ترقية الحساب

  • TAMBUA MASHARTI YA NJIWA KABLA YA KUCHUKUA HATUA YA KUWAFUGA.

    1:Kwanza kabisa Njiwa ukiwanunua kwa mtu,sharti wawe wawili pair (dume na jike).

    2:Kama muuzaji aliwafuga kwa banda la juu,hakikisha unakowapeleka uwaandalie banda la juu,ukiwaweka banda la chini wanaondoka.

    3:Kama banda lako la chini,tafuta muuzaji mwenye banda la chini ndipo ununue vinginevyo unashauliwa uwanyonyoe manyoya na kuwafungia siku 40 kabla ya kuwafungulia.

    4:Njiwa wakiwa mbele yako usipende kuwajadili,hawapendi masimango wataondoka!.

    5:Ukifuga Njiwa nao hufatilia nyendo zako,ukiwa mlevi hawakai wanaondoka.Vurugu na kelele hawapendi.

    6:Njiwa wana nguvu kiimani,hawapendi mfugaji awe Mmbea,kugombana na majirani.Kwa sababu wakatika wa ugomvi Njiwa hukaa juu ya Paa wakisikiliza halafu huondoka na hawarudi tena.

    7:Njiwa hawapendi kuona umechinja Njiwa mwenzao mbele yao,wakiona wanahama wote kwa sababu wanahisi utawachinja.

    8:Njiwa hawapendi makelele ya kushtukiza kams honi kali,kuwarushia jiwe na miziki mikubwa.Ukifanya hayo wanahama.

    9:Njiwa akifa mmoja,huomboleza.Unashauliwa umtafute mwenza haraka kwa Njiwa anaebaki la sivyo wanaondoka/kuondoka.

    10:Hakikisha Njiwa huwachanganyi na kuku mwenye vifaranga,wakiparuliwa huondoka mazima.

    11:Njiwa wanaofugwa banda la Uani/nyuma/jikoni huzaliana haraka zaidi kwa sababu ya mazingira tulivu.

    12:Hakikisha Pakashume hawazoei kufika nyumbani kwako!.Njiwa hawapatani na Paka pori la sivyo wanahama wote!

    13:Inasemekana Njiwa ni wa pili kwa wivu baada ya Nyegele!,Nyegere anawivu sana kwa jike lake na huwa anatembea akiwa nyuma ya jike.Kama ikitokea hata jani likagusa sehemu ya uzazi wa jike,Nyegere dume huanzisha vita na jani hilo.

    #Note: Hakikisha unawafuga Njiwa wawili wawili.

    ~Tukutane siku nyingine kwa habari za kuhusu mnyama hatari sana Nyegere...
    TAMBUA MASHARTI YA NJIWA KABLA YA KUCHUKUA HATUA YA KUWAFUGA. 1:Kwanza kabisa Njiwa ukiwanunua kwa mtu,sharti wawe wawili pair (dume na jike). 2:Kama muuzaji aliwafuga kwa banda la juu,hakikisha unakowapeleka uwaandalie banda la juu,ukiwaweka banda la chini wanaondoka. 3:Kama banda lako la chini,tafuta muuzaji mwenye banda la chini ndipo ununue vinginevyo unashauliwa uwanyonyoe manyoya na kuwafungia siku 40 kabla ya kuwafungulia. 4:Njiwa wakiwa mbele yako usipende kuwajadili,hawapendi masimango wataondoka!. 5:Ukifuga Njiwa nao hufatilia nyendo zako,ukiwa mlevi hawakai wanaondoka.Vurugu na kelele hawapendi. 6:Njiwa wana nguvu kiimani,hawapendi mfugaji awe Mmbea,kugombana na majirani.Kwa sababu wakatika wa ugomvi Njiwa hukaa juu ya Paa wakisikiliza halafu huondoka na hawarudi tena. 7:Njiwa hawapendi kuona umechinja Njiwa mwenzao mbele yao,wakiona wanahama wote kwa sababu wanahisi utawachinja. 8:Njiwa hawapendi makelele ya kushtukiza kams honi kali,kuwarushia jiwe na miziki mikubwa.Ukifanya hayo wanahama. 9:Njiwa akifa mmoja,huomboleza.Unashauliwa umtafute mwenza haraka kwa Njiwa anaebaki la sivyo wanaondoka/kuondoka. 10:Hakikisha Njiwa huwachanganyi na kuku mwenye vifaranga,wakiparuliwa huondoka mazima. 11:Njiwa wanaofugwa banda la Uani/nyuma/jikoni huzaliana haraka zaidi kwa sababu ya mazingira tulivu. 12:Hakikisha Pakashume hawazoei kufika nyumbani kwako!.Njiwa hawapatani na Paka pori la sivyo wanahama wote! 13:Inasemekana Njiwa ni wa pili kwa wivu baada ya Nyegele!,Nyegere anawivu sana kwa jike lake na huwa anatembea akiwa nyuma ya jike.Kama ikitokea hata jani likagusa sehemu ya uzazi wa jike,Nyegere dume huanzisha vita na jani hilo. #Note: Hakikisha unawafuga Njiwa wawili wawili. ~Tukutane siku nyingine kwa habari za kuhusu mnyama hatari sana Nyegere...
    Like
    1
    ·15 مشاهدة
  • PICHANI anaonekana aliyekuwa kiongozi wa Ujerumani bwana Adolf Hitler akipiga saluti. Hiyo inaitwa saluti ya kinazi, au kwa kingereza *'Nazi Salute'* ambayo ilikuwa ikipigwa na wananchi wa ujerumani kama ishara ya kutoa heshima kwa kiongozi wao.

