• Performance ya rapa Kendrick Lamar kwenye usiku wa kilele cha mashindano ya NFL Superbowl 2025 imevunja rekodi na kuwa performance ya Superbowl iliyotazamwa zaidi kuliko performance nyingine ndani ya muda mfupi.

    Mpaka sasa performance hiyo imejikusanyia jumla ya watazamaji Milioni 133.5 huku ikijikusanyia watazamaji zaidi kwa asilimia 3 kupita performance ya mwaka jana.

    Takwimu hizo zimetolewa na Roc Nation ambao ni hushirikiana na Apple Music katika kuandaa performance za Superbowl.
    Performance ya rapa Kendrick Lamar kwenye usiku wa kilele cha mashindano ya NFL Superbowl 2025 imevunja rekodi na kuwa performance ya Superbowl iliyotazamwa zaidi kuliko performance nyingine ndani ya muda mfupi. Mpaka sasa performance hiyo imejikusanyia jumla ya watazamaji Milioni 133.5 huku ikijikusanyia watazamaji zaidi kwa asilimia 3 kupita performance ya mwaka jana. Takwimu hizo zimetolewa na Roc Nation ambao ni hushirikiana na Apple Music katika kuandaa performance za Superbowl.
    0 Comments 0 Shares 122 Views
  • Msanii wa Nigeria , Wizkid achangia kumpa Bob Marley tuzo yake akiwa ni Marehemu.

    Pamoja na mafanikio makubwa aliyoyapata akiwa hai, Mwanamziki nguli Duniani, Raia wa Jamaica , Bob Marley hakuwahi kushinda tuzo ya Grammy katika maisha yake, lakini miaka michache iliopita familia yake walimtafuta Msanii kutoka Nchini Nigeria, Wizkid kwa ajili ya kufanya Collabo na Bob Marley ili waweze kuifanya upya kazi ya Bob Marley "One love, Music inspired by the Film, Album.

    Baada ya albamu hiyo kutoka ambapo Wizkid ameifanya upya imeshinda albamu bora ya mwaka ya Reggae 2025 kwenye tuzo za Grammy na kuweka rekodi ya kuwa tuzo ya kwanza ya Grammy ya Bob Marley huku shukurani kubwa amepewa Wizkid.

    Aidha, Wizkid amepokea cheti kutoka kwenye Uongozi wa Grammy na barua ya shukurani kutoka kwa familia ya Marley kwa kuifanya heshima ya baba yao kuendelea kuwepo Duniani na kumsaidia Mwanamziki huyo Mkongwe wa muziki wa Reggae kushinda Grammy yake ya kwanza.

    Msanii wa Nigeria 馃嚦馃嚞, Wizkid achangia kumpa Bob Marley tuzo yake akiwa ni Marehemu. Pamoja na mafanikio makubwa aliyoyapata akiwa hai, Mwanamziki nguli Duniani, Raia wa Jamaica 馃嚡馃嚥, Bob Marley hakuwahi kushinda tuzo ya Grammy katika maisha yake, lakini miaka michache iliopita familia yake walimtafuta Msanii kutoka Nchini Nigeria, Wizkid kwa ajili ya kufanya Collabo na Bob Marley ili waweze kuifanya upya kazi ya Bob Marley "One love, Music inspired by the Film, Album. Baada ya albamu hiyo kutoka ambapo Wizkid ameifanya upya imeshinda albamu bora ya mwaka ya Reggae 2025 kwenye tuzo za Grammy na kuweka rekodi ya kuwa tuzo ya kwanza ya Grammy ya Bob Marley huku shukurani kubwa amepewa Wizkid. Aidha, Wizkid amepokea cheti kutoka kwenye Uongozi wa Grammy na barua ya shukurani kutoka kwa familia ya Marley kwa kuifanya heshima ya baba yao kuendelea kuwepo Duniani na kumsaidia Mwanamziki huyo Mkongwe wa muziki wa Reggae kushinda Grammy yake ya kwanza.
    0 Comments 0 Shares 361 Views
  • Kulingana na ripoti ya Duetti, Mtandao wa kusikiliza na kuuza muziki wa Apple Music unalipa Wasanii zaidi ya mara mbili (2) ya kiasi kinacholipwa na Spotify kwa kila "streams" 1,000.

