Upgrade to Pro

  • *1. Siku Moja Utastaafu.*
    Hautakua ukienda kazini, hautakua na madaraka tena, hautakua na nguvu ya ushawishi, mzunguko wako wa pesa utapungua kabisa!
    Chunguza/fuatilia tarehe yako ya kustaafu kwenye risiti yako ya malipo ya mshahara.

    *2. Tumia Vizuri Siku Zako za Likizo ya Mwaka.*
    Chochote utakachokifanya Likizo ndio utakachokifanya ukistaafu.Kama unatumia likizo kulala au kuagalia Luninga ndicho utakachokifanya ukistaafu.Tumia wakati wako wa ziada kujifunza kitu, kitakuja kuwa na manufaa ukistaafu.

    *3. Wekeza Kwa Ajili ya Kustaafu Kwako.*
    Watoto wako sio uwekezaji kwa ajili ya kustaafu kwako. Usiwategemee watoto, ndugu, au marafiki kama benki yako. Utapoteza heshima na utu wako.

    *4. Tafuta Shughuli Unayoipenda/Unayoifurahia* wakati bado upo kazini ikuongozee katika kustaafu kwako mfano kufuga kuku au miliki duka pata ujuzi unaojiuza (sio vyeti visivyo na matumizi)

    *5. Utastaafia Wapi?.*
    Jijengee nyumba. Usistaafu ukiwa bado unapanga nyumba.
    Usigome kutoka kwenye nyumba ya serikali.

    @PM SPORTS
    #PM96
    *1. Siku Moja Utastaafu.* Hautakua ukienda kazini, hautakua na madaraka tena, hautakua na nguvu ya ushawishi, mzunguko wako wa pesa utapungua kabisa! Chunguza/fuatilia tarehe yako ya kustaafu kwenye risiti yako ya malipo ya mshahara. *2. Tumia Vizuri Siku Zako za Likizo ya Mwaka.* Chochote utakachokifanya Likizo ndio utakachokifanya ukistaafu.Kama unatumia likizo kulala au kuagalia Luninga ndicho utakachokifanya ukistaafu.Tumia wakati wako wa ziada kujifunza kitu, kitakuja kuwa na manufaa ukistaafu. *3. Wekeza Kwa Ajili ya Kustaafu Kwako.* Watoto wako sio uwekezaji kwa ajili ya kustaafu kwako. Usiwategemee watoto, ndugu, au marafiki kama benki yako. Utapoteza heshima na utu wako. *4. Tafuta Shughuli Unayoipenda/Unayoifurahia* wakati bado upo kazini ikuongozee katika kustaafu kwako mfano kufuga kuku au miliki duka pata ujuzi unaojiuza (sio vyeti visivyo na matumizi) *5. Utastaafia Wapi?.* Jijengee nyumba. Usistaafu ukiwa bado unapanga nyumba. Usigome kutoka kwenye nyumba ya serikali. @PM SPORTS #PM96
    Like
    1
    1 Comments ·523 Views
  • ·178 Views
  • Kondoo alikuwa anapita akamuona simba akilia akiwa amenasa kwenye boksi la chuma(grili), simba akamsihi sana kondoo amuokoe na kumuahidi kuwa hatamuua wala kumla, lakini kondoo akakataa.... Baada ya simba kubembeleza sana na kwa upumbavu wa kondoo, akafungua lile boksi la chuma.

    Sasa simba alikuwa na njaa kali mno baada ya kukaa kifungoni kwa siku kadhaa bila kula chakula... Mara moja alimrukia kondoo na kukaribia kumuua ili amle, lakini kondoo alimkumbusha kiapo chake.

    Waliendelea kubishana hadi wanyama wengine waliokuwa wanapita wakauliza kulikoni? Basi simba na kondoo wote wakaelezea jinsi ilivyokuwa, lakini kwa hofu ya simba na kutaka kupata huruma machoni pa simba, wanyama wote wakamsapoti simba isipokuwa kobe ambaye alidai kuwa hakuelewa mazingira na stori yenyewe.

