0 Σχόλια
·0 Μοιράστηκε
·143 Views
-
-
Kikao cha mazungumzo ya kumaliza mzozo wa Nchi ya Ukraine na Nchi ya Urusi kinaendelea Nchini Saudi Arabia 🇸 ambapo Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Urusi chini ya Sergie Lavrov na Marekani chini ya Marco Rubio. Hata hivyo, Ukraine na Umoja wa Ulaya (EU) hawajashirikishwa huku Ukraine upande wake inapinga kikao hicho kuwa makubaliano yoyote haitayatambua.
Katika kusisitiza hilo Ukraine imeendelea kusisitiza kwamba itaendelea kupigana vita kwa kutegemea Ulaya sio Marekani kama mwanzo huku Rais wa Nchi hiyo Volodmiry Zelensky akisema Ukraine ni Taifa huru, hivyo haliwezi kuamuliwa mambo yake na Marekani, itautetea uhuru wake hadi tone la mwisho. Marekani imejibu kwa kusema inaitaka Ukraine irejeshe haraka deni lote la usaidizi wa vita lililotolewa na Marekani tangu Februari 2022 Oparesheni ya Urusi ilipoanza.
Kikao hiki kinachoendelea ni hatua muhimu kuelekea mkutano wa Rais Putin na Rais Trump uliopangwa mwezi Mei katika sherehe za Mashujaa wa Urusi utakaofanyika Jijini Moscow, Urusi ambapo pia mkutano huo utamwalika Rais wa China Xi Ping kama Mgeni mwalikwa muhimu.
Kikao cha mazungumzo ya kumaliza mzozo wa Nchi ya Ukraine 🇺🇦 na Nchi ya Urusi 🇷🇺 kinaendelea Nchini Saudi Arabia 🇸 ambapo Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Urusi chini ya Sergie Lavrov na Marekani 🇺🇸 chini ya Marco Rubio. Hata hivyo, Ukraine na Umoja wa Ulaya (EU) hawajashirikishwa huku Ukraine upande wake inapinga kikao hicho kuwa makubaliano yoyote haitayatambua. Katika kusisitiza hilo Ukraine imeendelea kusisitiza kwamba itaendelea kupigana vita kwa kutegemea Ulaya sio Marekani kama mwanzo huku Rais wa Nchi hiyo Volodmiry Zelensky akisema Ukraine ni Taifa huru, hivyo haliwezi kuamuliwa mambo yake na Marekani, itautetea uhuru wake hadi tone la mwisho. Marekani imejibu kwa kusema inaitaka Ukraine irejeshe haraka deni lote la usaidizi wa vita lililotolewa na Marekani tangu Februari 2022 Oparesheni ya Urusi ilipoanza. Kikao hiki kinachoendelea ni hatua muhimu kuelekea mkutano wa Rais Putin na Rais Trump uliopangwa mwezi Mei katika sherehe za Mashujaa wa Urusi utakaofanyika Jijini Moscow, Urusi ambapo pia mkutano huo utamwalika Rais wa China 🇨🇳 Xi Ping kama Mgeni mwalikwa muhimu.0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·699 Views -
Mkojo wa Sungura wageuka dhahabu Nchini Kenya.
Kumekukuwa na wimbi kubwa la mahitaji ya mkojo wa Sungura Nchini Kenya huku lita moja (1) ikiuzwa kwa Shilingi elfu moja (1,000) ambazo ni takribani Shilingi 19,885 za Kitanzania hali ambayo imepelekea Wakulima wengi kuvutiwa zaidi kuwekeza katika ufugaji wa Wanyama hao.
Sanjari na kitoweo cha Sungura kuuzwa kwa kati ya Shilingi elfu moja (1,000) na elfu elfu mbili (2,000) za Kenya (39,790 Tsh) kwa kilo, Wakulima sasa wanapata faida kutokana na mkojo wa Mnyama huyo, ambao hutumika kama mbolea ya asili na dawa ya kuua Wadudu wanaoshambulia mimea.
