Rais wa Marekani , DonaldTrump, ameibua mjadala mkali baada ya kusema kuwa kuna uwezekano wa yeye kuwania muhula wa tatu, licha ya Katiba ya Marekani kupiga marufuku jambo hilo kupitia Marekebisho ya 22. Katika mahojiano na NBCNews, Rais huyo hakutaka kufuta uwezekano wa kuwania tena Urais baada ya kumaliza mihula miwili, akidai kuwa kuna njia za kufanya hilo kutokea. Alisisitiza kuwa "hakuwa anatania," jambo ambalo limeibua hofu miongoni mwa Wachambuzi wa siasa na Wanaharakati wa demokrasia Nchini humo.
Kwa mujibu wa Katiba ya Marekani, Rais haruhusiwi kutawala kwa zaidi ya mihula miwili ya miaka minne minne. Marekebisho ya 22 yaliwekwa ili kuzuia Mtu mmoja kuwa na mamlaka ya muda mrefu kama ilivyokuwa kwa Franklin D. Roosevelt, ambaye altawala kwa zaidi ya mihula miwili kabla ya marekebisho hayo kuidhinishwa mwaka 1951.
Kauli ya Trump imeibua maswali kuhusu mbinu anazoweza kutumia kutafuta muhula wa tatu. Wachambuzi wa sheria wanabainisha kuwa ili hilo litokee, ama katiba ibadilishwe rasmi kwa marekebisho mapya, au ipatikane tafsiri mpya ya kisheria inayomruhusu kugombea tena. Hata hivyo, mchakato wa kubadili katiba ni mgumu na unahitaji ridhaa ya Bunge pamoja na Majimbo mengi ya Marekani.
Baadhi ya Wafuasi wa Donald Trump wameunga mkono kauli yake, wakidai kuwa anastahili muda zaidi wa kuongoza Nchi. Hata hivyo, Wakosoaji wake wanasema kuwa hatua yoyote ya kupindua Marekebisho ya 22 inaweza kuwa tishio kwa demokrasia ya Marekani na kuweka msingi wa uongozi wa kiimla.

Rais wa Marekani 🇺🇸, DonaldTrump, ameibua mjadala mkali baada ya kusema kuwa kuna uwezekano wa yeye kuwania muhula wa tatu, licha ya Katiba ya Marekani kupiga marufuku jambo hilo kupitia Marekebisho ya 22. Katika mahojiano na NBCNews, Rais huyo hakutaka kufuta uwezekano wa kuwania tena Urais baada ya kumaliza mihula miwili, akidai kuwa kuna njia za kufanya hilo kutokea. Alisisitiza kuwa "hakuwa anatania," jambo ambalo limeibua hofu miongoni mwa Wachambuzi wa siasa na Wanaharakati wa demokrasia Nchini humo.
Kwa mujibu wa Katiba ya Marekani, Rais haruhusiwi kutawala kwa zaidi ya mihula miwili ya miaka minne minne. Marekebisho ya 22 yaliwekwa ili kuzuia Mtu mmoja kuwa na mamlaka ya muda mrefu kama ilivyokuwa kwa Franklin D. Roosevelt, ambaye altawala kwa zaidi ya mihula miwili kabla ya marekebisho hayo kuidhinishwa mwaka 1951.
Kauli ya Trump imeibua maswali kuhusu mbinu anazoweza kutumia kutafuta muhula wa tatu. Wachambuzi wa sheria wanabainisha kuwa ili hilo litokee, ama katiba ibadilishwe rasmi kwa marekebisho mapya, au ipatikane tafsiri mpya ya kisheria inayomruhusu kugombea tena. Hata hivyo, mchakato wa kubadili katiba ni mgumu na unahitaji ridhaa ya Bunge pamoja na Majimbo mengi ya Marekani.
Baadhi ya Wafuasi wa Donald Trump wameunga mkono kauli yake, wakidai kuwa anastahili muda zaidi wa kuongoza Nchi. Hata hivyo, Wakosoaji wake wanasema kuwa hatua yoyote ya kupindua Marekebisho ya 22 inaweza kuwa tishio kwa demokrasia ya Marekani na kuweka msingi wa uongozi wa kiimla.
0 Reacties
·0 aandelen
·18 Views