Mise à niveau vers Pro

Tunaishi chini ya jua lenye ushindani mwingi na wa kipuuzi sana kwa kizazi cha sasa.Wale tuliopaswa kurithi ama kujifunza mambo mema kutoka kwao ndo hao wengi wao wanafanya ujinga na kujificha kwenye kivuli cha unavyofikiri sivyo ilivyo.
Binadamu siku hizi anakufanyia ubaya alaf anakujia Kwa mgongo wa utani.Na bahati mbaya dini na charity siku hizi zinatumika kama kichaka cha kuficha uovu wa watu.Binadamu amekuwa si binadamu tena. Wakati mwingine anae kuchukia na asiyekutakia mema ni ndugu wa damu kabisa,ndo dunia ilipofika.
Tunaishi kwenye hatari tuliyoamua kuibatiza jina la salama.
Shari tumeigeuza shwari.
Maumivu na huzuni ya mtu ni furaha ya mwingine.Huku tukitumia hadhara kutengeneza mazingira ya kuendelea kutekeleza maovu.Kwa kivuli cha nani ameniona?au nani anajua?
Kile kitu Dunia imeshindwa kutambua majira na nyakati yamebadilika sana.
Zamani zile kulikuwa hakuna siri ya watu wawili ila zamani hizi hakuna siri ya mtu mmoja.Wakati twasema ni siri kuna mtu mahala fulani anaijua hiyo siri.
Na hapo ndo tunasema mtu anapigana na kivuli chake mwenyewe Kwa kujiongopea kuwa hakuna maumivi.
Lakini swali la kujiuliza kati ya kivuli cha mtu na mtu mwenyewe ni nani anaumia? Tutafakari
Tunaishi chini ya jua lenye ushindani mwingi na wa kipuuzi sana kwa kizazi cha sasa.Wale tuliopaswa kurithi ama kujifunza mambo mema kutoka kwao ndo hao wengi wao wanafanya ujinga na kujificha kwenye kivuli cha unavyofikiri sivyo ilivyo. Binadamu siku hizi anakufanyia ubaya alaf anakujia Kwa mgongo wa utani.Na bahati mbaya dini na charity siku hizi zinatumika kama kichaka cha kuficha uovu wa watu.Binadamu amekuwa si binadamu tena. Wakati mwingine anae kuchukia na asiyekutakia mema ni ndugu wa damu kabisa,ndo dunia ilipofika. Tunaishi kwenye hatari tuliyoamua kuibatiza jina la salama. Shari tumeigeuza shwari. Maumivu na huzuni ya mtu ni furaha ya mwingine.Huku tukitumia hadhara kutengeneza mazingira ya kuendelea kutekeleza maovu.Kwa kivuli cha nani ameniona?au nani anajua? Kile kitu Dunia imeshindwa kutambua majira na nyakati yamebadilika sana. Zamani zile kulikuwa hakuna siri ya watu wawili ila zamani hizi hakuna siri ya mtu mmoja.Wakati twasema ni siri kuna mtu mahala fulani anaijua hiyo siri. Na hapo ndo tunasema mtu anapigana na kivuli chake mwenyewe Kwa kujiongopea kuwa hakuna maumivi. Lakini swali la kujiuliza kati ya kivuli cha mtu na mtu mwenyewe ni nani anaumia? Tutafakari
Like
Love
2
·48 Vue