    Hii inatokana na ukweli kwamba Apple Music inategemea malipo ya Watumiaji bila kuwa na huduma za bure. Spotify, ambayo ina kiwango kikubwa cha matangazo kwenye huduma yake ya bure na pia inaongoza kwa kuwa na Wasikilizaji wengi, lakini inalipa Wasanii pesa kidogo hata kuliko mtandao wa YouTube, ambao pia hutegemea matangazo.

    Ripoti hiyo pia inaonyesha hali ya wasiwasi ambapo Spotify inaongeza bei kwa Watumiaji wake lakini malipo kwa Wasanii yanaendelea kupungua. Pia Spotify inabagua sana kwa kuangalia eneo, "brand" na Lebo ya Msanii na sio Wasanii wote wanalipwa kiwango sawa.

    Hata hivyo, Spotify imekanusha ripoti hiyo, ikisema wanazingatia kuongeza ushirikiano wa Watumiaji ili malipo ya jumla kwa wasanii yaweze kuongezeka. Kwa mwaka 2024, viwango vya malipo ambavyo Wasanii wamelipwa na mitandao ya kusikiliza na kuuza muziki Duniani (streaming platforms) kwa "streams" 1,000 ni hizi hapa:

    1. Amazon: $8.80 (TZS 22,413)
    2. Apple Music: $6.20 (TZS 15,791)
    3. YouTube: $4.80 (TZS 12,225)
    4. Spotify: $3.00 (TZS 7,641)

    Hivyo wimbo ukisikilizwa mara moja, kwenye Apple Music inalipa Shilingi 15.7; Spotify inalipa Shilingi 7.6, YouTube inalipa Shilingi 12.2 na Amazon inalipa Shilingi 22.4.


    #Chukuahii
    Kulingana na ripoti ya Duetti, Mtandao wa kusikiliza na kuuza muziki wa Apple Music unalipa Wasanii zaidi ya mara mbili (2) ya kiasi kinacholipwa na Spotify kwa kila "streams" 1,000. Hii inatokana na ukweli kwamba Apple Music inategemea malipo ya Watumiaji bila kuwa na huduma za bure. Spotify, ambayo ina kiwango kikubwa cha matangazo kwenye huduma yake ya bure na pia inaongoza kwa kuwa na Wasikilizaji wengi, lakini inalipa Wasanii pesa kidogo hata kuliko mtandao wa YouTube, ambao pia hutegemea matangazo. Ripoti hiyo pia inaonyesha hali ya wasiwasi ambapo Spotify inaongeza bei kwa Watumiaji wake lakini malipo kwa Wasanii yanaendelea kupungua. Pia Spotify inabagua sana kwa kuangalia eneo, "brand" na Lebo ya Msanii na sio Wasanii wote wanalipwa kiwango sawa. Hata hivyo, Spotify imekanusha ripoti hiyo, ikisema wanazingatia kuongeza ushirikiano wa Watumiaji ili malipo ya jumla kwa wasanii yaweze kuongezeka. Kwa mwaka 2024, viwango vya malipo ambavyo Wasanii wamelipwa na mitandao ya kusikiliza na kuuza muziki Duniani (streaming platforms) kwa "streams" 1,000 ni hizi hapa: 1. Amazon: $8.80 (TZS 22,413) 2. Apple Music: $6.20 (TZS 15,791) 3. YouTube: $4.80 (TZS 12,225) 4. Spotify: $3.00 (TZS 7,641) Hivyo wimbo ukisikilizwa mara moja, kwenye Apple Music inalipa Shilingi 15.7; Spotify inalipa Shilingi 7.6, YouTube inalipa Shilingi 12.2 na Amazon inalipa Shilingi 22.4. #Chukuahii
    Like
    1
    0 Comments 0 Shares 373 Views
  • MUSICIAN/BAND
    MUSICIAN/BAND
    0 Comments 0 Shares 153 Views
  • "The Unforgetable THROW BACK
    Ilikuwa mwaka 2003 takribani Miaka 22 iliyopita nikiwa naingia kwenye ukumbi wa DIAMOND JUBILEE - UPANGA kwa kusukuma Mkokoteni 'KiZALI LA MENTALI' feat @sir_nature kwenye uzinduzi wa Album yangu ya pili ya MAPINDUZI HALISI ambayo baadae ilikuja kutangazwa na KILIMANJARO MUSIC AWARDS wakati huo (sasa TMA) kuwa album bora ya HIP HOP kwa mwaka 2003, Nilikuwa nimezungukwa na MIILI VIBANDA (Bouncers) pamoja na Producer wangu bora wa muda wote Tanzania @majani187 of BONGO RECORDS na @solothang_aka_ulamaa

