• "Simba SC wamepoteza lakini HII WANAVUKA, NO DOUBT. Sioni Al Masry wakileta ubishi kwa Mkapa, dhahiri watatii Sheria iwe kwa shuruti au bila shuruti. Heads up boys, come finish your job. TANZANIA KWANZA" - Jemedari Said, Mchambuzi.

    "Simba SC wamepoteza lakini HII WANAVUKA, NO DOUBT. Sioni Al Masry wakileta ubishi kwa Mkapa, dhahiri watatii Sheria iwe kwa shuruti au bila shuruti. Heads up boys, come finish your job. TANZANIA 🇹🇿 KWANZA" - Jemedari Said, Mchambuzi.
    0 Комментарии ·0 Поделились ·5 Просмотры
  • “Kila siku Robo tu , Kocha naye amechangia Dakika ya kwanza tu toa Ateba weka Mukwala , Halftime toa Ngoma weka Mavambo mwarabu alikuwa anakufa” Mwisho wa kunukuu

    Kuna kibanda umiza nipo hapa nimenukuu maneno ya shabiki Ingawa sijafanikiwa kujua ni shabiki wa timu gani" - Shaffih Dauda, Mchambuzi

    “Kila siku Robo tu , Kocha naye amechangia Dakika ya kwanza tu toa Ateba weka Mukwala , Halftime toa Ngoma weka Mavambo mwarabu alikuwa anakufa” Mwisho wa kunukuu Kuna kibanda umiza nipo hapa nimenukuu maneno ya shabiki Ingawa sijafanikiwa kujua ni shabiki wa timu gani" - Shaffih Dauda, Mchambuzi ✍️
    0 Комментарии ·0 Поделились ·6 Просмотры
  • "Goli mbili ni nyingi kwenye soka la Africa,tena kwa bahati mbaya ni 2-0,hivyo kwenye mechi ya pili Simba wanatakiwa kufunga goli tatu huku wakipambana kutoruhusu goli lolote….huu ni mlima mkubwa sana.

    Kuna mtu atakwambia Simba wamecheza vizuri,walikuwa na on target 7 na total shots 18 ila mwisho wa Siku hakuna goli.

    Narudia tena mechi za mtoano watu hawaangalii umiliki wa mpira bali matokeo ya mwisho,ndio maana ushangai kuona Al ahly anapaki Bus kwenye mechi za ugenini.

    Ni kweli Simba walikuwa na umiliki mkubwa ila nyuma hawakuwa na nidhamu,Al Masry walikuwa tishio kwenye counter na hata goli la pili limetokana na counter.

    Haya ni makosa ya miaka yote ya Simba kutaka umiliki mkubwa kuliko matokeo ya kupita.

    Nilitarajia Simba kupaki bus na kupiga counter ila imekuwa tofauti na goli mbili wamefungwa baada ya kuingia kwenye mtego wa Masry

    Simba wametengeneza mlima mkubwa sana" - Hans Rafael, Mchambuzi.

    "Goli mbili ni nyingi kwenye soka la Africa,tena kwa bahati mbaya ni 2-0,hivyo kwenye mechi ya pili Simba wanatakiwa kufunga goli tatu huku wakipambana kutoruhusu goli lolote….huu ni mlima mkubwa sana. Kuna mtu atakwambia Simba wamecheza vizuri,walikuwa na on target 7 na total shots 18 ila mwisho wa Siku hakuna goli. Narudia tena mechi za mtoano watu hawaangalii umiliki wa mpira bali matokeo ya mwisho,ndio maana ushangai kuona Al ahly anapaki Bus kwenye mechi za ugenini. Ni kweli Simba walikuwa na umiliki mkubwa ila nyuma hawakuwa na nidhamu,Al Masry walikuwa tishio kwenye counter na hata goli la pili limetokana na counter. Haya ni makosa ya miaka yote ya Simba kutaka umiliki mkubwa kuliko matokeo ya kupita. Nilitarajia Simba kupaki bus na kupiga counter ila imekuwa tofauti na goli mbili wamefungwa baada ya kuingia kwenye mtego wa Masry🥲 Simba wametengeneza mlima mkubwa sana" - Hans Rafael, Mchambuzi.
    0 Комментарии ·0 Поделились ·6 Просмотры
  • Mahakama Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imebatilisha hukumu ya kifo waliyopewa Raia watatu (3) wa Marekani kwa makosa ya jinai, ugaidi na kujaribu kuipindua Serikali ya Nchi hiyo.

    Shirika la Habari la Reuters, limeripoti leo Aprili 2,2025, kuwa taarifa ya Ikulu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeeleza watatu hao sasa hawatotumikia adhabu ya kifo badala yake watatumikia kifungo cha maisha jela. Walikuwa miongoni mwa Watu (37) waliohukumiwa kifo Septemba mwaka jana (2024) na Mahakama ya Kijeshi Nchini DR Congo katika mashitaka hayo ambayo hata hivyo waliyakanusha.

    Watatu hao ambao ni Mtoto wa Raia wa Marekani mwenye asili ya DR Congo, Christian Malanga, Marcel Malanga Malu, Rafiki zake Tylor Thomson na Zalman Polun Benjamin, walipewa msamaha kutoka kwa Rais Felix Tshisekedi. Walishtakiwa kwa kuongoza genge la uhalifu lililotekeleza shambulio dhidi ya ikulu na makazi ya Mshirika wa Rais wa Nchi nchi hiyo, Mei, 2024.

    Katika Taarifa iliyosomwa na Msemaji wa Rais Félix Tshisekedi, Tyna Salama kwenye Televisheni ya Taifa, imesema kuwa Rais Tshisekedi ametoa msamaha huo kwa kubatilisha hukumu ya kifo kwa Rais hao na kuwa ya kifungo cha maisha Jela kwa sababu ya kudumisha mahusiano mazuri kimataifa na Nchi ya Marekani.