Mkojo wa Sungura wageuka dhahabu Nchini Kenya. Kumekukuwa na wimbi kubwa la mahitaji ya mkojo wa Sungura Nchini Kenya 🇰🇪 huku lita moja (1) ikiuzwa kwa Shilingi elfu moja (1,000) ambazo ni takribani Shilingi 19,885 za Kitanzania hali ambayo imepelekea Wakulima wengi kuvutiwa zaidi kuwekeza katika ufugaji wa Wanyama hao. Sanjari na kitoweo cha Sungura kuuzwa kwa kati ya Shilingi elfu moja (1,000) na elfu elfu mbili (2,000) za Kenya (39,790 Tsh) kwa kilo, Wakulima sasa wanapata faida kutokana na mkojo wa Mnyama huyo, ambao hutumika kama mbolea ya asili na dawa ya kuua Wadudu wanaoshambulia mimea.0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·687 Views -
"Kwa mijadala ambayo nimeitazama inaendelea baada ya mchezo wa Yanga na Singida Black Stars inaonyesha kuwa asilimia kubwa ya watu walikuwa na matokeo ya Singida kushinda kwenye mechi hiyo.
Kikawaida mwalimu anaweza kupanga kikosi kulingana na mahitaji ya mchezo husika na namna ambavyo amewasoma wapinzani na sio mchezaji bora anaweza kuanza kwenye mechi.
Kinachoendelea kwasasa ni kuzinyima uhuru hizi timu za madaraja ya chini kuamua wachezaji zitakazowatumia kwenye michezo yake dhidi ya Simba na Yanga.
Hii pia ni aina moja wapo ya kudumaza soka letu. Yanga kwenye ubora wao kila timu imepata ilichokitegemea, kila timu imevuna ilichokipanda.Ili timu isiwe imepanga matokeo lazima iifunge Yanga? Na ikifungwa tu basi imepanga matokeo?
Tuwape uhuru makocha wa kuamua nyota watakaocheza kwenye michezo husika kulingana na mbinu za wapinzani wao." - Lameck Shabahanga Mwandishi wa habari.
"Kwa mijadala ambayo nimeitazama inaendelea baada ya mchezo wa Yanga na Singida Black Stars inaonyesha kuwa asilimia kubwa ya watu walikuwa na matokeo ya Singida kushinda kwenye mechi hiyo. Kikawaida mwalimu anaweza kupanga kikosi kulingana na mahitaji ya mchezo husika na namna ambavyo amewasoma wapinzani na sio mchezaji bora anaweza kuanza kwenye mechi. Kinachoendelea kwasasa ni kuzinyima uhuru hizi timu za madaraja ya chini kuamua wachezaji zitakazowatumia kwenye michezo yake dhidi ya Simba na Yanga. Hii pia ni aina moja wapo ya kudumaza soka letu. Yanga kwenye ubora wao kila timu imepata ilichokitegemea, kila timu imevuna ilichokipanda.Ili timu isiwe imepanga matokeo lazima iifunge Yanga? Na ikifungwa tu basi imepanga matokeo? Tuwape uhuru makocha wa kuamua nyota watakaocheza kwenye michezo husika kulingana na mbinu za wapinzani wao." - Lameck Shabahanga Mwandishi wa habari.0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·798 Views -
"Watu wanaizungumza tu Singida na Yanga hata Simba kuna timu wanapata nazo fever, wakati ninachezea Azam maandalizi ya mchezo dhidi ya Yanga yalikuwa ya hali ya juu, lakini maandalizi ya mechi dhdi ya Simba yalikuwa ya kawaida ni kama maandalizi ya mechi ya Kengold" - Amri Kiemba, Mchezaji wa zamani wa klabu ya Azam FC na Mchambuzi.
"Watu wanaizungumza tu Singida na Yanga hata Simba kuna timu wanapata nazo fever, wakati ninachezea Azam maandalizi ya mchezo dhidi ya Yanga yalikuwa ya hali ya juu, lakini maandalizi ya mechi dhdi ya Simba yalikuwa ya kawaida ni kama maandalizi ya mechi ya Kengold" - Amri Kiemba, Mchezaji wa zamani wa klabu ya Azam FC na Mchambuzi.0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·409 Views -
Zakazakazi amjibu Amri Kiemba.
