Upgrade to Pro

Jacob alikuwa na mke aitwae Leah. Jacob tokea mwanzo hakumhitaji Leah kwa sababu tokea hapo awali Jacob alikuwa akimpenda mdogo wake na Leah aitwae Raheli.

Leah alikuwa akilifahamu hilo. Sasa imagine maumivu aliyokua anayapata ya kumtazama mume wake akimpenda mwanamke mwingine na mbaya zaidi ni mdogo wake.

Maandiko yanaeleza namna ambavyo Leah ali-expirience maumivu ya kutopendwa na Rejections kwa majina aliyowapa watoto aliozaa na Jacob.

Muda mwingine katika safari ya mahusiano tunaumizwa kwa kupenda tusipopendwa. Tunapoteza muda mwingi sana kufanya kila jambo ili kujaribu kuwafanya wale tunaowapenda watambue upendo tulio nao juu yao.

Tunajaribu kujipa moyo kwamba huenda tukiwapikia chakula kizuri, au tukiwanunulia zawadi, kuwapa pesa au kubeba ujauzito wao basi watatupenda na bahati mbaya haiwi hivyo, inauma mno.

Wakati tukipoteza muda na watu wasiotupenda, wanaotupenda wako tu pembeni wanashuhudia namna tunavyoumia mioyo kwa kupenda tusipopendwa.

Kama hataki mawasiliano na wewe au mawasiliano yako finyu ni kwamba hauko kwenye akili zake. Kama yeye anaona kwake ni sawa tu kuku-disappoint ni kwa sababu hakujali tena. Kama hafanyi jitihada zozote zile za kukaa chini na kuelewana ni kwamba haheshimu hata kdogo hisia zako na anaona unampotezea muda tu.

Ni vigumu sana kwa mtu kutamka kuwa HAKUPENDI direct hasa ukizingatia kama hapo awali mlikua mko vizuri. Utaziona dalili tu za kubadilika kwake. Huo ni ujumbe kwamba ujiongeze, sikuhitaji tena.

Mahusiano thabiti yanahusisha sana na kijitoa. Unahitaji mtu ambae atajitoa kwako kwa hali na mali. Unahitahiji kujibiwa texts zako, unahitaji kupigiwa simu, unahitaji kuonana nae na kupanga mikakati. Unahitaji kupendwa na zaidi unahitaji mahala salama pa kuegama!!

Nakutakia kila la kheri katika kukabiliana na kutibu maumivu ya moyo wa kupenda usipopendwa!

!!
Jacob alikuwa na mke aitwae Leah. Jacob tokea mwanzo hakumhitaji Leah kwa sababu tokea hapo awali Jacob alikuwa akimpenda mdogo wake na Leah aitwae Raheli. Leah alikuwa akilifahamu hilo. Sasa imagine maumivu aliyokua anayapata ya kumtazama mume wake akimpenda mwanamke mwingine na mbaya zaidi ni mdogo wake. Maandiko yanaeleza namna ambavyo Leah ali-expirience maumivu ya kutopendwa na Rejections kwa majina aliyowapa watoto aliozaa na Jacob. Muda mwingine katika safari ya mahusiano tunaumizwa kwa kupenda tusipopendwa. Tunapoteza muda mwingi sana kufanya kila jambo ili kujaribu kuwafanya wale tunaowapenda watambue upendo tulio nao juu yao. Tunajaribu kujipa moyo kwamba huenda tukiwapikia chakula kizuri, au tukiwanunulia zawadi, kuwapa pesa au kubeba ujauzito wao basi watatupenda na bahati mbaya haiwi hivyo, inauma mno. Wakati tukipoteza muda na watu wasiotupenda, wanaotupenda wako tu pembeni wanashuhudia namna tunavyoumia mioyo kwa kupenda tusipopendwa. Kama hataki mawasiliano na wewe au mawasiliano yako finyu ni kwamba hauko kwenye akili zake. Kama yeye anaona kwake ni sawa tu kuku-disappoint ni kwa sababu hakujali tena. Kama hafanyi jitihada zozote zile za kukaa chini na kuelewana ni kwamba haheshimu hata kdogo hisia zako na anaona unampotezea muda tu. Ni vigumu sana kwa mtu kutamka kuwa HAKUPENDI direct hasa ukizingatia kama hapo awali mlikua mko vizuri. Utaziona dalili tu za kubadilika kwake. Huo ni ujumbe kwamba ujiongeze, sikuhitaji tena. Mahusiano thabiti yanahusisha sana na kijitoa. Unahitaji mtu ambae atajitoa kwako kwa hali na mali. Unahitahiji kujibiwa texts zako, unahitaji kupigiwa simu, unahitaji kuonana nae na kupanga mikakati. Unahitaji kupendwa na zaidi unahitaji mahala salama pa kuegama!! Nakutakia kila la kheri katika kukabiliana na kutibu maumivu ya moyo wa kupenda usipopendwa! 🔥🔥🔥🍹🍹🍹!!
·108 Views