0 Commentarii
·0 Distribuiri
·136 Views
-
-
-
-
-
JAMBAZI MTUKUTU.
Nchini Tanzania, kuna manju 'Dj' fulani wa muziki anayejulikana kwa jina maarufu la 'DJ JD' au kwa kirefu *'DJ John Dilinga'.* Huyu ni moja kati ya maDj wakongwe na mahiri sana tuliobahatika kuwa nao hapa nchini Tanzania. Kwa wale wapenzi na wadau wa muziki wa 'bongofleva' hususani wa miaka ya nyumanyuma kidogo, bila shaka mtakua mnamfahamu Dj huyu.
Kwa muda mrefu nimekuwa nikitamani kufahamu ni kwanini anaitwa John Dilinga..nikiwa nataka kujua kama hilo ni jina lake halisi au ni 'a.k.a'. Maana ni kawaida kuona watu mbalimbali hususani walio kwenye tasnia ya burudani wakitumia majina ya ziada (a.k.a) kuliko majina yao halisi.
Kitu kilichonifanya nianze na DJ JD ni baada ya kugundua kuwa leo ni tarehe 22 Julai. Tarehe ambayo ulimwengu mzima unamtaja bwana mmoja mtukutu sana, aliyewahi kusumbua vichwa vya maofisa usalama wa nchi ya Marekani, akifahamika kama *John Dillinger.* Huyu alikuwa ni moja kati ya wahuni wakubwa nchini Marekani aliyetamba sana katika miaka ya 1930 kwa kujihusisha na matukio ya kihalifu hususani uporaji wa fedha kwenye mabenki.
Tofauti ni kwamba John Dilinga wa Tanzania ni DJ, wakati John Dillinger wa Marekani alikuwa ni jambazi mtukutu.
Utukutu wake ulianza angali ana umri mdogo na hata aliweza kuacha shule ili kwenda kutafuta pesa!! Alianza kama mdokozi wa vitu vidogovidogo lakini tukio lake la kwanza lilikuwa ni *kuiba gari*, kisha 'kwenda misele' kwa mpenzi wake mpya. Siku chache baadae alikuja kukamatwa na mapolisi akiwa anazurula mtaani japokuwa alifanikiwa kuchoropoka na 'kutokomea kusikojulikana'.
Baadae alipata kazi katika jeshi la majini 'navy', akifanya katika meli ya jeshi ya 'USS Uttah'. Baada ya miezi kadhaa John Dillinger alitoroka kazini.
April 1924 akiwa hana shughuli ya kumuingizia kipato, John Dillinger alifunga ndoa na mwanadada Beryl Hovious ambapo walienda kuishi kwenye nyumba ya baba yake ambapo John Dillinger aliahidi kwamba sasa atatulia na kuacha utukutu wote. Lakini wiki chache baada ya ndoa, Dillinger alikamatwa na hata kufikishwa mahakamani kwa kosa la wizi wa kuku, "nadhani alikuwa anatafuta mboga ya kwenda kula na mkewe".
Lakini kwa msaada wa Baba yake, kesi ya Dillinger iliweza kufutwa. Baadae Dillinger aliamua kutoka kwenye nyumba ya baba yake na kwenda kuishi kwenye nyumba ya wazazi wa mwanamke ambapo huko alibahatika kupata kazi kwenye duka la kuuza vifaa vya ujenzi. Akiwa huko, Dillinger alikutana na rafiki yake wa muda mrefu aitwaye *Edgar Singleton,* ambapo walipanga mikakati ya kuiba pesa. Ndipo tarehe 6 septemba 1924 waliiba pesa katika moja ya Grocery japokuwa walikamatwa na kufikishwa mahakamani ambapo John Dillinger alihukumiwa kifungo cha miaka 20 katika Gereza la "Indiana State Reformatory in Pendleton".
Alipokuwa jela, alikutana na wafungwa wengine ambao walimfundisha mbinu nyingine za uhalifu mkubwa hususani uporaji wa fedha kwenye mabenki. Alitumikia kifungo chake hadi mwaka 1933 kwa paroli. Siku chache tu baada ya kutoka jela, John Dillinger alifanya uhalifu mkubwa, safari hii akivamia benki na kuiba pesa benki ingawa alikamatwa na kuhukumiwa kifungo katika gereza la Lima.
Siku chache baada ya Dillinger kuingia jela, wafungwa 12 ambao baadhi yao ni rafiki zake Dillinger, waliweza kutoroka katika gereza la "Indiana State Prison". Hili ni gereza alilowahi kufungwa John Dillinger baada ya kuhamishwa toka kwenye gereza lile la awali.
Miongoni mwa hao waliotoroka, ambao baadhi yao ni marafiki wa Dillinger, walifika katika gereza alilofungwa Dillinger lengo ni kumtorosha rafiki yao. Walimuua askari mmoja na kuchukua funguo kisha kufungua mlango wa selo alilomo Dillinger kisha kutoroka naye. Baada ya kutoroka, John Dillinger na wenzake walielekea mjini Chicago ambapo waliunda genge kubwa la kihalifu *Dillinger Gang*. Genge hili lilipora pesa kwenye mabenki mbalimbali, na ili kuongeza nguvu, walivamia ghala la silaha na kuiba silaha nzitonzito walizozotumia katika shughuli zao za kihalifu.
Wahuni hao walitokea kupata umaarufu mkubwa pale Marekani, hususani huyu Dillinger ambaye alikuwa maarufu sana mithili ya 'nyota wa hollywood' kwani kila siku jina lake lilikuwa likitajwa kwenye vyombo vya habari na kuandikwa magazetini. Sifa nyingine ya genge hili ni kwamba walikuwa watanashati mno wakipendelea kuvaa suti na kofia nyeusi.
Januari 15 1934, Dillinger alivamia benki kuiba pesa. Katika tukio la majibizano ya risasi, Dillinger alimuua askari mmoja aliyejulikana kwa jina la William O'Malley. Yeye alipigwa risasi kadhaa japokuwa hakufa kwasababu alivaa 'bullet proof'.
