Upgrade to Pro

Katika nchi ya Italy, Ottorino Barassi anafika ofisini kwake na moja kwa moja anaenda katika 'vaux', yaani chumba au kabati maalumu kunamohifadhiwa vitu nyeti au vyenye thamani. Vaux ni mahali salama ambapo si rahisi kwa mtu yeyote kuingia na kuiba.

Kwa umakini na usiri mkubwa, Ottorino Barassi anafika katika 'vaux' na kulichukua. Kisha anaenda nalo nyumbani kwake na kulificha. Yote hiyo ni kwa sababu hakutaka kuona wanajeshi wa nazi wanakuja kulichukua.

Ilikuwa ni katika vita ya pili ya dunia, ambapo majeshi ya Nazi, yakiongozwa na Adolf Hitler walikuwa wakilitafuta kwa udi na uvumba ili wapate kulitia mkononi.

Walifika hadi nyumbani kufanya upekuzi lakini hawakuweza kulipata. Kumbe Barassi alikuwa amelificha uvunguni mwa kitanda anacholala.

Unajua ni kitu gani nazungumzia hapo?.

Ni Kombe la dunia. Hitler alitaka kulinyakua kinguvu mnamo 1939, mwaka mmoja baada ya taifa la Italia kushinda michuano ya mpira wa mguu.

Kombe hilo lilikuwa likiitwa Jules Rimet, likipewa jina la aliyekuwa rais wa kwanza wa FIFA. Ottonio Barrasi alikuwa ni rais wa chama cha soka nchini Italy
Katika nchi ya Italy, Ottorino Barassi anafika ofisini kwake na moja kwa moja anaenda katika 'vaux', yaani chumba au kabati maalumu kunamohifadhiwa vitu nyeti au vyenye thamani. Vaux ni mahali salama ambapo si rahisi kwa mtu yeyote kuingia na kuiba. Kwa umakini na usiri mkubwa, Ottorino Barassi anafika katika 'vaux' na kulichukua. Kisha anaenda nalo nyumbani kwake na kulificha. Yote hiyo ni kwa sababu hakutaka kuona wanajeshi wa nazi wanakuja kulichukua. Ilikuwa ni katika vita ya pili ya dunia, ambapo majeshi ya Nazi, yakiongozwa na Adolf Hitler walikuwa wakilitafuta kwa udi na uvumba ili wapate kulitia mkononi. Walifika hadi nyumbani kufanya upekuzi lakini hawakuweza kulipata. Kumbe Barassi alikuwa amelificha uvunguni mwa kitanda anacholala. Unajua ni kitu gani nazungumzia hapo?. Ni Kombe la dunia. Hitler alitaka kulinyakua kinguvu mnamo 1939, mwaka mmoja baada ya taifa la Italia kushinda michuano ya mpira wa mguu. Kombe hilo lilikuwa likiitwa Jules Rimet, likipewa jina la aliyekuwa rais wa kwanza wa FIFA. Ottonio Barrasi alikuwa ni rais wa chama cha soka nchini Italy
·65 Ansichten