TUONGEE KWA FACT
Ni kweli kwamba Amri Kiemba alicheza Azam FC kwa mkopo wa miezi 6 akitokea Simba, 2014/15.
Alisajiliwa dirisha dogo lililofunguliwa Disemba 15, 2014, na walikuja wawili, yeye na Saad Kawemba kama mtendaji mku (CEO).
Akiwa Azam FC, Kiemba alikutana na mechi mbili dhidi ya Simba,
24/01/2015
Azam FC 1-1 Simba
Hii mechi ndiyo ile ambayo Aggrey Morris alimfanyia madhambi Okwi hadi akapoteza fahamu...akaenda kuzindukia hospitali.
02/05/2015
Simba 2-1 Azam FC
Hii mechi kwa asilimia kubwa iliamuliwa na kadi nyekundu ya Salum Abubakar dakika 38, na kuumia kwa Frank Domayo dakika chache baadaye.
Lakini hadi wakati huo, Azam FC ilikuwa imeushika mchezo hasa. Kipindi cha pili Simba wakapata goli, Azam FC ikiwa pungufu ikasawazisha...dakika za jioni Simba wakapata bao la pili.
Hii ilikuwa mechi ya kwanza ya Simba kuifunga Azam FC tangu Oktoba 27, 2012 kwenye ile mechi ambayo Azam FC ilisimamisha wachezaji wanne ikiwatuhumu kuihujumu timu.
Wachezaji hawa ni Agrey Morris, Erasto Nyoni, Dida na Said Morad...na walisimamishwa hadi Aprili 2013. Yaani timu ifanye maandalizi finyu halafu isimamishe wachezaji wanne kwa takribani miezi 6?
Simba baada ya kushinda mchezo huo, hawakushinda tena ndiyo hadi 2015...na 2016...tena hadi 2018.
Kuanzia 2013 hadi 2017 Simba walishinda mechi mbili tu dhidi ya Azam...halafu Kiemba anasema alikuwa haoni maandalizi...maandalizi gani?
Kama adui yako anakufa kwa asali, kwanini umpige bunduki?
Kiemba alikuwa Simba ambayo ilifungwa mfululizo na Azam FC kwa miaka mitatu...walikuwa wanajiandaaje huko?
Kiemba anaheshimika sana, lakini huu ushuhuda wake wa kupika unamvunjia heshima.
Eti maandalizi dhidi ya Yanga yalikuwa tofauti. Ok...akiwa Azam FC, Kiemba alikutana na mechi mbili dhidi ya Yanga.
28/12/2014
Yanga 2-2 Azam FC
06/05/2015
Azam FC 2-1 Yanga
Hii mechi ndiyo ile ya siku ya mvua nyingi, Yanga wameshakuwa mabingwa.
Coutinho anataka kupiga faulo, Ngassa anamnyang'anya mpira.
Kwa wanaokumbuka, wataikumbuka mechi hii.
Huu ulikuwa mchezo wa kwanza Azam FC kuifunga Yanga tangu 2013, lakini katika kipindi hicho, Simba akichomoka kwa Azam, ni sare!