Baadae, 'Dillinger Gang' walikuja kukamatwa, ambapo Dillinger alipelekwa katika gereza la *crown point* kwa kosa la kumuua Askari. Gereza hilo lilipewa jina la 'escape proof' kwakuwa lilikuwa nj ngumu kutoroka hapo. Umaarufu wake ulipelekea wananchi kufurika mahakamani na gerezani kwa ajili ya kutaka kumuona John Dillinger.
Tarehe 3 Machi 1934, John Dillinger alifanikiwa kutoroka tena katika gereza la *Crown point,* safari hii akitoroka kwa kutumia 'bunduki feki' aliyoichonga kwa kutumia mbao na kuipaka rangi nyeusi. Aliitumia bunduki hiyo kumtisha askari kisha akapora gari la askari na kutoroka nalo. Kitendo hiko kiliwafanya polisi waombe msaada kutoka *FBI* ambao walifanya msako kabambe wa kumkamata John Dillinger.
Alipotoroka, alikimbilia mjini Chicago ambako huko aliunda Genge jipya safari hii akimchukua mtu hatari aliyejulikana kama 'Baby Face Nelson'. Genge hilo liliendelea kufanya matukio mengi ya uporaji wa pesa benki na hata wizi wa silaha. Katika kipindi hiki, John Dillinger alianzisha mahusiano na binti aliyeitwa 'Polly Hamilton' mhudumu wa mgahawa pale Chicago ambaye hapo kabla alikuwa akijihusisha na ukahaba. Ifahamike kuwa kipindi yupo jela, Dillinger alitalikiana na yule mkewe.
MSAKO wa kumpata John Dillinger ulikuwa ukiendelea ambapo FBI walisambaza picha za Dillinger pamoja na kutangaza dau nono kwa yeyote atakayefanikisha upatikanaji wake. FBI walitangaza dau la dola $10,000 kwa yeyote atakayefakiwa kumkamata Dillinger na $5,000 kwa yule atakayetoa taarifa za kupatikana kwake. John Dillinger alisumbua sana vichwa vya maafisa usalama kiasi cha FBI kumtangaza kuwa *"Public Enemy Nō 1".* Ukiona hadi mtu anaitwa Public Enemy Nō 1 ujue huyo alikuwa ni 'kiboko pasua kichwa'.
John Dillinger naye hakuwa nyuma katika kuhakikisha hakamatwi. Unajua alifanyaje??.
Aliamua kufanya operesheni ya uso *"plastic surgery"* ili kubadilisha muonekano wa sura yake. Pia alifanya uperesheni ya kubadilisha alama za vidole yaani 'finger prints'.
Mkuu wa FBI bwana J. Edgar Hoover alimteua bwana Samuel Cowley kuongoza misheni ya kumkamata John Dillinger. Cowley naye aliungana na Afisa *Mervin Purvis* kutoka mjini Chicago. Kwa pamoja walishirikiana na polisi kuhakikisha huyu 'Adui namba moja' anapatikana.
Ilikuwa ni siku ya tarehe 21 Julai 1934 ambapo maafisa usalama walipokea simu kutoka kwa mwanadada mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Anna. Binti huyu alitoa taarifa za siri kwamba 'kesho jioni, yeye, John Dillinger pamoja na mpenzi wake, Polly Hamilton, wataenda kuangalia filamu kwenye moja ya majumba ya sinema, akaeleza kwamba watachagua kwenda aidha Biograph Theater au Marbo Theater. Na wakapanga kwamba atavaa vazi la rangi nyekundu ili iwe rahisi kwa maofisa hao kumtambua.
Ilipofika kesho yake, maofisa wakampigia simu Anna Sage ili 'ku-comfirm' ni wapi wataenda kati ya Biograph au Marbo??. Lakini kwakua Anna alikuwa bado hajui ni wapi haswa wataenda, tuliona maofisa usalama wakiongozwa na Marvin Purvis wakijigawa kwenda 'kukava' sehemu zote mbili.
Hatimaye ilipofika majira ya saa 2:30 usiku, Anna, John Dillinger pamoja na Polly Hamilton, walionekana wakiingia kwenye jumba la sinema la *Biograph Theater*. Baada ya kina Dillinger kuingia, tukaona wale maofisa wengine waliokuwepo kule 'Marbo Theater' wakiwasili haraka pale 'Biograph Theater' kwa ajili ya kuongeza nguvu.
Saa 4:30 usiku, baada ya filamu kumalizika, alionekana John Dillinger akiwa na wale warembo wake wawili, mmoja kulia mwingine kushoto, wakiwa wanatoka nje. Wakati wanakuja usawa wa aliposimama ofisa Purvis. Purvis aliwasha sigara yake kama ishara ya wale wenzake kusogea jirani. Wakati anafanya hivyo, kumbe Dillinger alikuwa *'ameshahisi hali ya hatari',* akatoa bastola yake huku akijihami kwa kujaribu kukimbia.
Lakini kabla hajafika mbali, risasi tatu zilifika kwenye mwili wa John Dillinger. Risasi moja ikipenya upande wa nyuma wa shingo na kutokezea kwenye sikio. Dakika chache zilizofuata, hospitali ya Alexian Brothers ilitangaza kifo cha John Dillinger. Na hiyo ndio ikawa mwisho wa mtukutu huyu ambaye alifariki tarehe kama ya leo *22 Julai 1934.* Baada ya kuenea taarifa za kifo chake watu wengi walifurika eneo la tukio angalau waweze kuuona mwili wa John Dillinger.
****
Lakini nafahamu utakuwa unajiuliza yule mwanadada aliyetoa taarifa za siri za kurahisisha kukamatwa kwa John Dillinger ni nani na kwanini alifanya hivyo?!! Baadae nitaeleza kisa hiko. Lakini kwa sasa tuishie hapa.
Ahsante.