    Kubatilishwa kwa hukumu hiyo kunakuja kabla ya ziara ya Mshauri mpya Mwandamizi wa Marekani barani Afrika, Massad Boulos. Ambapo ziara hiyo ililenga kwenda DR Congo.
    Mahakama Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩 imebatilisha hukumu ya kifo waliyopewa Raia watatu (3) wa Marekani 🇺🇸 kwa makosa ya jinai, ugaidi na kujaribu kuipindua Serikali ya Nchi hiyo. Shirika la Habari la Reuters, limeripoti leo Aprili 2,2025, kuwa taarifa ya Ikulu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeeleza watatu hao sasa hawatotumikia adhabu ya kifo badala yake watatumikia kifungo cha maisha jela. Walikuwa miongoni mwa Watu (37) waliohukumiwa kifo Septemba mwaka jana (2024) na Mahakama ya Kijeshi Nchini DR Congo katika mashitaka hayo ambayo hata hivyo waliyakanusha. Watatu hao ambao ni Mtoto wa Raia wa Marekani mwenye asili ya DR Congo, Christian Malanga, Marcel Malanga Malu, Rafiki zake Tylor Thomson na Zalman Polun Benjamin, walipewa msamaha kutoka kwa Rais Felix Tshisekedi. Walishtakiwa kwa kuongoza genge la uhalifu lililotekeleza shambulio dhidi ya ikulu na makazi ya Mshirika wa Rais wa Nchi nchi hiyo, Mei, 2024. Katika Taarifa iliyosomwa na Msemaji wa Rais Félix Tshisekedi, Tyna Salama kwenye Televisheni ya Taifa, imesema kuwa Rais Tshisekedi ametoa msamaha huo kwa kubatilisha hukumu ya kifo kwa Rais hao na kuwa ya kifungo cha maisha Jela kwa sababu ya kudumisha mahusiano mazuri kimataifa na Nchi ya Marekani. Kubatilishwa kwa hukumu hiyo kunakuja kabla ya ziara ya Mshauri mpya Mwandamizi wa Marekani barani Afrika, Massad Boulos. Ambapo ziara hiyo ililenga kwenda DR Congo.
    0 Комментарии ·0 Поделились ·32 Просмотры
  • Pamoja na uwezo wa ugomvi wa Mashabiki ambao ulitokea kwenye mchezo wa jana kati ya Mamelodi Sundowns dhidi ya Esperence kwenye mchezo wa klabu bingwa barani Afrika (CAF Champions League) lakini hiki kitendo kimesisimua zaidi Mashabiki wengi.

    Picha hii inaeleza sababu milioni ya upendo ambao unatakiwa pindi Mashabiki wawapo Uwanjani. Mpira wa miguu unatufanya kuwa ndugu hii ndio maana unaitwa Football kwa kiingereza.

    Pamoja na uwezo wa ugomvi wa Mashabiki ambao ulitokea kwenye mchezo wa jana kati ya Mamelodi Sundowns 🇿🇦dhidi ya Esperence 🇹🇳 kwenye mchezo wa klabu bingwa barani Afrika (CAF Champions League) lakini hiki kitendo kimesisimua zaidi Mashabiki wengi. Picha hii inaeleza sababu milioni ya upendo ambao unatakiwa pindi Mashabiki wawapo Uwanjani. Mpira wa miguu unatufanya kuwa ndugu hii ndio maana unaitwa Football kwa kiingereza.
    0 Комментарии ·0 Поделились ·37 Просмотры
  • Uongozi wa Ligi Kuu ya mpira wa miguu Nchini Marekani , Major League Soccer (MLS), umempiga marufuku Mlinzi binafsi (Bodyguard) wa Lionel Messi, Yassine Cheuko, kuwa kando na kuingia katikati ya Uwanja wakati wa mechi za Inter Miami kwa lengo lake la kumlinda Mwajiri wake Messi.

    Ikumbukwe kwamba Yassine Cheuko, ni Mwanajeshi wa zamani wa kikosi maalumu cha operesheni za kijeshi cha Jeshi la Majini la Marekani (U.S. Navy) kinachobobea katika vita visivyo vya kawaida, kupambana na ugaidi, mashambulizi ya moja kwa moja, na upelelezi wa kijeshi. Tangu Yessine Cheuko aanze kufanya kazi na Messi amejizolea umaarufu mkubwa Duniani kwani ameonekana mara nyingi akiwadhibiti Wavamizi mbalimbali ambao wengi lengo lao huwa sio baya, zaidi wanataka kupiga picha na Messi.

    Tayari uongozi wa Ligi hiyo umemzuia kuingia Uwanjani, sasa ataruhusiwa tu kuwa kwenye Vyumba vya kubadilishia nguo na maeneo ya Waandishi wa habari siku za mechi. Uamuzi huu ni sehemu ya mpango wa (MLS) wa kuchukua mamlaka kamili ya usalama wa mechi.

    Baada ya katazo, Yassine Cheuko ameonyesha kutoridhishwa na hatua hiyo, akisema kuwa Wavamizi wa Uwanja ni tatizo kubwa zaidi Nchini Marekani kuliko Ulaya. Kwa mujibu wake, katika miaka saba aliyofanya kazi Ulaya, kulikuwa na matukio sita pekee ya uvamizi Uwanjani, ilhali katika miezi 20 Nchini Marekani, tayari yameshuhudiwa matukio 16.

    Mlinzi huyo ameendelea kusema kuwa Uongozi wa Ligi Kuu ya Marekani haukutakiwa kumzuia kufanye kazi yake bali walitakiwa kumpa ushirikiano ili kazi hiyo waifanye kwa pamoja kwa sababu eti kipindi yupo barani Ulaya, alipata ushirikiano wa kutosha kutoka kwenye Uongozi na alifanya kazi yake kwa uhuru. Pamoja na kuzuiliwa kuingia Uwanjani au kukaa kando ya Uwanja, Cheuko amesema kuwa ataendelea kufanya kazi yake kama kawaida bila kuvunja sheria au utaratibu uliopo kwenye mchezo wa mpira wa miguu.

    Uongozi wa Ligi Kuu ya mpira wa miguu Nchini Marekani 🇺🇸, Major League Soccer (MLS), umempiga marufuku Mlinzi binafsi (Bodyguard) wa Lionel Messi, Yassine Cheuko, kuwa kando na kuingia katikati ya Uwanja wakati wa mechi za Inter Miami kwa lengo lake la kumlinda Mwajiri wake Messi. Ikumbukwe kwamba Yassine Cheuko, ni Mwanajeshi wa zamani wa kikosi maalumu cha operesheni za kijeshi cha Jeshi la Majini la Marekani (U.S. Navy) kinachobobea katika vita visivyo vya kawaida, kupambana na ugaidi, mashambulizi ya moja kwa moja, na upelelezi wa kijeshi. Tangu Yessine Cheuko aanze kufanya kazi na Messi amejizolea umaarufu mkubwa Duniani kwani ameonekana mara nyingi akiwadhibiti Wavamizi mbalimbali ambao wengi lengo lao huwa sio baya, zaidi wanataka kupiga picha na Messi. Tayari uongozi wa Ligi hiyo umemzuia kuingia Uwanjani, sasa ataruhusiwa tu kuwa kwenye Vyumba vya kubadilishia nguo na maeneo ya Waandishi wa habari siku za mechi. Uamuzi huu ni sehemu ya mpango wa (MLS) wa kuchukua mamlaka kamili ya usalama wa mechi. Baada ya katazo, Yassine Cheuko ameonyesha kutoridhishwa na hatua hiyo, akisema kuwa Wavamizi wa Uwanja ni tatizo kubwa zaidi Nchini Marekani kuliko Ulaya. Kwa mujibu wake, katika miaka saba aliyofanya kazi Ulaya, kulikuwa na matukio sita pekee ya uvamizi Uwanjani, ilhali katika miezi 20 Nchini Marekani, tayari yameshuhudiwa matukio 16. Mlinzi huyo ameendelea kusema kuwa Uongozi wa Ligi Kuu ya Marekani haukutakiwa kumzuia kufanye kazi yake bali walitakiwa kumpa ushirikiano ili kazi hiyo waifanye kwa pamoja kwa sababu eti kipindi yupo barani Ulaya, alipata ushirikiano wa kutosha kutoka kwenye Uongozi na alifanya kazi yake kwa uhuru. Pamoja na kuzuiliwa kuingia Uwanjani au kukaa kando ya Uwanja, Cheuko amesema kuwa ataendelea kufanya kazi yake kama kawaida bila kuvunja sheria au utaratibu uliopo kwenye mchezo wa mpira wa miguu.
    0 Комментарии ·0 Поделились ·55 Просмотры
  • Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imepanga kufanya mazungumzo na Kundi la Waasi wa M23, April 9 mwaka huu, Nchini Qatar , yenye nia ya kutafuta amani katika eneo la Mashariki mwa Nchi hiyo. Kikao hicho kitakachofanyika Jijini Doha n kitakuwa kikao cha kwanza kwa pande zote mbili kukaa na kuzungumza baada ya kuthibitisha kuwa watashiriki.

    Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩 imepanga kufanya mazungumzo na Kundi la Waasi wa M23, April 9 mwaka huu, Nchini Qatar 🇶🇦, yenye nia ya kutafuta amani katika eneo la Mashariki mwa Nchi hiyo. Kikao hicho kitakachofanyika Jijini Doha n kitakuwa kikao cha kwanza kwa pande zote mbili kukaa na kuzungumza baada ya kuthibitisha kuwa watashiriki.
    0 Комментарии ·0 Поделились ·39 Просмотры
  • Aliyetiwa hatiani kuwa Mhalifu wa kivita na Mahakama ya kimataifa ya (ICC) kwa makosa mbalimbali, Thomas Lubanga, ametangaza kuunda kundi jipya la Waasi lenye lengo la kuiangusha Serikali ya Jimbo la Ituri, lililopo Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo .

    Nchi ya DR Congo imekuwa ikikabiliwa na tishio la kiusalama katika Mikoa ya mashariki ambapo makundi ya Waasi ikiwemo Muungano wa Waasi wa AFC/M23 unaoshikilia Miji ya Goma, Bukavu, Nyabibwe na Walikale.

    Hata hivyo, uamuzi wa Thomas Lubanga ambaye ni Mzaliwa wa Mkoa wa Ituri Nchini DR Congo na anayeishi Nchini Uganda , kutangaza kuanzisha Kundi lake la Waasi alilolipa jina Convention for the Popular Revolution (CPR) ambalo litaongeza hofu ya machafuko Nchini humo wakati huu ambao Serikali ya Rais Felix Tshisekedi inatafuta maridhiano na M23 kwa njia ya mazungumzo.

    Shirika la Habari la Reuters, limeripoti leo Jumanne Aprili Mosi, 2025, kuwa Lubanga ambaye ni Mzaliwa wa Ituri, alihukumiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) mwaka 2012 kwa makosa ya kuwasajili Watoto kama Askari na akapewa kifungo cha miaka 14 Gerezani, baadaye aliachiliwa mwaka 2020 na Rais wa DR Congo, Felix Tshisekedi kisha akamteua kuwa sehemu ya kikosi kazi cha kuleta amani Jimboni Ituri.

    Hata hivyo, mwaka 2022 alitekwa nyara kwa miezi miwili na kundi la Waasi, tukio analodai kupangwa na Serikali ya DR Congo kwa lengo kumpoteza ila kwa sasa anaishi Nchini Uganda.

    Aliyetiwa hatiani kuwa Mhalifu wa kivita na Mahakama ya kimataifa ya (ICC) kwa makosa mbalimbali, Thomas Lubanga, ametangaza kuunda kundi jipya la Waasi lenye lengo la kuiangusha Serikali ya Jimbo la Ituri, lililopo Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩. Nchi ya DR Congo imekuwa ikikabiliwa na tishio la kiusalama katika Mikoa ya mashariki ambapo makundi ya Waasi ikiwemo Muungano wa Waasi wa AFC/M23 unaoshikilia Miji ya Goma, Bukavu, Nyabibwe na Walikale. Hata hivyo, uamuzi wa Thomas Lubanga ambaye ni Mzaliwa wa Mkoa wa Ituri Nchini DR Congo na anayeishi Nchini Uganda 🇺🇬, kutangaza kuanzisha Kundi lake la Waasi alilolipa jina Convention for the Popular Revolution (CPR) ambalo litaongeza hofu ya machafuko Nchini humo wakati huu ambao Serikali ya Rais Felix Tshisekedi inatafuta maridhiano na M23 kwa njia ya mazungumzo. Shirika la Habari la Reuters, limeripoti leo Jumanne Aprili Mosi, 2025, kuwa Lubanga ambaye ni Mzaliwa wa Ituri, alihukumiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) mwaka 2012 kwa makosa ya kuwasajili Watoto kama Askari na akapewa kifungo cha miaka 14 Gerezani, baadaye aliachiliwa mwaka 2020 na Rais wa DR Congo, Felix Tshisekedi kisha akamteua kuwa sehemu ya kikosi kazi cha kuleta amani Jimboni Ituri. Hata hivyo, mwaka 2022 alitekwa nyara kwa miezi miwili na kundi la Waasi, tukio analodai kupangwa na Serikali ya DR Congo kwa lengo kumpoteza ila kwa sasa anaishi Nchini Uganda.
    0 Комментарии ·0 Поделились ·86 Просмотры
  • Mke wa Mchezaji wa kimataifa wa Burkina Faso n'a klabu ya Yanga SC, Hamisa Mobetto (Tanzania ) ameingia kwenye orodha ya WAGS (Wives And Girlfriends of Footballers) ambao ni Wake (Wapenzi au Wachumba) wa Wachezaji wenye Wafuasi (followers) wengi zaidi kwenye mtandao wa Instagram Duniani.

    1. @georginagio (Mrs. Ronaldo) :+65.5M
    2. antonelaroccuzzo (Mrs. Messi) : +39.9M
    3. @iambeckyg (Mrs. Sebastian) : +37.2M
    4. @victoriabeckham (Mrs. Beckham) : +32.9M
    5. @perrieedwards (Mrs. Alex) :+19M

    6. @alishalehmann7 (Mrs. Douglas Luiz) : +16.6M
    7. @brunabiancardi (Mrs. Neymar Jr) : +13.6M
    8. @hamisamobetto (Mrs. Aziz Ki) : +12.1M
    9. @pilarrubio (Mrs. Sergio Ramos) : +11.1M
    10. @leighannepinnock (Mrs. Andre Gray) : +10M

    Mke wa Mchezaji wa kimataifa wa Burkina Faso 🇧🇫 n'a klabu ya Yanga SC, Hamisa Mobetto (Tanzania 🇹🇿) ameingia kwenye orodha ya WAGS (Wives And Girlfriends of Footballers) ambao ni Wake (Wapenzi au Wachumba) wa Wachezaji wenye Wafuasi (followers) wengi zaidi kwenye mtandao wa Instagram Duniani. 1. @georginagio (Mrs. Ronaldo) :+65.5M 2. antonelaroccuzzo (Mrs. Messi) : +39.9M 3. @iambeckyg (Mrs. Sebastian) : +37.2M 4. @victoriabeckham (Mrs. Beckham) : +32.9M 5. @perrieedwards (Mrs. Alex) :+19M 6. @alishalehmann7 (Mrs. Douglas Luiz) : +16.6M 7. @brunabiancardi (Mrs. Neymar Jr) : +13.6M 8. @hamisamobetto (Mrs. Aziz Ki) : +12.1M 9. @pilarrubio (Mrs. Sergio Ramos) : +11.1M 10. @leighannepinnock (Mrs. Andre Gray) : +10M
    0 Комментарии ·0 Поделились ·179 Просмотры
  • Rais wa Nchi ya Burkina Faso , Kapteni Ibrahim Traoré ametoa msamaha kwa Wanajeshi (21) waliojaribu kufanya mapinduzi ya Serikali ya Septemba mwaka 2015. Katika amri iliyosainiwa Machi 24 na kuwekwa hadharani Jumapili hii, Kapteni Traore aliweka masharti ya msamaha huu, ambao ulipigiwa kura na Bunge la Nchi hiy Desemba iliyopita.