Zakazakazi amjibu Amri Kiemba. TUONGEE KWA FACT Ni kweli kwamba Amri Kiemba alicheza Azam FC kwa mkopo wa miezi 6 akitokea Simba, 2014/15. Alisajiliwa dirisha dogo lililofunguliwa Disemba 15, 2014, na walikuja wawili, yeye na Saad Kawemba kama mtendaji mku (CEO). Akiwa Azam FC, Kiemba alikutana na mechi mbili dhidi ya Simba, 24/01/2015 Azam FC 1-1 Simba Hii mechi ndiyo ile ambayo Aggrey Morris alimfanyia madhambi Okwi hadi akapoteza fahamu...akaenda kuzindukia hospitali. 02/05/2015 Simba 2-1 Azam FC Hii mechi kwa asilimia kubwa iliamuliwa na kadi nyekundu ya Salum Abubakar dakika 38, na kuumia kwa Frank Domayo dakika chache baadaye. Lakini hadi wakati huo, Azam FC ilikuwa imeushika mchezo hasa. Kipindi cha pili Simba wakapata goli, Azam FC ikiwa pungufu ikasawazisha...dakika za jioni Simba wakapata bao la pili. Hii ilikuwa mechi ya kwanza ya Simba kuifunga Azam FC tangu Oktoba 27, 2012 kwenye ile mechi ambayo Azam FC ilisimamisha wachezaji wanne ikiwatuhumu kuihujumu timu. Wachezaji hawa ni Agrey Morris, Erasto Nyoni, Dida na Said Morad...na walisimamishwa hadi Aprili 2013. Yaani timu ifanye maandalizi finyu halafu isimamishe wachezaji wanne kwa takribani miezi 6? Simba baada ya kushinda mchezo huo, hawakushinda tena ndiyo hadi 2015...na 2016...tena hadi 2018. Kuanzia 2013 hadi 2017 Simba walishinda mechi mbili tu dhidi ya Azam...halafu Kiemba anasema alikuwa haoni maandalizi...maandalizi gani? Kama adui yako anakufa kwa asali, kwanini umpige bunduki? Kiemba alikuwa Simba ambayo ilifungwa mfululizo na Azam FC kwa miaka mitatu...walikuwa wanajiandaaje huko? Kiemba anaheshimika sana, lakini huu ushuhuda wake wa kupika unamvunjia heshima. Eti maandalizi dhidi ya Yanga yalikuwa tofauti. Ok...akiwa Azam FC, Kiemba alikutana na mechi mbili dhidi ya Yanga. 28/12/2014 Yanga 2-2 Azam FC 06/05/2015 Azam FC 2-1 Yanga Hii mechi ndiyo ile ya siku ya mvua nyingi, Yanga wameshakuwa mabingwa. Coutinho anataka kupiga faulo, Ngassa anamnyang'anya mpira. Kwa wanaokumbuka, wataikumbuka mechi hii. Huu ulikuwa mchezo wa kwanza Azam FC kuifunga Yanga tangu 2013, lakini katika kipindi hicho, Simba akichomoka kwa Azam, ni sare!0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·752 Views -
-
-
Zakazakazi azidi kumshushia nondo Amri Kiemba.
MUONGO!
Amri Kiemba alicheza Simba kwa misimu mitano na nusu, kuanzia 2009/10 hadi Disemba 2014.
Katika kipindi hicho, Azam FC na Simba zilikutana mara 10, Simba ikishinda mara tano na Azam FC mara tatu, na mara mbili sare...angalia picha ya pili.
Katika hizo mara tano ambazo Simba ilishinda, mbili ni za msimu wa 2009/10.
24/10/2009
Simba 1-0 Azam FC
14/3/2010
Azam FC 0-2 Simba
Huu ulikuwa msimu ambao Simba ilikuwa kwenye ubora mkubwa sana na ikamaliza ligi bila kupoteza hata mchezo mmoja.
Walishinda mechi zote za mzunguko wa kwanza, wakaja kupata sare mbili tu mzunguko wa pili, dhidi ya Kagera Sugar na African Lyon.
Kwa ubora huo, huwezi kuilamu Azam FC ilhali timu zote zilifungwa...kiungwana unawasifia Simba kwamba walikuwa kwenye ubora wa hali ya juu.
Lakini baada ya msimu huo, Azam FC na Simba zililingana matokeo hadi Kiemba alipoondoka Simba kwenda Azam FC.
Swali ni je, Kiemba anapata wapi uhalali wa kutilia shaka maandalizi yaliyoleta matokeo kama haya?
Msimu wa 2013/14, Azam FC ikawa kwenye ubora mkubwa na kumaliza ligi bila kupoteza hata mchezo mmoja, ikiwemo kushinda nje ndani dhidi ya Simba ya Kiemba na maandalizi yao ya hali ya juu.
28/10/2013
Simba 1-2 Azam FC
30/3/2014
Azam FC 2-1 Simba
Baada ya mechi hizi Kiemba akaenda Azam FC...na mechi yake ya kwanza ikaisha kwa sare ya 1-1.