    Saluti hiyo hupigwa kwa kunyoosha mkono wa kulia mbele usawa wa uso, huku vidole vikiwa vimenyooka....Na Mara zote, saluti hiyo huenda sanjari na maneno ..'''Heil Hitler..Heil, mein Führer""..yaani "Salaam Hitler, Salaam kiongozi wangu"

    Saluti hii ilianza kutumika katika miaka ya 1930, wakati wa kipindi cha Adolf Hitler na chama chake cha *Nazi Party.* Saluti hii ilikuwa ikifanywa na raia wa wajerumani, hususani wanajeshi, katika kutoa salamu na heshima kwa Hitler pamoja na kulitukuza taifa la ujerumani.

    Tarehe 13 Julai 1933, Serikali ilitoa Agizo kuwaamuru wafanyakazi wote wa serikali ya ujerumani kutumia saluti hiyo. Pia agizo hilo liliwataka watu wote kupiga saluti hiyo wakati wa kuimba wimbo wa taifa au wimbo wa chama...Na yeyote atakayekaidi, adhabu kali itatolewa juu yake.

    Mwaka 1934, tulishuhudia kuanzishwa kwa mahakama maalumu kwa ajili ya kuwahukumu wale wanaopinga saluti hiyo. Bwana mmoja aliyejulikana kwa jina la Paul Schneider, alipokea kipigo kikali kutoka kwa wafuasi wa itikadi za kiNazi baada ya kugoma kupiga saluti hiyo. Kwa ufupi niseme kwamba saluti hiyo ilikuwa ni sehemu ya maisha ya kila siku ambapo Watu walikuwa wakisalimiana kwa saluti hiyo au kwa kutamka 'Hail Hilter'.

    Kama nilivyosema hapo awali kwamba, Saluti hii ilikuwa ikitumika wakati wa Adolf Hitler tuu, kwani baada ya kuanguka kwa utawala wake, saluti hii ilikomeshwa.

    Leo hii, ni kosa kubwa sana kutumia saluti hii. Na mtu yeyote atakayebainika kuonesha ishara hii, adhabu kali itatolewa dhidi yake. Mfano, Mwaka 2007 kuna mtu mmoja aliyeitwa Horst Mahler, alihukumiwa miezi sita jela baada ya kuonekana kutumia ishara hii.

    Pia mwaka 2013, mchezaji wa klabu ya soka ya AEK Athens FC, alifungiwa kucheza soka katika timu yake ya taifa ya Ugiriki, baada ya kutumia saluti hiyo wakati akishangilia goli aliloshinda katika mechi dhidi ya klabu ya Veria F.C.

