Обновить до Про

FADLU NI KOCHA WA KISASA HANA KIKOSI CHA KWANZA.

Nimemnukuu mchambuzi na mtangazaji mahari wa kabumbu nchini Nazareth Upete kupitia kipindi cha Bao la Asubuhi, amesema makocha wengi wa kisasa Duniani hawana First Eleven yaani kikosi cha kwanza.

Hili linaangukia kwa kocha mkuu wa klabu ya Simba Fadlu Davids, ambaye amekuwa hatabiriki katika kikosi chake cha kwanza huku watu wengi wakionekana kutoelewa namna anavyobadilisha wachezaji wake wa kikosi cha kwanza.

Upete pia aliendelea kusema, licha ya hayo lakini kumekuwa na wachezaji ambao wamekuwa wakianza mara zote kama ilivyo kwa Che Malone, Abdulrazack Hamza na Moussa Camara.

Uchambuzi huu unayonyesha wana Simba wanapaswa kujipiga kifua kuwa wamepata bonge moja la kocha na wataraji kuwa na kikosi kipana katika klabu yao.

Mnyama ndiye kinara wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara na alimpasua vibaya mno Singida Fountain Gate katika dimba lake la CCM Liti, Singida.

#paulswai
🚨 FADLU NI KOCHA WA KISASA HANA KIKOSI CHA KWANZA. Nimemnukuu mchambuzi na mtangazaji mahari wa kabumbu nchini Nazareth Upete kupitia kipindi cha Bao la Asubuhi, amesema makocha wengi wa kisasa Duniani hawana First Eleven yaani kikosi cha kwanza. Hili linaangukia kwa kocha mkuu wa klabu ya Simba Fadlu Davids, ambaye amekuwa hatabiriki katika kikosi chake cha kwanza huku watu wengi wakionekana kutoelewa namna anavyobadilisha wachezaji wake wa kikosi cha kwanza. Upete pia aliendelea kusema, licha ya hayo lakini kumekuwa na wachezaji ambao wamekuwa wakianza mara zote kama ilivyo kwa Che Malone, Abdulrazack Hamza na Moussa Camara. Uchambuzi huu unayonyesha wana Simba wanapaswa kujipiga kifua kuwa wamepata bonge moja la kocha na wataraji kuwa na kikosi kipana katika klabu yao. Mnyama ndiye kinara wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara na alimpasua vibaya mno Singida Fountain Gate katika dimba lake la CCM Liti, Singida. #paulswai
Like
4
1 Комментарии ·234 Просмотры