• Rais wa Nchi ya Liberia , Joseph Boakai amewasimamisha kazi zaidi ya Maafisa 450 wa Serikali yake akiwemo Waziri anayesimamia bajeti pamoja na Mabalozi kwa kushindwa kutangaza mali zao ndani ya muda uliowekwa. Uamuzi huo unafuatia agizo la Rais huyo lililotolewa Novemba 27, 2024, ambalo lilitoa muda wa nyongeza wa siku kumi (10) kwa Maafisa hao kutekeleza agizo hilo lakini wakashindwa kufanya hivyo.

    Maafisa hao wamesimamishwa kazi kwa muda wa mwezi mmoja bila mshahara au hadi watakapowasilisha tamko la mali zao kama inavyotakiwa.

    Rais wa Nchi ya Liberia 🇱🇷, Joseph Boakai amewasimamisha kazi zaidi ya Maafisa 450 wa Serikali yake akiwemo Waziri anayesimamia bajeti pamoja na Mabalozi kwa kushindwa kutangaza mali zao ndani ya muda uliowekwa. Uamuzi huo unafuatia agizo la Rais huyo lililotolewa Novemba 27, 2024, ambalo lilitoa muda wa nyongeza wa siku kumi (10) kwa Maafisa hao kutekeleza agizo hilo lakini wakashindwa kufanya hivyo. Maafisa hao wamesimamishwa kazi kwa muda wa mwezi mmoja bila mshahara au hadi watakapowasilisha tamko la mali zao kama inavyotakiwa.
    0 Kommentare ·0 Anteile ·487 Ansichten
  • 0 Kommentare ·0 Anteile ·153 Ansichten
  • Utani
    Utani 😂
    0 Kommentare ·0 Anteile ·179 Ansichten
  • Mtengeneza maudhui (Content Creator) kwenye mtandao wa Tiktok, Fanuel John Masamaki maarufu Zerobrainer0, ameshinda kipengele cha mtengeneza maudhui bora wa michezo kwa mwaka 2024 barani Afrika, katika tuzo zilizofanyika Februari 8, 2025 Nchini Afrika Kusini.

    Zerobrainer0 ana Wafuasi zaidi ya milioni (12) kwenye mtandao wake wa TikTok huku TikToker huyo akjizoelea umaarufu kwa maudhui yake ya kuchekekesha kwenye mchezo wa mpira wa miguu. Pia anatajwa kama ‘TikToker’ wa kuangaliwa zaidi kwa mwaka 2025.

    Mtengeneza maudhui (Content Creator) kwenye mtandao wa Tiktok, Fanuel John Masamaki maarufu Zerobrainer0, ameshinda kipengele cha mtengeneza maudhui bora wa michezo kwa mwaka 2024 barani Afrika, katika tuzo zilizofanyika Februari 8, 2025 Nchini Afrika Kusini. Zerobrainer0 ana Wafuasi zaidi ya milioni (12) kwenye mtandao wake wa TikTok huku TikToker huyo akjizoelea umaarufu kwa maudhui yake ya kuchekekesha kwenye mchezo wa mpira wa miguu. Pia anatajwa kama ‘TikToker’ wa kuangaliwa zaidi kwa mwaka 2025.
    0 Kommentare ·0 Anteile ·757 Ansichten
  • 0 Kommentare ·0 Anteile ·179 Ansichten
  • 0 Kommentare ·0 Anteile ·180 Ansichten
  • Love
    1
    · 0 Kommentare ·0 Anteile ·177 Ansichten
  • Love
    1
    · 0 Kommentare ·0 Anteile ·181 Ansichten
  • Wapiganaji wa kundi la Waasi wa M23 na Askari wanaodhaniwa kuwa ni Rwanda wameendelea kusonga mbele katika maeneo ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo . Hayo ni kwa mujibu wa vyanzo vya eneo hilo pamoja na vya mashirika ya kibinadamu. Miji iliyotekwa ni Ihusi na Kalehe, iliyoko karibu kiliomita sitini (60) kutoka Mji wa Bukavu.

    Katika taarifa, Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeitisha mkutano wa dharura wa mataifa ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kutathmini hali hiyo na "kutathmini hali na matokeo ya kitendo hiki kipya cha uchokozi", ikitoa wito wa vikwazo.

