Katibu Mkuu wa UN asema Afrika lazima iwe na uwawakilishi kamili kwenye meza ya Dunia.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, amesisitiza umuhimu wa bara la Afrika katika maamuzi ya kimataifa, akisisitiza kuwa bara hilo linastahili uwakilishi wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Akihutubia kwenye Mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) Mjini Addis Ababa, Guterres alisema: “Afrika lazima iwe mezani.”
Kauli hiyo inatokana na hali ya dunia iliyogawanyika na migogoro mingi, ambapo Guterres alibainisha kuwa Umoja wa Afrika ni mhimili muhimu wa ushirikiano wa kimataifa. Alisisitiza kuwa ukosefu wa uwakilishi wa kudumu wa Afrika katika Baraza la Usalama hauna msingi wa haki wala mantiki: “Huu ni mwaka 2026, si 1946.”
Aidha, Katibu Mkuu wa UN alitoa wito wa amani na utulivu katika maeneo yaliyo hatarini barani Afrika, ikiwemo Sudan na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Pia alisisitiza umuhimu wa mageuzi ya kifedha ya kimataifa na kuchukua hatua madhubuti za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, akisema: “Afrika itaendelea kuwa kipaumbele cha Umoja wa Mataifa.”
Kauli hizi zinaonesha msukumo wa Umoja wa Mataifa kushirikisha bara la Afrika kikamilifu katika maamuzi makuu ya kimataifa, huku likipatiwa nafasi sawa na mataifa mengine katika masuala ya usalama, uchumi, na mazingira.
Hii ni sehemu ya jitihada zinazoongeza msukumo wa mabadiliko ya kimfumo, na kutoa ishara kwamba dunia inatambua Afrika kama mchezaji muhimu wa kimataifa.
Toa maoni yako
#Habari

0 Comentários
0 Compartilhamentos
10 Visualizações