JAMBAZI MTUKUTU. Nchini Tanzania, kuna manju 'Dj' fulani wa muziki anayejulikana kwa jina maarufu la 'DJ JD' au kwa kirefu *'DJ John Dilinga'.* Huyu ni moja kati ya maDj wakongwe na mahiri sana tuliobahatika kuwa nao hapa nchini Tanzania. Kwa wale wapenzi na wadau wa muziki wa 'bongofleva' hususani wa miaka ya nyumanyuma kidogo, bila shaka mtakua mnamfahamu Dj huyu. Kwa muda mrefu nimekuwa nikitamani kufahamu ni kwanini anaitwa John Dilinga..nikiwa nataka kujua kama hilo ni jina lake halisi au ni 'a.k.a'. Maana ni kawaida kuona watu mbalimbali hususani walio kwenye tasnia ya burudani wakitumia majina ya ziada (a.k.a) kuliko majina yao halisi. Kitu kilichonifanya nianze na DJ JD ni baada ya kugundua kuwa leo ni tarehe 22 Julai. Tarehe ambayo ulimwengu mzima unamtaja bwana mmoja mtukutu sana, aliyewahi kusumbua vichwa vya maofisa usalama wa nchi ya Marekani, akifahamika kama *John Dillinger.* Huyu alikuwa ni moja kati ya wahuni wakubwa nchini Marekani aliyetamba sana katika miaka ya 1930 kwa kujihusisha na matukio ya kihalifu hususani uporaji wa fedha kwenye mabenki. Tofauti ni kwamba John Dilinga wa Tanzania ni DJ, wakati John Dillinger wa Marekani alikuwa ni jambazi mtukutu. Utukutu wake ulianza angali ana umri mdogo na hata aliweza kuacha shule ili kwenda kutafuta pesa!! Alianza kama mdokozi wa vitu vidogovidogo lakini tukio lake la kwanza lilikuwa ni *kuiba gari*, kisha 'kwenda misele' kwa mpenzi wake mpya. Siku chache baadae alikuja kukamatwa na mapolisi akiwa anazurula mtaani japokuwa alifanikiwa kuchoropoka na 'kutokomea kusikojulikana'. Baadae alipata kazi katika jeshi la majini 'navy', akifanya katika meli ya jeshi ya 'USS Uttah'. Baada ya miezi kadhaa John Dillinger alitoroka kazini. April 1924 akiwa hana shughuli ya kumuingizia kipato, John Dillinger alifunga ndoa na mwanadada Beryl Hovious ambapo walienda kuishi kwenye nyumba ya baba yake ambapo John Dillinger aliahidi kwamba sasa atatulia na kuacha utukutu wote. Lakini wiki chache baada ya ndoa, Dillinger alikamatwa na hata kufikishwa mahakamani kwa kosa la wizi wa kuku, "nadhani alikuwa anatafuta mboga ya kwenda kula na mkewe". Lakini kwa msaada wa Baba yake, kesi ya Dillinger iliweza kufutwa. Baadae Dillinger aliamua kutoka kwenye nyumba ya baba yake na kwenda kuishi kwenye nyumba ya wazazi wa mwanamke ambapo huko alibahatika kupata kazi kwenye duka la kuuza vifaa vya ujenzi. Akiwa huko, Dillinger alikutana na rafiki yake wa muda mrefu aitwaye *Edgar Singleton,* ambapo walipanga mikakati ya kuiba pesa. Ndipo tarehe 6 septemba 1924 waliiba pesa katika moja ya Grocery japokuwa walikamatwa na kufikishwa mahakamani ambapo John Dillinger alihukumiwa kifungo cha miaka 20 katika Gereza la "Indiana State Reformatory in Pendleton". Alipokuwa jela, alikutana na wafungwa wengine ambao walimfundisha mbinu nyingine za uhalifu mkubwa hususani uporaji wa fedha kwenye mabenki. Alitumikia kifungo chake hadi mwaka 1933 kwa paroli. Siku chache tu baada ya kutoka jela, John Dillinger alifanya uhalifu mkubwa, safari hii akivamia benki na kuiba pesa benki ingawa alikamatwa na kuhukumiwa kifungo katika gereza la Lima. Siku chache baada ya Dillinger kuingia jela, wafungwa 12 ambao baadhi yao ni rafiki zake Dillinger, waliweza kutoroka katika gereza la "Indiana State Prison". Hili ni gereza alilowahi kufungwa John Dillinger baada ya kuhamishwa toka kwenye gereza lile la awali. Miongoni mwa hao waliotoroka, ambao baadhi yao ni marafiki wa Dillinger, walifika katika gereza alilofungwa Dillinger lengo ni kumtorosha rafiki yao. Walimuua askari mmoja na kuchukua funguo kisha kufungua mlango wa selo alilomo Dillinger kisha kutoroka naye. Baada ya kutoroka, John Dillinger na wenzake walielekea mjini Chicago ambapo waliunda genge kubwa la kihalifu *Dillinger Gang*. Genge hili lilipora pesa kwenye mabenki mbalimbali, na ili kuongeza nguvu, walivamia ghala la silaha na kuiba silaha nzitonzito walizozotumia katika shughuli zao za kihalifu. Wahuni hao walitokea kupata umaarufu mkubwa pale Marekani, hususani huyu Dillinger ambaye alikuwa maarufu sana mithili ya 'nyota wa hollywood' kwani kila siku jina lake lilikuwa likitajwa kwenye vyombo vya habari na kuandikwa magazetini. Sifa nyingine ya genge hili ni kwamba walikuwa watanashati mno wakipendelea kuvaa suti na kofia nyeusi. Januari 15 1934, Dillinger alivamia benki kuiba pesa. Katika tukio la majibizano ya risasi, Dillinger alimuua askari mmoja aliyejulikana kwa jina la William O'Malley. Yeye alipigwa risasi kadhaa japokuwa hakufa kwasababu alivaa 'bullet proof'. Baadae, 'Dillinger Gang' walikuja