    Sasa kobe akamuomba simba aoneshe mahali alipokuwa kabla ya kondoo kumuokoa, simba akamuonesha kobe kwa mguu wake wa mbele, pale... Kobe akamuuliza tena, "ulikuwa ndani ama nje kabla ya kondoo kuja??"...Simba akamjibu, "nilikuwa ndani".

    Kobe akamuuliza tena simba, "sawa, embu ingia tena ili tuone jinsi ilivyokuwia vigumu kukaa ndani ya grili kwani sielewi stori hii yote vizuri"... Simba akaingia, na mara moja(chapu!), kobe akafunga lile boksi la chuma (grili)... Na simba sasa alikuwa amenasa tena!!

    Kwa mshangao mkubwa, wale wanyama wengine wakamuuliza kobe "Kwanini?" na kobe akawajibu..."Kama tukimruhusu simba amle kondoo leo, bado atasikia njaa tena kesho na hatujui kati yetu ni nani atakayeliwa kesho..!!"

    *#FUNDISHO*

    Usiunge mkono uovu leo kwa vile haukuathiri moja kwa moja, pengine kesho inaweza kuwa zamu yako.!!

    Nafikri tunahitaji kobe wengi zaidi katika jamii yetu. Umejifunza nini?

    Asante kwa kusoma ujumbe huu sambazia wengine

    Nimeitoa Mahali.... #Majulajr
    Kondoo alikuwa anapita akamuona simba akilia akiwa amenasa kwenye boksi la chuma(grili), simba akamsihi sana kondoo amuokoe na kumuahidi kuwa hatamuua wala kumla, lakini kondoo akakataa.... Baada ya simba kubembeleza sana na kwa upumbavu wa kondoo, akafungua lile boksi la chuma. Sasa simba alikuwa na njaa kali mno baada ya kukaa kifungoni kwa siku kadhaa bila kula chakula... Mara moja alimrukia kondoo na kukaribia kumuua ili amle, lakini kondoo alimkumbusha kiapo chake. Waliendelea kubishana hadi wanyama wengine waliokuwa wanapita wakauliza kulikoni? Basi simba na kondoo wote wakaelezea jinsi ilivyokuwa, lakini kwa hofu ya simba na kutaka kupata huruma machoni pa simba, wanyama wote wakamsapoti simba isipokuwa kobe ambaye alidai kuwa hakuelewa mazingira na stori yenyewe. Sasa kobe akamuomba simba aoneshe mahali alipokuwa kabla ya kondoo kumuokoa, simba akamuonesha kobe kwa mguu wake wa mbele, pale... Kobe akamuuliza tena, "ulikuwa ndani ama nje kabla ya kondoo kuja??"...Simba akamjibu, "nilikuwa ndani". Kobe akamuuliza tena simba, "sawa, embu ingia tena ili tuone jinsi ilivyokuwia vigumu kukaa ndani ya grili kwani sielewi stori hii yote vizuri"... Simba akaingia, na mara moja(chapu!), kobe akafunga lile boksi la chuma (grili)... Na simba sasa alikuwa amenasa tena!! Kwa mshangao mkubwa, wale wanyama wengine wakamuuliza kobe "Kwanini?" na kobe akawajibu..."Kama tukimruhusu simba amle kondoo leo, bado atasikia njaa tena kesho na hatujui kati yetu ni nani atakayeliwa kesho..!!" *#FUNDISHO* Usiunge mkono uovu leo kwa vile haukuathiri moja kwa moja, pengine kesho inaweza kuwa zamu yako.!! Nafikri tunahitaji kobe wengi zaidi katika jamii yetu. Umejifunza nini? Asante kwa kusoma ujumbe huu sambazia wengine Nimeitoa Mahali.... #Majulajr
    ·497 Views
More Stories