    NB: Ni wasanii wachache sana tuliokuwa na uwezo wa kuujaza ukumbi mkubwa wa DIAMOND JUBILEE na ukatapika kisawasawa
    Je wewe ulikuwa wapi kipindi hiki???" - Professor Jay, Msanii wa muziki Hip-hop Tanzania
    "The Unforgetable THROW BACK 馃敟馃敟馃敟 Ilikuwa mwaka 2003 takribani Miaka 22 iliyopita nikiwa naingia kwenye ukumbi wa DIAMOND JUBILEE - UPANGA kwa kusukuma Mkokoteni 'KiZALI LA MENTALI' feat @sir_nature kwenye uzinduzi wa Album yangu ya pili ya MAPINDUZI HALISI ambayo baadae ilikuja kutangazwa na KILIMANJARO MUSIC AWARDS wakati huo (sasa TMA) kuwa album bora ya HIP HOP kwa mwaka 2003, Nilikuwa nimezungukwa na MIILI VIBANDA (Bouncers) pamoja na Producer wangu bora wa muda wote Tanzania @majani187 of BONGO RECORDS na @solothang_aka_ulamaa 馃憫 NB: Ni wasanii wachache sana tuliokuwa na uwezo wa kuujaza ukumbi mkubwa wa DIAMOND JUBILEE na ukatapika kisawasawa馃挭馃挭馃挭 Je wewe ulikuwa wapi kipindi hiki???" - Professor Jay, Msanii wa muziki Hip-hop Tanzania
    Like
    1
    0 Comments 0 Shares 405 Views
  • Jibu la Wakazi kwa Vanessa Mdee.

    "IT IS NOT FAIR: Ushirikina uko kila mahali kuzidi muziki !!

    Sidhani kama ni sahihi kusema Music peke yake ndio una mambo ya KISHIRIKINA hapo Tanzania! Au kwamba kila anayeufanya au aliyefanikiwa amefanya hivyo sababu ya Maagano ya kishetani.

    Imani za kimila kweli zipo Tanzania, ila hiyo ni sehemu ya utamaduni wetu. Sidhani kama mambo ya uchawi na kulogana ya kwenye muziki, yanafikia hata robo ya yanayotokea kwenye MAPENZI, SIASA, KAZINI, MICHEZO!!

    Watu wanataka kufanikiwa, na wakifikia hiyo desperation ya juu, basi wanaweza kushawishika kufanya lolote ili jambo lao liende. Ila sio wote pia…

    Na kingine, sidhani kama kutoa Sadaka au kwenda kwa Sheikh atie Baraka kabla ya kutoa kazi, huo ni ushirikina. Mimi sio Muislamu, ila nina marafiki Wasanii ambao wanafanya hivyo… na naona ni sawa (kuomba kheri kwenye kazi yako).

    Ila uchawi upo, maagano ya kishetani yapo, na ni kila mahali kwa wanaoamini na walio desperate enough, au wenye husda juu ya mafanikio ya wengine.

    Pia Suala la baadhi nyimbo za dini (“Gospel”) kutosema Yesu, sidhani kama ni sababu ya ushetani. Gospel iligeuka kuwa muziki wa kibiashara na wadau wakubwa walifanya conscious decision ya kuhimiza kusema Mungu ili wasiwatenge baadhi ya walaji, maana tukiwa wakweli, sio Wakristo tu ambao wamekuwa wanafurahia nyimbo za dini. So hakuna conspiracy hapo, maana pia kama hata mahubiri ya kanisani yalivyokuwa sometimes yanahusu maisha, ndoa, mafanikio, nk, hata muziki nao sometimes unatoa mafunzo tu ya kimaisha.

