Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina, amesema amejificha “mahali salama” baada ya jaribio la kumuua, kufuatia wiki kadhaa za maandamano yanayomtaka ajiuzulu.

Kupitia matangazo ya moja kwa moja kwenye Facebook, Rajoelina (51) alidai kuwa kundi la wanajeshi na wanasiasa lilipanga kumuua, bila kufichua alipo. Ripoti ambazo hazijathibitishwa zinadai huenda alitoroka nchini kwa ndege ya kijeshi ya Ufaransa.

Maandamano makubwa yanayoongozwa na vijana yamekuwa yakiendelea kote nchini, wakilalamikia hali ngumu ya kiuchumi na utawala wa kiimla. Serikali haijatoa tamko rasmi kuhusu jaribio hilo, huku hali ya taharuki ikiendelea katika mji mkuu, Antananarivo.

Tufuatilie kupitia YouTube ya NIOKOE TV
Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina, amesema amejificha “mahali salama” baada ya jaribio la kumuua, kufuatia wiki kadhaa za maandamano yanayomtaka ajiuzulu. Kupitia matangazo ya moja kwa moja kwenye Facebook, Rajoelina (51) alidai kuwa kundi la wanajeshi na wanasiasa lilipanga kumuua, bila kufichua alipo. Ripoti ambazo hazijathibitishwa zinadai huenda alitoroka nchini kwa ndege ya kijeshi ya Ufaransa. Maandamano makubwa yanayoongozwa na vijana yamekuwa yakiendelea kote nchini, wakilalamikia hali ngumu ya kiuchumi na utawala wa kiimla. Serikali haijatoa tamko rasmi kuhusu jaribio hilo, huku hali ya taharuki ikiendelea katika mji mkuu, Antananarivo. 🔴 Tufuatilie kupitia YouTube ya NIOKOE TV
0 Commentarios ·0 Acciones ·25 Views