    Wanajeshi hao (21), wakiwemo Maafisa, Maafisa wasio na kamisheni na Vyeo vingine, walifikishwa mahakamani na kutiwa hatiani kwa matendo yaliyofanywa Septemba 15 na 16, 2015, inasema amri iliyotiwa saini na Rais wa Nchi hiyo Kapteni Ibrahim Traore. Amri hii iliyopitishwa na Bunge mwishoni mwa Desemba 2024 ya msamaha na masharti ya kutoa msamaha kwa Watu waliopatikana na hatia kuhusiana na mapinduzi yaliyofeli ya 2015.

    Sheria hii pia imeweka wazi kwamba Askari waliotiwa hatiani au kufunguliwa mashtaka kuhusiana na kesi hii, wakionyesha kujitolea katika mapambano dhidi ya ugaidi Nchini humo, wanaweza kupata fursa ya neema ya msamaha ili kupandishwa cheo kazini.

    Rais wa Nchi ya Burkina Faso 🇧🇫, Kapteni Ibrahim Traoré ametoa msamaha kwa Wanajeshi (21) waliojaribu kufanya mapinduzi ya Serikali ya Septemba mwaka 2015. Katika amri iliyosainiwa Machi 24 na kuwekwa hadharani Jumapili hii, Kapteni Traore aliweka masharti ya msamaha huu, ambao ulipigiwa kura na Bunge la Nchi hiy Desemba iliyopita. Wanajeshi hao (21), wakiwemo Maafisa, Maafisa wasio na kamisheni na Vyeo vingine, walifikishwa mahakamani na kutiwa hatiani kwa matendo yaliyofanywa Septemba 15 na 16, 2015, inasema amri iliyotiwa saini na Rais wa Nchi hiyo Kapteni Ibrahim Traore. Amri hii iliyopitishwa na Bunge mwishoni mwa Desemba 2024 ya msamaha na masharti ya kutoa msamaha kwa Watu waliopatikana na hatia kuhusiana na mapinduzi yaliyofeli ya 2015. Sheria hii pia imeweka wazi kwamba Askari waliotiwa hatiani au kufunguliwa mashtaka kuhusiana na kesi hii, wakionyesha kujitolea katika mapambano dhidi ya ugaidi Nchini humo, wanaweza kupata fursa ya neema ya msamaha ili kupandishwa cheo kazini.
    0 Комментарии ·0 Поделились ·100 Просмотры
  • Rais wa Marekani , DonaldTrump, ameibua mjadala mkali baada ya kusema kuwa kuna uwezekano wa yeye kuwania muhula wa tatu, licha ya Katiba ya Marekani kupiga marufuku jambo hilo kupitia Marekebisho ya 22. Katika mahojiano na NBCNews, Rais huyo hakutaka kufuta uwezekano wa kuwania tena Urais baada ya kumaliza mihula miwili, akidai kuwa kuna njia za kufanya hilo kutokea. Alisisitiza kuwa "hakuwa anatania," jambo ambalo limeibua hofu miongoni mwa Wachambuzi wa siasa na Wanaharakati wa demokrasia Nchini humo.

    Kwa mujibu wa Katiba ya Marekani, Rais haruhusiwi kutawala kwa zaidi ya mihula miwili ya miaka minne minne. Marekebisho ya 22 yaliwekwa ili kuzuia Mtu mmoja kuwa na mamlaka ya muda mrefu kama ilivyokuwa kwa Franklin D. Roosevelt, ambaye altawala kwa zaidi ya mihula miwili kabla ya marekebisho hayo kuidhinishwa mwaka 1951.

    Kauli ya Trump imeibua maswali kuhusu mbinu anazoweza kutumia kutafuta muhula wa tatu. Wachambuzi wa sheria wanabainisha kuwa ili hilo litokee, ama katiba ibadilishwe rasmi kwa marekebisho mapya, au ipatikane tafsiri mpya ya kisheria inayomruhusu kugombea tena. Hata hivyo, mchakato wa kubadili katiba ni mgumu na unahitaji ridhaa ya Bunge pamoja na Majimbo mengi ya Marekani.

    Baadhi ya Wafuasi wa Donald Trump wameunga mkono kauli yake, wakidai kuwa anastahili muda zaidi wa kuongoza Nchi. Hata hivyo, Wakosoaji wake wanasema kuwa hatua yoyote ya kupindua Marekebisho ya 22 inaweza kuwa tishio kwa demokrasia ya Marekani na kuweka msingi wa uongozi wa kiimla.

    Rais wa Marekani 🇺🇸, DonaldTrump, ameibua mjadala mkali baada ya kusema kuwa kuna uwezekano wa yeye kuwania muhula wa tatu, licha ya Katiba ya Marekani kupiga marufuku jambo hilo kupitia Marekebisho ya 22. Katika mahojiano na NBCNews, Rais huyo hakutaka kufuta uwezekano wa kuwania tena Urais baada ya kumaliza mihula miwili, akidai kuwa kuna njia za kufanya hilo kutokea. Alisisitiza kuwa "hakuwa anatania," jambo ambalo limeibua hofu miongoni mwa Wachambuzi wa siasa na Wanaharakati wa demokrasia Nchini humo. Kwa mujibu wa Katiba ya Marekani, Rais haruhusiwi kutawala kwa zaidi ya mihula miwili ya miaka minne minne. Marekebisho ya 22 yaliwekwa ili kuzuia Mtu mmoja kuwa na mamlaka ya muda mrefu kama ilivyokuwa kwa Franklin D. Roosevelt, ambaye altawala kwa zaidi ya mihula miwili kabla ya marekebisho hayo kuidhinishwa mwaka 1951. Kauli ya Trump imeibua maswali kuhusu mbinu anazoweza kutumia kutafuta muhula wa tatu. Wachambuzi wa sheria wanabainisha kuwa ili hilo litokee, ama katiba ibadilishwe rasmi kwa marekebisho mapya, au ipatikane tafsiri mpya ya kisheria inayomruhusu kugombea tena. Hata hivyo, mchakato wa kubadili katiba ni mgumu na unahitaji ridhaa ya Bunge pamoja na Majimbo mengi ya Marekani. Baadhi ya Wafuasi wa Donald Trump wameunga mkono kauli yake, wakidai kuwa anastahili muda zaidi wa kuongoza Nchi. Hata hivyo, Wakosoaji wake wanasema kuwa hatua yoyote ya kupindua Marekebisho ya 22 inaweza kuwa tishio kwa demokrasia ya Marekani na kuweka msingi wa uongozi wa kiimla.
    0 Комментарии ·0 Поделились ·131 Просмотры
  • Raia wa Marekani wanazidi kuelekeza pesa zao kwenye kamari ya michezo (Betting) badala ya kufanya uwekezaji wa muda mrefu, jambo linalozua wasiwasi kuhusu hali ya kifedha Nchini humo. Utafiti wa hivi karibuni unaonyesha kuwa katika majimbo ambako kamari ya michezo imehalalishwa, kumekuwa na kupungua kwa akiba na uwekezaji katika mali thabiti kama vile hisa.

