Upgrade to Pro

Mshambuliaji Ranga Chivaviro wa Kaizer Chiefs ambaye aliwahi kuwindwa na Yanga akachomoa dakika za mwisho, amesema Yanga iliwaweka kwenye wakati mgumu ambapo nidhamu yao wakati hawana mpira ni ilikuwa kitu kigumu kwao kuweza kuhimili.

Chivaviro ambaye ana asili ya Zimbabwe, alisema walikutana na kipimo kigumu katika mchezo wa kwanza wa kirafiki tangu waanze maandalizi.

"Ilikuwa ngumu kwetu, ni kama hawakutupa nafasi ya kujipanga wakati tukiwa tuna mpira, walikuwa wanalazimisha haraka tuupoteze uwe chini yao nadhani ndio silaha waliyoitumia kutengeneza ushindi kama ule," alisema mshambuliaji huyo wa zamani wa Marumo Gallants.

"Unajua huu ulikuwa mchezo wetu wa kwanza wa kirafiki wenzetu walionekana kuwa wepesi kuliko sisi ilitufanya kuonekana hatukuwa tayari kukutana na watu kama wao, nadhani tutabadilika kwa kuwa tupo chini ya makocha wapya ambao wanaaanza kutupa falsafa mpya."
Mshambuliaji Ranga Chivaviro wa Kaizer Chiefs ambaye aliwahi kuwindwa na Yanga akachomoa dakika za mwisho, amesema Yanga iliwaweka kwenye wakati mgumu ambapo nidhamu yao wakati hawana mpira ni ilikuwa kitu kigumu kwao kuweza kuhimili. Chivaviro ambaye ana asili ya Zimbabwe, alisema walikutana na kipimo kigumu katika mchezo wa kwanza wa kirafiki tangu waanze maandalizi. "Ilikuwa ngumu kwetu, ni kama hawakutupa nafasi ya kujipanga wakati tukiwa tuna mpira, walikuwa wanalazimisha haraka tuupoteze uwe chini yao nadhani ndio silaha waliyoitumia kutengeneza ushindi kama ule," alisema mshambuliaji huyo wa zamani wa Marumo Gallants. "Unajua huu ulikuwa mchezo wetu wa kwanza wa kirafiki wenzetu walionekana kuwa wepesi kuliko sisi ilitufanya kuonekana hatukuwa tayari kukutana na watu kama wao, nadhani tutabadilika kwa kuwa tupo chini ya makocha wapya ambao wanaaanza kutupa falsafa mpya."
·236 Views