    Pengine tukianza ku-appreciate muziki kwa ubora na utofauti wake, badala ya kuwawekea pressure artist kuwa na stereotypical hits, basi wataacha kuwa desperate na kuhamia kwenye uchawi. Ila bottom line sidhani kama ni sahihi kuwanyooshea kidole wao tu… Mambo ya Jadi ni masuala ya nchi.

    SWALI: Zamani wahayudi walikuwa wanatoa sadaka kwa kichinja kondoo… ili Mungu awabariki. Je mtu akifanya tambiko la kimila@kwa kuchinja mbuzi kwanini aonekane kafanya kitu cha ajabu?! Je tunatofautishaje good magic & dark magic?! ana pia kuna secular artists wameimba nyimbo ambazo ni sawa na hawa Gospel artists wanazofanya, do we accept their songs as gospel? ( Phina - “Sisi Ni Wale”, MwanaFA - “Mfalme”)" - Wakazi, Msanii wa muziki wa Hip-hop Tanzania (wa zamani).

    Jibu la Wakazi kwa Vanessa Mdee. "IT IS NOT FAIR: Ushirikina uko kila mahali kuzidi muziki !! Sidhani kama ni sahihi kusema Music peke yake ndio una mambo ya KISHIRIKINA hapo Tanzania! Au kwamba kila anayeufanya au aliyefanikiwa amefanya hivyo sababu ya Maagano ya kishetani. Imani za kimila kweli zipo Tanzania, ila hiyo ni sehemu ya utamaduni wetu. Sidhani kama mambo ya uchawi na kulogana ya kwenye muziki, yanafikia hata robo ya yanayotokea kwenye MAPENZI, SIASA, KAZINI, MICHEZO!! Watu wanataka kufanikiwa, na wakifikia hiyo desperation ya juu, basi wanaweza kushawishika kufanya lolote ili jambo lao liende. Ila sio wote pia… Na kingine, sidhani kama kutoa Sadaka au kwenda kwa Sheikh atie Baraka kabla ya kutoa kazi, huo ni ushirikina. Mimi sio Muislamu, ila nina marafiki Wasanii ambao wanafanya hivyo… na naona ni sawa (kuomba kheri kwenye kazi yako). Ila uchawi upo, maagano ya kishetani yapo, na ni kila mahali kwa wanaoamini na walio desperate enough, au wenye husda juu ya mafanikio ya wengine. Pia Suala la baadhi nyimbo za dini (“Gospel”) kutosema Yesu, sidhani kama ni sababu ya ushetani. Gospel iligeuka kuwa muziki wa kibiashara na wadau wakubwa walifanya conscious decision ya kuhimiza kusema Mungu ili wasiwatenge baadhi ya walaji, maana tukiwa wakweli, sio Wakristo tu ambao wamekuwa wanafurahia nyimbo za dini. So hakuna conspiracy hapo, maana pia kama hata mahubiri ya kanisani yalivyokuwa sometimes yanahusu maisha, ndoa, mafanikio, nk, hata muziki nao sometimes unatoa mafunzo tu ya kimaisha. Pengine tukianza ku-appreciate muziki kwa ubora na utofauti wake, badala ya kuwawekea pressure artist kuwa na stereotypical hits, basi wataacha kuwa desperate na kuhamia kwenye uchawi. Ila bottom line sidhani kama ni sahihi kuwanyooshea kidole wao tu… Mambo ya Jadi ni masuala ya nchi. SWALI: Zamani wahayudi walikuwa wanatoa sadaka kwa kichinja kondoo… ili Mungu awabariki. Je mtu akifanya tambiko la kimila@kwa kuchinja mbuzi kwanini aonekane kafanya kitu cha ajabu?! Je tunatofautishaje good magic & dark magic?! ana pia kuna secular artists wameimba nyimbo ambazo ni sawa na hawa Gospel artists wanazofanya, do we accept their songs as gospel? ( Phina - “Sisi Ni Wale”, MwanaFA - “Mfalme”)" - Wakazi, Msanii wa muziki wa Hip-hop Tanzania (wa zamani).
    Like
    1
    0 Comments 0 Shares 492 Views
  • Why will Paul force war with Tanzanian musician
    Why will Paul force war with Tanzanian musician
    Love
    1
    0 Comments 0 Shares 237 Views