mahala pema peponi. Hiyo nafasi haipo kabisa maana mara baada ya kufa ni hukumu. = Mara mtu akifa, hukumu hufanyika halafu wafu huwekwa eneo la mangojeo yaani kuzimu Kwa wenye dhambi na peponi kwa watakatifu wakingojea ujio wa Yesu Kristo. Baada ya hapo kutakuwa na mauti ya pili kwa wenye dhambi, yaani kutupwa kwenye ziwa la moto. >> Waebrania 9:27 Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu; = Kwa hiyo, mtu asipotengeneza maisha yake akiwa hai asitarajie kuombewa aende peponi akiisha kufa. Pia waliokufa hata kama waliishi maisha matakatifu hatuwezi kuwaomba watuombee maana tutakuwa tunaomba wafu. Ibada ya wafu ni chukizo kwa Mungu. >> Kumbukumbu la Torati 18:10-11 10 Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, 11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu. = Tunao waombezi wawili wakuu kule mbinguni; Yesu Kristo na Roho Mtakatifu. = Mtu akishakufa mawasiliano hukatwa kati ya walio hai na waliokufa. Hakuna namna unaweza kumwombea chochote ili kubadilisha chochote wala huwezi kumwomba akuombee. >> Mhubiri 9:5 5 kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa. = Mfano sahihi angalia kwa tajiri na masikini Lazaro; >>Luka 16: 20-30 19 Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa. 20 Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi, 21 naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake. 22 Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa. 23 Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake. 24 Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu. 25 Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa. 26 Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu. 27 Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu, 28 kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso. 29 Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao. 30 Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu. 31 Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu.
Love
1
·594 Views