    Naam!..Na hiyo ndio 'Nazi Salute' ambayo Mara nyingine huitwa Hitler Salute, ambayo Leo hii ni marufuku kutumika, na endapo utakamatwa umenyoosha mkono hivyo, Utapata tabu sana!!

    ***

    PICHANI anaonekana aliyekuwa kiongozi wa Ujerumani bwana Adolf Hitler akipiga saluti. Hiyo inaitwa saluti ya kinazi, au kwa kingereza *'Nazi Salute'* ambayo ilikuwa ikipigwa na wananchi wa ujerumani kama ishara ya kutoa heshima kwa kiongozi wao. Saluti hiyo hupigwa kwa kunyoosha mkono wa kulia mbele usawa wa uso, huku vidole vikiwa vimenyooka....Na Mara zote, saluti hiyo huenda sanjari na maneno ..'''Heil Hitler..Heil, mein Führer""..yaani "Salaam Hitler, Salaam kiongozi wangu" Saluti hii ilianza kutumika katika miaka ya 1930, wakati wa kipindi cha Adolf Hitler na chama chake cha *Nazi Party.* Saluti hii ilikuwa ikifanywa na raia wa wajerumani, hususani wanajeshi, katika kutoa salamu na heshima kwa Hitler pamoja na kulitukuza taifa la ujerumani. Tarehe 13 Julai 1933, Serikali ilitoa Agizo kuwaamuru wafanyakazi wote wa serikali ya ujerumani kutumia saluti hiyo. Pia agizo hilo liliwataka watu wote kupiga saluti hiyo wakati wa kuimba wimbo wa taifa au wimbo wa chama...Na yeyote atakayekaidi, adhabu kali itatolewa juu yake. Mwaka 1934, tulishuhudia kuanzishwa kwa mahakama maalumu kwa ajili ya kuwahukumu wale wanaopinga saluti hiyo. Bwana mmoja aliyejulikana kwa jina la Paul Schneider, alipokea kipigo kikali kutoka kwa wafuasi wa itikadi za kiNazi baada ya kugoma kupiga saluti hiyo. Kwa ufupi niseme kwamba saluti hiyo ilikuwa ni sehemu ya maisha ya kila siku ambapo Watu walikuwa wakisalimiana kwa saluti hiyo au kwa kutamka 'Hail Hilter'. Kama nilivyosema hapo awali kwamba, Saluti hii ilikuwa ikitumika wakati wa Adolf Hitler tuu, kwani baada ya kuanguka kwa utawala wake, saluti hii ilikomeshwa. Leo hii, ni kosa kubwa sana kutumia saluti hii. Na mtu yeyote atakayebainika kuonesha ishara hii, adhabu kali itatolewa dhidi yake. Mfano, Mwaka 2007 kuna mtu mmoja aliyeitwa Horst Mahler, alihukumiwa miezi sita jela baada ya kuonekana kutumia ishara hii. Pia mwaka 2013, mchezaji wa klabu ya soka ya AEK Athens FC, alifungiwa kucheza soka katika timu yake ya taifa ya Ugiriki, baada ya kutumia saluti hiyo wakati akishangilia goli aliloshinda katika mechi dhidi ya klabu ya Veria F.C. Naam!..Na hiyo ndio 'Nazi Salute' ambayo Mara nyingine huitwa Hitler Salute, ambayo Leo hii ni marufuku kutumika, na endapo utakamatwa umenyoosha mkono hivyo, Utapata tabu sana!! ***
    Like
    1
    ·15 مشاهدة
  • MAANA YA 'HANSARD' ZA BUNGE

    NENO "Hansard" ni maarufu sana katika shughuli za Bunge nchini Tanzania, na pia katika nchi zote za Jumuiya ya Madola (Commonwealth Countries). Hutamkwa kwa haraka, "han-sadi."

    Maana yake ni Kumbukumbu Rasmi za Majadiliano katika mijadala na hoja kati ya Wabunge na Serikali , ambayo hufanyika ndani ya Ukumbi wa Bunge la Jamhuri.

    Kimsingi, ni mtiririko wa nukuu mbalimbali za hoja za wabunge (ambao ni wawakilishi wa wananchi) na Mawaziri (ambao ni Serikali), katika mijadala yao kwa ruksa ya Spika wa Bunge.