Ni vipi Kiemba hakuridhika na maandalizi ya Azam FC yaliyoleta sare lakini aliridhika na maandalizi ya Simba yaliyowafanya wafungwe nje ndani msimu mmoja tu nyuma yake?
Msimu mmoja kabla Kiemba hajasajiliwa Simba, Azam FC ilishinda 2-0 na mashabiki wa Simba wakaenda kushusha kinyesi nyumbani kwa mwenyekiti wao Hassan Dalali.
Ina maana maandalizi ya Azam FC yangekuwa hafifu yangewatoa kinyesi Simba kweli?
Azam FC ilikuwa inaifunga Simba kabla yeye hajaenda, na ikaifunga akiwemo...kwa maandalizi yale yale...halafu anakuja hadharani leo, miaka zaidi ya 10 na kusema aliona maandalizi hafifu...sasa walikuwa wanashindaje kwa maandalizi hafifu?
Ni mbaya sana kumuita mtu muongo...lakini Kiemba kwenye hili itoshe tu kusema kwamba WEWE NI MUONGO!
Zakazakazi azidi kumshushia nondo Amri Kiemba. MUONGO! Amri Kiemba alicheza Simba kwa misimu mitano na nusu, kuanzia 2009/10 hadi Disemba 2014. Katika kipindi hicho, Azam FC na Simba zilikutana mara 10, Simba ikishinda mara tano na Azam FC mara tatu, na mara mbili sare...angalia picha ya pili. Katika hizo mara tano ambazo Simba ilishinda, mbili ni za msimu wa 2009/10. 24/10/2009 Simba 1-0 Azam FC 14/3/2010 Azam FC 0-2 Simba Huu ulikuwa msimu ambao Simba ilikuwa kwenye ubora mkubwa sana na ikamaliza ligi bila kupoteza hata mchezo mmoja. Walishinda mechi zote za mzunguko wa kwanza, wakaja kupata sare mbili tu mzunguko wa pili, dhidi ya Kagera Sugar na African Lyon. Kwa ubora huo, huwezi kuilamu Azam FC ilhali timu zote zilifungwa...kiungwana unawasifia Simba kwamba walikuwa kwenye ubora wa hali ya juu. Lakini baada ya msimu huo, Azam FC na Simba zililingana matokeo hadi Kiemba alipoondoka Simba kwenda Azam FC. Swali ni je, Kiemba anapata wapi uhalali wa kutilia shaka maandalizi yaliyoleta matokeo kama haya? Msimu wa 2013/14, Azam FC ikawa kwenye ubora mkubwa na kumaliza ligi bila kupoteza hata mchezo mmoja, ikiwemo kushinda nje ndani dhidi ya Simba ya Kiemba na maandalizi yao ya hali ya juu. 28/10/2013 Simba 1-2 Azam FC 30/3/2014 Azam FC 2-1 Simba Baada ya mechi hizi Kiemba akaenda Azam FC...na mechi yake ya kwanza ikaisha kwa sare ya 1-1. Ni vipi Kiemba hakuridhika na maandalizi ya Azam FC yaliyoleta sare lakini aliridhika na maandalizi ya Simba yaliyowafanya wafungwe nje ndani msimu mmoja tu nyuma yake? Msimu mmoja kabla Kiemba hajasajiliwa Simba, Azam FC ilishinda 2-0 na mashabiki wa Simba wakaenda kushusha kinyesi nyumbani kwa mwenyekiti wao Hassan Dalali. Ina maana maandalizi ya Azam FC yangekuwa hafifu yangewatoa kinyesi Simba kweli? Azam FC ilikuwa inaifunga Simba kabla yeye hajaenda, na ikaifunga akiwemo...kwa maandalizi yale yale...halafu anakuja hadharani leo, miaka zaidi ya 10 na kusema aliona maandalizi hafifu...sasa walikuwa wanashindaje kwa maandalizi hafifu? Ni mbaya sana kumuita mtu muongo...lakini Kiemba kwenye hili itoshe tu kusema kwamba WEWE NI MUONGO!0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·867 Views