kukamatwa, ambapo Dillinger alipelekwa katika gereza la *crown point* kwa kosa la kumuua Askari. Gereza hilo lilipewa jina la 'escape proof' kwakuwa lilikuwa nj ngumu kutoroka hapo. Umaarufu wake ulipelekea wananchi kufurika mahakamani na gerezani kwa ajili ya kutaka kumuona John Dillinger. Tarehe 3 Machi 1934, John Dillinger alifanikiwa kutoroka tena katika gereza la *Crown point,* safari hii akitoroka kwa kutumia 'bunduki feki' aliyoichonga kwa kutumia mbao na kuipaka rangi nyeusi. Aliitumia bunduki hiyo kumtisha askari kisha akapora gari la askari na kutoroka nalo. Kitendo hiko kiliwafanya polisi waombe msaada kutoka *FBI* ambao walifanya msako kabambe wa kumkamata John Dillinger. Alipotoroka, alikimbilia mjini Chicago ambako huko aliunda Genge jipya safari hii akimchukua mtu hatari aliyejulikana kama 'Baby Face Nelson'. Genge hilo liliendelea kufanya matukio mengi ya uporaji wa pesa benki na hata wizi wa silaha. Katika kipindi hiki, John Dillinger alianzisha mahusiano na binti aliyeitwa 'Polly Hamilton' mhudumu wa mgahawa pale Chicago ambaye hapo kabla alikuwa akijihusisha na ukahaba. Ifahamike kuwa kipindi yupo jela, Dillinger alitalikiana na yule mkewe. MSAKO wa kumpata John Dillinger ulikuwa ukiendelea ambapo FBI walisambaza picha za Dillinger pamoja na kutangaza dau nono kwa yeyote atakayefanikisha upatikanaji wake. FBI walitangaza dau la dola $10,000 kwa yeyote atakayefakiwa kumkamata Dillinger na $5,000 kwa yule atakayetoa taarifa za kupatikana kwake. John Dillinger alisumbua sana vichwa vya maafisa usalama kiasi cha FBI kumtangaza kuwa *"Public Enemy Nō 1".* Ukiona hadi mtu anaitwa Public Enemy Nō 1 ujue huyo alikuwa ni 'kiboko pasua kichwa'. John Dillinger naye hakuwa nyuma katika kuhakikisha hakamatwi. Unajua alifanyaje??. Aliamua kufanya operesheni ya uso *"plastic surgery"* ili kubadilisha muonekano wa sura yake. Pia alifanya uperesheni ya kubadilisha alama za vidole yaani 'finger prints'. Mkuu wa FBI bwana J. Edgar Hoover alimteua bwana Samuel Cowley kuongoza misheni ya kumkamata John Dillinger. Cowley naye aliungana na Afisa *Mervin Purvis* kutoka mjini Chicago. Kwa pamoja walishirikiana na polisi kuhakikisha huyu 'Adui namba moja' anapatikana. Ilikuwa ni siku ya tarehe 21 Julai 1934 ambapo maafisa usalama walipokea simu kutoka kwa mwanadada mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Anna. Binti huyu alitoa taarifa za siri kwamba 'kesho jioni, yeye, John Dillinger pamoja na mpenzi wake, Polly Hamilton, wataenda kuangalia filamu kwenye moja ya majumba ya sinema, akaeleza kwamba watachagua kwenda aidha Biograph Theater au Marbo Theater. Na wakapanga kwamba atavaa vazi la rangi nyekundu ili iwe rahisi kwa maofisa hao kumtambua. Ilipofika kesho yake, maofisa wakampigia simu Anna Sage ili 'ku-comfirm' ni wapi wataenda kati ya Biograph au Marbo??. Lakini kwakua Anna alikuwa bado hajui ni wapi haswa wataenda, tuliona maofisa usalama wakiongozwa na Marvin Purvis wakijigawa kwenda 'kukava' sehemu zote mbili. Hatimaye ilipofika majira ya saa 2:30 usiku, Anna, John Dillinger pamoja na Polly Hamilton, walionekana wakiingia kwenye jumba la sinema la *Biograph Theater*. Baada ya kina Dillinger kuingia, tukaona wale maofisa wengine waliokuwepo kule 'Marbo Theater' wakiwasili haraka pale 'Biograph Theater' kwa ajili ya kuongeza nguvu. Saa 4:30 usiku, baada ya filamu kumalizika, alionekana John Dillinger akiwa na wale warembo wake wawili, mmoja kulia mwingine kushoto, wakiwa wanatoka nje. Wakati wanakuja usawa wa aliposimama ofisa Purvis. Purvis aliwasha sigara yake kama ishara ya wale wenzake kusogea jirani. Wakati anafanya hivyo, kumbe Dillinger alikuwa *'ameshahisi hali ya hatari',* akatoa bastola yake huku akijihami kwa kujaribu kukimbia. Lakini kabla hajafika mbali, risasi tatu zilifika kwenye mwili wa John Dillinger. Risasi moja ikipenya upande wa nyuma wa shingo na kutokezea kwenye sikio. Dakika chache zilizofuata, hospitali ya Alexian Brothers ilitangaza kifo cha John Dillinger. Na hiyo ndio ikawa mwisho wa mtukutu huyu ambaye alifariki tarehe kama ya leo *22 Julai 1934.* Baada ya kuenea taarifa za kifo chake watu wengi walifurika eneo la tukio angalau waweze kuuona mwili wa John Dillinger. **** Lakini nafahamu utakuwa unajiuliza yule mwanadada aliyetoa taarifa za siri za kurahisisha kukamatwa kwa John Dillinger ni nani na kwanini alifanya hivyo?!! Baadae nitaeleza kisa hiko. Lakini kwa sasa tuishie hapa. Ahsante. -
Mnamo Mwaka 2006, wiki kadhaa baada ya kustaafu nafasi ya ukatibu mkuu, Kofi Annan alienda nchini Italia kwa ajili ya mapumziko.
