ASANTE SANA KWA MAUMIVU

Ningetamani kuwa nawe katika maisha yote, nyakati zote, lakini upepo wa maisha na tamaa zimetuweka mbali.

Nilitamani kuiweka dunia yangu kifuani mwako, lakini huenda dunia ninayoishi mimi ni tofauti na dunia yako.

Dunia ya ufukara ninayoishi mimi dhidi ya dunia yako ya pesa na starehe za gharama.

Nilishindwa mimi na ufukara wangu, nimedondoka, nimekuacha uende.

Nimeamini kuwa, ukiwa huna pesa, kitu pekee unachoweza kumiliki kwa mwanamke mrembo ni picha zake tu na sio moyo wake.

Moyo wa mwanamke ni kama mluzi wa ng'ombe mnadani, kadri miluzi inavyoongezeka ndivyo anavyozidi kupanda bei.

Nasikitika kuyajua haya leo, ni kweli inauma sana, nimekubali.

Nimeelewa nguvu ya ukimya wako, nimeelewa kwanini umeondoka kwangu, bora umeondoka tu, ni ngumu kusubiri ahadi zangu zisizotimia.

Hongera kwa kumpata mtu wa maisha yako, bado natafuta maisha yangu, nimekubali uende kipepeo wangu wa zamani, japo kumbukumbu zetu zinauma.

Kwaheri, Mungu akuongoze huko ulikochagua.

Nashusha karamu yangu chini, ngoja niache kuwaza upuuzi wa mapenzi.
ASANTE SANA KWA MAUMIVU 💔 Ningetamani kuwa nawe katika maisha yote, nyakati zote, lakini upepo wa maisha na tamaa zimetuweka mbali. Nilitamani kuiweka dunia yangu kifuani mwako, lakini huenda dunia ninayoishi mimi ni tofauti na dunia yako. Dunia ya ufukara ninayoishi mimi dhidi ya dunia yako ya pesa na starehe za gharama. Nilishindwa mimi na ufukara wangu, nimedondoka, nimekuacha uende. Nimeamini kuwa, ukiwa huna pesa, kitu pekee unachoweza kumiliki kwa mwanamke mrembo ni picha zake tu na sio moyo wake. Moyo wa mwanamke ni kama mluzi wa ng'ombe mnadani, kadri miluzi inavyoongezeka ndivyo anavyozidi kupanda bei. Nasikitika kuyajua haya leo, ni kweli inauma sana, nimekubali. Nimeelewa nguvu ya ukimya wako, nimeelewa kwanini umeondoka kwangu, bora umeondoka tu, ni ngumu kusubiri ahadi zangu zisizotimia. Hongera kwa kumpata mtu wa maisha yako, bado natafuta maisha yangu, nimekubali uende kipepeo wangu wa zamani, japo kumbukumbu zetu zinauma. Kwaheri, Mungu akuongoze huko ulikochagua. Nashusha karamu yangu chini, ngoja niache kuwaza upuuzi wa mapenzi.
Love
1
· 0 Commentarios ·0 Acciones ·28 Views