    Mwelekeo huu umeambatana na ongezeko la madeni ya kadi za mkopo, alama za chini za mkopo, na kuongezeka kwa kufilisika. Ingawa majimbo yamefaidika na mapato makubwa ya kodi kutoka kwa upanuzi huu wa kamari, athari zake pana za kiuchumi zinaonyesha mwenendo wa kusikitisha.

    Raia wa Marekani 🇺🇸 wanazidi kuelekeza pesa zao kwenye kamari ya michezo (Betting) badala ya kufanya uwekezaji wa muda mrefu, jambo linalozua wasiwasi kuhusu hali ya kifedha Nchini humo. Utafiti wa hivi karibuni unaonyesha kuwa katika majimbo ambako kamari ya michezo imehalalishwa, kumekuwa na kupungua kwa akiba na uwekezaji katika mali thabiti kama vile hisa. Mwelekeo huu umeambatana na ongezeko la madeni ya kadi za mkopo, alama za chini za mkopo, na kuongezeka kwa kufilisika. Ingawa majimbo yamefaidika na mapato makubwa ya kodi kutoka kwa upanuzi huu wa kamari, athari zake pana za kiuchumi zinaonyesha mwenendo wa kusikitisha.
    0 Комментарии ·0 Поделились ·102 Просмотры
  • "Marekani mpaka sasa hawajasaini mkataba wa kuilinda Congo mchakato umekuwa mrefu. Jiulize vile vikwazo vya Magharibi walivyoiwekea Rwanda vimeishia wapi

    Kagame anajua anachokifanya ndio maana licha ya ripoti za UN , US na EU kuonyesha Rwanda wanaifadhili M23 plus Vikwazo hakuna kilichobadilika Congo

    Wanachokifanya wanaoibia Congo na Africa ni ile ile mbinu ya wakati wa ukoloni inaitwa "Divided and Rule " yaani wagawanywe uwatawale nakumbuka hii mbinu pia enzi hizo ndio iliyozaa utani wa jadi wa Yanga na Simba

    Oooh Africa " - Zungu, Mchambuzi wa Siasa na Mtangazaji.

    "Marekani mpaka sasa hawajasaini mkataba wa kuilinda Congo mchakato umekuwa mrefu. Jiulize vile vikwazo vya Magharibi walivyoiwekea Rwanda vimeishia wapi 😀😀😀😀 Kagame anajua anachokifanya ndio maana licha ya ripoti za UN , US na EU kuonyesha Rwanda wanaifadhili M23 plus Vikwazo hakuna kilichobadilika Congo 😭😭😭😭 Wanachokifanya wanaoibia Congo na Africa ni ile ile mbinu ya wakati wa ukoloni inaitwa "Divided and Rule " yaani wagawanywe uwatawale nakumbuka hii mbinu pia enzi hizo ndio iliyozaa utani wa jadi wa Yanga na Simba Oooh Africa🌍 😭" - Zungu, Mchambuzi wa Siasa na Mtangazaji.
    0 Комментарии ·0 Поделились ·118 Просмотры
  • https://ormatz.com/pages/login/index?invite=u81s2uxl
    Tengeneza pesa bila kiingilio chochote. Jaribu kujisajili utanishukuru badae
    https://ormatz.com/pages/login/index?invite=u81s2uxl Tengeneza pesa bila kiingilio chochote. Jaribu kujisajili utanishukuru badae
    0 Комментарии ·0 Поделились ·57 Просмотры
  • Jarida la Forbes toleo la mwaka huu wa 2025 limemtaja Manyabiashara wa Tanzania Mohamed Dewjl, kuwa miongoni mwa Watu Matajiri Duniani, akiwa na utajiri wa USD 2.2 bilioni sawa na Shilingi Trilioni 5.7 za Kitanzania. Mo Dewji, anakuwa tajiri namba 12 barani Afrika na namba moja Afrika Mashariki kwa kiwango hicho.

    2. Orodha ya mwaka huu inaonyesha utajiri wa Mo
    Dewji umeongezeka na kufikia, dola bilioni 2.2 kutoka dola bilioni 1.8 mwaka jana.

    3. Orodha ya Forbes ya Matajiri wa Afrika kwa mwaka 2024 ilibainisha kuwa utajiri wa Mo Dewji umeongezeka kutoka dola bilioni 1.5 hadi bilioni 1.8.

    4. Licha ya utajiri huo, MO Dewji kupitia kampuni ya Mohamed Entrprises Limited (MeTL) imezalisha ajira 40,000 kwa Watanzania, kupitia biashara 126 zinazofanywa na kampuni hiyo.

    5. Lengo la Mo Dewji ni kuongeza ajira hadi kufikia laki moja kwa Watanzania na wana-Afrika Mashariki.

    6. Mo Dewji kupitia MoDewjl Foundation, imeshirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Maji, kuchimba visima, kukarabati na kutibu maji mkakati uliosaidia Watu zaidi ya 15,000 kupata maji salama ya kunywa.

    7. Utajiri wa Mo Dewji haikushia kwenye maji na afya pekee, umekwenda zaidi na kuwekeza katika tasnia ya michezo ambako ni sehemu ya Mmiliki akiwekeza
    asilimia 49 kwenye klabu ya Simba SC.