Akiwa huko, Siku moja aliamua kutoka nje kidogo na kwenda kununua gazeti, lakini ghafla akashangaa Watu wengi wanamzonga. Lengo lao ni kutaka sahihi kutoka kwake. (Kama uonavyo nyota wa filamu au wachezaji mpira, wanavyochora sahihi zao kwenye mashati ya wafuasi).
Lakini kumbe, Watu hao walimfananisha Kofi Annan na yule nyota wa filamu wa marekani bwana Morgan Freeman .
Ila, kwa kutotaka kuwaangusha Watu hao, Kofi Annan alichora sahihi kwa kutumia jina la Freeman.
(Angalia picha zao)
Koffi Anan, alifaliki akiwa na umri wa miaka 80 huko nchini Switzerland.
Alihudumu nafasi ya ukatibu mkuu kwanzia Mwaka 1997 hadi 2006, akiwa ndiye mwafrika mweusi wa kwanza kushika nafasi hiyo.
RIP koffi Annan.Mnamo Mwaka 2006, wiki kadhaa baada ya kustaafu nafasi ya ukatibu mkuu, Kofi Annan alienda nchini Italia kwa ajili ya mapumziko. Akiwa huko, Siku moja aliamua kutoka nje kidogo na kwenda kununua gazeti, lakini ghafla akashangaa Watu wengi wanamzonga. Lengo lao ni kutaka sahihi kutoka kwake. (Kama uonavyo nyota wa filamu au wachezaji mpira, wanavyochora sahihi zao kwenye mashati ya wafuasi). Lakini kumbe, Watu hao walimfananisha Kofi Annan na yule nyota wa filamu wa marekani bwana Morgan Freeman . Ila, kwa kutotaka kuwaangusha Watu hao, Kofi Annan alichora sahihi kwa kutumia jina la Freeman. (Angalia picha zao) Koffi Anan, alifaliki akiwa na umri wa miaka 80 huko nchini Switzerland. Alihudumu nafasi ya ukatibu mkuu kwanzia Mwaka 1997 hadi 2006, akiwa ndiye mwafrika mweusi wa kwanza kushika nafasi hiyo. RIP koffi Annan. -
MBWA ALIYEZIKWA NACHINGWEA 1950
Na Victor Richard..
Judy ni mbwa jike aliyeishi kati ya mwaka 1936 hadi Februari 17, 1950. Mbwa huyu alikuwa
akiishi melini katika meli za HMS Gnat na HMS Grasshopper ambazo zilitia nanga huko Yangtze kabla na wakati wa vita kuu ya pili ya Dunia.
Alidhihirisha uwezo wake wa kusikia ndege za maadui zilizokuwa zikiwajia na kutoa ishara kwa wanamaji waliokuwapo.
Baada ya baadhi ya wanamaji kuhamishwa kutoka meli ya Gnat na kupelekwa katika meli ya Grasshopper mwaka 1939,meli ilipelekwa Singapore na hii ni baada ya Uingereza kuamua kuingia vitani dhidi ya Ujerumani.
Judy alikuwa melini wakati wa mapambano ya Singapore ambapo alikuwapo pia wakati Grasshopper ikiwahamisha wanamaji wake kuelekea Dutch East Indies lakini ikiwa njiani meli hiyo ilizama na Judy alikaribia kupoteza maisha kutokana na kunaswa na mlolongo wa makabati yaliyoanguka, hata hivyo aliokolewa na wanamaji waliorudi melini wakitafuta masalia.
Katika kisiwa hicho kikame akiwa na wanamaji waliosalimika,Judy aliweza kutafuta vyanzo
vya maji safi vilivyowasaidia wote. Baadae walifanya safari kuelekea Singkep,Dutch East India na kisha Sumatra kwa lengo la kutengeneza namna ya kuyaokoa majeshi ya Uingereza.
Baada ya safari ngumu iliyokatisha maili 200 za pori kwa wiki tano wakati ambapo pia Judy alinusurika kuuawa na mamba, wanamaji waliwasili siku moja baada ya meli ya mwisho kuondoka na hivyo kuangukia kwenye mikono ya wajapani na kufanywa wafungwa wa kivita, Judy akiwa miongoni mwa wafungwa hao.
Judy alihamishwa kinyemela na kupelekwa kambi ya Medan ambako alikutana kwa mara ya kwanza na kiongozi mwandamizi wa Jeshi la anga anayeitwa Frank Williams ambaye aliishi naye kwa kipindi chote kilichosalia cha maisha yake.
Williams alimshawishi Kamanda wa kikosi kumsajili Judy kama mfungwa wa kivita akipatiwa namba ‘81A Gloergoer Medan’.Judy alikuwa ni mbwa pekee aliyesajiliwa kama mfungwa wa kivita katika Vita kuu ya pili ya Dunia.
Judy alizunguuka katika kambi kadhaa,akisalimika/nusulika kifo baada ya meli ya mizigo ya SS Van Warwyck kuzama ambapo kipindi kifupi baadae aliweza kuwaokoa abiria katika meli iliyokuwa ikizama.
Les Searly kutoka katika meli ya Grasshopper ilimuiba tena Judy na kumpeleka katika kambi nyingine ambako aliungana tena na Frank Williams.
Baada ya Vita ya pili ya Dunia kuisha,maisha ya Judy yalikuwa hatarini kwa mara nyingine..........
