USIMSAHAU

Kabla hajaaga dunia mzee mmoja alimpa maneno ya hekima kwa machozi mtoto wake .Alimuambia haya ,"Mwanangu hali yangu ni mbaya naendea safari ya wasafiri wote duniani lakini ninakuhusia neno hili ,katika maisha yako usije kuwasahau watu wawili wafuatao"

Wakwanza
Mwanangu usimsahau mtu yule aliyekaa nawe katika magumu yako.
Yule aliyesema wewe ni mwema,wengine waliposema wewe ni mbaya.
Yule aliyesonga mbele akabaki nawe,wengine waliporudi nyuma kuachana nawe.
Yule uliyemfanyia wema mmoja akautumia huo kupuuza mabaya yako yote.
Yule ambaye katika giza nene la dhiki zako,akaleta nuru ya faraja ya ulimi wake.
Yule ambaye katika masika ya mateso yako,alifanyiza hema la mwili wake akukinge usinyeshewe.
Yule ambaye katika joto kali la kuandamwa na watesi wako alileta baridi kwa tabasamu lake akufariji.
Yule ambaye kwenye upweke wako ,uwepo wake ukafanyika upo na kundi kubwa.
USIMSAHAU

Wapili
Mwanangu usimsahau mtu aliyekuacha kipindi cha mateso yako.
Aliyetakiwa akusaidie, akakudhihaki.
Aliyetakiwa akupe msaada, akageuka mwiba.
Aliyetakiwa akushukuru akakulaumu.
Aliyesahau wema wako wote na kukumbuka ubaya wako mmoja.
Aliyetakiwa akufariji ,akakuletea jeuri.
Aliyewaona wengine wanakukimbia,akaungana nao.
Aliyeona upweke wako akakuacha,akijihesabu yeye ni wa muhimu na akuoneshe unamhitaji.
USIMSAHAU
Kwaheri mwanangu!!!
USIMSAHAU😭😭😭 Kabla hajaaga dunia mzee mmoja alimpa maneno ya hekima kwa machozi mtoto wake .Alimuambia haya ,"Mwanangu hali yangu ni mbaya naendea safari ya wasafiri wote duniani lakini ninakuhusia neno hili ,katika maisha yako usije kuwasahau watu wawili wafuatao" Wakwanza Mwanangu usimsahau mtu yule aliyekaa nawe katika magumu yako. Yule aliyesema wewe ni mwema,wengine waliposema wewe ni mbaya. Yule aliyesonga mbele akabaki nawe,wengine waliporudi nyuma kuachana nawe. Yule uliyemfanyia wema mmoja akautumia huo kupuuza mabaya yako yote. Yule ambaye katika giza nene la dhiki zako,akaleta nuru ya faraja ya ulimi wake. Yule ambaye katika masika ya mateso yako,alifanyiza hema la mwili wake akukinge usinyeshewe. Yule ambaye katika joto kali la kuandamwa na watesi wako alileta baridi kwa tabasamu lake akufariji. Yule ambaye kwenye upweke wako ,uwepo wake ukafanyika upo na kundi kubwa. USIMSAHAU Wapili Mwanangu usimsahau mtu aliyekuacha kipindi cha mateso yako. Aliyetakiwa akusaidie, akakudhihaki. Aliyetakiwa akupe msaada, akageuka mwiba. Aliyetakiwa akushukuru akakulaumu. Aliyesahau wema wako wote na kukumbuka ubaya wako mmoja. Aliyetakiwa akufariji ,akakuletea jeuri. Aliyewaona wengine wanakukimbia,akaungana nao. Aliyeona upweke wako akakuacha,akijihesabu yeye ni wa muhimu na akuoneshe unamhitaji. USIMSAHAU Kwaheri mwanangu!!!
Love
1
· 0 Comments ·0 Shares ·2 Views