Kikosi cha Simba kinaondoka kesho Jumatano kwenda Algeria katika mchezo wa pili wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi dhidi ya CS Constantine, huku kocha wa timu hiyo, Fadlu Davids akieleza wazi anawatambua vyema wapinzani hao. . Fadlu alisema Constantine ni timu nzuri na yenye wachezaji wazuri ingawa jopo la benchi lao la ufundi lilianza kuwafuatia kwa ukaribu na kugundua wana muunganiko mzuri, kuanzia katikati ya kiwanja hadi ushambuliaji. . “Ni timu nzuri ndio maana hata ukiangalia mchezo wao wa kwanza walipata pia ushindi tena ugenini, hii inaonyesha wazi sio rahisi kwetu na tunapaswa kujipanga vizuri ili kuendeleza rekodi nzuri ambayo tumeanza nayo nyumbani,” . Constantine inayonolewa na Kocha Mkuu, Kheireddine Madoui inaongoza Ligi Kuu ya Algeria ikiwa imecheza michezo 11, imeshinda mitano, sare nne na kupoteza miwili ikiongoza msimamo kwa pointi 19.
#paulswai

·204 Views