    Ni mtiririko wa nukuu ya majadiliano ya wabunge wakati wote wa vikao vya Bunge la Jamhuri, ambapo kila baada ya vikao husika majadiliano hayo huchapishwa na huhifadhiwa kama kumbukumbu mahsusi, hususan kwa ajili ya matumizi katika kumbukumbu za historia.

    Aidha, Hansard ni jina la heshima kutokana na kazi ya mwandishi na mchapishaji wa nyaraka na vitabu wa nchini Uingereza, Thomas Curson Hansard, ambaye alikuwa mwandishi na mchapishaji wa kwanza wa kumbukumbu za Bunge la Uingereza kule Westminster, mjini London.

    Kutokana na kazi hiyo ya mwandishi huyo, Thomas Hansard, ndipo majadiliano ya wabunge wa Uingereza yakapewa jina la Hansard.

    Hiyo ni kwa vile kila baada ya vikao husika vya wabunge, majadiliano yao yalikuwa tayari yamechapishwa na kusomwa na wao wenyewe, na pia watu wengine, kuhusiana na kile kilichokuwa kinajadiliwa na wabunge ndani ya Bunge.

    PICHA: Thomas Curson Hansard, ambaye alifariki mwaka 1833 akiwa na umri wa miaka 57.
    MAANA YA 'HANSARD' ZA BUNGE NENO "Hansard" ni maarufu sana katika shughuli za Bunge nchini Tanzania, na pia katika nchi zote za Jumuiya ya Madola (Commonwealth Countries). Hutamkwa kwa haraka, "han-sadi." Maana yake ni Kumbukumbu Rasmi za Majadiliano katika mijadala na hoja kati ya Wabunge na Serikali , ambayo hufanyika ndani ya Ukumbi wa Bunge la Jamhuri. Kimsingi, ni mtiririko wa nukuu mbalimbali za hoja za wabunge (ambao ni wawakilishi wa wananchi) na Mawaziri (ambao ni Serikali), katika mijadala yao kwa ruksa ya Spika wa Bunge. Ni mtiririko wa nukuu ya majadiliano ya wabunge wakati wote wa vikao vya Bunge la Jamhuri, ambapo kila baada ya vikao husika majadiliano hayo huchapishwa na huhifadhiwa kama kumbukumbu mahsusi, hususan kwa ajili ya matumizi katika kumbukumbu za historia. Aidha, Hansard ni jina la heshima kutokana na kazi ya mwandishi na mchapishaji wa nyaraka na vitabu wa nchini Uingereza, Thomas Curson Hansard, ambaye alikuwa mwandishi na mchapishaji wa kwanza wa kumbukumbu za Bunge la Uingereza kule Westminster, mjini London. Kutokana na kazi hiyo ya mwandishi huyo, Thomas Hansard, ndipo majadiliano ya wabunge wa Uingereza yakapewa jina la Hansard. Hiyo ni kwa vile kila baada ya vikao husika vya wabunge, majadiliano yao yalikuwa tayari yamechapishwa na kusomwa na wao wenyewe, na pia watu wengine, kuhusiana na kile kilichokuwa kinajadiliwa na wabunge ndani ya Bunge. PICHA: Thomas Curson Hansard, ambaye alifariki mwaka 1833 akiwa na umri wa miaka 57.
    Like
    1
    ·15 مشاهدة
  • HISTORIA YA *MBIO ZA MARATHON*

    WATU WENGI TUMEZOEA KUANGALIA MASHINDANO YA MBIO ZA MARATHON KATIKA MICHEZO YA OLIMPIKI AU KWENGINEKO LAKINI HATUJAPATA KUFAHAMU NINI CHANZO AU HISTORIA YA MBIO HIZI.

    SASA UNGANA NAMI ILI KUJUA HISTORIA YAKE.

