*Anaandika Askofu Bagonza*
UJINGA NI MZIGO Vs UJINGA NI MTAJI
Leo 6 Julai 2024, KKKT- DAYOSISI YA KARAGWE, imehitimisha kundi la pili la watu wazima 125 katika kisomo cha watu wazima (EWW). Kundi la kwanza lilihitimishwa mwaka jana 2023. Watu wazima wasiojua Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) wanapata fursa ya kuelimishwa kupitia mradi maalum jimboni Murongo katika Tarafa ya Murongo-Kyerwa. Wahitimu wamepewa vyeti vya kuhitimu.
Mradi huu unafadhiliwa kwa ushirikiano na shirika la Bread for the World la nchini Ujerumani. Majimbo ya Murongo (Tanzania) na Gutersloh (Ujerumani) ndio watekelezaji wa mradi huu. Labda kama kuna takwimu za kipekee, lakini kwa macho yangu naona ujinga unaongezeka katila maeneo mengi ya vijijini.
Tulizoea kusema UJINGA NI MZIGO lakini kwa sasa UJINGA NI MTAJI wa makundi mbalimbali:
1. Viongozi wa Dini: Wanahitaji wajinga wengi ili wawauzie wokovu, utajiri hewa, uponyaji nk.
2. Wanasiasa: Wanahitaji wajinga wengi ili wawadanganye bila kukamatwa na wawajaze ahadi hewa.
3. Waganga wa kienyeji: Wanahitaji wajinga wengi wa kuwaletea kuku huku hao wajinga wakilishwa vinyesi na mikojo.
4. Walimu: Wanajitaji wajinga wengi ili wafanye mazoezi ya kufuta ujinga kwa kuuongeza.
5. Watumishi wa serikali wasio waaminifu: Wanahitaji wajinga wengi ili wawatoze rushwa na kuwauzia haki zao.
6. Wahisani na Wafadhili: Wanahitaji wajinga wengi ili wapate pa kupeleka misaada inayodumaza na kuwasaidia kumiliki uchumi wa wajinga.
7. Serikali: Inahitaji wajinga wengi ili waiogope. Kwa kawaida serikali huwaogopa wananchi wanaojielewa.
8. Matapeli wa Mitandaoni: wanahitaji wajinga wengi ili waweze kutajirika bila kufanya kazi.
9. Wafanya biashara: Wanahitaji wajinga wengi ili wanaoamini kuwa kuna duka la bei nafuu.
10. Umaskini na Maradhi: Wanahitajika wajinga wengi ili hawa ndugu waendelea kustawi.
Vita ya kupambana na ujinga haijaanza. Ikianza mniamshe. Hakuna kundi lisilo na mjinga. Ukichunguza kundi usimuone mjinga, tambua wewe ndiye mjinga.

1 Commentarios
·172 Views