Uongozi wa Ligi Kuu ya mpira wa miguu Nchini Marekani , Major League Soccer (MLS), umempiga marufuku Mlinzi binafsi (Bodyguard) wa Lionel Messi, Yassine Cheuko, kuwa kando na kuingia katikati ya Uwanja wakati wa mechi za Inter Miami kwa lengo lake la kumlinda Mwajiri wake Messi.
Ikumbukwe kwamba Yassine Cheuko, ni Mwanajeshi wa zamani wa kikosi maalumu cha operesheni za kijeshi cha Jeshi la Majini la Marekani (U.S. Navy) kinachobobea katika vita visivyo vya kawaida, kupambana na ugaidi, mashambulizi ya moja kwa moja, na upelelezi wa kijeshi. Tangu Yessine Cheuko aanze kufanya kazi na Messi amejizolea umaarufu mkubwa Duniani kwani ameonekana mara nyingi akiwadhibiti Wavamizi mbalimbali ambao wengi lengo lao huwa sio baya, zaidi wanataka kupiga picha na Messi.
Tayari uongozi wa Ligi hiyo umemzuia kuingia Uwanjani, sasa ataruhusiwa tu kuwa kwenye Vyumba vya kubadilishia nguo na maeneo ya Waandishi wa habari siku za mechi. Uamuzi huu ni sehemu ya mpango wa (MLS) wa kuchukua mamlaka kamili ya usalama wa mechi.
Baada ya katazo, Yassine Cheuko ameonyesha kutoridhishwa na hatua hiyo, akisema kuwa Wavamizi wa Uwanja ni tatizo kubwa zaidi Nchini Marekani kuliko Ulaya. Kwa mujibu wake, katika miaka saba aliyofanya kazi Ulaya, kulikuwa na matukio sita pekee ya uvamizi Uwanjani, ilhali katika miezi 20 Nchini Marekani, tayari yameshuhudiwa matukio 16.
Mlinzi huyo ameendelea kusema kuwa Uongozi wa Ligi Kuu ya Marekani haukutakiwa kumzuia kufanye kazi yake bali walitakiwa kumpa ushirikiano ili kazi hiyo waifanye kwa pamoja kwa sababu eti kipindi yupo barani Ulaya, alipata ushirikiano wa kutosha kutoka kwenye Uongozi na alifanya kazi yake kwa uhuru. Pamoja na kuzuiliwa kuingia Uwanjani au kukaa kando ya Uwanja, Cheuko amesema kuwa ataendelea kufanya kazi yake kama kawaida bila kuvunja sheria au utaratibu uliopo kwenye mchezo wa mpira wa miguu.

Uongozi wa Ligi Kuu ya mpira wa miguu Nchini Marekani 馃嚭馃嚫, Major League Soccer (MLS), umempiga marufuku Mlinzi binafsi (Bodyguard) wa Lionel Messi, Yassine Cheuko, kuwa kando na kuingia katikati ya Uwanja wakati wa mechi za Inter Miami kwa lengo lake la kumlinda Mwajiri wake Messi.
Ikumbukwe kwamba Yassine Cheuko, ni Mwanajeshi wa zamani wa kikosi maalumu cha operesheni za kijeshi cha Jeshi la Majini la Marekani (U.S. Navy) kinachobobea katika vita visivyo vya kawaida, kupambana na ugaidi, mashambulizi ya moja kwa moja, na upelelezi wa kijeshi. Tangu Yessine Cheuko aanze kufanya kazi na Messi amejizolea umaarufu mkubwa Duniani kwani ameonekana mara nyingi akiwadhibiti Wavamizi mbalimbali ambao wengi lengo lao huwa sio baya, zaidi wanataka kupiga picha na Messi.
Tayari uongozi wa Ligi hiyo umemzuia kuingia Uwanjani, sasa ataruhusiwa tu kuwa kwenye Vyumba vya kubadilishia nguo na maeneo ya Waandishi wa habari siku za mechi. Uamuzi huu ni sehemu ya mpango wa (MLS) wa kuchukua mamlaka kamili ya usalama wa mechi.
Baada ya katazo, Yassine Cheuko ameonyesha kutoridhishwa na hatua hiyo, akisema kuwa Wavamizi wa Uwanja ni tatizo kubwa zaidi Nchini Marekani kuliko Ulaya. Kwa mujibu wake, katika miaka saba aliyofanya kazi Ulaya, kulikuwa na matukio sita pekee ya uvamizi Uwanjani, ilhali katika miezi 20 Nchini Marekani, tayari yameshuhudiwa matukio 16.
Mlinzi huyo ameendelea kusema kuwa Uongozi wa Ligi Kuu ya Marekani haukutakiwa kumzuia kufanye kazi yake bali walitakiwa kumpa ushirikiano ili kazi hiyo waifanye kwa pamoja kwa sababu eti kipindi yupo barani Ulaya, alipata ushirikiano wa kutosha kutoka kwenye Uongozi na alifanya kazi yake kwa uhuru. Pamoja na kuzuiliwa kuingia Uwanjani au kukaa kando ya Uwanja, Cheuko amesema kuwa ataendelea kufanya kazi yake kama kawaida bila kuvunja sheria au utaratibu uliopo kwenye mchezo wa mpira wa miguu.
0 Reacties
路0 aandelen
路26 Views