MBWA ALIYEZIKWA NACHINGWEA 1950 Na Victor Richard.. Judy ni mbwa jike aliyeishi kati ya mwaka 1936 hadi Februari 17, 1950. Mbwa huyu alikuwa akiishi melini katika meli za HMS Gnat na HMS Grasshopper ambazo zilitia nanga huko Yangtze kabla na wakati wa vita kuu ya pili ya Dunia. Alidhihirisha uwezo wake wa kusikia ndege za maadui zilizokuwa zikiwajia na kutoa ishara kwa wanamaji waliokuwapo. Baada ya baadhi ya wanamaji kuhamishwa kutoka meli ya Gnat na kupelekwa katika meli ya Grasshopper mwaka 1939,meli ilipelekwa Singapore na hii ni baada ya Uingereza kuamua kuingia vitani dhidi ya Ujerumani. Judy alikuwa melini wakati wa mapambano ya Singapore ambapo alikuwapo pia wakati Grasshopper ikiwahamisha wanamaji wake kuelekea Dutch East Indies lakini ikiwa njiani meli hiyo ilizama na Judy alikaribia kupoteza maisha kutokana na kunaswa na mlolongo wa makabati yaliyoanguka, hata hivyo aliokolewa na wanamaji waliorudi melini wakitafuta masalia. Katika kisiwa hicho kikame akiwa na wanamaji waliosalimika,Judy aliweza kutafuta vyanzo vya maji safi vilivyowasaidia wote. Baadae walifanya safari kuelekea Singkep,Dutch East India na kisha Sumatra kwa lengo la kutengeneza namna ya kuyaokoa majeshi ya Uingereza. Baada ya safari ngumu iliyokatisha maili 200 za pori kwa wiki tano wakati ambapo pia Judy alinusurika kuuawa na mamba, wanamaji waliwasili siku moja baada ya meli ya mwisho kuondoka na hivyo kuangukia kwenye mikono ya wajapani na kufanywa wafungwa wa kivita, Judy akiwa miongoni mwa wafungwa hao. Judy alihamishwa kinyemela na kupelekwa kambi ya Medan ambako alikutana kwa mara ya kwanza na kiongozi mwandamizi wa Jeshi la anga anayeitwa Frank Williams ambaye aliishi naye kwa kipindi chote kilichosalia cha maisha yake. Williams alimshawishi Kamanda wa kikosi kumsajili Judy kama mfungwa wa kivita akipatiwa namba ‘81A Gloergoer Medan’.Judy alikuwa ni mbwa pekee aliyesajiliwa kama mfungwa wa kivita katika Vita kuu ya pili ya Dunia. Judy alizunguuka katika kambi kadhaa,akisalimika/nusulika kifo baada ya meli ya mizigo ya SS Van Warwyck kuzama ambapo kipindi kifupi baadae aliweza kuwaokoa abiria katika meli iliyokuwa ikizama. Les Searly kutoka katika meli ya Grasshopper ilimuiba tena Judy na kumpeleka katika kambi nyingine ambako aliungana tena na Frank Williams. Baada ya Vita ya pili ya Dunia kuisha,maisha ya Judy yalikuwa hatarini kwa mara nyingine.......... -
#FAHAMU
"ALCATRAZ" GEREZA HATARI ZAIDI KUWAHI KUTOKEA ULIMWENGUNI.
Alcatraz lilikuwa gereza hatari na maarufu zaidi Nchini Marekani. Hapa ndipo nyumbani kwa watukutu walioshindikana wa Marekani miaka hiyo.
Alcatraz inapatikana katika jimbo la California kwenye kisiwa cha Alcatraz. Lilifunguliwa rasmi mwaka 1934 hadi mwaka 1935 tayari lilikuwa na wafungwa 242. Gereza hili lilifungwa rasmi tarehe 21 March 1963 hivyo lilidumu kwa miaka 29 tu.
Mambo yaliolifanya gereza hili kuwa maarufu zaidi ulimwenguni ni yafuatayo:
(A). Aina ya watuhumiwa waliopatikana humu
(B). Lilikuwa likizungukwa na bahari, pia ulinzi usiokifani.
(C). Mazingira na maisha ndani ya gereza lenyewe yalikuwa tatanishi yenye kuhitaji roho ngumu kuyavumilia.
HAWA NI BAADHI YA WATEMI WALIOWAHI KUFUNGWA GEREZA HILI.
I). George Kelly.
Huyu mtemi alifahamika kwa jina "The Machine Gun" alipewa jina hili kutokana na utundu wake kwenye zana hii wakati wa utekelezaji uhalifu wake. Huyu alikuwa kiongozi wa kundi la mamafia wa wizi wa mabenki na utekaji. Alifungwa gerezani humu baada ya kumteka mfanyabiashara tajiri wa kutupwa bwana Charles F. Urschek na kujipatia kiasi cha dollars 200,0000.
(II). Alivin Fransis Karps.
Mbabe huyu alikuwa kiongizi wa kundi lililoitwa "barber-Karpis" mbishi huyu pekee ndiye mfungwa aliyekaa miaka mingi katika gereza hili kwa miaka 26.
Alcatraz ilikuwa limegawanywa katika blocks nne, block A, B, C na D, chumba cha Mkuu was Gereza, chumba ya wageni, Maktaba na Saluni ya kunyolea wafungwa, huku block "D" likiwa ndio block hatari zaidi kwa msoto kiasi kwamba pamoja na uhalifu wao katika uhalifu, watukutu hawa waliligwaya sana block hili!.
Gereza lilizungushiwa uzio wa umeme. Hatari zaidi ni kwamba gereza lilijengwa kwenye kisiwa kilichozungukwa na maji ya baridi mno pande zote huku yakiwa na mkondo mkali sana.
Mazingira haya ndio yaliyolifanya gereza hili kuwa la kipekee na kuaminika kuwa gumu kuliko yote kwa mfungwa kutoroka.
Watemi waliopata kupitia ndani ya Alcatraz mara kadhaa walinukuniliwa wakisema
"haikuwa sehemu salama kwa kiumbe chochote kilichoumbwa na Mungu kuishi", kulikuwa na ukatili na maisha magumu sana, watemi walipata shuruba Kali kutoka kwa walinzi lakini wao kwa wao walifanyiana ukatili mkubwa mno. Mfungwa "Edward Wulke" ni mmoja wa watukutu aliyekutana na ukatili humo ndani, huyu alikatwa mikono yake kwa shoka na baadae alikuja kujinyonga.
