Waziri wa Mambo ya Ndani, Eng. Hamad Masauni amesema kuanzia July, 2023 hadi April, 2024 jumla ya vitambulisho 7,698,819 vimezalishwa na hivyo kufanya jumla ya vitambulisho vilivyozalishwa kufikia 20,578,325 sawa na asilimia 99 ya idadi ya Namba za Utambulisho 20,701,956 zilizozalishwa ambapo ametoa rai kwa Wananchi wote ambao bado hawajachukua vitambulisho vyao vya Taifa kufika katika ofisi za Serikali za Mitaa walipojiandikisha kwa ajili ya kuvichukua.
Akiwasilisha Bungeni Jijini Dodoma Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa Mwaka 2024/2025, Masauni amesema “Katika mwaka 2024/25 Shilingi bilioni 2.9 zimetengwa kwa ajili ya kusajili na kutambua Watu 2,389,290 wenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea, lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa kila Mwananchi mwenye namba ya Utambulisho Tanzania Bara na Zanzibar anapata Kitambulisho cha Taifa”
“Hadi Aprili, 2024 NIDA imeunganisha Taasisi 21 katika mfumo wa usajili na utambuzi, hivyo kufanya jumla ya taasisi zilizounganishwa kufikia 107, katika mwaka wa fedha 2024/25 jumla ya Taasisi 35 za umma na binafsi zinatarajiwa kuunganishwa katika mfumo huo ili kuwezesha ushirikishanaji wa taarifa na hivyo kuchochea shughuli za kiuchumi na kijamii, naomba nitumie fursa hii kuwahamasisha watoa huduma kujiunga na Mfumo wa NIDA ili kuwezesha upatikanaji wa taarifa sahihi za Wateja”
#MillardAyoUPDATES

4 Comments
·426 Views