SHEREHEKEENI PAMOJA SIKU YENU
Picha inaiieleza kwamba ni ya mwaka 1948, waasisi wa klabu ya Yanga wakiwa na wenzao wa Africa Sports ya Zanzibar.
Picha hii inatufundisha kwamba Muungano wa Tanganyika na Zanzibar haukuwa mwaka 1964 bali zamani sana...mwaka 1964 ulikuwa mkataba tu.
Na hata kutengana kuliletwa na wakoloni, wakaweka mipaka na kuigawana ardhi...mjerumani akachukua Bara na mwingereza akachukua Zanzibar.
Lakini kabla ya mipaka yao, hii nchi ilikuwa moja tu, na hata mji wa Dar es Salaam ulianzishwa na Sultan Majid wa Zanzibar.
Yaani aliamua tu kutoka sehemu moja ya nchi yake na kwenda kuanzisha mji sehemu nyingine ya nchi yake.
Lakini hilo lengo la andiko hili...
Lengo la kuandika hapa ni kutaka kuwakumbusha watu kwamba waliopo kwenye picha ni waasisi wa Yanga, na pia hawa ndiyo waasisi wa Simba.
Na hii ni kwa sababu walioanzisha Simba ni wale wale walioanzisha Yanga, lakini wakajitenga na wenzao.
Ni hivi
Kulikuwa na timu iliyoitwa New Young, ambayo ilianzishwa mwaka 1935 na kuanza kushiriki ligi mwaka huo huo.
Wakati huo ligi ilikuwa moja tu, ya Dar es Salaam...na Dar es Salaam yenyewe ilikuwa wilaya ya jimbo la Mashariki.
Hakukuwa na ligi nyingine yoyote nchini, japo miaka michache baadaye wilaya zingine nazo zikaanzisha ligi...ikianza wilaya ya Iringa. Stori yake itakuja siku nyingine.
Ligi ya Dar es Salaam ambayo ilianza 1929 ikiwa na daraja moja tu, la kwanza...ilikua na kuongeza daraja la pili kwenye miaka ya 1930.
Kwa hiyo New Young ilipojiunga na ligi mwaka 1935, ikaanzia daraja la pili.
Ikashinda ubingwa na kupanda daraja la kwanza, mwaka 1936. Hata hivyo ilicheza ligi kwa mtindo wa VIEW ONCE kwani ilishuka mwaka huo huo.
Kushuka kwao ndiko kulikoleta mpasuko na wengine kujitenga.
Waliojitenga ndiyo hawa ambao sasa ni Simba, na waliobaki wakabadili jina kutoka New Young na kujiita Young Africans ambao ndiyo Yanga.
Lakini hawa watu walikuwa pamoja mwaka mmoja tu uliopita...na ndiyo waliopo kwenye picha hii.
Kwa hiyo leo inatakiwa hii sherehe iwe yao wote! Happy Birthday Yanga na Simba. Furahieni siku yenu kwa amani. Sisi tunajua nyinyi ni ndugu ila mnatuzuga tu!
(Zakazakazi )

(Zakazakazi 鉁嶏笍)