    Rais wa Burundi , Evariste Ndayishimiye amesema yeyote atakayeishambulia Nchi yake naye atashambuliwa. Wakati huo huo, Viongozi wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Nchini DR Congo na ule wa Kanisa la Kristo la DR Congo umekutana na kundi la Waasi wa M23 Mjini Goma katika juhudi za hivi karibuni kabisa za kusaka amani na mazungumzo. Walikutana na kiongozi wa kisiasa wa kundi la M23 Corneille Nangaa.
    (DW Swahili)

    Wapiganaji wa kundi la Waasi wa M23 na Askari wanaodhaniwa kuwa ni Rwanda 🇷🇼 wameendelea kusonga mbele katika maeneo ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩. Hayo ni kwa mujibu wa vyanzo vya eneo hilo pamoja na vya mashirika ya kibinadamu. Miji iliyotekwa ni Ihusi na Kalehe, iliyoko karibu kiliomita sitini (60) kutoka Mji wa Bukavu. Katika taarifa, Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeitisha mkutano wa dharura wa mataifa ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kutathmini hali hiyo na "kutathmini hali na matokeo ya kitendo hiki kipya cha uchokozi", ikitoa wito wa vikwazo. Rais wa Burundi 🇧🇮, Evariste Ndayishimiye amesema yeyote atakayeishambulia Nchi yake naye atashambuliwa. Wakati huo huo, Viongozi wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Nchini DR Congo na ule wa Kanisa la Kristo la DR Congo umekutana na kundi la Waasi wa M23 Mjini Goma katika juhudi za hivi karibuni kabisa za kusaka amani na mazungumzo. Walikutana na kiongozi wa kisiasa wa kundi la M23 Corneille Nangaa. (DW Swahili)
    Love
    1
    · 0 Kommentare ·0 Anteile ·1KB Ansichten
  • Rais wa Rwanda , Paul Kagame ameweka wazi kuwa hana hofu na vitisho vya vikwazo vinavyotolewa na Mataifa ya Magharibi dhidi ya Nchi yake akisisitiza kuwa Rwanda itachukua hatua zozote zinazohitajika kulinda maslahi yake, akizungumza na Gazeti la Jeune Afrique, Kagame amezungumzia kwa kina mzozo kati ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo pamoja na shinikizo kutoka Ulaya na Marekani .

    Kagame amesisitiza kuwa hatakubali mashinikizo yanayoelekezwa kwa Rwanda kwa lengo la kuidhoofisha akisema Nchi yake inayo haki ya kujilinda dhidi ya vitisho vyovyote vya nje ambapo Mataifa ya Magharibi yanaishutumu Rwanda kwa kuwaunga mkono kundi la Waasi wa M23 wanaopigana mashariki mwa DR Congo jambo ambalo Rwanda imekanusha mara kadhaa.

    Kauli Kagame inakuja wakati mvutano kati ya Rwanda na DR Congo ukiendelea huku mataifa ya Magharibi yakitoa wito wa mazungumzo ya amani lakini licha ya hivyo Rwanda imeendelea kusisitiza kuwa haitakubali kushinikizwa kwa njia yoyote ikibainisha kuwa hatua zake zitalenga kulinda usalama wa Taifa lake kwa gharama yoyote.
    (DW Swahili)

    Rais wa Rwanda 🇷🇼, Paul Kagame ameweka wazi kuwa hana hofu na vitisho vya vikwazo vinavyotolewa na Mataifa ya Magharibi dhidi ya Nchi yake akisisitiza kuwa Rwanda itachukua hatua zozote zinazohitajika kulinda maslahi yake, akizungumza na Gazeti la Jeune Afrique, Kagame amezungumzia kwa kina mzozo kati ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩 pamoja na shinikizo kutoka Ulaya na Marekani 🇺🇸. Kagame amesisitiza kuwa hatakubali mashinikizo yanayoelekezwa kwa Rwanda kwa lengo la kuidhoofisha akisema Nchi yake inayo haki ya kujilinda dhidi ya vitisho vyovyote vya nje ambapo Mataifa ya Magharibi yanaishutumu Rwanda kwa kuwaunga mkono kundi la Waasi wa M23 wanaopigana mashariki mwa DR Congo jambo ambalo Rwanda imekanusha mara kadhaa. Kauli Kagame inakuja wakati mvutano kati ya Rwanda na DR Congo ukiendelea huku mataifa ya Magharibi yakitoa wito wa mazungumzo ya amani lakini licha ya hivyo Rwanda imeendelea kusisitiza kuwa haitakubali kushinikizwa kwa njia yoyote ikibainisha kuwa hatua zake zitalenga kulinda usalama wa Taifa lake kwa gharama yoyote. (DW Swahili)
    Love
    1
    · 0 Kommentare ·0 Anteile ·687 Ansichten