Обновить до Про

Unayemuona hapo pichani ni mwanaanga anayeitwa Bruce McCandless, huyu jamaa alikiuka taratibu za kiusalama ambazo ziliwekwa kufuatwa na wanaanga wote wakiwa nje ya Dunia kwa usalama wao. Jamaa alitoka kwenye chombo na kusogea umbali wa mita 100 kutokea kwenye chombo kilipokuwepo kisha akawa anaelea huru juu ya Dunia pasipo kuwa na kamba yoyote iliyounganishwa kutokea kwenye chombo kwa usalama wake. Tukio hili liliwaudhi NASA kiasi cha kwamba waliwapiga marufuku wanaanga kutembea huru nje ya Dunia pasipo kufuata taratibu za kiusalama zilizowekwa. Kitu pekee ambacho huyo mwanaanga alikuwa anakitegemea kimrudishe kwenye chombo ni kifaa maalumu kinachoitwa MMU (Manned Maneuvering Unit) ambacho huwa kinatumika kuwasukuma kutoka eneo moja kwenda lingine kwenye ombwe na kama ingetokea hicho kifaa kingegoma kufanya kazi huyo jamaa hapo asingeweza kuokolewa na hatma yake ingekuwa ni kuizunguka Dunia kwa miaka miwili kama satelaiti kabla hajavutwa chini na kuanza kuunguzwa kwenye anga la juu mpaka kufa au angeendelea kuelea huku akisogea kuelekea kule gizani mpaka angepotea na kufa peke yake baada ya oksijeni kumuishia. Tukio hili linahesabika kama moja ya matukio hatari zaidi kuwahi kufanywa na mwanadamu akiwa nje ya Dunia.

·24 Просмотры