    Hebu fatilia kisa hiki👇🏿

    Mnamo miaka ya 490 BC, Dola ya uajemi *(Persian empire)* ikiwa chini ya mfalme Darius ilikuwa inavamia mji wa *anthens* ambao ndio makao makuu ya *ugiriki*

    Uvamizi huo ulikuja kama shambulio la kutaka kulipa kisasi kwa anthens kufuatia kitendo chao cha kuwasaidia watu wa mji wa *Ionia* waliokuwa wanataka kupindua utawala wa *Darius*(mfalme wa Persia) katika mapambano yaliyofanyika katika mji wa lade *(battle of lade)*mnamo 493BC

    Ingawa Persia waliweza kushinda vita hiyo dhidi ya watu wa ionia , Mfalme Darius wa Persia aliapa kuwaadhibu miji ya anthens na eretria kwa kitendo chao cha kuisaidia Ionia.

    Hivyo basi, mwaka 490BC, mfalme Darius alipeleka majeshi yakiongozwa na kamanda Datis, kwenda kuvamia, kuangamiza na kuteka miji ya anthens na eretria, na hatimaye kuitawala ugiriki yote.

    Persian ilivamia miji ya Aegean, kupitia cyclade na kufanikiwa kuiteka eretrea, na kuendelea kuukaribia mji wa anthen.

    Lakini walipofika mji wa marathon, majeshi ya anthens wakawa tayari wamefika eneo hilo. Na ndipo mapigano yalifanyika katika mji huo wa *marathon*

    Anthens walimtuma mtu mmoja aitwaye *Philippides* kwenda mji wa Spartan ili kuwaomba msaada wa kuongezewa nguvu dhidi ya Persian.

    *Philippides* akakimbia mojakwa moja hadi mji wa Spartans, lakini siku ile akakuta watu wa mji huo (spartan) wapo katika sherehe za kuabudu, hivyo hawakuweza kuja kuwasaidia anthens kwenye vita.

    Vita iliendelea na hatimaye anthens wakaweza kushinda vita dhidi ya Persian empire.
    *philippides* kama ilivyo kawaida yake, alivoona anthens wameshinda vita akajawa na furaha kubwa, akakimbia bila kupumzika kutoka mji wa *marathon* ambapo vita vilifanyika hadi mji wa anthens kwenda kutoa ripoti ya ushindi.

    Alipofika offisini aliingia kwa pupa pasipo kubisha hodi.
    kulikuwa na viongozi kadhaa ofisini humo.

    Phillipides akatamka maneno haya *"we have won"* (tumeshinda) na akakata roho papo hapo.

    ......

    Hivyo basi, haya mashindano ya mbio za marathon , yalianzishwa kama kumbukumbu ya shujaa *phillippides* ambaye alikimbia kutoka mji wa marathon hadi anthens.

    .....
    Mbio za kwanza za marathon zilifanyika mnamo mwaka 1896 kwenye michezo ya kwanza ya *olimpiki mpya.* -kama mtakuwa mnakumbuka vizuri nilitoa historia ya michezo ya olimpiki kwamba ilikuwa na awàmu mbili (ancients olimpic 776 BC na modern olimpik 1896.)

    Mbio hizi za marathon, zina umbali wa kilometa 40.2km
    Baada ya kufanyika marekebisho kutoka 40km.- Na huu umbali ni makadirio ya umbali kutoka mji wa marathon hadi Anthen.

    Mwisho.