    Jarida la Forbes toleo la mwaka huu wa 2025 limemtaja Manyabiashara wa Tanzania Mohamed Dewjl, kuwa miongoni mwa Watu Matajiri Duniani, akiwa na utajiri wa USD 2.2 bilioni sawa na Shilingi Trilioni 5.7 za Kitanzania. Mo Dewji, anakuwa tajiri namba 12 barani Afrika na namba moja Afrika Mashariki kwa kiwango hicho. 2. Orodha ya mwaka huu inaonyesha utajiri wa Mo Dewji umeongezeka na kufikia, dola bilioni 2.2 kutoka dola bilioni 1.8 mwaka jana. 3. Orodha ya Forbes ya Matajiri wa Afrika kwa mwaka 2024 ilibainisha kuwa utajiri wa Mo Dewji umeongezeka kutoka dola bilioni 1.5 hadi bilioni 1.8. 4. Licha ya utajiri huo, MO Dewji kupitia kampuni ya Mohamed Entrprises Limited (MeTL) imezalisha ajira 40,000 kwa Watanzania, kupitia biashara 126 zinazofanywa na kampuni hiyo. 5. Lengo la Mo Dewji ni kuongeza ajira hadi kufikia laki moja kwa Watanzania na wana-Afrika Mashariki. 6. Mo Dewji kupitia MoDewjl Foundation, imeshirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Maji, kuchimba visima, kukarabati na kutibu maji mkakati uliosaidia Watu zaidi ya 15,000 kupata maji salama ya kunywa. 7. Utajiri wa Mo Dewji haikushia kwenye maji na afya pekee, umekwenda zaidi na kuwekeza katika tasnia ya michezo ambako ni sehemu ya Mmiliki akiwekeza asilimia 49 kwenye klabu ya Simba SC.
    0 Комментарии ·0 Поделились ·142 Просмотры
  • Najua umesalitiwa na wale uliowaamini, umeachwa ulipohitaji kupendwa, na umedhihakiwa wakati ulichotaka ni kuungwa mkono. Najua umechoka. Najua umepigana vita hakuna mtu aliyeona, kulia kimya, na kuvumilia maumivu ambayo maneno hayawezi kuelezea.

    Maisha hayajakuwa sawa kwako. Milango imegongwa usoni mwako. Umewatazama wengine wakiinuka huku wewe ukiwa umekwama katika sehemu moja. Umeomba, kutumaini, na kungoja, lakini hakuna kinachoonekana kubadilika. Inaumiza. Ni chungu. Inachosha.

    Lakini nisikilizeni, na nisikilize kwa makini: USIKATE TAMAA.

    Kila mtu mkubwa unayekuvutia leo alikuwa hapo ulipo sasa. Walihisi kile unachohisi. Walihangaika, walilia, na walitilia shaka wenyewe. Lakini hawakuacha. Hawakuruhusu maumivu yao yawafafanue. Waliendelea kusonga mbele, hata pale nguvu zao zilipopungua. Na ndio maana leo, ulimwengu unawaadhimisha.

    Lazima uelewe ukweli huu: Kadiri hatima yako inavyokuwa kubwa, ndivyo vita yako inavyokuwa kubwa. KILA KIWANGO KIPYA UNACHOFIKIA, KUNA SHETANI MPYA ANAKUSUBIRI. Ulipokuwa maskini, hakuna aliyekuonea wivu. Lakini unapoanza kufanya maendeleo, ghafla, watu wanaanza kukuchukia. Ulipokuwa huna kazi, hakuna aliyezungumza juu yako. Lakini mara tu unapopata kazi nzuri, wanaanza kueneza uvumi. Ulipokuwa ukihangaika, hakuna aliyejali. Lakini wakati unapoanza kufanikiwa, maadui huonekana kutoka popote.

    Ibilisi hapigani na watu ambao hawaendi popote. Sababu ya wewe kukabiliwa na vita vingi ni kwa sababu hatima yako ni kubwa; sababu ya maisha kukujaribu sana ni kwa sababu kesho yako ni kubwa. Huna mateso kwa sababu wewe ni dhaifu. Unateseka kwa sababu wewe ni IMARA, na maisha yanajua kwamba mara tu unapopitia, hautazuilika.

    Kwa hivyo, usikatishwe tamaa na vita unavyokabili sasa. Wao ni ishara kwamba unasonga mbele. Usiruhusu maumivu yakufanye uchungu. Usiruhusu tamaa kuua ndoto zako. Endelea kupigana. Endelea kusukuma. Endelea kuamini. Wakati wako utafika.

    Kuna toleo lako katika siku zijazo ambalo lina nguvu zaidi, busara, na mafanikio zaidi kuliko wewe sasa. Toleo hilo lako linasubiri. Lakini ili kuwa mtu huyo, lazima upitie moto huu. Sio rahisi, lakini nakuahidi, itafaa.

    Lia ikiwa ni lazima, lakini baada ya kulia, futa machozi yako na uendelee kusonga. Lalamika ikibidi, lakini baada ya kulalamika, simama na upigane tena. Jisikie dhaifu ikiwa ni lazima, lakini usiache kujaribu.

    Wakati wako unakuja. Ufanisi wako umekaribia. Maumivu hayatadumu milele. Siku moja, utaangalia nyuma na kugundua kuwa kila kitu ulichopitia kilikufanya kuwa mtu mwenye nguvu, aliyefanikiwa ambaye unakusudiwa kuwa.

    Kwa hivyo, endelea kusonga mbele. Ushindi wako uko njiani.

    Quadic Bangura
    Najua umesalitiwa na wale uliowaamini, umeachwa ulipohitaji kupendwa, na umedhihakiwa wakati ulichotaka ni kuungwa mkono. Najua umechoka. Najua umepigana vita hakuna mtu aliyeona, kulia kimya, na kuvumilia maumivu ambayo maneno hayawezi kuelezea. Maisha hayajakuwa sawa kwako. Milango imegongwa usoni mwako. Umewatazama wengine wakiinuka huku wewe ukiwa umekwama katika sehemu moja. Umeomba, kutumaini, na kungoja, lakini hakuna kinachoonekana kubadilika. Inaumiza. Ni chungu. Inachosha. Lakini nisikilizeni, na nisikilize kwa makini: USIKATE TAMAA. Kila mtu mkubwa unayekuvutia leo alikuwa hapo ulipo sasa. Walihisi kile unachohisi. Walihangaika, walilia, na walitilia shaka wenyewe. Lakini hawakuacha. Hawakuruhusu maumivu yao yawafafanue. Waliendelea kusonga mbele, hata pale nguvu zao zilipopungua. Na ndio maana leo, ulimwengu unawaadhimisha. Lazima uelewe ukweli huu: Kadiri hatima yako inavyokuwa kubwa, ndivyo vita yako inavyokuwa kubwa. KILA KIWANGO KIPYA UNACHOFIKIA, KUNA SHETANI MPYA ANAKUSUBIRI. Ulipokuwa maskini, hakuna aliyekuonea wivu. Lakini unapoanza kufanya maendeleo, ghafla, watu wanaanza kukuchukia. Ulipokuwa huna kazi, hakuna aliyezungumza juu yako. Lakini mara tu unapopata kazi nzuri, wanaanza kueneza uvumi. Ulipokuwa ukihangaika, hakuna aliyejali. Lakini wakati unapoanza kufanikiwa, maadui huonekana kutoka popote. Ibilisi hapigani na watu ambao hawaendi popote. Sababu ya wewe kukabiliwa na vita vingi ni kwa sababu hatima yako ni kubwa; sababu ya maisha kukujaribu sana ni kwa sababu kesho yako ni kubwa. Huna mateso kwa sababu wewe ni dhaifu. Unateseka kwa sababu wewe ni IMARA, na maisha yanajua kwamba mara tu unapopitia, hautazuilika. Kwa hivyo, usikatishwe tamaa na vita unavyokabili sasa. Wao ni ishara kwamba unasonga mbele. Usiruhusu maumivu yakufanye uchungu. Usiruhusu tamaa kuua ndoto zako. Endelea kupigana. Endelea kusukuma. Endelea kuamini. Wakati wako utafika. Kuna toleo lako katika siku zijazo ambalo lina nguvu zaidi, busara, na mafanikio zaidi kuliko wewe sasa. Toleo hilo lako linasubiri. Lakini ili kuwa mtu huyo, lazima upitie moto huu. Sio rahisi, lakini nakuahidi, itafaa. Lia ikiwa ni lazima, lakini baada ya kulia, futa machozi yako na uendelee kusonga. Lalamika ikibidi, lakini baada ya kulalamika, simama na upigane tena. Jisikie dhaifu ikiwa ni lazima, lakini usiache kujaribu. Wakati wako unakuja. Ufanisi wako umekaribia. Maumivu hayatadumu milele. Siku moja, utaangalia nyuma na kugundua kuwa kila kitu ulichopitia kilikufanya kuwa mtu mwenye nguvu, aliyefanikiwa ambaye unakusudiwa kuwa. Kwa hivyo, endelea kusonga mbele. Ushindi wako uko njiani. Quadic Bangura
    Love
    1
    · 0 Комментарии ·0 Поделились ·178 Просмотры
  • JE, UNAMLETEA UHAI MPENZI WAKO, AU UNALETA KISU?

