Polisi nchini Gambia wamewafungulia mashtaka wanawake watatu kufuatia kifo cha mtoto wa kike mwenye umri wa mwezi mmoja, aliyefanyiwa ukeketaji (FGM), tukio lililoibua hasira kitaifa licha ya marufuku iliyowekwa miaka kumi iliyopita.
Kwa mujibu wa Polisi, mashtaka hayo yamewasilishwa chini ya Sheria ya Marekebisho ya Wanawake ya mwaka 2015, inayopiga marufuku ukeketaji. Mmoja wa wanawake hao anakabiliwa na kifungo cha maisha na amewekwa rumande, huku wengine wawili wakishtakiwa kama washirika na kupewa dhamana.
Mwenyekiti wa Tume ya Kitaifa ya Haki za Binadamu (NHRC), Emmanuel Joof, amesema tukio hilo ni onyo kwa taifa, akisisitiza kuwa ukeketaji si utamaduni tu bali ni kosa la jinai, ukiukaji wa haki za binadamu, na katika visa vingine, husababisha vifo. NHRC inasisitiza kuwa hakuna sababu za kitamaduni au kiasili zinazoweza kuhalalisha madhara kwa watoto. Licha ya marufuku, ukeketaji bado umeenea nchini Gambia, na mwaka jana wabunge walikataa muswada wa kufuta marufuku hiyo

0 Commentarii
·0 Distribuiri
·120 Views