Mazingira yalikuwa machafu mno kama inavyofahamika magerezani, kazi ngumu kwa muda mrefu huku likiwa ni kawaida sana kupitisha Siku tatu hadi nne bila kula.
Block "D" ndio lilikuwa kiboko yao hii ilikuwa na selo zilizochimbwa shimo, yaani ukiingizwa humu lazima uzame kwenye maji kama usiposimama. Pia humu kulikuwa hakuna umeme na kulikuwa na baridi Kali sana, huku wafungwa wanakuwa nusu uchi. Vitanda kamwe havikuwa vikipatikana ndani ya block D, wafungwa walitembea peku peku, harufu mbaya ilikuwa nyumbani kwake!
Mmoja wa watu waliopata kuishi anakili kwamba Alcatraz ilikuwa ni kama jehanum na kama wangepewa nafasi ya kuchagua kuishi humo na kifo basi wangechagua kifo.
Kiufupi watukutu hawa walikuwa ni kama wafu walio hai, hadi hapo walikuwa na wazo moja tu, kutoroka Au uendelee kuwa maiti inayoishi Alcatraz.
Ndani ya miaka 29 ya uhai wa gereza hili, yalifanyika majaribio zaidi ya 14 yakihusisha watu 46, kati ya hapo wawili walikufa maji, sita walipigwa risasi, 23 walikamatwa na watatu hawajulikani walipo hadi sasa!.
Mtu wa kwanza kujaribu aliitwa Joseph Bowers juhudi zake ziliishia mikononi kwa walinzi, walipigwa risasi baada ya kugoma kutii amri ya kujisalimisha.
Baaadae Theodore Cole na Raph Rae walikuja kufanikiwa kutoroka baada ya kukata nondo ya dirisha lakini wakafia majini kutokana na baridi kali.
June 11 mwaka 1962 wabishi watatu, Frank Morris, John Anglin na Clearance Anglin walifanikiwa kuvunja mwiko wa gereza hili kwa wafungwa kushindwa kutoroka. Hawa walikuwa wakiishi kwenye sello ndani ya block "B" ambako pembeni ya sello yao lilikuwa na korido isiyolindwa, walichofanya ni kutoboa tundu kuunganisha selo yao na korido, shughuli ilifanywa kwa kutumia vijiko na drill walizochomoa kwenye mota ya cleaner, na walifanya kazi hiyo pindi unapopigwa mziki ili kuepuka kusikika wakichimba. Baadae waliondoa feni kwenye roof, na kuweka nondo ambazo ziliacha uwazi wa kupita. Hapa walitumia faida ya korido kutokuwa na walinzi na kuwa sehemu yenye giza, siku ya kutoroka walitengeneza vinyago walivyovivika nywele na kuviweka sehemu wanazolala ili kuwapoteza walinzi.
Baada ya tukio hili FBI walifanya upepelezi kwa muda wa miaka 7 hadi mwaka 1969 walipofunga kesi hii bila kuwa wameona miili ya hawa jamaa wala kujua walipo, wakaamua kuhitimisha kwamba jamaa walikufa maji!.
Hadi sasa kuna utata juu ya hilo, kwani wapo wanaodai watukutu hawa walifanikiwa kutoroka salama na wamekuwa wakiwasiliana na ndugu zao na kwamba walishawahi baadhi yao kuonekana Rio de Janeiro Brazil.
JE HILI UNAWEZA UKALIFANANISHA NA GEREZA LIPI LA TANZANIA.#FAHAMU "ALCATRAZ" GEREZA HATARI ZAIDI KUWAHI KUTOKEA ULIMWENGUNI. Alcatraz lilikuwa gereza hatari na maarufu zaidi Nchini Marekani. Hapa ndipo nyumbani kwa watukutu walioshindikana wa Marekani miaka hiyo. Alcatraz inapatikana katika jimbo la California kwenye kisiwa cha Alcatraz. Lilifunguliwa rasmi mwaka 1934 hadi mwaka 1935 tayari lilikuwa na wafungwa 242. Gereza hili lilifungwa rasmi tarehe 21 March 1963 hivyo lilidumu kwa miaka 29 tu. Mambo yaliolifanya gereza hili kuwa maarufu zaidi ulimwenguni ni yafuatayo: (A). Aina ya watuhumiwa waliopatikana humu (B). Lilikuwa likizungukwa na bahari, pia ulinzi usiokifani. (C). Mazingira na maisha ndani ya gereza lenyewe yalikuwa tatanishi yenye kuhitaji roho ngumu kuyavumilia. HAWA NI BAADHI YA WATEMI WALIOWAHI KUFUNGWA GEREZA HILI. I). George Kelly. Huyu mtemi alifahamika kwa jina "The Machine Gun" alipewa jina hili kutokana na utundu wake kwenye zana hii wakati wa utekelezaji uhalifu wake. Huyu alikuwa kiongozi wa kundi la mamafia wa wizi wa mabenki na utekaji. Alifungwa gerezani humu baada ya kumteka mfanyabiashara tajiri wa kutupwa bwana Charles F. Urschek na kujipatia kiasi cha dollars 200,0000. (II). Alivin Fransis Karps. Mbabe huyu alikuwa kiongizi wa kundi lililoitwa "barber-Karpis" mbishi huyu pekee ndiye mfungwa aliyekaa miaka mingi katika gereza hili kwa miaka 26. Alcatraz ilikuwa limegawanywa katika blocks nne, block A, B, C na D, chumba cha Mkuu was Gereza, chumba ya wageni, Maktaba na Saluni ya kunyolea wafungwa, huku block "D" likiwa ndio block hatari zaidi kwa msoto kiasi kwamba pamoja na uhalifu wao katika uhalifu, watukutu hawa waliligwaya sana block hili!. Gereza lilizungushiwa uzio wa umeme. Hatari zaidi ni kwamba gereza lilijengwa kwenye kisiwa kilichozungukwa na maji ya baridi mno pande