    Upendo unakusudiwa kujenga, sio kuvunja. Uhusiano unakusudiwa kuwa patakatifu, sio kichinjio. Nafsi mbili zinapokutana, zinapaswa kuleta uhai kwa kila mmoja, sio majeraha, sio makovu, sio huzuni. Hata hivyo, ukweli wa kusikitisha ni kwamba watu wengi huingia kwenye mahusiano wakitarajia kupendwa lakini hupokea maumivu. Wanatazamia furaha lakini wanakutana na taabu. Badala ya mwenzi anayeleta uzima, wanajikuta wanaishi na mtu ambaye ana kisu, akipunguza ujasiri wao, amani na heshima. Kwa hiyo, unaleta uhai kwa mpenzi wako, au unaleta kisu? Upendo unakusudiwa kumpa uhai yule unayedai kumpenda. Katika Mwanzo Mungu alimpulizia Adamu pumzi ya uhai, naye akawa nafsi hai. Kwa njia hiyo hiyo, uhusiano unapaswa kupumua maisha ndani ya mtu, sio kukimbia maisha kutoka kwao. Unapomhimiza mwenzako kufuata ndoto zake, unaleta uzima. Unapozungumza maneno ya fadhili, heshima, na uthibitisho, unaleta uzima. Unapovumilia mapungufu yao na kutembea nao katika mapambano yao, unaleta uhai. Wakati uwepo wako ni chanzo cha amani na si chanzo cha msongo wa mawazo, unaleta uhai. Upendo haupaswi kamwe kuhisi kama kutembea kwenye uwanja wa vita, ambapo kila neno, kila kitendo na kila siku huhisi kama kupigania kuishi. Mpenzi wako hapaswi kujisikia salama nje kuliko ndani ya uhusiano. Ikiwa unampenda mtu, anapaswa kustawi chini ya upendo wako, sio kukauka.

    Kisu sio lazima kiwe cha mwili kila wakati. Vidonda vingine huenda zaidi kuliko mwili; wanachoma roho. Baadhi yetu, badala ya kuleta uhai, kuleta kisu. Tunaleta kisu cha maneno makali, kukata ndani ya kujithamini kwa mpenzi wetu. Tunaleta kisu cha kulinganisha, na kuwafanya wahisi kama hawatoshi vya kutosha. Tunakuja na kisu cha kupuuza, na njaa ya upendo na tahadhari wanayotamani. Kwa namna fulani, pia kuja na kisu cha usaliti, ambapo uaminifu wetu ni kwa maneno tu lakini si kwa vitendo. Watu wengine wanakufa kihisia na kiroho kwa sababu ya mtu wanayempenda. Furaha yao inafifia taratibu. Kujiamini kwao kunatoweka. Kicheko chao hakitoki tena moyoni. Kwa nini? Kwa sababu aliyekusudiwa kuwalisha sasa ndiye anayewaangamiza. Je, wewe ni mtoaji wa uzima au mleta maumivu? Je, watu hupata amani mbele yako au wasiwasi wako? Je, unainua au kubomoa? Ikiwa mtu unayempenda anafurahi zaidi wakati haupo kuliko wakati haupo, ni ishara kwamba unaweza kuwa unaleta kisu, sio maisha. Upendo unapaswa kuwa kama bustani ambayo watu wawili hukua pamoja. Lakini upendo unawezaje kukua ikiwa mwenzi mmoja anamwaga maji wakati mwingine anamwaga sumu? Ikiwa mmoja anapanda mbegu wakati mwingine anang'oa? Chagua kusema maneno ya uhai badala ya maneno yanayoua kujiamini. Chagua kukumbatia dosari badala ya kuzitumia kama silaha. Chagua kuunga mkono ndoto badala ya kuzikejeli. Chagua kuwa mahali salama, sio eneo la vita.

    Upendo unapaswa kuwa zawadi, sio mzigo. Baraka, si laana. Nguvu ya uponyaji, sio chanzo cha majeraha. Je, katika maisha ya mwenzako wewe ni mganga au mharibifu? Unaleta uhai au kisu?