    HISTORIA YA *MBIO ZA MARATHON* WATU WENGI TUMEZOEA KUANGALIA MASHINDANO YA MBIO ZA MARATHON KATIKA MICHEZO YA OLIMPIKI AU KWENGINEKO LAKINI HATUJAPATA KUFAHAMU NINI CHANZO AU HISTORIA YA MBIO HIZI. SASA UNGANA NAMI ILI KUJUA HISTORIA YAKE. Hebu fatilia kisa hiki👇🏿 Mnamo miaka ya 490 BC, Dola ya uajemi *(Persian empire)* ikiwa chini ya mfalme Darius ilikuwa inavamia mji wa *anthens* ambao ndio makao makuu ya *ugiriki* Uvamizi huo ulikuja kama shambulio la kutaka kulipa kisasi kwa anthens kufuatia kitendo chao cha kuwasaidia watu wa mji wa *Ionia* waliokuwa wanataka kupindua utawala wa *Darius*(mfalme wa Persia) katika mapambano yaliyofanyika katika mji wa lade *(battle of lade)*mnamo 493BC Ingawa Persia waliweza kushinda vita hiyo dhidi ya watu wa ionia , Mfalme Darius wa Persia aliapa kuwaadhibu miji ya anthens na eretria kwa kitendo chao cha kuisaidia Ionia. Hivyo basi, mwaka 490BC, mfalme Darius alipeleka majeshi yakiongozwa na kamanda Datis, kwenda kuvamia, kuangamiza na kuteka miji ya anthens na eretria, na hatimaye kuitawala ugiriki yote. Persian ilivamia miji ya Aegean, kupitia cyclade na kufanikiwa kuiteka eretrea, na kuendelea kuukaribia mji wa anthen. Lakini walipofika mji wa marathon, majeshi ya anthens wakawa tayari wamefika eneo hilo. Na ndipo mapigano yalifanyika katika mji huo wa *marathon* Anthens walimtuma mtu mmoja aitwaye *Philippides* kwenda mji wa Spartan ili kuwaomba msaada wa kuongezewa nguvu dhidi ya Persian. *Philippides* akakimbia mojakwa moja hadi mji wa Spartans, lakini siku ile akakuta watu wa mji huo (spartan) wapo katika sherehe za kuabudu, hivyo hawakuweza kuja kuwasaidia anthens kwenye vita. Vita iliendelea na hatimaye anthens wakaweza kushinda vita dhidi ya Persian empire. *philippides* kama ilivyo kawaida yake, alivoona anthens wameshinda vita akajawa na furaha kubwa, akakimbia bila kupumzika kutoka mji wa *marathon* ambapo vita vilifanyika hadi mji wa anthens kwenda kutoa ripoti ya ushindi. Alipofika offisini aliingia kwa pupa pasipo kubisha hodi. kulikuwa na viongozi kadhaa ofisini humo. Phillipides akatamka maneno haya *"we have won"* (tumeshinda) na akakata roho papo hapo. ...... Hivyo basi, haya mashindano ya mbio za marathon , yalianzishwa kama kumbukumbu ya shujaa *phillippides* ambaye alikimbia kutoka mji wa marathon hadi anthens. ..... Mbio za kwanza za marathon zilifanyika mnamo mwaka 1896 kwenye michezo ya kwanza ya *olimpiki mpya.* -kama mtakuwa mnakumbuka vizuri nilitoa historia ya michezo ya olimpiki kwamba ilikuwa na awàmu mbili (ancients olimpic 776 BC na modern olimpik 1896.) Mbio hizi za marathon, zina umbali wa kilometa 40.2km Baada ya kufanyika marekebisho kutoka 40km.- Na huu umbali ni makadirio ya umbali kutoka mji wa marathon hadi Anthen. Mwisho.
    Like
    1
    ·16 مشاهدة
  • : Jifunze kukaa na dhoruba zako;
