Upgrade to Pro

Katika historia ya Muziki wa Bongo fleva, maisha ya Diamond Platinumz, Rich Mavoco na Harmonize matukio ya wasanii hawa kufanya kazi pamoja na kutengeneza moments zilizowaaminisha wananchi kwamba ushirikiano wao utadumu muda mrefu alafu wakapishana ghafla na kupelekana hadi Basata aisee ni katika mambo yaliotengeneza pressure kubwa baina yao na hata mitaani.

Maranyingi nimekua nikimtaja Harmonize kama msanii aliotoka WCB na kufanikiwa kutengeneza mianya mingi ya biashara na mafanikio nje ya WCB tofauti na ilivyokua ikizungumzwa na wengi.

Rich Mavoco nimemvulia kofia kwa sababu ni ngumu sana msanii kupitia mapito yake alafu akafanikiwa kurudi kwenye game na kua na nguvu kama ambayo anayo lakini umewahi kufikiria upande wa Diamond Platinumz ambae ali invest kuwapa thamani zaidi wasanii hawa na baadae akawapoteza katika mazingira ambayo naamini kabisa hata yeye hakua tayari.

Kuna tetesi kwamba Harmonize alikua na migogoro na Sallam SK kabla hajaondoka WCB na CEO alijikuta kaekwa kwenye kona ambayo ilimlazimu afanye maamuzi magumu la sivyo mambo yangezidi kuharibika. Nimeshuhudia wasanii wengi wakiua lebo zao kutokana na migogoro kama hio lakini pia wadau wengi wameachana na biashara ya muziki kutokana na sintofahamu nyingi zilizopo ndani ya Game.

Upande wa Diamond Platinumz ni tofauti kidogo, pamoja na drama zote anazopitia bado lebo yake ipo imara na wasanii waliobaki kama Mbosso, Zuchu, Lavalava na D Voice wanafanya vizuri kila mtu kwa nafasi yake.

Kwa kijana kutoka Tandale kuana uvumilivu, mbinu na mipango ya kukabiliana na changamoto zote alizokumbana nazo Diamond Platinumz anastahili pongezi maana inaonesha ukomavu wake na weledi mkubwa alionao kwenye field anayojihusisha nayo.
(Jr Junior)

Katika historia ya Muziki wa Bongo fleva, maisha ya Diamond Platinumz, Rich Mavoco na Harmonize matukio ya wasanii hawa kufanya kazi pamoja na kutengeneza moments zilizowaaminisha wananchi kwamba ushirikiano wao utadumu muda mrefu alafu wakapishana ghafla na kupelekana hadi Basata aisee ni katika mambo yaliotengeneza pressure kubwa baina yao na hata mitaani. Maranyingi nimekua nikimtaja Harmonize kama msanii aliotoka WCB na kufanikiwa kutengeneza mianya mingi ya biashara na mafanikio nje ya WCB tofauti na ilivyokua ikizungumzwa na wengi. Rich Mavoco nimemvulia kofia kwa sababu ni ngumu sana msanii kupitia mapito yake alafu akafanikiwa kurudi kwenye game na kua na nguvu kama ambayo anayo lakini umewahi kufikiria upande wa Diamond Platinumz ambae ali invest kuwapa thamani zaidi wasanii hawa na baadae akawapoteza katika mazingira ambayo naamini kabisa hata yeye hakua tayari. Kuna tetesi kwamba Harmonize alikua na migogoro na Sallam SK kabla hajaondoka WCB na CEO alijikuta kaekwa kwenye kona ambayo ilimlazimu afanye maamuzi magumu la sivyo mambo yangezidi kuharibika. Nimeshuhudia wasanii wengi wakiua lebo zao kutokana na migogoro kama hio lakini pia wadau wengi wameachana na biashara ya muziki kutokana na sintofahamu nyingi zilizopo ndani ya Game. Upande wa Diamond Platinumz ni tofauti kidogo, pamoja na drama zote anazopitia bado lebo yake ipo imara na wasanii waliobaki kama Mbosso, Zuchu, Lavalava na D Voice wanafanya vizuri kila mtu kwa nafasi yake. Kwa kijana kutoka Tandale kuana uvumilivu, mbinu na mipango ya kukabiliana na changamoto zote alizokumbana nazo Diamond Platinumz anastahili pongezi maana inaonesha ukomavu wake na weledi mkubwa alionao kwenye field anayojihusisha nayo. (Jr Junior)
Like
1
·332 Views