    Credit
    Albert Nwosu
    JE, UNAMLETEA UHAI MPENZI WAKO, AU UNALETA KISU? Upendo unakusudiwa kujenga, sio kuvunja. Uhusiano unakusudiwa kuwa patakatifu, sio kichinjio. Nafsi mbili zinapokutana, zinapaswa kuleta uhai kwa kila mmoja, sio majeraha, sio makovu, sio huzuni. Hata hivyo, ukweli wa kusikitisha ni kwamba watu wengi huingia kwenye mahusiano wakitarajia kupendwa lakini hupokea maumivu. Wanatazamia furaha lakini wanakutana na taabu. Badala ya mwenzi anayeleta uzima, wanajikuta wanaishi na mtu ambaye ana kisu, akipunguza ujasiri wao, amani na heshima. Kwa hiyo, unaleta uhai kwa mpenzi wako, au unaleta kisu? Upendo unakusudiwa kumpa uhai yule unayedai kumpenda. Katika Mwanzo Mungu alimpulizia Adamu pumzi ya uhai, naye akawa nafsi hai. Kwa njia hiyo hiyo, uhusiano unapaswa kupumua maisha ndani ya mtu, sio kukimbia maisha kutoka kwao. Unapomhimiza mwenzako kufuata ndoto zake, unaleta uzima. Unapozungumza maneno ya fadhili, heshima, na uthibitisho, unaleta uzima. Unapovumilia mapungufu yao na kutembea nao katika mapambano yao, unaleta uhai. Wakati uwepo wako ni chanzo cha amani na si chanzo cha msongo wa mawazo, unaleta uhai. Upendo haupaswi kamwe kuhisi kama kutembea kwenye uwanja wa vita, ambapo kila neno, kila kitendo na kila siku huhisi kama kupigania kuishi. Mpenzi wako hapaswi kujisikia salama nje kuliko ndani ya uhusiano. Ikiwa unampenda mtu, anapaswa kustawi chini ya upendo wako, sio kukauka. Kisu sio lazima kiwe cha mwili kila wakati. Vidonda vingine huenda zaidi kuliko mwili; wanachoma roho. Baadhi yetu, badala ya kuleta uhai, kuleta kisu. Tunaleta kisu cha maneno makali, kukata ndani ya kujithamini kwa mpenzi wetu. Tunaleta kisu cha kulinganisha, na kuwafanya wahisi kama hawatoshi vya kutosha. Tunakuja na kisu cha kupuuza, na njaa ya upendo na tahadhari wanayotamani. Kwa namna fulani, pia kuja na kisu cha usaliti, ambapo uaminifu wetu ni kwa maneno tu lakini si kwa vitendo. Watu wengine wanakufa kihisia na kiroho kwa sababu ya mtu wanayempenda. Furaha yao inafifia taratibu. Kujiamini kwao kunatoweka. Kicheko chao hakitoki tena moyoni. Kwa nini? Kwa sababu aliyekusudiwa kuwalisha sasa ndiye anayewaangamiza. Je, wewe ni mtoaji wa uzima au mleta maumivu? Je, watu hupata amani mbele yako au wasiwasi wako? Je, unainua au kubomoa? Ikiwa mtu unayempenda anafurahi zaidi wakati haupo kuliko wakati haupo, ni ishara kwamba unaweza kuwa unaleta kisu, sio maisha. Upendo unapaswa kuwa kama bustani ambayo watu wawili hukua pamoja. Lakini upendo unawezaje kukua ikiwa mwenzi mmoja anamwaga maji wakati mwingine anamwaga sumu? Ikiwa mmoja anapanda mbegu wakati mwingine anang'oa? Chagua kusema maneno ya uhai badala ya maneno yanayoua kujiamini. Chagua kukumbatia dosari badala ya kuzitumia kama silaha. Chagua kuunga mkono ndoto badala ya kuzikejeli. Chagua kuwa mahali salama, sio eneo la vita. Upendo unapaswa kuwa zawadi, sio mzigo. Baraka, si laana. Nguvu ya uponyaji, sio chanzo cha majeraha. Je, katika maisha ya mwenzako wewe ni mganga au mharibifu? Unaleta uhai au kisu? Credit Albert Nwosu
    Love
    1
    · 0 Комментарии ·0 Поделились ·164 Просмотры
  • Elimu Nchini Japani huanza bila mitihani hadi darasa la nne, karibu na umri wa miaka 10. Katika miaka mitatu ya kwanza, mkazo ni kukuza tabia njema na ukuzaji wa Maendeleo.

    Walimu hutanguliza ujuzi wa kijamii kwa kuwafundisha kazi na ukuaji wa kibinafsi, wakiamini haya ni muhimu kabla ya kuanzisha majaribio ya kitaaluma Darasani.

    Kwa kuangazia ujenzi wa tabia mapema, shule zinalenga kulea Watoto waliokamilika ambao wanathamini heshima na kazi ya pamoja, na kutoa msingi thabiti wa kujifunza siku zijazo.

    Elimu Nchini Japani 🇯🇵 huanza bila mitihani hadi darasa la nne, karibu na umri wa miaka 10. Katika miaka mitatu ya kwanza, mkazo ni kukuza tabia njema na ukuzaji wa Maendeleo. Walimu hutanguliza ujuzi wa kijamii kwa kuwafundisha kazi na ukuaji wa kibinafsi, wakiamini haya ni muhimu kabla ya kuanzisha majaribio ya kitaaluma Darasani. Kwa kuangazia ujenzi wa tabia mapema, shule zinalenga kulea Watoto waliokamilika ambao wanathamini heshima na kazi ya pamoja, na kutoa msingi thabiti wa kujifunza siku zijazo.
    0 Комментарии ·0 Поделились ·135 Просмотры
  • Mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa , N’Golo Kanté, ameonyesha moyo wa upendo kwa jamii kwa kujenga hospitali ya kisasa yenye thamani ya dola milioni tano (5) Nchini Mali, ikiwa ni msaada kwa Watoto na familia zisizojiweza kupata huduma bora za afya.

    Kanté, ambaye alizaliwa Jijini Paris, Ufaransa, ana asili ya Mali, Wazazi wake wakiwa Wahamiaji waliotoka Nchini Mali mwaka 1980. Jina lake N’Golo linatokana na Mfalme wa zamani wa Mali aliyewahi kutawala. Katika ziara yake Mali, Kanté alitumia muda na familia yake huku akitoa heshima kwa Baba yake na Kaka yake Marehemu.

    Mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa 🇫🇷, N’Golo Kanté, ameonyesha moyo wa upendo kwa jamii kwa kujenga hospitali ya kisasa yenye thamani ya dola milioni tano (5) Nchini Mali, ikiwa ni msaada kwa Watoto na familia zisizojiweza kupata huduma bora za afya. Kanté, ambaye alizaliwa Jijini Paris, Ufaransa, ana asili ya Mali, Wazazi wake wakiwa Wahamiaji waliotoka Nchini Mali mwaka 1980. Jina lake N’Golo linatokana na Mfalme wa zamani wa Mali aliyewahi kutawala. Katika ziara yake Mali, Kanté alitumia muda na familia yake huku akitoa heshima kwa Baba yake na Kaka yake Marehemu.
    0 Комментарии ·0 Поделились ·149 Просмотры
  • Mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa , N’Golo Kanté, ameonyesha moyo wa upendo kwa jamii kwa kujenga hospitali ya kisasa yenye thamani ya dola milioni tano (5) Nchini Mali, ikiwa ni msaada kwa Watoto na familia zisizojiweza kupata huduma bora za afya.

    Kanté, ambaye alizaliwa Jijini Paris, Ufaransa, ana asili ya Mali, Wazazi wake wakiwa Wahamiaji waliotoka Nchini Mali mwaka 1980. Jina lake N’Golo linatokana na Mfalme wa zamani wa Mali aliyewahi kutawala. Katika ziara yake Mali, Kanté alitumia muda na familia yake huku akitoa heshima kwa Baba yake na Kaka yake Marehemu.
    Mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa 🇫🇷, N’Golo Kanté, ameonyesha moyo wa upendo kwa jamii kwa kujenga hospitali ya kisasa yenye thamani ya dola milioni tano (5) Nchini Mali, ikiwa ni msaada kwa Watoto na familia zisizojiweza kupata huduma bora za afya. Kanté, ambaye alizaliwa Jijini Paris, Ufaransa, ana asili ya Mali, Wazazi wake wakiwa Wahamiaji waliotoka Nchini Mali mwaka 1980. Jina lake N’Golo linatokana na Mfalme wa zamani wa Mali aliyewahi kutawala. Katika ziara yake Mali, Kanté alitumia muda na familia yake huku akitoa heshima kwa Baba yake na Kaka yake Marehemu.
    0 Комментарии ·0 Поделились ·148 Просмотры
Расширенные страницы