Upgrade to Pro

Moja ya kitu kinaweza kukuchosha kwenye maisha yako ni pale ambapo kila siku unaona haupati matokeo ya unachofanya ni kama haupati mavuno unayotaka, watu wengi sana wamekata tamaa wanapopitia hali hii ndio maana Robert Louis Stevenson aliwahi kusema “Usiitathmini siku yako kwa MAVUNO unayovuna Bali kwa MBEGU ambazo UNAPANDA”(Don't judge each day by the harvest you reap but by the seeds that you plant)

Kumbuka kila siku una fursa na nafasi mpya ya kupanda kitu kwa ajili ya KESHO yako na sio kila siku utakuwa unavuna. Kuna wakati UAMINIFU wako utakuwa kama unaona hauna faida, kuna wakati BIDII yako itakuwa kama haileti tofauti, kuna wakati NIDHAMU yako itakuwa kama ni bure: Usiache kwa sababu hauoni matokeo ya nje.
kumbuka hiyo ni MBEGU kuna siku ITAOTA.

Unapokuwa MKULIMA kuna wakati watu wataona kama vile unapoteza MUDA kwa sababu mbegu ulizopanda shambani zitakuwa bado HAZIJAOTA. Usiache KUMWAGILIA kwa sababu HAZIJACHIPUA. Kumbuka kuna mambo yanachukua MUDA MFUPI na mengine yanachukua MUDA MREFU sana Kuyakamilisha.

Je, kesho unatapanda mbegu gani..?
Moja ya kitu kinaweza kukuchosha kwenye maisha yako ni pale ambapo kila siku unaona haupati matokeo ya unachofanya ni kama haupati mavuno unayotaka, watu wengi sana wamekata tamaa wanapopitia hali hii ndio maana Robert Louis Stevenson aliwahi kusema “Usiitathmini siku yako kwa MAVUNO unayovuna Bali kwa MBEGU ambazo UNAPANDA”(Don't judge each day by the harvest you reap but by the seeds that you plant) Kumbuka kila siku una fursa na nafasi mpya ya kupanda kitu kwa ajili ya KESHO yako na sio kila siku utakuwa unavuna. Kuna wakati UAMINIFU wako utakuwa kama unaona hauna faida, kuna wakati BIDII yako itakuwa kama haileti tofauti, kuna wakati NIDHAMU yako itakuwa kama ni bure: Usiache kwa sababu hauoni matokeo ya nje. kumbuka hiyo ni MBEGU kuna siku ITAOTA. Unapokuwa MKULIMA kuna wakati watu wataona kama vile unapoteza MUDA kwa sababu mbegu ulizopanda shambani zitakuwa bado HAZIJAOTA. Usiache KUMWAGILIA kwa sababu HAZIJACHIPUA. Kumbuka kuna mambo yanachukua MUDA MFUPI na mengine yanachukua MUDA MREFU sana Kuyakamilisha. Je, kesho unatapanda mbegu gani..?
·342 Views