    Sio kila sikio linapaswa kusikia ngurumo yako ... Asili, upweke, maombi ya kina, kufunga na kufuli juu ya kinywa changu, ilinisaidia kushinda vitu vingi ambavyo watu walinirushia ili kuniangamiza. Baadhi ya wale ambao watakuchoma kisu, pia watatuma baadhi ya watu ambao watakuja kukufariji, ili wale watoa habari wanaojifanya kuwa marafiki, wapeleke habari kuhusu hali yako ya huzuni au kuhusu hatua yako inayofuata; Kuwa na busara na hekima. Baadhi ya waliokuumiza hawana huruma; Hawakudhuru na kupumzika, badala yake wanaleta watu ambao watasikia kutoka kwako na kuripoti kwao. Mara nyingi mimi hunusurika nyakati za dhoruba na misimu katika maisha yangu, na kutoka nje nikinuka kama Rose, kwa sababu mara nyingi mimi huketi na dhoruba zangu katika maombi ya kina, na mara nyingi huwa sisemi maneno kwa kujibu mtu yeyote. Ninajua vizuri sana kwamba wengi watataka kusikia kutoka kwako, si kwa sababu wanataka kukusaidia, lakini kwa sababu wanataka kuwa na kitu dhidi yako, lakini jaribu kuwa kama Kristo, kusimama mbele yao, bila kusema neno lolote. Nilizuia ulimi wangu wakati nilipaswa kuzungumza na kutoa sikio lolote la kusikiliza. Nilimgeukia Mungu na kuzungumza naye, badala ya kuzungumza nao, kwa sababu najua vizuri sana kwamba baadhi ya sauti hizo za kufariji zinazotuzunguka, ndiyo sababu hasa ya sisi kulia na kulia bila kujizuia. Nimejifunza kwamba si kila sikio linalopaswa kusikia ngurumo kubwa wakati wa majira ya dhoruba ya maisha yangu, na si kila bega linalopatikana ambalo ninapaswa kuegemea. Ninatumia goti langu na ninawaombea wasaidizi halali wajitokeze. Jifunze kutembea hadi kwenye kanisa na kupiga magoti huko kimya. Hata ukikosa maneno, kumbuka kwamba huhitaji maneno ili kumsukuma Mungu; Anasoma moyo wako kama barua na anafanya kwa njia ambazo hukuwahi kufikiria. Jifunze kunyamaza wanapotarajia uitikie na kuongea ovyo. Wakati mwingine, tabasamu na kucheka pamoja nao, lakini usiache maombi yako Kwa Yesu kwenye Sakramenti Takatifu. Yesu alijua Yuda alikuwa akipanga njama ya kumuuza, lakini alimwita "rafiki." Dhoruba hizo za maisha zinapokuja, kumbuka kuwa hauko peke yako. Kwangu mimi, ni bora kutoweka bila kuwaeleza, kuliko wewe kuzunguka kuzungumza na kila sikio linalosikiliza. Nilijifunza kwamba watu hawana wasiwasi sana juu ya wasiwasi wako; Ndiyo, wanaweza kukusemea neno moja au mawili ya kufariji, lakini mara nyingi, hakuna anayejali sana. Ni afadhali ngurumo zingurume ukiwa katika uwepo wa Mungu, badala ya kuzunguka huku na huku ukilia kama mtoto mchanga kwa kujihurumia. Ni bora kwenda kwa Yesu katika Sakramenti Takatifu na kulia na moyo wako huko, kuliko kuchukua simu yako na kwenda Whatsapp na kuwalilia kana kwamba wao ni Mungu. Sababu kwa nini baadhi yetu bado tunazunguka katika miduara katika maisha haya ni kwa sababu hatujajifunza jinsi ya kutumia kanuni ya kuweka ngurumo katika dhoruba za maisha yetu kutoka kwa kila sikio linalosikiliza. Mwambie Mungu na ufunge kinywa chako. Ongea na mtu sahihi, lakini sio kwa kila mtu. Jifunze kukaa na dhoruba zako;