zote huku yakiwa na mkondo mkali sana. Mazingira haya ndio yaliyolifanya gereza hili kuwa la kipekee na kuaminika kuwa gumu kuliko yote kwa mfungwa kutoroka. Watemi waliopata kupitia ndani ya Alcatraz mara kadhaa walinukuniliwa wakisema "haikuwa sehemu salama kwa kiumbe chochote kilichoumbwa na Mungu kuishi", kulikuwa na ukatili na maisha magumu sana, watemi walipata shuruba Kali kutoka kwa walinzi lakini wao kwa wao walifanyiana ukatili mkubwa mno. Mfungwa "Edward Wulke" ni mmoja wa watukutu aliyekutana na ukatili humo ndani, huyu alikatwa mikono yake kwa shoka na baadae alikuja kujinyonga. Mazingira yalikuwa machafu mno kama inavyofahamika magerezani, kazi ngumu kwa muda mrefu huku likiwa ni kawaida sana kupitisha Siku tatu hadi nne bila kula. Block "D" ndio lilikuwa kiboko yao hii ilikuwa na selo zilizochimbwa shimo, yaani ukiingizwa humu lazima uzame kwenye maji kama usiposimama. Pia humu kulikuwa hakuna umeme na kulikuwa na baridi Kali sana, huku wafungwa wanakuwa nusu uchi. Vitanda kamwe havikuwa vikipatikana ndani ya block D, wafungwa walitembea peku peku, harufu mbaya ilikuwa nyumbani kwake! Mmoja wa watu waliopata kuishi anakili kwamba Alcatraz ilikuwa ni kama jehanum na kama wangepewa nafasi ya kuchagua kuishi humo na kifo basi wangechagua kifo. Kiufupi watukutu hawa walikuwa ni kama wafu walio hai, hadi hapo walikuwa na wazo moja tu, kutoroka Au uendelee kuwa maiti inayoishi Alcatraz. Ndani ya miaka 29 ya uhai wa gereza hili, yalifanyika majaribio zaidi ya 14 yakihusisha watu 46, kati ya hapo wawili walikufa maji, sita walipigwa risasi, 23 walikamatwa na watatu hawajulikani walipo hadi sasa!. Mtu wa kwanza kujaribu aliitwa Joseph Bowers juhudi zake ziliishia mikononi kwa walinzi, walipigwa risasi baada ya kugoma kutii amri ya kujisalimisha. Baaadae Theodore Cole na Raph Rae walikuja kufanikiwa kutoroka baada ya kukata nondo ya dirisha lakini wakafia majini kutokana na baridi kali. June 11 mwaka 1962 wabishi watatu, Frank Morris, John Anglin na Clearance Anglin walifanikiwa kuvunja mwiko wa gereza hili kwa wafungwa kushindwa kutoroka. Hawa walikuwa wakiishi kwenye sello ndani ya block "B" ambako pembeni ya sello yao lilikuwa na korido isiyolindwa, walichofanya ni kutoboa tundu kuunganisha selo yao na korido, shughuli ilifanywa kwa kutumia vijiko na drill walizochomoa kwenye mota ya cleaner, na walifanya kazi hiyo pindi unapopigwa mziki ili kuepuka kusikika wakichimba. Baadae waliondoa feni kwenye roof, na kuweka nondo ambazo ziliacha uwazi wa kupita. Hapa walitumia faida ya korido kutokuwa na walinzi na kuwa sehemu yenye giza, siku ya kutoroka walitengeneza vinyago walivyovivika nywele na kuviweka sehemu wanazolala ili kuwapoteza walinzi. Baada ya tukio hili FBI walifanya upepelezi kwa muda wa miaka 7 hadi mwaka 1969 walipofunga kesi hii bila kuwa wameona miili ya hawa jamaa wala kujua walipo, wakaamua kuhitimisha kwamba jamaa walikufa maji!. Hadi sasa kuna utata juu ya hilo, kwani wapo wanaodai watukutu hawa walifanikiwa kutoroka salama na wamekuwa wakiwasiliana na ndugu zao na kwamba walishawahi baadhi yao kuonekana Rio de Janeiro Brazil. JE HILI UNAWEZA UKALIFANANISHA NA GEREZA LIPI LA TANZANIA. -
Wakati wa utawala wa Rais Fernand Marcos nchini Ufilipino, miaka ya 1965 mpaka alipofurushwa Madarakani mwaka 1986 Mkewe alikuwa ni kipenzi cha Viatu na Mikufu ya dhahabu!
Imelda Marcos akiwa Mke wa Rais alikuwa na jozi za viatu vya kike zipatazo 1700 yaani alikuwa anauwezo wa kuvaa viatu bila kurudia kwa miaka 4. Mwaka 1986 Marcos alipopinduliwa mapambo ya mkewe na viatu vilihamishiwa kwenye Makumbusho ya Jiji la Marikina!
Hivi karibuni kumefanyika mnada wa viatu 420 na kupatikana kwa fedha nyingi.
Imelda anabaki katika historia kama "Mke wa Rais aliyekuwa na viatu vingi ulimwenguni"Wakati wa utawala wa Rais Fernand Marcos nchini Ufilipino, miaka ya 1965 mpaka alipofurushwa Madarakani mwaka 1986 Mkewe alikuwa ni kipenzi cha Viatu na Mikufu ya dhahabu! Imelda Marcos akiwa Mke wa Rais alikuwa na jozi za viatu vya kike zipatazo 1700 yaani alikuwa anauwezo wa kuvaa viatu bila kurudia kwa miaka 4. Mwaka 1986 Marcos alipopinduliwa mapambo ya mkewe na viatu vilihamishiwa kwenye Makumbusho ya Jiji la Marikina! Hivi karibuni kumefanyika mnada wa viatu 420 na kupatikana kwa fedha nyingi. Imelda anabaki katika historia kama "Mke wa Rais aliyekuwa na viatu vingi ulimwenguni"