MABADILIKO NI MZIZI WA MAISHA
"Mabadiliko ni kiini cha maisha; kitu pekee ambacho kinabaki bila kubadilika ni sheria ya mabadiliko" Heraclitus
Asili ya kila kitu kinabadilika,wale tuliokuwa 2024 sio ambao tutakuwa 2025, kwasababu hata wewe ukikataa kubadilika bado utabadilika kwa namna ya kiasili
Ulimwengu unapo yaendea mabadiliko ya kiasili unahitaji kujiboresha, unahitaji kuwaonesha watu taswira ya jinsi ya kuufanya uwe sehemu bora ya wengine kuishi, kuna wakati tunabadilika ili kuboresha na pia tuna badilika ili kutengeneza uwili wa maisha
Maisha yanatuambia ni vigumu kuyagusa maji ya mto mara mbili yalio katika mtiririko hivyo kwakua maji yanasonga nasi tunahitajika kusonga, miaka inaongezeka kuonesha jinsi gani tunahitajika kujiboresha
Matukio,watu na mawazo katika maisha ni sawa mtiririko wa maji hivyo badala ya kung'ang'ania yaliyopita, ni wakati wa kujifunza jinsi ya kukumbatia mabadiliko yasiyoepukika ambayo maisha hutupa
Anasema Anatole ""Mtu kamwe asipoteze muda katika kujutia bure yaliyopita au katika kulalamika dhidi ya mabadiliko ambayo yanatuletea usumbufu, kwa maana mabadiliko ndio kiini cha maisha."
Mwaka umebadilika , kuna mambo ambayo hatutaweza kuyabadilisha lakini kwaye ni sisi tutahitajika kujidhibiti kwa kubadilika namna ya kuyakabili, hatuwezi kubadilisha kwakua ni nje ya uwezo wetu lakini tunaweza kubadilisha namna ya kukabili kwasababu ipo ndani ya uwezo wetu
Kadiri tunavyokubali mabadiliko yanapotokea, ndivyo tunavyozidi kupunguza woga, na kuwa makini na kufahamu mawazo na hisia zetu tunaongeza hali kujiamini na kusadiki kwamba tutakuwa sawa mambo yanapobadilika. Mabadiliko daima yatakuwa, mara kwa mara katika maisha yetu.
Sekomba Ngovi