    Si kila sikio linastahili kusikia ngurumo yako ...


    Credit Albert Nwosu
    : Jifunze kukaa na dhoruba zako; Sio kila sikio linapaswa kusikia ngurumo yako ... Asili, upweke, maombi ya kina, kufunga na kufuli juu ya kinywa changu, ilinisaidia kushinda vitu vingi ambavyo watu walinirushia ili kuniangamiza. Baadhi ya wale ambao watakuchoma kisu, pia watatuma baadhi ya watu ambao watakuja kukufariji, ili wale watoa habari wanaojifanya kuwa marafiki, wapeleke habari kuhusu hali yako ya huzuni au kuhusu hatua yako inayofuata; Kuwa na busara na hekima. Baadhi ya waliokuumiza hawana huruma; Hawakudhuru na kupumzika, badala yake wanaleta watu ambao watasikia kutoka kwako na kuripoti kwao. Mara nyingi mimi hunusurika nyakati za dhoruba na misimu katika maisha yangu, na kutoka nje nikinuka kama Rose, kwa sababu mara nyingi mimi huketi na dhoruba zangu katika maombi ya kina, na mara nyingi huwa sisemi maneno kwa kujibu mtu yeyote. Ninajua vizuri sana kwamba wengi watataka kusikia kutoka kwako, si kwa sababu wanataka kukusaidia, lakini kwa sababu wanataka kuwa na kitu dhidi yako, lakini jaribu kuwa kama Kristo, kusimama mbele yao, bila kusema neno lolote. Nilizuia ulimi wangu wakati nilipaswa kuzungumza na kutoa sikio lolote la kusikiliza. Nilimgeukia Mungu na kuzungumza naye, badala ya kuzungumza nao, kwa sababu najua vizuri sana kwamba baadhi ya sauti hizo za kufariji zinazotuzunguka, ndiyo sababu hasa ya sisi kulia na kulia bila kujizuia. Nimejifunza kwamba si kila sikio linalopaswa kusikia ngurumo kubwa wakati wa majira ya dhoruba ya maisha yangu, na si kila bega linalopatikana ambalo ninapaswa kuegemea. Ninatumia goti langu na ninawaombea wasaidizi halali wajitokeze. Jifunze kutembea hadi kwenye kanisa na kupiga magoti huko kimya. Hata ukikosa maneno, kumbuka kwamba huhitaji maneno ili kumsukuma Mungu; Anasoma moyo wako kama barua na anafanya kwa njia ambazo hukuwahi kufikiria. Jifunze kunyamaza wanapotarajia uitikie na kuongea ovyo. Wakati mwingine, tabasamu na kucheka pamoja nao, lakini usiache maombi yako Kwa Yesu kwenye Sakramenti Takatifu. Yesu alijua Yuda alikuwa akipanga njama ya kumuuza, lakini alimwita "rafiki." Dhoruba hizo za maisha zinapokuja, kumbuka kuwa hauko peke yako. Kwangu mimi, ni bora kutoweka bila kuwaeleza, kuliko wewe kuzunguka kuzungumza na kila sikio linalosikiliza. Nilijifunza kwamba watu hawana wasiwasi sana juu ya wasiwasi wako; Ndiyo, wanaweza kukusemea neno moja au mawili ya kufariji, lakini mara nyingi, hakuna anayejali sana. Ni afadhali ngurumo zingurume ukiwa katika uwepo wa Mungu, badala ya kuzunguka huku na huku ukilia kama mtoto mchanga kwa kujihurumia. Ni bora kwenda kwa Yesu katika Sakramenti Takatifu na kulia na moyo wako huko, kuliko kuchukua simu yako na kwenda Whatsapp na kuwalilia kana kwamba wao ni Mungu. Sababu kwa nini baadhi yetu bado tunazunguka katika miduara katika maisha haya ni kwa sababu hatujajifunza jinsi ya kutumia kanuni ya kuweka ngurumo ⚡ katika dhoruba za maisha yetu kutoka kwa kila sikio linalosikiliza. Mwambie Mungu na ufunge kinywa chako. Ongea na mtu sahihi, lakini sio kwa kila mtu. Jifunze kukaa na dhoruba zako; Si kila sikio linastahili kusikia ngurumo yako ⚡... Credit Albert Nwosu
    Like
    Love
    2
    1 التعليقات ·10 مشاهدة
  • hello
    hello
    ·9 مشاهدة
  • Rais Samia Suluhu amempangia Balozi Dkt. Stephen John Simbachawene kuwa Balozi wa Tanzania nchini Brazil akichukua nafasi ya Prof. Adelardus Kilangi ambaye amepangiwa majukumu mengine.

    Rais Samia Suluhu amempangia Balozi Dkt. Stephen John Simbachawene kuwa Balozi wa Tanzania nchini Brazil akichukua nafasi ya Prof. Adelardus Kilangi ambaye amepangiwa majukumu mengine.
    Like
    1
    ·11 مشاهدة
  • Rais Samia Suluhu amemteua Uledi Abbas Mussa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kipindi cha pili.

    Rais Samia Suluhu amemteua Uledi Abbas Mussa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kipindi cha pili.
    Like
    1
    ·10 مشاهدة
  • Rais Samia Suluhu amemteua Jaji George Mcheche Masaju kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.

    Kabla ya uteuzi huo, Jaji Masaju alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu na Mshauri wa Rais katika masuala ya sheria.

    Rais Samia Suluhu amemteua Jaji George Mcheche Masaju kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi huo, Jaji Masaju alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu na Mshauri wa Rais katika masuala ya sheria.
    Like
    1
    ·10 مشاهدة
  • Angry
    1
    ·8 مشاهدة